Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

MKJJ
Mnaouzungumzia ni ukabila upi? Je ni ajira ya watu wa kabila moja zaidi? Kama ni hilo nileteeni basi idadi kuna wachagga wangapi TRA ukilinganisha na makabila mengine?

Mbona wewe unapoulizwa kuwahoji viongozi wa juu wa TRA kuhusu ukabila unagoma? Lakini mengine yote unafanya na hili liko katika profession yako. unaogopa kuwauliza maswali magumu? Iwaje leo unakataa kufanya hivyo na wakati wote unaomba wanabodi hata kukusaidia na maswali gani ya kuuliza?

Kama ni suala la uwezo, nilinganishie basi wachagga waliopo hapo na watu wa makabila mengine waliopo hapo!

Tumesema mfano moja ni James Mbatia ambaye aliajiriwa pale na cheti cha Form VI, je ni mazingira yapi yalitumika kumwajiri mtu aliyechukua Engineering as a proffesion na cheti cha form VI?

Sawa, lakini ukabila una athari zake siyo tu ajira bali pia kimahusiano na uchumi. Kama kuna njama ya kuajiri wachagga peke yao bila ya shaka kuna watu wananufaika!

Kwa nini watu wasinufaike na viongozi wakuu wa pale ndio waliobobea katika kufanya michango (harambee) ya Kilimanjaro forum chini ya Msuya kama mwenyekiti wake.

THE Tanzania Revenue Authority (TRA) is fighting corruption among its staff by among other things, ensuring that before they are fully employed declaration of their personal assets is an imperative requirement and then they undergo a probation period of one year. However, it is possible some undeserving people manage to go through........................................................

Hii ni issue ya corruption sasa kama tafsiri yako ya ukabila ndio hiyo ni sawa tu. Lakini kama unataka kuongelea corruption ni vema ufungue thread nyingine kuhusu hilo.

Hili suala la TRA linahusu pesa na wachagga, hakuna cha ukabila wala nini? Kama ni ndugu kupeana ajira au watu wanaojuana kwanini tuishie TRA peke yake, na kwanini tuanzie TRA peke yake? Je Bosi Mchagga akimuajiri kijana aliyehitimu na mfanisi ambaye ni mchagga lakini hajuani naye ni baya zaidi kuliko bosi mchagga atakayemuajiri Mkwere anayejuana naye na ambaye hana qualifications? Wateteao ukabila watapiga kelele hilo la kwanza, lakini hilo la pili hawataki hata kuliangalia! kwani kwao Mchagga hawezi kumuajiri Mchagga mwenzake mahali pa taasisi za umma! akifanya hivyo ni Ukabila!!

Hatukusema tunaishia TRA pekee angalia kichwa cha habari.

jokakuu

Kichuguu: Hapana, najua kuwa wakati Chuo Kikuu Dar kinafungwa na Mwinyi mwaka 1989 hivi nilikuwa bado nafundisha pale. James Mbatia aliyekuwa kiongozi wa mgomo ule hakuwa mwanafunzi wa engineering ingawa alikuwa na wasaidizi kadhaa kutoka engineering kama vile Blasio Loloma ambaye sijui yuko wapi. Baada ya kufukuzwa chuo ndipo Mbatia alipoingia kwenye siasa dhidi ya serikali ya mwinyi iliyomkatisha masomo. Sidhani kama aliwahi tena kurudi chuo chochote kusoma engineering kwani najua kuwa muda wote amekuwa mbunge.

Nani anasema ukweli kuhusu alichokuwa anasoma james Mbatia pale Mlimani? Nafikiria wewe ndio husemi ukweli hapa kwa sababu ya agenda yako ya kutetea ukabila.
 
63 pages and counting discussing UKABILA?

kweli "nyuki hafumbatwi"
 
DUA,
On page 60 nimejibu swali lako kuhusu James Mbatia. Naomba nisijirudie hapa, lakini kwa kifupi ni hivi:
1.James Mbatia alifukuzwa UDSM akiwa mwaka wa 3 Faculty of Engineering.
2.Mwaka 1995 - 2000 James Mbatia alikuwa mbunge wa vunjo.
3.TRA ilianza kazi rasmi mwaka 1996 kwa hiyo siyo rahisi James Mbatia awe ameajiriwa pale.
 
Kwa maslahi ya taifa letu naomba admin aifunge hii topic. Uhanithi huu, kuna issue kibao humu ndani waungwana wanabishana ukabila.
 
jokakuu

Hilo swali hukulijibu au linatofautiana na maelezo yako. Kichuguu alikuwa anafundisha mlimani ukisoma maelezo yake ni tofauti kabisa na ya kwako i.e. Hakuwa anachukua Engineering. Sasa unasema habari mpya tena kwamba James hakufanya kazi pale TRA, je kwa nini hukusema ukweli huu tangu mwanzo? Kwa sababu ulionyesha kumtetea na kufahamu yaliyo jikoni. Una maana yote unayoandika tusiyaamini?
 
Dua,
sikumbuki kutamka popote pale katika forum hii kwamba James Mbatia aliajiriwa TRA. Kuna uwezekano umechanga michango yangu na ya mtu mwingine. Maelezo yangu ktk pg 60 ndiyo msimamo wangu kuhusu suala hili.

Hili la James Mbatia nina uhakika na source yangu. Nafahamu Kichuguu ni mchangiaji mwenye heshima zake ktk forum hii, lakini nadhani ktk kipengele hiki "ameteleza." Kichuguu hakueleza Mbatia alikuwa akisomea nini pale Mlimani. Kwani Kichuguu alikuwa akifundisha kitivo cha uhandisi?

Sina maelezo zaidi kuhusu suala hili zaidi ya hicho nilichoandika. Katika mazingira kama haya, ya wachangiaji wawili kutofautiana, nadhani ukweli utapatikana nje ya forum hii.

NB:Labda iko siku Mwanakijiji, au Butiama, atafanya mahojiano na James Mbatia na atamuuliza historia ya maisha yake.
 
Mkandara.

hawa ndio watendaji wanaopitisha documents zote na kufanya assessment za kodi.
akina chijoriga wao ni policy makers tu, hawawezi kuona document ya MENGI Reginald wala Ndesamburo watendaji ndio hao ma RRO ambao sasa wanaitwa managers, HDO NA Officers incharge ndio wahusika. .....

Mmmmhhh!

In reading between the lines, Mswahili is focused not on ajira per se but something else? Nilifikiri Mswahili angeanza kuona kuwa wakubwa wengi mno wa kabila fulani, badala yake anaangalia wa chini. Wakubwa ndo wanawasimamia wadogo, na hao k=ndo wenye power. Sasa unapoamua kuwaona wadogo kwa sababu tu ni wa kabila fulani ....

Au kuna kitu gani kinachovutia zaidi katika hizo documents za kodi? hilo nawaachia wanamtandao!

Nafikiri inawezekana kabisa ajira hiyo iko skewed kufuatana na wingi (au uchache) wa wasomi wa makabila yaliyopo. Kwa mfano sitegemei kwamba Wandengereko watakuwa wengi kwenye ajira kuliko Wakwere, nasema hivyo kwa maana njema tu.

Its unfortunate, lakini cha maana ni hao wanaozitaka hizo ajira kujifunga vibwebwe na kuzitafuta kwa juhudi. Nchi ni yetu sote na kila mtu ana haki sawa kufuatana na juhudi yake halali. Hata hivyo ni makosa kumwacha mwenye sifa, hata kama anatoka kule walikosoma zaidi, ili kumpendelea asiye na sifa kwa kutumia vigezo vya ukabila, udini nk.

MKIMBIZE ALIYE MBELE ILI UMPITE, USITAKE ASIMAMISHWE ALIYE MBELE ILI UMKUTE KWA KISINGIZIO CHA USAWA.

Narudia tena: Kama hakuna level playing field katika ajira hizo, hilo latakiwa kusemwa!!
 
wale wanaosema kuwa ajira TRA imetokana na ukabila, hebu watueleze ni utaratibu gani uliopo TRA wa kuajiri watu ambao una mwanya wa ukabila. Hivi mtu akitaka kuajiriwa TRA katika kitendo au idara yoyote anapitia hatua gani, hatua ambazo utekelezaji wake umesababisha ukabila? Tukielewa taratibu hizo basi tunaweza kutafuta suluhisho la jinsi gani tunaweza kupunguza idadi ya wachagga ngazi za chini huko TRA na hivyo kuondoa ukabila wa idadi ya watu wa kabila moja.
 
MKJJ kwa kupinga hoja ya wingi wa kabila moja katika kitengo fulani kama kigezo cha Ukabila unakusudia kwamba: Kuwapendelea watu kwa makabila yao au dini zao au eneo wanalotoka au …. yote yana maana sawa?

Maana nakumbuka Iliwahi kuundwa tume ya kuchunguza tatizo la Udini katika chuo cha Diplomasia kutokana na kuwa na idadi kubwa ya Waislam ngazi za juu.

Huko nyuma Mh Fares Kabuye aliwahi kulilalamikia Bunge kwamba kuna tatizo watu wa Tanga kupendeleana na kujazana katika Shirika la Bima.

Imewahi kuundwa tume ya kuchunguza tatizo la ukabila pale Baraza la Mitihani wakati wa uongozi wa katibu Mtendaji aliyepita.

Mwanasiasa ametaja Mkuu wa Kituo cha Kompyuta UDSM (UCC) kuwapendelea watu wa kabila lake na kuwanyima nafasi vijana wengine wa Kitanzania wenye uwezo

Yupo Bwana mmoja aliyepata kuwa waziri katika awamu ya pili na tatu. Mtu toka mkoani kwake akifika ofisini kwake, Mheshimiwa huyo alikuwa kwanza anamsemesha kwa lugha ya kabila lake, akigunduwa kuwa hajui lugha yake (kwani kuna makabila kadhaa), anajuwa sio “mwenzake” na hapo hakuna nafasi ya kusaidiwa. Mifano ni mingi.

Kwa tafsiri yako, wote hawa walichokuwa wanafanya ni – UNDUGUNIZATION?

Kama ndivyo, basi tofauti ya maneno hayo ipo wapi?

Kuyakabili na kuyajadili masuala tata ni hatuwa muhimu katika kujenga misingi ya jamii imara na isiyoyumba.
 
Nungunungu, kama mtu mmoja anaamua kupendelea watu wa kabila lake hatuwezi kusema kitengo kizima kinafanya hivyo! Kama mtu huyo yupo na ikathibitika amefanya hivyo hana budi kufukuzwa kazi! Katika mifano uliyotoa baada ya uchunguzi wa tume hizo ni mahali wapi palipothibitika kuwa kuna ukabila au udini? Kuunda tume kuchunguza kitu fulani haina maana kitu hicho kipo. Nimeweka ripoti iliyochunguza TRA na URA na mojawapo ya lililochunguzwa ni patronage na ukabila, URA walionekana kulalamikia Ukabila lakini TRA hawakuliona hilo ingawa waliona mapungufu mengine! Haitoshi tu kusema kuna kitu fulani kwenye kitengo fulani ati kwa sababu mtu mmoja amefanya jambo fulani! this is what is called haste generalization...
 
NUNGUNUNGU.

Karibu sana jamvini.

nakubaliana na wewe asilimia 100 na nakubaliana na Mwanasiasa kwa kutuambia ukabila wa chuo kikuu huko nako nitakwenda deep kuona wachagga na wahaya walivyokuwa wakicheza fouls kali sana. Mwanasiasa hapo UDSM ndio wakaja akina Baisi NA phd feki na kutetewa na wahaya wenzake kuwa baisi hajakidanganya chuo kwa kupeleka phd feki ila Baisi ndiye kadanganya na chuo kwa kupewa cheti feki.

Mwanakijiji

anayoyasema Nungunungu ni sahihi kabisa inawezekana ukawa na person interest kuitetea TRA lakini ukabila upo na watu wanaumia nao sana.

mimi napata Private message nyingi tu na za vitishi kwa watu wanaounga mkono Ukabila TRA. naambiwa sina maana Mswahili tu. na mengine siwezi kuayaweka hapa.
ila nakuuliza Mwanakijiji WAziri mkuu mstaafu Sumaye aliunda bodi ya parole iliyokuwa inatakiwa kwa nature ya kazi yake kuwa na watu wa dini za aina mbalimbali lakini kwa vile Mheshimiwa Sumaye aliweka udini (ukristu)mbele aliweka watu wote wakristu.kutokana na kelele za wananchi Mkapa akaivunja bodi hiyo kwa kusema ilikuwa na misingi ya udini na dini moja tu imewakilishwa. kama Sumaye hakuona aibu wala haya kukuumbatia udini vipi Kitillya atashindwa?
naomba pia ukanushe maneno ya Mwanasiasa kuwa chuo kikuu kitengo cha Computer hakuna ukabila ila ni undugu tu?

Wanabodi.

Nilijaribu kukaa pembeni na kuona upepo unavyokwenda. lakini wamekuja kina mikael na uongo kibao nitapangua na kumsuta kila nukta kama nilivyofanya huko nyuma mara aseme KDF NI TIC mara alete uongo ana majina 1000 analeta 40 nikamchambulia yote.

PM nakusiliza njoo na ukweli acha kuongopa mtu mzima wewe.

mimi nipo na nitaendelea kuwepo kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu na hapa haogopwi mtu.jembe tutaita jembe na kijiko tutaita kijiko, hatuwezi kuita jembe ni kijiko au makengeza kuita ni chongo. ukabila tutaita ukabila na undugu tutaita undugu.
Aluta continua!
 
Phillimon Mikael.

naomba ukija uanze kujibu hoja za Bakaa. ULIOMBA utajiwe vituo na amekwambia kituo cha Tanga kuna wachagga zaidi ya asilimia 80. Horohoro na Holili ni ngome yenu.

swala lingine ilikuwaje kituo cha ushuru cha bandari ya Tanga kipelekwe jimboni kwa Mramba(Holili) huko hakuna bandari ila ni jimboni kwa waziri aliye na dhamana na TRA wakati huo(fedha).

Pia Bandari ya Mombasa ipo karibu sana na Tanga lakini Mramba akishirikiana na Wachagga wa TRA wakaona wivu na kuudhulumu mkoa wa Tanga na kukipeleka kituo hicho KIlimanjaro tena jimboni kwa Mramba kisa na mkasa ni kuupa nguvu ya kiuchumi Rombo. hata KIPIMO CHA T-SCAN kimepekwa jimboni kwa mramba Holili huo ndio ukabila ulivyo na athari mbaya.

leo hii mkoa wa Tanga umekufa kiuchumi na mmoja wa wauaji ni hawa wachagga wa TRA KWA kuwaondolea kipimo cha ushuru ambacho kilikuwa kinawapatia mapato wana Tanga, ni sawa na kumwambia mtu avae suti au nguo Tanga halafu viatu akavalie moshi halafu aje kazini TANGA.

kama kungekuwa na uwezekano hata Bandari ya Tanga wangeipeleka Moshi.

jamani Phillimon Mikael nyinyi huko mna mlima kilimanjaro bado tu hamtosheki?
mtu yeyote ajiulize mtu anapakua mzigo wake bandari ya Tanga lakini mzigo huo ausafirishe hadi jimboni kwa Mramba kwa ajili ya kupimwa halafu arudi nao Tanga au sehemu nyingine ya nchi. na hili jambo halijatokea kibahati mbaya.

mheshimiwa JK katika watu wanaoua maendeleo ya Tanga ni hao kina Mramba na watu wake wa TRA. Tunaomba T-SCAN ilirudishwe Tanga kwani ndio kwenye bandari kuwafumbia macho hawa wakabila wa kichagga iko siku Bandari ya bagamoyo NAYO ikianza tutaambiwa twende machame kupima mzigo na kuurudisha tena bagamoyo hiyo hata kiuchumi haipo.

Mwanakjj kama mkweli waonee huruma Tanga huko wewe si ulisoma? unaowatetea wanadhulumu hadi haki za mkoa uliokusomesha.

Phillimon.

naomba majina 1000 mbona umekaa nayo kimya tu?

Mkandara.

nakupongeza kuwapa somo hawa na kuongezea tu hawa wanajitia wamesoma wakati miaka ya 80s walikuwa busy kuuza vitenge vya zaire, vilemba vya burundi,kuzaa kanga za mombosa kimagendo, kukimbilia magereji. hawa si wasomi.

mwanakjj amekuwa akiona jina tu anaamini ni mchagga. hatufanyi utafiti kwa majina bali ushahidi halisi kuwa TRA kuna wachagga hao majaji watatu hatuna ushahidi kama wachagga ni jina tu

. TARIQ AZIZ aliyekuwa msaidizi wa Saddam Hussein kwa jina utasema ni muislam kumbe ni mkristu. nakusisitiza tena Mwanakjj jina si njia ya kujua mtu ni kabila gani.fanya utafiti usiwe mwepesi wa ku kopi na kupaste tu.ANNA MKAPA ni mmakonde? Salma salmin ni mzanzibar? acha hizo!
 
mswahili .ulianza vizuri kwenye hiyo post hapo juu lakini mwisho umeishia kwenye vijembe tena...maana nilijiweka kando kwa sababu ya lugha mbovu za kambi yako...tukubaliane kuheshimu hoja ndio tuendelee ,najua hilo hutakubali..
wewe umewekewa hapa hadi ripoti ya TRA unajifanya huoni...sasa angalia maajabu yako unataka uwekewe majina na hapo hapo una jicontradict kwa kusema majina ya majaji si lazima yawakilishe makabila yao...hayawezi kuwa indicative?...
kama tutakubaliana kuheshimu facts itakuwa busara...wewe fact pekee uliyoleta ni majina kumi ,na ushee...na reference mliyoleta ya mmanda...
 
Tukubaliane tu kwamba Mswahili ameshindwa kuitetea hoja yake!
 
Mswahili sawa nasikia hoja yako na uko karibu kunishawishi. Nisaidie hata hivyo:

Je TRA ina wafanyakazi wangapi kiujumla
Kati ya hao Wachagga ni wangapi?
 
Sidhani kama ni kweli kwamba chombo kinachotakiwa kupima mizigo bandarini Tanga kimewekwa Rombo. Mtu ashushe mzigo bandarini Tanga, aubebe hadi Rombo kuupima, kisha ndio aurudishe Tanga? Naamini haiwezi kuwa kweli.

Kuna bidhaa nyingi zinaingia nchini kupitia Holili. Kwa hivyo, inabidi kuwepo vifanyia kazi Holili. Lakini siamini kwamba hilo linafanya mizigo ya Tanga ikapimwe Rombo. Kama mizigo inayoshushwa bandarini Tanga ingebidika kupimwa mahali pengine, basi ingepimiwa Dar.

Nakupongeza Mzee wa Kijiji kwa kutumia LOGIC. Your counterparts are not doing the same. The law of evidence requires Mswahili and his cohorts to produce evidence that there is tribalism at TRA, and that this tribalism is perpetrated by the Wachagga. Instead of doing that, they have merely used the following illogical argument: there are many Wachagga at TRA, and therefore there is Chagga Tribalism at TRA. Well, non sequitur (it does not follow). As has been pointed out by Mzee wa Kijiji and others, you also have many Wachagga in faculty positions at UDSM, MUCHS, Sokoine, and so on. Are Mswahili and co. claiming Chagga Tribalism in all these places? Note also that we have very many Wachagga in the City of Dar, in Mwanza and in Arusha. Is this state of affairs due to tribalism?

I can see a certain amount of unholy jealousy in some of the arguments presented. Mswahili expresses outright hatred of the claim that the Wachagga are relatively better educated. It is the truth, and the truth does seem to hurt some people. We should emulate rather than hate the Wachagga in their education endeavor.

Augustine Moshi
 
Hayo majina 100 yako wapi?


Mbona Jeshini mko kimya? au wizara ya Mipango?
 
Kuna vitu tutakuwa tunavikosea sana iwapo tutaamua kuwa na msimamo kabla ya kusikiliza hoja.

Tuiangalia mada hii kwa uzito wa hoja na upana wa mantiki [LOGIC]

Si rahisi kuthibitisha udini/ukabila au upendeleo wa aina yeyote kwa takwimu ingawa katika baadhi ya nyakati huwa inawezekana.

Mfano kwa muda mrefu nadhani tangu uhuru waislamu wamekuwa wakipiga kelele kuwa kuna upendeleo unafanywa na wakristo dhidi yao. Nyerere aliwahi kukiri mara baada ya uhuru kuwa nafasi za waislamu kielimu na kwenye madaraka ni finyu na atafanya awezalo kubadilisha. Kauli hizi zimefifilishwa sana [REJEA Said, Mohamed. The Life and times of Abdulawahid Sykes: Untold Story of Muslims Struggle in Tanganyika's Independence.]

Lakini hata watawale waliofuatia wamekuwa wakifumbia macho badala yake kuanza kuwalaumu waislamu kwa kuchochea vurugu.

Waislamu mara kwa mara wamekuwa wakitoa majina ya wafanyakazi wa mashirika mbali mbali na kuainisha idadi ya waislamu na wakristo kuwa haiwiani na takwimu za mgawanyo wa waislamu na wakristo nchi nzima.

Ukiangalia perception effects za kuwa na waislamu wengi ni kuwa nchi imekuwa ikiendeshwa kana kwamba ni taifa la kikristo watu hawaoni tabu wanapoenda mabenki na mashirika mengine na kukuta christmass trees na nyimbo za bwana kwa wingi. Hii ndio Perception effect wanayofeel waislamu.

Mkapa aliwahi kukiri kuwa bodi ya Parole ina walakini kwa vile ina wakristo wengi kuliko waislamu.

Sasa nimetumia mifano ya waislamu hapo kuelezea namna nionavyo kwamba kuna tatizo katika kuangalia issue hii ya uchagga, unachohitaji ni kuangalia perception ya watu ilivyo, iwapo kuna mchagga mmoja yupo juu na kisha kila anaemuajiri katika senior position ni mchagga hapa pana tatizo, mwanakijiji nakukubalia kwanza hatuna budi kumuondoa huyo wa juu then kuangalia namna ya kusafisha.

Kusafisha sio kutoajiri wachaga au kuwaondoa waliopo bali ni kuhakikisha kunakuwa na muafaka na mgawanyiko sawia. Haiingi akilini iwapo waziri mmoja analaumiwa kwa uchagga na kila aendako kwenye threshold zake wanaoingia ni wachagga hapa kuna walakini.

Ukabila ni tatizo kwa hakika katika baadhi ya idara, sio wachagga peke yao manake kama wasemavyo jeshini kuna kabila limedominate. Imekuwa tendency ya baadhi ya watu wakiona 'mtu wao' yupo pale basi hawatafuti kazi kwingine...

Lakini hii haipunguzi uzito wa mjadala hapa, for some reasona muanzilishi wa mada hii kaamua kupick wachagga, ni kweli uchagga umestawi kwa wingi tu katika baadhi ya idara, mswahili ana point. to criticise him is to hide our head in the sand.

It must be sorted.
 
Back
Top Bottom