Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Mie naona ili kuepuka kabisa ukabila katika maofisi ni vyema usaili kwa ajili ya kazi ufanywe na wageni. Ikiwezekana wafanye wazungu ambao hawajui kabila la mtu na wala hawajali dini ya mtu. maana kama wenyewe hatuwezi kutenda haki na pia kuaminiana ni vyema watusaidie watu wengine. Jamani tujitahidi kuwasomesha watoto wetu ili baadaye kusiwe na watu watakaojidai kuwa wao wamesoma zaidi!!
 
Msijali Ndugu Mwanangu Hatakuwa Profesa ,
Kwa sasa anapiga soka ,mipango yote akachezee hata Leeds kwa malkia ,so idadi yetu kwenye hizo ofisi ulizozitaja haitaongezeka 🙂
 
As long mtu ana sifa apewe nafasi,hiv nitamtosa wakwetu mwenye sifa nimchukue mtu from nowhere! Akiharib utamfatia wap? Kwanza hapa inajenga undugu na ufanisi kazini coz wote ni wachapakazi na wana sifa
 
Mjadala ulishafungwa na bandiko la nne tu, sasa mnaendelea kujadili nini?
 

Mzee mwanakijiji, majawabu ya Nyerere yalikuwa very valid wakati huo, kwa sasa tukikuta kabila moja kwenye idara moja sio sawa. makabila yote sasa yana watu waliosoma.
 
Kwenye suala hili nasikitika sana kwani kuna juhudi za makusudi za kutaka kufukarisha matajiri badala ya kuwa na juhudi za makusudi za kutajirisha maskini.
Na mbaya zaidi kwani kwenye masuala haya hakuna shortcut. Shule lazima usome miaka 14 au zaidi ndipo uwe na degree. Njia muafaka ni kujenga shule katika maeneo ya nchi yetu ambako wapo wachache serikalini.
Mwanakijiji anaongelea affirmative action ni kweli tunahitaji kwa baadhi ya wenzetu kwani binafsi nitajiskia vibaya kuona kuna mtindiga graduate halafu hana kazi. Huyu atatumiwa na wazee wa kwao kujustify kuwa kusoma hakuna maana ni kupoteza muda tu.
Tatizo la kuimplement affirmative action kwenye nchi yetu kwa sasa ni kwamba nchi "haina wenye nchi" wale aliokuwa nao Nyerere ambao unaweza ukawapa kazi ya kufuatilia mambo hayo ya kuona ni jinsi gani wenzetu wachache pale wanapojitokeza wanatendewa haki bila kuathiri wengine.
 
Acha maswala yako ya ajabu;kasome na wewe uajiliwe UDSM mnafiki mkubwa ww
 
Wasukuma waacheni tu...hawana ukabila Nyerere alifanikiwa kuwanyima kupendeleana. Kama baba yako ni Mkurugenzi wewe msukuma usitegemee mteremko. Hata hivyo wanasema miaka hii baada ya 2015 uchumi wa Tanzania utategemea Science (Mahospitali, viwandani n.k) I bet! Wasukuma watakuwa kila mahali maana madaktari wasukuma ni wengi sana, wahandisi balaa na mtaani watafurika maana hadi sasa tunakadiria zaidi ya 1/3 ya watanzania ni wasukuma na zaidi ya 2/3 wanazungumza kisukuma. La msingi ni kutangaza Wasukuma kuanzia sasa siyo Kabila (tuwape hadhi tofauti....amua tuwaitaje?) na lugha yao ni lugha rasmi kwa taifa la Tanzania baada ya Kiingereza na Kiswahili
 
daah mi kabila langu muwanji. joto la jiwe naliona saizi na degree yangu mkononi ukizingatia kabila letu halijashika idara yoyote hata umgambo
 
Sipendi ukabila.naomba watz tujitahidi kwenye elimu ili wote twende pamoja tusiachane.tunalalamika humu ndani lakini ukweli tuliopita shule na kukaa mitaani tunaujua.taasisi nyingi za elimu nilikopita nakumbuka usongo wa hao jamaa kutoka hizo kabila 3.hawana utani hata kidogo.nakumbuka negligence yetu wengi wakati walimu wanatupigia kelele tusome,negligence iliyokuwa influenced na mazingira yetu nyumbani,ratiba na tabia za wazazi wetu,tamaduni za koo na kabila zetu n.k.huko mitaani pia zipo tofauti.hawa jamaa wana discipline ya maisha ambayo wengi wetu tunaona mateso kuifuata lakini this is what makes the difference.mie nadhani tubadili tamaduni zetu kwanza kabla hatujanyooshea vidole wachaga na wengine wenye maendeleo.ukweli unauma!namkumbuka rafiki yangu mmoja aliyekuwa akitimuliwa ada mara kwa mara wakati tukiwa shule na kuja kunilalamikia kuwa mama yake(single parent) alimwambia hana hela lakini kesho yake walisafiri kwenda kwao Tanga kufagilia makaburi na kufanya matambiko shughuli iliyomgharimu mama huyo pesa nyingi tu!ni vitu vidoogo sana ndio vinatuletea tofauti kubwa ktk maisha.
 

Hahahaha! wasukuma eeh! wewe huwajui vizuri wachaga usijidanganye kabisa,wachaga wame dominate kilamahali na wengi kweli mashuleni na vyuo vikuu.mimi nafanya kazi sehemu ya science wachaga kibao! nenda muhimbili,nenda engineering UDSM,wako kibao sababu wachaga wako very aggressive ndugu yangu.Ukiniambia wasukuma nakushangaa kabisa! wachaga,wahaya,wanyakyusa wana juhudi sana ktk elimu,angalia hata shule nyingi zimerundikana Kilimanjaro,Mbeya,BKB na siku hizi na Iringa wanakuja juu.shinyanga Mmm!
 
J.J.Mungai once said "tukiruhusu watu wenye performance za hali ya juu kwenda shule za sekondari, basi shule hizo zitajazwa na watu wanafunzi wa kutoka Mara...hivyo lazima tubane ili na maeneo mengine wapate nafasi za sekondari" Hii ilichangia sana kudidimiza baadhi ya maeneo jamani..kwa lengo zuri tu kuweka uwiano kumbe ndo ilkuwa kuua maendeleo ya mikoa na watu wake wale...Madingi kibao kule ni mageneous kinyama, lakini hawakupata fursa ili wenzao wapate kwenda shule na ku-avoid u-dominance wa watu wa mahali fulani kuonekana wao wako juu...
 

wewe hapana chezea MANGI hata kidogo!!! hata mngekuwa nusu ya watanzania bado sisi ni zaidi na acheni kudanganyika na sijui ukabila , watu wanachapa kazi nyie mnaendeleza misifa ya kijinga tu, mtasema sana siye twasonga mbele! karbuni katika ulimwengu wa kazi na juhudi bila kukata tamaa.
 

mkabila huyoooooooooo
 

mhhhhh
 
Ya ikulu na hizo idara zingine siyajuwi ila TRA ni kiboko kwa ukabila. Wewe kama si mpare au mchagga na mtoto wa mjomba kupata kazi pale ni vigumu.
 
nilopokuwa chuo kulikuwa na wachaga zaidi ya robo kamasio nusu.....mkinga 1,,wasukuma hawakuwa zaidi ya 20..wahaya kama 30..+wengine warabu na wahindi kama wawili wawili waioppenda kujulikana ukabila wapia walikuwepo,,,,,ila wachaga walikuwa wengi zaidi kimakundi waislamu ndio usisema walikuwa chini ya robo ya darasa.....tegemea tuipata kazi wote swala la ubaguzi lisitokee ni ajabu............
 
mbona hautaji ukabila pale Muh2 na, UDSM?

PRO shayo, Pro Kinasha, Pro Mushi, Pro Temu, Dr Kisanga, Dr Temu, Dr Lema, Dr Mtei, Dr Kundi, Dr Matee, na wengineo. ukienda Muh2 utawakuta wanatibu nashangaa hawa hawauliziwi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…