kwa mtu makini haitaji tena ushahidi kujua TRA kulivyochafuka na ukabila(uchagga).
Nauliza kwa mara ya mwisho, ukabila unaozungumzia wewe ni upi? Wingi wa watu wa kabila moja kwenye mahala pa kazi au upendeleo wa mtu kuona kabila lake ni bora kuliko makabila mengine yote na hivyo wanastahili zaidi?
cha kujiuliza ilikuwaje Bwana MMANDA atoe press release mwaka jana july na kuwatetea wachagga kuwa wako TRA kwa sifa, kwanini asitaje kabila lingine? au alikurupuka tu bila kuwa na tuhuma hizo? kifupi alikuwa akijibu tuhuma kama hizi zetu. na yeye hakukanusha kama hakuna wachagga ila aliwatetea kuwa ni shule yao.
Ili kuonesha jinsi gani makabila mengine yamepiga hatua kubwa kielimu naomba unioneshe data zinazoonesha kuwa wachagga wamerudi nyuma kielimu wakati makabila mengine yamesonga mbele. Kama wachagga wameendelea kusomesha watoto wao zaidi kuliko makabila mengine itakuwaje wasiwe na watu wengi mahali pa kazi unless tuamue kwa makusudi kabisa kuzuia wachagga wasipeleke watoto sekondari, vyuoni n.k ili makabila mengine yawafikie!!! Sasa tuhuma zimetolewa kuhusu idara yake kwanini asijibu? Nani ulitaka awajibie TRA?
inawezekana miaka ya 1970s ikawa kweli wachagga walikuwa mbele kielimu. lakini hivi hata mkagua documents au mkadiria kodi hakuna makabila mengine hadi awe mchaga? sio kweli watu hivi sasa wamesoma sana makabila yote, tizama maombi ya kazi watu wanavyoomba toka makabila yote.
Inawezekana? huwezi kuficha hoja dhaifu kwa kutumia kivuli cha maneno. Je wachagga walikuwa mbele kielimu miaka ya 70 au hawakuwa? jibu ni ndiyo au hapana. Kama jibu ni "hapana" basi hoja yako ina uzito zaidi kwani itaelezea kwanini kuna "idadi kubwa ya wachagga kazini -iitwayo ukabila". Hebu nithibitishie madai yako kuwa "
watu hivi sasa wamesoma sana makabila yote, tizama maombi ya kazi watu wanavyoomba toka makabila yote" Kama watu "wamesoma sana makabila yote" kauli hiyo inawahusu Wahaya, Wachagga, na Wanyakyusa? au unahesabu makabila mengine yote na makabila hayo matatu siyo makabila yaliyosoma?
Kama makabila mengine yamesoma sana je makabila hayo matatu yaliacha lini kusoma? Nipe ratio ya Wachagga to Wazigua, Wahaya to Wamatumbi na Wanyakyusa to Wafipa ndio nitaamini maneno yako kuwa makabila hayo yamefikia. Ratio pekee itakayokubalika ni ya one to one.. Kila Mhaya mwenye digrii moja kuna Mmatumbi mwenye digrii moja n.k!!
phillimon jiulize tena MMANDA alikuwa anayatolea maelezo mambo ambayo hayapo? na fikiria sana watu kulipeleka bungeni suala la uchagga TRA iwe bila kuwa na chembe ya ukweli? wewe mwenyewe unajikanyaga kwa kusema hata kama wachagga wamekusanya kiasi kadhaa cha kodi. hapa hatulalamikii kuwa kodi haikusanywi ila taratibu za ajira ni mbaya na kama wote kabila moja hata ufanisi utakuwa ni mdogo.
Sasa hii hoja haina hata mantiki. Hivi watu wakilizungumzia jambo fulani ina maana jambo hilo lipo. Hivi tukikubaliana hapa na kuzungumza kuhusu uwepo wa viumbe toka Mars inafanya viumbe hivyo viwepo? Watu wakizungumzia ukabila inafanya ukabila uwepo hata kama haupo. Suala la "perception" ni suala gumu sana kushinda kwani kwa watu wengine perception is reality. Jifunze mfano wa pango wa Plato kwenye kitabu chake cha "Republic". Wewe na wenzako mmeng'ang'ani tutafsiri kuwa uwepo wa wachagga, wahaya, wengi mahala pengi pa kazi ni matokeo ya UKABILA TU. Hauko tayari kukubali maelezo mengine kama historia, kujuana, kufahamiana, eneo la jiografia n.k.
Mnataka tuiname na kukubali kuwa Wahaya, Wanyakyusa, na Wachagga ni wabaguzi wa kikabila kuliko watu wengine. Hilo mimi nalikataa kwani hadi hivi sasa hakuna ushahidi wa hilo.
Kuhusu TRA, hebu nitafutie majina ya wafanyakazi wa ngazi za juu wa mikoa yote, wilaya zote na vitengo vyote nioneshe kuwa Wachagga wanazidi asilimia 50! hapo nitashtuka. Of course, naelewa kwanini TRA, sote tunajua bias tuliyonayo kuhusu "Wachagga na kupenda fedha". Nakumbuka all kinds of jokes we used to say about wachagga na pesa! Kutokana na bias hii katika jamii hivi kweli kama kun mahali pa kuona jinsi wachagga wanapenda pesa haitakuwa kwenye TRA, Hazina, na Wizara ya Fedha!? We are projecting our biases toward these institutions and then we find tribalism!!!
nimekupa maelekezo mengi na vielelezo nani yuko wapi? lakini bado unaona sina nia njema na wachagga, ilikuwa uje na facts kama mswahili umesema wharf TRA kuna mchagga lakini ukweli kuna msukuma. hayo hujafanya ila umekuja kukashfu tu.
"maelezo mengi na vielelezo"? really!? Nipe maelezo na vielelezo vya mikoa yote, vitengo vyote vya makao makuu TRA na vituo vyote vya mipaka, nioneshe Mswahili majina na makabila ya watu hao!! please I beseech thee!!
DR.Who amekuuliza maswali juu ya NSSF hajajibu kitu zaidi ya kuishi kwa tetesi tu.
mie siamini kuwa hata kalani wa TRA lazima awe mchagga tukiuliza tunaambiwa sababu za kihistoria. kweli ndani ya miaka 40 ya uhuru hakuna makabila mengine yanayoweza kuwa makalani TRA?
Si useme tu kuwa kama kijana mchagga asiye na Elimu naye anataka ukarani basi asiajiliwe TRA kwa vile kuna wachagga wengi. Nakushauri mnapomkatilia kijana huyo hiyo nafasi mumuambie kuwa "hatuwezi kukuajiri kwa kuwa wewe ni mchagga, na tayari quota yetu ya wachagga hapa imeshajaa!" You'll make him a millionare!! go ahead and do it!! Tuambieni mahali pa kazi kuwa na quota ya wachagga, wahaya, na wanyakyusa wangapi?
KAMA hivyo ndivyo basi hatuna haja kuwa na uhuru ikiwa katika kipindi chote hatuna makalani toka makabila mengine.
Uzalendo uliojificha kwenye ubaguzi! Hivi makarani wote Tanzania ni Wachagga? Je wachagga hawastahili kuwa Makarani? Haya naomba uwachagulie ajira basi maana wakiwa mabosi hutaki, wakiwa makarani hutaki, wawe nani sasa?!
mikael
suala hili la ukabila la wachagga hata VETA hashiki mtu mwingine cheo cha juu hadi uwe mchagga na hili limefikishwa kwa waziri muhusika hapo ndio ujue kuwa hii kansa kuinyamazia au kutafuta justification yeyote si dawa. tatizo dawa ni kulikabili na si kutafuta njia ya kulikwepa.
Give me a break, kwanini waende kwa waziri? Kama kuna huo ushahidi nendeni mahakamani.. oops! Mahakamani kumejaa wachagga, wanyakyusa na wahaya!!
wanabodi fuatilieni kwa makini tuhuma hizi kama tunataka jamboforum iwe sehemu ya kukata issue basi hii ya ukabila TRA ni issue nzito.
Absolutely! na hatuwezi kuacha watu wachache watuburuze wengine alimradi wanatumia maneno "ukabila" hoja hujibiwa kwa hoja!!
Mwanakijiji.
sisemi mengi ila najua kuwa wewe nawe kabila lako lina kashfa hii sasa unajua mwenzio akinyolewa wewe tia maji.
nadhani kutokana na kashfa ya ukabila katika kitengo mlichokimiliki ilibidi serikali kipindi cha mwinyi ibadilishe utaratibu wa ajira ili kuzuia kabila lenu kumiliki taasisi ile nyeti. ikawa kila mkoa unaleta watu wake.
kama serikali iliyaona kwenu tunaomba na TRA nako kumulikwe.
So somehow you think you know me? pole... I'm not one of the three tribes.. jina langu laweza kuwachanganya wengi...(ni historia ndefu)... and I'm not the subject na sijawahi kuajiriwa Tanzania au kushika kitengo chochote!