Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Mzeee PM na wazee wote, heshima mbele!,

punguzeni jazba mimi ni muoga sana na deal za ukabila na udini, maana ninajua kuwa ni vigumu kubadili misimamo ya wanaohusika nayo, lakini I am enjoying huuu mjadala sioni noma yoyote,

Lakini Mzee PM, I am not serious bro!, ila nafikiri baaad ay amijadala mikali iliyopita na inayoendelea ni vyema watu waka-relax na hiii kitu kwani kwangu ni kiburudisho ki-kali sana, kwa hiyo ninawaomba wote mnaochangia kuwa mukiacha jazba huu mjadala utakuwa mtamu sana!

Shukrani!
 
Mkandara.

pole sana kwa maelezo marefu unayowapa kina mikael phillimon.

lakini tayari wana majibu yao. ninavyoamini mimi dawa ya tatizo ni kulitatua na si kulifumbia macho au kulifunika kwa hali yeyote ile.

kwa mtu makini haitaji tena ushahidi kujua TRA kulivyochafuka na ukabila(uchagga).
cha kujiuliza ilikuwaje Bwana MMANDA atoe press release mwaka jana july na kuwatetea wachagga kuwa wako TRA kwa sifa, kwanini asitaje kabila lingine? au alikurupuka tu bila kuwa na tuhuma hizo? kifupi alikuwa akijibu tuhuma kama hizi zetu. na yeye hakukanusha kama hakuna wachagga ila aliwatetea kuwa ni shule yao.

inawezekana miaka ya 1970s ikawa kweli wachagga walikuwa mbele kielimu. lakini hivi hata mkagua documents au mkadiria kodi hakuna makabila mengine hadi awe mchaga? sio kweli watu hivi sasa wamesoma sana makabila yote, tizama maombi ya kazi watu wanavyoomba toka makabila yote.

phillimon jiulize tena MMANDA alikuwa anayatolea maelezo mambo ambayo hayapo? na fikiria sana watu kulipeleka bungeni suala la uchagga TRA iwe bila kuwa na chembe ya ukweli? wewe mwenyewe unajikanyaga kwa kusema hata kama wachagga wamekusanya kiasi kadhaa cha kodi. hapa hatulalamikii kuwa kodi haikusanywi ila taratibu za ajira ni mbaya na kama wote kabila moja hata ufanisi utakuwa ni mdogo.

nimekupa maelekezo mengi na vielelezo nani yuko wapi? lakini bado unaona sina nia njema na wachagga, ilikuwa uje na facts kama mswahili umesema wharf TRA kuna mchagga lakini ukweli kuna msukuma. hayo hujafanya ila umekuja kukashfu tu.

DR.Who amekuuliza maswali juu ya NSSF hajajibu kitu zaidi ya kuishi kwa tetesi tu.

mie siamini kuwa hata kalani wa TRA lazima awe mchagga tukiuliza tunaambiwa sababu za kihistoria. kweli ndani ya miaka 40 ya uhuru hakuna makabila mengine yanayoweza kuwa makalani TRA?

KAMA hivyo ndivyo basi hatuna haja kuwa na uhuru ikiwa katika kipindi chote hatuna makalani toka makabila mengine.

mikael

suala hili la ukabila la wachagga hata VETA hashiki mtu mwingine cheo cha juu hadi uwe mchagga na hili limefikishwa kwa waziri muhusika hapo ndio ujue kuwa hii kansa kuinyamazia au kutafuta justification yeyote si dawa. tatizo dawa ni kulikabili na si kutafuta njia ya kulikwepa.

wanabodi fuatilieni kwa makini tuhuma hizi kama tunataka jamboforum iwe sehemu ya kukata issue basi hii ya ukabila TRA ni issue nzito.

Mwanakijiji.

sisemi mengi ila najua kuwa wewe nawe kabila lako lina kashfa hii sasa unajua mwenzio akinyolewa wewe tia maji.

nadhani kutokana na kashfa ya ukabila katika kitengo mlichokimiliki ilibidi serikali kipindi cha mwinyi ibadilishe utaratibu wa ajira ili kuzuia kabila lenu kumiliki taasisi ile nyeti. ikawa kila mkoa unaleta watu wake.
kama serikali iliyaona kwenu tunaomba na TRA nako kumulikwe.
 
Mzeee FD,

Punguza munhali bro, we can have fun sometimes lakini stilll kuna some important points, wazeee mwageni vitu Mswahili weka maneno mwanangu na mzee MMMJ lete vitu mzee,

Mswahili Kumkoma Nyani Giladi, milima ya Golani lete vitu mwanangu!
 
Labda ninge jaribu ku-repost maswali yangu ya awali ili tuende na DATA pamoja na facts:

swali kwa Philemon Michael lilikuwa ni:

Dr DAU aliingia NSSF lini?

Alikuta makusanyo pale NSSF chini ya MKULO yalikuwa kiasi gani?

Sasa hivi yako kiasi gani?

Je Kulikuwa na investments za kiasi gani?

Sasa hivi investments zimefikia kiasi gani?

Na ni Propaganda zipi anazitumia kuendesha shirika kubwa la wanachi la NSSF?

Na imekuwaje ameweza kusurvive pale muda wote huo tangu MKAPA amuweke pale?

Na ikiwa unaweza kuniconvince katika hayo then nitakuwa mtu wa kwanza kuanzisha "MWANAKIJIJI STYLE" kampeni zakumuondoa pale NSSF
 
SWALI LA WALI KWA KICHUGUU

quote=kichuguu;21589]

Quote:
Professor Malima alipopata skolaship ya kwenda marekani kusoma kati ya mwaka 1964 na 66 hivi wakati huo akiwa katibu mtendaji wa TANU wilaya fulani mkoa wa pwani, hakuna aliejua kuwa atakuja kuwa mzigo sana kwa nchi. Aliporudi alipewa kazi ya katibu Mkuu wizara ya mipango chini ya Waziri Professor Abdurlahmani Babu ambaye mara moja aliona weakness yake na kumkataa.

HEBU EXPAND HIII maana nilikuwa siijui hii

Quote:
Ndipo Nyerere alipoamua kumpa kazi ya kufundisha Chuo kikuu ambapo alipata uprofessor kutokana na mshahara aliotoka nao serikalini wa katibu mkuu wa wizara. Huyu mtu hakuwa professor on merit. Niliwahi kusoma review iliyoandikwa na Professor Shivji kuhusu profesorial inaugural lecture ya Malima iliyokuwa ikiitwa kitu kama " The Political Economy of Devaluation in Developing Countries "; Shivji alionyesha kuwa this guy was really bogus.

Nimejaribu kuGOOGLE hiyo ya Shivji uliyoitaja hapo juu lakini sijaona kitu lakini that said naomba unielezee CRITIQUE ya Shivji kwa malima ilikuwa kwenye maeneo yepi ya kisomi, je ilikuwa Law au Developing economics ? Na ilikuwa based on which grounds ? na kama unayo basi imwage humu ili na sisi wengine tupate kuweka arguments zetu....na haswa upande wa developing economics

Quote:
Unfortunately professor Malima hakuwahi kuandika technical paper yoyote kudhihirisha umahiri wake kama mtaalamu wa uchumi, alichoacha ni technical reports kadhaa zisizokuwa na maana yoyote na ambazo hakuna hata moja ilyowahi kuwa cited.

Hili nilikuwa silijui lakini hebu nipe mfano wa paper au reports ambazo aliandika Malima ambazo hazikuwa na maana yoyote ile

Nilifikiri kuwa Prof Rweikiza Mukandala aliwahi kufanya citation za Malima hapo nyuma lakini sina hakika ila naomba unipe mwangaza katika hili

Quote:
hata hivyo nadhani Malima alitia fora kwa kuvurunda.

kivipi? kukataa mapendekezo ya WORLD BANK kuuza NBC au? hebu tupe emperical evidence jinsi gani alivyo vurunda...natumai kuwa you understand economics na niko tayari kufanya mjadala na wewe kuhusu hili...
 
umesema mwenyewe kama Watanzania watakuwa hawana uwezo wa kufanya kazi hiyo!... jibu safi kabisa na hakuna aliyesema hapa kuwa kazi za TRA haziwezwi na makabila mengine!..

Yebo Yebo kusema kweli mimi ningekuwa mwajiri, kuandika CV sio kabisa kigezo cha kumpa mtu kazi. CV unaweza kui - download toka ktk website kibao, wala cheti cha mtu hakiwezi kuwa kivutio kikubwa cha mimi kutoa ajira. Ila cheti ni pasi ya mtu kuingia ktk ushindani kisha huko ndani watakutana na maswali yanayohusu kazi yenyewe kwa kuzingatia nani customer wangu. Bongo mnaajiri tu watu wenye CV kubwa hali watu hawa hawafahamu kabisa mbinu za kukuza biashara, communication na costomer mbovu na wajeuri ati mnachotazama ni communication ya kule mna konunua mali! Ulaya....very strange! Ulaya ndio wanatakiwa kujifunza lugha yako kwa sababu wewe ni customer wao!....not vise verse.

No wonder wahindi wanahonga sana TRA kiasi kwamba Viongozi wanahesabu millioni zilikusanywa badala ya kuhakikisha system haitoi mwanya wa kuiba. What if tanzania ilitakiwa kukusanya billioni 3 badala ya hizi tunazojivunia kutokana na kuwepo kwa system mbove ya ukusanyaji kodi?... Tunayaona kwa barricks na wachimbaji wengine kiais kwamba ukusanyaji kodi tanzania ni adhabu kwa raia na wenye biashara ndogo. Wadanganyika wanapiga makofi
na kufurahia ukusanyaji wa fedha tena basi nini - local taxes na imports from small business!...

Mkandara UNATISHA

btw jina lako nishalichukua na nitaendela kukusoma kadri siku zinavyokwenda

Japo kuna baadhi ya mambo napingana na wewe lakini still nitakuwa mnafiki kama nitaaangalia differences zetu ili hali kuna mengi ambayo naamini kuwa mimi na wewe tunaonana macho kwa macho

Thanks for looking at this matter on a different perspective

@MSWAHILI

kimya chako kilikuwa kirefu na mshindo wako ni mkuuu japo style yako inawaudhi baadhi ya watu lakini nadhani kama utakuja na style ulioingina nayo leo basi naaminu kutakuwa na mwanga

Unanikumbusha Tafiti then Jadili ambaye inasemekana kuwa ameamua kujiwekea embargo ya kutokukuja kujadili na kwa kweli pengo lake LINAZIDI KUWA KUBWA KADRI SIKU ZINAVYOZIDI KWENDA na hii inanipelekea kuuliza swali kuwa je. TAFITI THEN JADILI ame cut and run?
 
Guys

I think we should stop looking a specific issues and instead pay attension to the whole enviroment ya uajiri serikalini. Kama kuna mabadiliko yanatakiwa then tuyakubali na kuyatekeleza badala ya kulaumu tu.
 
kwa mtu makini haitaji tena ushahidi kujua TRA kulivyochafuka na ukabila(uchagga).

Nauliza kwa mara ya mwisho, ukabila unaozungumzia wewe ni upi? Wingi wa watu wa kabila moja kwenye mahala pa kazi au upendeleo wa mtu kuona kabila lake ni bora kuliko makabila mengine yote na hivyo wanastahili zaidi?

cha kujiuliza ilikuwaje Bwana MMANDA atoe press release mwaka jana july na kuwatetea wachagga kuwa wako TRA kwa sifa, kwanini asitaje kabila lingine? au alikurupuka tu bila kuwa na tuhuma hizo? kifupi alikuwa akijibu tuhuma kama hizi zetu. na yeye hakukanusha kama hakuna wachagga ila aliwatetea kuwa ni shule yao.

Ili kuonesha jinsi gani makabila mengine yamepiga hatua kubwa kielimu naomba unioneshe data zinazoonesha kuwa wachagga wamerudi nyuma kielimu wakati makabila mengine yamesonga mbele. Kama wachagga wameendelea kusomesha watoto wao zaidi kuliko makabila mengine itakuwaje wasiwe na watu wengi mahali pa kazi unless tuamue kwa makusudi kabisa kuzuia wachagga wasipeleke watoto sekondari, vyuoni n.k ili makabila mengine yawafikie!!! Sasa tuhuma zimetolewa kuhusu idara yake kwanini asijibu? Nani ulitaka awajibie TRA?

inawezekana miaka ya 1970s ikawa kweli wachagga walikuwa mbele kielimu. lakini hivi hata mkagua documents au mkadiria kodi hakuna makabila mengine hadi awe mchaga? sio kweli watu hivi sasa wamesoma sana makabila yote, tizama maombi ya kazi watu wanavyoomba toka makabila yote.

Inawezekana? huwezi kuficha hoja dhaifu kwa kutumia kivuli cha maneno. Je wachagga walikuwa mbele kielimu miaka ya 70 au hawakuwa? jibu ni ndiyo au hapana. Kama jibu ni "hapana" basi hoja yako ina uzito zaidi kwani itaelezea kwanini kuna "idadi kubwa ya wachagga kazini -iitwayo ukabila". Hebu nithibitishie madai yako kuwa "watu hivi sasa wamesoma sana makabila yote, tizama maombi ya kazi watu wanavyoomba toka makabila yote" Kama watu "wamesoma sana makabila yote" kauli hiyo inawahusu Wahaya, Wachagga, na Wanyakyusa? au unahesabu makabila mengine yote na makabila hayo matatu siyo makabila yaliyosoma? Kama makabila mengine yamesoma sana je makabila hayo matatu yaliacha lini kusoma? Nipe ratio ya Wachagga to Wazigua, Wahaya to Wamatumbi na Wanyakyusa to Wafipa ndio nitaamini maneno yako kuwa makabila hayo yamefikia. Ratio pekee itakayokubalika ni ya one to one.. Kila Mhaya mwenye digrii moja kuna Mmatumbi mwenye digrii moja n.k!!

phillimon jiulize tena MMANDA alikuwa anayatolea maelezo mambo ambayo hayapo? na fikiria sana watu kulipeleka bungeni suala la uchagga TRA iwe bila kuwa na chembe ya ukweli? wewe mwenyewe unajikanyaga kwa kusema hata kama wachagga wamekusanya kiasi kadhaa cha kodi. hapa hatulalamikii kuwa kodi haikusanywi ila taratibu za ajira ni mbaya na kama wote kabila moja hata ufanisi utakuwa ni mdogo.

Sasa hii hoja haina hata mantiki. Hivi watu wakilizungumzia jambo fulani ina maana jambo hilo lipo. Hivi tukikubaliana hapa na kuzungumza kuhusu uwepo wa viumbe toka Mars inafanya viumbe hivyo viwepo? Watu wakizungumzia ukabila inafanya ukabila uwepo hata kama haupo. Suala la "perception" ni suala gumu sana kushinda kwani kwa watu wengine perception is reality. Jifunze mfano wa pango wa Plato kwenye kitabu chake cha "Republic". Wewe na wenzako mmeng'ang'ani tutafsiri kuwa uwepo wa wachagga, wahaya, wengi mahala pengi pa kazi ni matokeo ya UKABILA TU. Hauko tayari kukubali maelezo mengine kama historia, kujuana, kufahamiana, eneo la jiografia n.k. Mnataka tuiname na kukubali kuwa Wahaya, Wanyakyusa, na Wachagga ni wabaguzi wa kikabila kuliko watu wengine. Hilo mimi nalikataa kwani hadi hivi sasa hakuna ushahidi wa hilo.

Kuhusu TRA, hebu nitafutie majina ya wafanyakazi wa ngazi za juu wa mikoa yote, wilaya zote na vitengo vyote nioneshe kuwa Wachagga wanazidi asilimia 50! hapo nitashtuka. Of course, naelewa kwanini TRA, sote tunajua bias tuliyonayo kuhusu "Wachagga na kupenda fedha". Nakumbuka all kinds of jokes we used to say about wachagga na pesa! Kutokana na bias hii katika jamii hivi kweli kama kun mahali pa kuona jinsi wachagga wanapenda pesa haitakuwa kwenye TRA, Hazina, na Wizara ya Fedha!? We are projecting our biases toward these institutions and then we find tribalism!!!

nimekupa maelekezo mengi na vielelezo nani yuko wapi? lakini bado unaona sina nia njema na wachagga, ilikuwa uje na facts kama mswahili umesema wharf TRA kuna mchagga lakini ukweli kuna msukuma. hayo hujafanya ila umekuja kukashfu tu.

"maelezo mengi na vielelezo"? really!? Nipe maelezo na vielelezo vya mikoa yote, vitengo vyote vya makao makuu TRA na vituo vyote vya mipaka, nioneshe Mswahili majina na makabila ya watu hao!! please I beseech thee!!

DR.Who amekuuliza maswali juu ya NSSF hajajibu kitu zaidi ya kuishi kwa tetesi tu.

mie siamini kuwa hata kalani wa TRA lazima awe mchagga tukiuliza tunaambiwa sababu za kihistoria. kweli ndani ya miaka 40 ya uhuru hakuna makabila mengine yanayoweza kuwa makalani TRA?

Si useme tu kuwa kama kijana mchagga asiye na Elimu naye anataka ukarani basi asiajiliwe TRA kwa vile kuna wachagga wengi. Nakushauri mnapomkatilia kijana huyo hiyo nafasi mumuambie kuwa "hatuwezi kukuajiri kwa kuwa wewe ni mchagga, na tayari quota yetu ya wachagga hapa imeshajaa!" You'll make him a millionare!! go ahead and do it!! Tuambieni mahali pa kazi kuwa na quota ya wachagga, wahaya, na wanyakyusa wangapi?

KAMA hivyo ndivyo basi hatuna haja kuwa na uhuru ikiwa katika kipindi chote hatuna makalani toka makabila mengine.

Uzalendo uliojificha kwenye ubaguzi! Hivi makarani wote Tanzania ni Wachagga? Je wachagga hawastahili kuwa Makarani? Haya naomba uwachagulie ajira basi maana wakiwa mabosi hutaki, wakiwa makarani hutaki, wawe nani sasa?!

mikael

suala hili la ukabila la wachagga hata VETA hashiki mtu mwingine cheo cha juu hadi uwe mchagga na hili limefikishwa kwa waziri muhusika hapo ndio ujue kuwa hii kansa kuinyamazia au kutafuta justification yeyote si dawa. tatizo dawa ni kulikabili na si kutafuta njia ya kulikwepa.

Give me a break, kwanini waende kwa waziri? Kama kuna huo ushahidi nendeni mahakamani.. oops! Mahakamani kumejaa wachagga, wanyakyusa na wahaya!!

wanabodi fuatilieni kwa makini tuhuma hizi kama tunataka jamboforum iwe sehemu ya kukata issue basi hii ya ukabila TRA ni issue nzito.

Absolutely! na hatuwezi kuacha watu wachache watuburuze wengine alimradi wanatumia maneno "ukabila" hoja hujibiwa kwa hoja!!

Mwanakijiji.

sisemi mengi ila najua kuwa wewe nawe kabila lako lina kashfa hii sasa unajua mwenzio akinyolewa wewe tia maji.

nadhani kutokana na kashfa ya ukabila katika kitengo mlichokimiliki ilibidi serikali kipindi cha mwinyi ibadilishe utaratibu wa ajira ili kuzuia kabila lenu kumiliki taasisi ile nyeti. ikawa kila mkoa unaleta watu wake.
kama serikali iliyaona kwenu tunaomba na TRA nako kumulikwe.

So somehow you think you know me? pole... I'm not one of the three tribes.. jina langu laweza kuwachanganya wengi...(ni historia ndefu)... and I'm not the subject na sijawahi kuajiriwa Tanzania au kushika kitengo chochote!
 
Mzee Mwanakijiji,

Najua sana kuwa maswali haya umeyaelekeza kwa Mswahili - Sintayajibu ila kipande kimoja tu ambacho umezungumzia. Kipande ambacho kusema kweli kimeniacha domo wazi!...
Pale ulipohoji elimu ya Wachagga kuwa wengi miaka ya 70 na kutoa mifano kibao!
Ndugu Mwanakijiji miaka ya 70 Wachagga, Wanyakyusa na Wahaya walikuwa WAMESOMA wengi hii haina ubishi lakini tambua maana ya wamesoma!... yaani waliokwisha hitimu. Sasa unapovuta mwaka 1970 hadi leo ni miaka zaidi ya 30 imeshapita na wengi wa hawa watu waliosoma ni wastaafu ama hawatafuti ajira tena. Hatuzungumzii watu hawa ktk swala la ajira!Tunazungumzia hesabu ya watu walioanza kusoma toka 70 kuja leo hii baada ya mfumo wa elimu kuwa wazi kwa watu wote. Mimi naamini kabisa sio perception, kuwa watu wa makabila mengine wameweza kujipatia elimu kirahisi na wengi wamehitimu tena kwa hesabu kubwa. hata hiyo mikoa ya Kilimanjaro, Mbeya na Ziwa magharibi yote ilikuwa na wanafunzi wengi wa makabila mengine sio wenyeji peke yao. Mchanganyiko ambao leo hii tunauzungumzia kuwa ndio sababu kubwa ya nchi yetu kutokuwa na Ukabila....Nitarudia bila perception tazama mwenyewe matokeo ya shule hizo za mikoa hiyo utakuta kwamba hata shule zilizofanya vizuri, top 10 ama 20 (schools) utakuta ni watoto wa makabila tofauti tofauti na ndio maana vhuo vikuu hawakujaa makabila haya peke yake. Shule iko wapi sio kabisa sababu ya wanafunzi kuwa wa kabila la pale. Ushindi haupatikani tena kwa makabila ila shule ambazo zina mchanganyiko wa kila kabila.
Sidhani kama kuna ushahidi zaidi wa kuonyesha ukweli wa elimu nchini kama hatuta tazama wanafunzi waliosoma vyuo vyetu wanatoka makabila gani! tazama majina ya graduates utapata ukweli na sio ku speculate vitu ili mradi kum-umbua Mswahili.
Hatuja wahi fanya hivyo na hatufanyi hivyo kwa sababu kama kweli makabila yale tuliyoyataja yangeendelea kuwa bado dominant ktk elimu basi leo hii ungesikia kelele hizi zikielekezwa ktk elimu!.lawama zingekuwa shule zinasajiri wanafunzi kwa makabila yao! but tatizo lipo ktk ajira sio elimu!
It worth looking at the problem if there is any!..
 
Labda ninge jaribu ku-repost maswali yangu ya awali ili tuende na DATA pamoja na facts:

swali kwa Philemon Michael lilikuwa ni:

Dr DAU aliingia NSSF lini?

Alikuta makusanyo pale NSSF chini ya MKULO yalikuwa kiasi gani?

Sasa hivi yako kiasi gani?

Je Kulikuwa na investments za kiasi gani?

Sasa hivi investments zimefikia kiasi gani?

Na ni Propaganda zipi anazitumia kuendesha shirika kubwa la wanachi la NSSF?

Na imekuwaje ameweza kusurvive pale muda wote huo tangu MKAPA amuweke pale?

Na ikiwa unaweza kuniconvince katika hayo then nitakuwa mtu wa kwanza kuanzisha "MWANAKIJIJI STYLE" kampeni zakumuondoa pale NSSF

dwho
heshima yako mkuu,

hili suala la perfomance ya dr dau anatakiwa ajibu mswahili badaya yake anayupa maneno matupu tu kuwa jamaa anafanya wounders...atupe data...nadhani mswahili unanipata ,pale nssf watu wengi wanamkumbuka mkullo mustapha ,bila ya kupigiwa debe wanajua kajenga ..mwalimu nyerere towers,former british embassy,mafuta house priject,ubungo plaza joint venture,bunge complex joint venture,arusha complex,mwanza complex,kinyerezi complex ets hizo ni baadhi ya project tu ninazokumbuka,nataka mswahili uje na data kuelezea mafanikio ya dr dau.

kimsingi mimi simpingi dau,bali nahitaji kuelezewa zaidi vitu vyake kwa kuwa bado sijaviona,najua kuwa kabla ya kuchaguliwa alikuwa one of departments pale bandari kama boss..
mswahili ukiwa unatuambia mambo ya nssf bila vivid datas tunabaki kufikiri unafanyia watu propaganda hapa...
 
Mzee Mwanakijiji,

Najua sana kuwa maswali haya umeyaelekeza kwa Mswahili - Sintayajibu ila kipande kimoja tu ambacho umezungumzia. Kipande ambacho kusema kweli kimeniacha domo wazi!...
Pale ulipohoji elimu ya Wachagga kuwa wengi miaka ya 70 na kutoa mifano kibao!
Ndugu Mwanakijiji miaka ya 70 Wachagga, Wanyakyusa na Wahaya walikuwa WAMESOMA wengi hii haina ubishi lakini tambua maana ya wamesoma!... yaani waliokwisha hitimu. Sasa unapovuta mwaka 1970 hadi leo ni miaka zaidi ya 30 imeshapita na wengi wa hawa watu waliosoma ni wastaafu ama hawatafuti ajira tena. Hatuzungumzii watu hawa ktk swala la ajira!

Mzee Mkandara wewe ndio umeniacha mimi mdomo wazi! Sasa wazee wa kichagga waliokuwa wamehitimu miaka ile waliacha lini kusomesha watoto wao na wajukuu wao? I'll argue that wachagga wanaolalamikiwa ni watoto na wajukuu wa wazee waliosoma enzi za mkoloni, you prove me otherwise! Nimeuliza tena, ni lini Wahaya, Wanyakyusa, na Wachagga waliacha kusomesha watoto wao? Kama kweli elimu ilifunguliwa kwa watu wote, je nafasi kwa watoto wa makabila hayo zilipungua au ziliongezeka pia?

Njia pekee ya kutatua tatizo lenu ni kuhakikisha kuwa makabila hayo matatu hawaajiriwi, na wakiomba nafasi hata kama they are more than qualified then they should be denied ili wasiwe wengi!!! Sioni njia nyingine ya kupunguza makabila hayo, naomba unisaidie, maana tunachozungumzia siyo ukabila ni idadi ya watu hao kwenye sehemu mbalimbali....tufanye nini ili Wachagga, Wahaya, na Wanyakyusa wapungua kwenye idara mbalimbali za serikali? Nitawaunga mkono 100% mkija na pendekezo ambalo halitakuwa na harufu ya ukabila.
 
Mzee MJJ,
You have posed very important questions and so far no one has come up with a sound response apart from confining themselves to their Utopian way of thinking..sadly, its now been considered that anybody who argues against this issue is a member of one of those tribes. Am sure that if we allow ourselves to look at this issue objectively we will come up with a plausible proposal that you are seeking.
The historical facts are undeniable; and the fact that that history has much influence in the present state of affairs cannot be denied either. It is also true that these same tribes are still in the forefront in education, in and outside the country. I even suggested that we look at the statistics at our universities- which will show us how things are moving from the colonial times to-date..it is a fact that the trend is the same, and so we should expect the more of these people in high positions.
I also suggested that we look at other institutions, not only TRA; you mentioned the judiciary..it is a fact that the three tribes are also dominant there...You suggested that they give us statistics of Regiopnal and District TRA offices, nobody will do that-why- the argument is biased, so biased that however much you try to show the other side of the argument with concrete facts those who argue against you side-step the issue and goes back to their original argument...Nakwambia ndugu yangu hapa pana mambo!
 
Kimsingi, kila mtu ana kabila lake. Lakini kwenye nchi ambayo tumekubaliana tuwe wajamaa (sijui kama bado tupo hivyo) wengi wa kabila moja wakiwa mahali pamoja (hasa hasa mahala pa kazi) tunauita ukabila. Look at Kenya's manpower set up accross the business, utaelewa.

Lakini pamoja na JK Nyerere kuelewa yote hayo (ambayo Mwanakijiji ame-quote) hakuachilia hapo, he went another step further. Alianzisha "Education quarter system" - ambayo kwa kifupi ni kwamba, kila mkoa utapata kiasi fulani za nafasi ya elimu ya sekondari ili angalau wakifika huko juu kuwe na mix ya makabila. That means say mkoa wa Mbeya hata kama wamefaulu watoto 1000 basi watatoa watoto say 100 tu, na mkoa wa Lindi say hatakama wamefaulu watoto 80 basi watatoa watoto 100.

The idea was very good, but the end results were very bad. Eventually the simplified equation remained with mostly wachaga, wahaya and wanyakyusa at the higher learning institutions. Because, were kin on education and able to pay school fees even on private schools.

The bottom line today are the ones you find in TRA, BoT, Ikulu n.k.
 
DR Who,

Nashukuru kwa jinsi unavyoshindwa kuelewa kisha baada ya muda mfupi unaelewa HARAKA. Ukiangalia aina ya maandishi ni kuwa mwishoni kuna kicheko, pili ukizungumzia "wazaramo" kwa sense ya utani ni wale typical waswahili wa Manerumango etc.

Nashukuru umeelewa lakini

FD
 
@PHILEMON MICHAEL

Salama Mheshimiwa?

anyway,swali niliamua kukuliza wewe baada ya kutoa statement ifuatayo:

kuhusu NSSF naona hakuna tofauti kati ya dau na mkullo au mattaka...tena sanasana DAU bado hajafanya vivid investment kulinganisha na enzi ya kina mkullo au mattaka [hata mkimsema ..jamaa ni kichwa ]....ila aendelee kujitahidi ..na nafikiri ni mtu anayetumia sana propaganda chini chini..natambua ni PAN AFRICA mzuri na mtoto wa mjini ,,,but we want more results...QUOTE]
Kutokana na umuhimu wa mjadala na points zako niliona bora nikuulize maswali haya maana tusije tukawa tuna zungumza bila ya kuwa na data za kutosha kusupport arguments kwani NSSF ni shirika letu wote na pale tunaposmell something fishy basi inabidi ti GANG up kuondoa au kuweka mambo sawa

mswali yangu yalikuwa ni:

Labda ninge jaribu ku-repost maswali yangu ya awali ili tuende na DATA pamoja na facts:

swali kwa Philemon Michael lilikuwa ni:

Dr DAU aliingia NSSF lini?

Alikuta makusanyo pale NSSF chini ya MKULO yalikuwa kiasi gani?

Sasa hivi yako kiasi gani?

Je Kulikuwa na investments za kiasi gani?

Sasa hivi investments zimefikia kiasi gani?

Kulikuwa na staff wangapi? na sasa wamebaki wa ngapi?

Performance yao ikoje?

Je wanachama nao wanasemaje kuhusu kupata mafao yao?

Na ni Propaganda zipi anazitumia kuendesha shirika kubwa la wanachi la NSSF?

Na imekuwaje ameweza kusurvive pale muda wote huo tangu MKAPA amuweke pale?

Na ikiwa unaweza kuniconvince katika hayo then nitakuwa mtu wa kwanza kuanzisha "MWANAKIJIJI STYLE" kampeni zakumuondoa pale NSSF
 
DR Who,

Nashukuru kwa jinsi unavyoshindwa kuelewa kisha baada ya muda mfupi unaelewa HARAKA. Ukiangalia aina ya maandishi ni kuwa mwishoni kuna kicheko, pili ukizungumzia "wazaramo" kwa sense ya utani ni wale typical waswahili wa Manerumango etc.

Nashukuru umeelewa lakini

FD

basi haina tatizo ukitaja jiko sema tuuu tutakufikiria (unataka aliyechezwa au la?)
 
Mzee MJJ,
You have posed very important questions and so far no one has come up with a sound response apart from confining themselves to their Utopian way of thinking..sadly, its now been considered that anybody who argues against this issue is a member of one of those tribes. Am sure that if we allow ourselves to look at this issue objectively we will come up with a plausible proposal that you are seeking.
The historical facts are undeniable; and the fact that that history has much influence in the present state of affairs cannot be denied either. It is also true that these same tribes are still in the forefront in education, in and outside the country. I even suggested that we look at the statistics at our universities- which will show us how things are moving from the colonial times to-date..it is a fact that the trend is the same, and so we should expect the more of these people in high positions.
I also suggested that we look at other institutions, not only TRA; you mentioned the judiciary..it is a fact that the three tribes are also dominant there...You suggested that they give us statistics of Regiopnal and District TRA offices, nobody will do that-why- the argument is biased, so biased that however much you try to show the other side of the argument with concrete facts those who argue against you side-step the issue and goes back to their original argument...Nakwambia ndugu yangu hapa pana mambo!

@Mwendapole

Its undeniable fact that we do have tribalism in Tanzania just like other African countries even though publicly we are in denial but deep down we know it is alive and many people are missing out due to this phenomenon that i call NATIONAL PSYCHOSIS which was and is still eating ating deep into the fabric of Tanzanian community.

Mwendapole if you look up the meaning of the word psychosis, it is explained as a severe mental derangement that results in the impairment or loss of contact with reality.In other words WE ARE IN DENIAL and if that definition is anything to go by, then we certainly have an arduous task to execute.

Even among the whites they have their own differences. The English feels he is superior to the Welsh, Irish, or Scottish. It is a chain-like sort of thing. I could go on and on. But JF will agree with me that the difference between what pertains in Africa and that in the West is the fact that the Westerners have not allowed this dichotomy to becloud their sense of judgement. When it comes to issues of national importance, they all attend to it with unparalleled unanimity. iN THEORY that is the spirit we want in Tanzania- unity in diversity but in PRACTICAL this is impossible since the same people who advocate UNITY are the tribalists rulling class and we dare not talk about it

In addition tothe above repercussions, we can also cite what I will call institutional tribalism. We have often complained about the issue of square pegs in round holes. Tribalism can partly be blamed for this. For example there is always the tendency to feel that once the Managing Director is a NYAKYUSA (for example), he must give me the job even though it is obvious Mohammed Hassan from PEMBA is more qualified than I am. This phenomenon does not auger well for the development of our nation.

The sooner we admit we have a problem then we might as well talk about how we can solve it and not living in DENIAL
 
Mzee MJJ,
You have posed very important questions and so far no one has come up with a sound response apart from confining themselves to their Utopian way of thinking..sadly, its now been considered that anybody who argues against this issue is a member of one of those tribes. Am sure that if we allow ourselves to look at this issue objectively we will come up with a plausible proposal that you are seeking.
The historical facts are undeniable; and the fact that that history has much influence in the present state of affairs cannot be denied either. It is also true that these same tribes are still in the forefront in education, in and outside the country. I even suggested that we look at the statistics at our universities- which will show us how things are moving from the colonial times to-date..it is a fact that the trend is the same, and so we should expect the more of these people in high positions.
I also suggested that we look at other institutions, not only TRA; you mentioned the judiciary..it is a fact that the three tribes are also dominant there...You suggested that they give us statistics of Regiopnal and District TRA offices, nobody will do that-why- the argument is biased, so biased that however much you try to show the other side of the argument with concrete facts those who argue against you side-step the issue and goes back to their original argument...Nakwambia ndugu yangu hapa pana mambo!

Mwendapole, waheshimiwa wapinga ukabila, wanata tuone ukabila, na tusipoona ukabila wanatuita sisi wakabila!!!
 
MKJJ

So somehow you think you know me? pole... I'm not one of the three tribes.. jina langu laweza kuwachanganya wengi...(ni historia ndefu)... and I'm not the subject na sijawahi kuajiriwa Tanzania au kushika kitengo chochote!

Aisifiaye mvua imemnyea

Hata kule Afrika ya Kusini wakati wa kupigania uhuru walikuwa wanasema hakuna ubaguzi wa rangi, lakini waliokuwa wanapata shida ni watu weusi. Zimbabwe walikuwa hawawaruhusu waafrika kupita First Street ni kwa wazungu tu. Utakuta sehemu zimegawanywa kwa waafrika na wazungu na walikuwa wanasema hawa waafrika ni wavivu hawataki maendeleo na ndio hivyo hivyo wengi ambao sio ndugu wa wakubwa kwenye mashirika wanaajiri watu kutoka kwao na ndio hivyo hivyo barabara kila uchwao zinajengwa kwa Basil Mramba na Msuya area; huu sio ukabila bali ni historia. GIVE ME A BREAK!
 
Back
Top Bottom