Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Jamberi, naona hujaelewa mada hii, kinachozungumzwa ni ukabila na si ubaguzi kiujumla. Kama huyo jamaa aliajiriwa na ndugu yake basi unathibisha pointi zangu kuwa tatizo letu kubwa katika mahala pa kazi ni undugu, ila kama jamaa aliajiriwa kwa sababu ya ukabila wake (kwa vile ndugu yake ni kabila lake - which make sense) basi unathibisha hoja za kina Dua na wenzake.
 
Pia sioni tofauti kati ya ndugu moja na kabila moja
UNDUGU NA UKABILA KITU ILE ILE, huwezi kuwa ndugu yangu wakati hatujachangiaukabila!!!
 
Huu mjadala utaenda sana bila makubaliano ya tatizo na hivyo basi kutoenda hatua ya pili kupendekeza suluhisho.

Kwa michango iliyotolewa hapa, nakubaliana na Mwanakijiji kuwa tatizo 'general' ni kujuana, kupendeleana au pia limeitwa undugunization. Nionavyo mimi, kujuana/kupendeleana huku kukiwa ni at random, bila factor fulani kutawala zaidi as sababu ya kujuana huko,.. basi kunabakia tu generally kuwa ni kujuana/kupendeleana .. full stop. Lakini inapotokea kuwa katika taasisi fulani kujuana/kupendeleana huku sababu yake imeelemea zaidi katika misingi ya dini, kwa wahusika kuwa wa dini moja, hapo tutasema pana UDINI. Vivyo hivyo basi, inapotokea katika taasisi fulani kujuana/kupendeleana huku kumetokana na wahusika kuwa ni wa kabila moja (kujuana/kupendeleana kwao kumetokana na kuwa wao ni kabila moja) .. basi bila shaka hapo tutasema pana UKABILA. It looks like this is the case for TRA.
 
Kulikoni, ili kuweza kutranspose hoja yako kwenda TRA inabidi utuoneshe hiyo pattern ya ukabila TRA.

Je, TRA kuna wafanyakazi wangapi?
Wangapi ni Wachagga?
Wangapi ni wa makabila mengine?
Je uwiano wa kuajiriwa na kuachishwa kazi kati ya wachagga na wasio wachagga ukoje?
 
Duuuh basi tanzania tuna ubaguzi wa rangi maanake ukitazama hesabu ya weusi ukalinganisha na rangi nyinginezo hakuna kabisa uuwiano!... Kulingana na tafsiri hii ya Mzee Mwanakijiji inaonyesha wazi kuwa TZ ni wabaguzi wa rangi.
 
daymn.. Mkandara wakati mwingine unaniacha hoi kweli.. yaani sijui nivunje vunje vipi hoja ili ziwe rahisi kueleweka. Huwezi kusema mahali kuna ubaguzi bila kuonesha mtiririko wa vitendo na tabia za kibaguzi. Ukabila si idadi!!
 
true Ukabila sio idadi sasa hii pattern ya TRA imetoka wapi?

Je, TRA kuna wafanyakazi wangapi?
Wangapi ni Wachagga?
Wangapi ni wa makabila mengine?
Je uwiano wa kuajiriwa na kuachishwa kazi kati ya wachagga na wasio wachagga ukoje?
 
Pattern gani hiyo...? wale wanaosema kuna ukabila wanaweza kuthibitishia kwa kujibu maswali hayo.. na hivyo itaanza kuonesha mtiririko wa tabia za kikabila..!
 
Mzee Mwanakijiji, Mbona unakimbia hoja?..
Umesema mwenyewe kumwambia Kulikoni kuwa ni lazima kuwepo na mtililiko wa tabia za Ukabila na ukayaorodhesha maswali yenye pattern za Ukabila TRA!.
Ukitazama hayo maswali yanajibu zaidi Idadi ya watu kwa makabila na si mtililiko wa vitendo vya Ukabila. Unajichanganya mwenyewe!
Tumesema toka mwanzo moja ya mtililiko wa Ukabila ni pale ajira inapotolewa kwa kigezo cha Ukabila!. Mifano yote ya kisayansi kakupeni Mswahili isipokuwa haijaweza kujibu hoja yetu kwa sababu mnachotaka ni hesabu na idadi ya watu.
 
Mkandara, watu kumi kwenye kampuni ya watu 3000 wakifanya vitendo vya kibaguzi huwezi kuita taasisi nzima ni wabaguzi! lazima tuangalie uwiano. Kwa vile hoja kubwa ya hapa ni kuwa TRA kuna wachagga wengi ndio maana kuna ukabila ndio maana najaribu kuliweka jambo hili kwenye maudhui yake. Mtu mmoja anaweza kuwa mkabila, lakini kusema taasisi nzima ina ukabila ni dai lisilo na msingi! Ili kuonesha taasisi nzima ina ukabila basi hatuna budi kuangalia picha nzima na siyo sehemu ya picha hiyo tu!
 
Mzee Mwanakijiji,

Unaendelea kutumia hesabu zako.
Mwajiri mmoja anayetumia kigezo cha kutoa ajira kwa Ukabila ni kosa kwa Taasisi nzima. Inachukua mtu mmoja tu ktk nafasi muhimu kuweza kutoa picha ya Taasisi nzima.
Kitendo cha kuvunja sheria kilichofanywa na CCM hakina watu wengi isipokuwa vitendo hivyo vinajenga image mbovu ya chama na hata nchi nzima.
Sii wana CCM wote walioshhiriki katika mauaji ya Pemba na wala sii CCM wote wanaounga mkono kitendo hicho ambacho kimeidhinishwa na watu wachache sana. Walioshiriki ni wachache na hata kesi zenye mfano wa Ditto sio nyingi. Yet, kila mmoja wetu anakubali kwamba kuna tatizo kubwa ktk katiba yetu na sheria ya nchi.
 
Mzee Mwanakijiji

Huo mfano sioni kama kweli unalingana na tunaloongelea hapa. Hao watu kumi ni wale wanaoajiri au vipi?

Nilikupa mfano kwenye post iliyopita kuhusu conservative party kuwa racist
Labour's Shahid Malik, for example, said the remarks showed the Tories remained the "nasty party". "It doesn't matter what they tell you, they still are the nasty, racist, sexist, homophobic party they have been for many, many, many years," he said.

Mr Cameron would undoubtedly reject that image of his party, but he knows it has occasionally been the public perception. That is precisely why he has been expending so much of his energy on changing the party in a fundamental way to make it more inclusive, diverse and tolerant.

Tukirudi kwenye mada yetu hao watu kumi kama ni waajiri na wanaajiri kwa kufuata ukabila, ni sawa kabisa TRA yote ina ukabila kwa sababu wanaoajiri ndio wenye nyenzo za kufanya hivyo na sio kila mfanyakazi.
 
Mkandara, tuhuma za ukabila si tuhuma ndogo. Hatari yake ni chuki juu ya kundi zima la watu na mahali pengine imefikia hata kusasabisha mauaji ya halaiki kwa makosa ya watu wachache. Kudai mtu ana ukabila si sawa na kudai mtu ni mwizi. Mtu mmoja kwenye taasisi akiibia haiwezekani hata chembe kuitangaza taasisi hiyo kuwa imejaa "wezi".

Kama mtu mmoja amedaiwa kufanya kitendo cha kikabila haifai na haistahili hata chembe kuitangaza taasisi nzima kuwa imejaa ukabila au ina ukabila. Hatari yake ni kuwa mtu akienda TRA kuomba kazi na akakutana na Bw. Tarimo, au Bi. Mushi wazo la kwanza ni "wachagga hawa hawataniajiri" hata kama Bw. Tarimo na Bi. Mushi hawana hata chembe ya ukabila!! Sasa ikatokea mtu huyo akanyimwa nafasi hiyo basi atatoka hapo na kutangaza hadharani "nilijua hawataniajiri kwa vile mimi si mchagga"!!

Mnaotetea ukabila huu wa jumla wa kuhusishwa (tribalism by association) mnataka watu wawashuku Wachagga na wawazie vibaya. Siku moja (Mungu aepushie mbali.. puu!) kuna mtu kwa haki atanyimwa kazi na Mchagga mahali popote pale na ataenda kuchukua silaha na kurudi na kuamua "kufanya" kweli kwa hawa wachagga maana "wamezidi"!

Mifano yako ni mizuri lakini ukiichukuwa kwa upana wake ni ya hatari. Ninachosema ni kuwa endapo mtu anatuhumiwa kuwa na ukabila, ni mtu huyo ambaye anastahili kuchunguzwa na kuchukuliwa hatua badala ya kuihamisha hatia ya mtu huyo na kuiweka kwenye kundi zima!

Sasa, endapo itaoneshwa pasipo chembe ya shaka kuwa uovu huu wa ukabila unafanywa na jumuiya nzima na siyo mtu mmoja mmoja (na si vigumu kuonesha hilo kama lipo) basi kuvunja jumuiya hiyo ni lazima kama ilivyotokea kwenye hoja ya bodi ya parole. Lakini kuwa na watu wa imani moja au kabila moja peke yake haitoshi kuwafanya wawe wadini au wakabila.

Narudia tena, mnaotetea uwepo wa ukabila wa wachagga TRA angalieni sana hoja zenu na madhumuni yenu kwani kikiungua kitarusha cheche hata kwa jirani!!
 
Kama unakubali hivyo ni jukumu la Serikali kufanya uchunguzi wa kina na ikibainika kweli wale wote wanaohusika wachukuliwe hatua. Tena inabidi wale wote wanaotuhumiwa kuachishwa kazi kwa muda ili madai haya yachunguzwe kwani kuwaachia waendelee na kazi ni kutaka kupindisha ukweli kama vile tunavyoona BOT wakati wanajaribu kuficha vielelezo muhimu kutokana na tuhuma za mamillioni ya pesa kupotea kule. Huwezi kufanya uchunguzi wakati wale wanaohofiwa kufanya madhambi hayo hawajasimamishwa kwa muda wakati wa uchunguzi huo.

Hatuwezi kuogopa kusema kwani ukweli ni lazima usemwe na kutibiwa sasa na sio kungoja kesho kwa sababu kesho haiwezi kuja. MFICHA MARADHI KIFO HUMFICHUA
 
Dua, tatizo ni kuwa mnaotetea uwepo wa ukabila hamuhitaji uchunguzi kwani mmeshaamua kuwa upo!
 
Dua, tatizo ni kuwa mnaotetea uwepo wa ukabila hamuhitaji uchunguzi kwani mmeshaamua kuwa upo!

MK ndugu yangu, sasa mmeshabishana vya kutosha naomba kama unaweza achana na hii topic sababu sasa unatuletea hata madhara sisi wa hilo kabila. Naona vijana wa mzee wanataka kukukomoa na kwa wewe kuwa mstari wa mbele na hili uswahili unaleta - more than + kwetu sisi. Nadhani umenipata.

If U are for personal gain continue but overall U are becoming a big liability especially now that U have attracted powerful foes.
 
Dar-es salaam,

Maneno yako sawa kabisa. Unajua hata mimi naanza kumwekea mashaka sana Mwanakijiji na hata yote ambayo huandika. Niliwahi kuwa na hisia hizo mwanzo kisha akaweza kuzifuta baada ya kuona baadhi ya riwaya zake zilizofuatia, lakini sasa naona kama karudi kule alikotoka zamani.
Kibaya zaidi huongeza maneno ya kubomoa kabisa hoja. Sijui nani hapa kadai Ukabila wa JUMLA?.. TRA sio kampuni ya Wachagga wala inayowakilisha wachagga.
Nitapenda sana nione JK akiajiri zaidi waislaam na hapo Mzee Mwanakijiji tutapambana hadi kufa... Chenga za mpira wa chandimu tunaziweza vile vile.
Kama tungekuwa tukitazama ubaguzi kwa vigezo vya huyu jamaa nadhani hata South Afrika wasingekuwa na hatia hata kidogo kwani asilimia 80 ya wazungu nchini humo hawakupenda kilichokuwa kikifanyika. Tatizo kubwa walilokuwa nalo ni kuelewa maana ya Mwafrika anapodai Ubaguzi huo kwa kuwataja Makaburu.
Haya ndio matatizo ya tafsiri za Wakenya na Ujamaa, kwani waliamini Kenyatta alipo waambia kuwa Wajamaa hu-share hata mke!.. hapo tena kwa mwafrika huwezi kupata kura hata kidogo.
 
Back
Top Bottom