Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

nimesema ni mabosi wenye uwezo wa kujua chochote kinachoendelea TRA na wana majibu.. sasa makabila yao yanahusu nini.. mnaona hatari mliyoianzisha Dua, Mswahili, Mkandara et al.. sasa hata kuzungumza na mtu inabidi ujue kabila lake... !!
 
haya tunasubiri ndugu zetu wakubali mahojiano tujue mbivu na mbichi. nafikiri jembajemba hakuwa na maana mbaya ila tu ametaka kujua kama hao mabosi watakuwa nyutro kwenye mahojiano yao .
 
Kinyau,

sawa mzee nadhani umenipata haswaaa

MKJJ

wasiwasi wangu ni kuwa hao Maboss kweli watakuwa wakweli kwa hicho ambacho watakuja kukizungumza?????? na si vyenginevyo
 
Jembajemba... nimechukua data zote alizoziweka Mswahili hapa na kuzipitisha kwa HR uko TRA na kwa wakubwa wa bodi ya TRA.. kwa karibu wiki mbili sasa wamechambua kila jina lililotajwa na mswahili na kuelezea nani aliajiriwa vipi na kwa mazingira gani!! ukweli hatimaye utajulikana!!
 
MKJJ,

tuwasubiri kina mswahili wajibu ili tuweze kusikiliza hayo mahojiano tukate huu mzizi wa fitna
 
MKJJ

Je, TRA wanasema nini? Mabosi wawili wa TRA wamekubali kushiriki kwenye mdahalo nitakaouandaa kuhusu ukabila TRA tukipitia "data" za ndugu yetu "Mswahili" moja baada ya nyingine. Hata hivyo ili mjadala huu unoge nawaomba "Mswahili" na "Dua" na mtu mwingine yeyote kama Mkandara hivi washiriki upande wa wale wanaotetea uwepo wa ukabila. Kama mko tayari ili kukata kizabizabina hiki cha ukabila tupangesiku katika ya weekend hii ya tarehe 17 na ile ya tarehe 24 kufanya majadiliano hayo kwa njia ya simu. Msiwe na shaka mitambo yangu inaweza kuunganisha hadi watu 6 kwa wakati mmoja.
Naomba mkubali ombi langu.

M. M.
naomba muwashinikize wakubali.... ili tuweza kujua zipi pumba na upi mchele!
Dua, Mswahili, et al... naombeni majibu yenu...!

Mbona una wasi wasi, umetuma hii message hata siku haijaisha umeanza kubwata ohh shinikizo wakubali etc............................... ................what the hell do you think?
I am ready anytime anywhere nitumie majina ya hao maboss kwenye PM.. Other details zitafuata.
 
nimeshakutumia... naona mlikuwa mnachukua muda kusema "ndiyo au hapa" na nikijua mko tayari kushiriki basi mipango iendelee kwa haraka.. jambo hili linahitaji majibu thabiti. Nashukuru kwa kukubali kwako. Namsubiri mheshimiwa Mkandara na Mswahili.
 
Inafurahisha sana kuona mtu anaandika msg then anajijibu.

Kweli mnaendelea vizuri sana siku hizi. Karibuni sana.

FD
 
nimeshakutumia... naona mlikuwa mnachukua muda kusema "ndiyo au hapa" na nikijua mko tayari kushiriki basi mipango iendelee kwa haraka.. jambo hili linahitaji majibu thabiti. Nashukuru kwa kukubali kwako. Namsubiri mheshimiwa Mkandara na Mswahili.

Kwani tunaingia kwenye mtandao wakati mmoja? Lazima uelewe kila mtu ana kuja kwa mpango wake na jinsi mtu anavyosoma ndio anajibu. Nimejibu kama mimi binafsi na ni muda mfupi tu ndio nimeingia.
 
Mzee Mwanakijiji,

Nipo ndani ya Dar -es-Salaaama
Mji watu wa na aso mwana aeleke jiwe! nitafuatilia swala hili kwa undani zaidi nikiwa ndani... subirini majibu.

Wanabodi wa Dar nitafuteni napatikana mitaa ya K Tea shop, Chef Pride kwa saaana na Steers. Unjuua tena wapambe wa mjini. Jioni leo ktk chips vumbi ngoma nzito hiyo wala sii mchezo. Home sweet home!
Looh bwana wee hizi speed ya internet mwenyewe nimeshachoka!...
 
Mkandara hilo litakuwa vizuri sana... nipe contacts zako PM tuwasiliane ukiwa huko....
 
Kwani tunaingia kwenye mtandao wakati mmoja? Lazima uelewe kila mtu ana kuja kwa mpango wake na jinsi mtu anavyosoma ndio anajibu. Nimejibu kama mimi binafsi na ni muda mfupi tu ndio nimeingia.

Dua r u ok? you are taking things very serious.. siyo nzuri kwa afya... !!
 
Mheshimiwa Dua,
Hii hapa chini ni kauli ya Mbunge baada ya utetezi wa Waziri wa Fedha:

quote from Hansard:
MHE. STEPHEN M. KAHUMBI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninakiri
aliyosema Waziri wa Fedha kwamba, tumefanya kazi kwa muda mrefu vizuri sana na
hatuna matatizo na ndiyo maana nilikuwa nasitasita kuzungumza wakati wa hotuba yake
ya kwanza. Sasa kilichonistusha mimi ni ile barua kwa sababu nilichangia tarehe 29
tarehe 2 ikaandikwa barua na ukichukua na yale majibu aliyoyajibu Waziri wa Kazi,

nikapewa nakala. Kwanza, mimi sikuwepo kwenye kesi, angepewa nakala aliyehukumu,
Waziri wa Kazi kwamba, hatukuikubali. Lakini maelezo aliyoyatoa Mheshimiwa Waziri,
yameniridhisha. Mimi sikujua yalivyokuwa huko ndani.
Kwa hiyo, mimi namwomba
Waziri wa Fedha, tuendelee kama kawaida. (Makofi)

Nadhani majibu ya maswali yako yanapatikana ktk kauli hiyo ya Mbunge. Ikiwa huridhiki, na bado una dukuduku, nitakuwa tayari kukupa ufafanuzi zaidi.

Well, inasikitisha mwakilishi wa wananchi anapokurupa na kutoa madai bila kuyafanyia utafiti. Hii inapunguza sana heshima ya bunge letu.
 
Mzee Mwanakijiji,

Nipo ndani ya Dar -es-Salaaama
Mji watu wa na aso mwana aeleke jiwe! nitafuatilia swala hili kwa undani zaidi nikiwa ndani... subirini majibu.

Wanabodi wa Dar nitafuteni napatikana mitaa ya K Tea shop, Chef Pride kwa saaana na Steers. Unjuua tena wapambe wa mjini. Jioni leo ktk chips vumbi ngoma nzito hiyo wala sii mchezo. Home sweet home!
Looh bwana wee hizi speed ya internet mwenyewe nimeshachoka!...
Hongera Baada ya miaka mingapi umeingia mjini?Vijiwe vingi havina shamra shamra uliyoizoea na wengi uliwazoea hawapo tena.Fuatilia tupate ukweli.Salaam kwa wote wa kunyumba!
 
nimesema ni mabosi wenye uwezo wa kujua chochote kinachoendelea TRA na wana majibu.. sasa makabila yao yanahusu nini.. mnaona hatari mliyoianzisha Dua, Mswahili, Mkandara et al.. sasa hata kuzungumza na mtu inabidi ujue kabila lake... !!
MKJJ!
Kweli umeamua kwenda nalo sambamba hili swala,wasikilizaji wa KLH NEWS, Tunasubiri mkao wa kupokea habari na kuzichuja.Kila la kheri!
 
jokaKuu

Nilikuuliza maswali haya hukujibu ukaingia mitini sasa unakuja na kuanza kuruka ruka hovyo, subiri maboss wako tutawauliza maswali kwa kina.

Ukijibu haya hapa chini then tutaendelea, huwezi kukimbia swali kwa kuuliza swali. NAFAHAMU UTASEMA ULIKUWA HUKUYAONA.

http://www.jamboforums.com/showthread.php?p=24634#post24634

1.) Kwa hiyo unakubali kwamba swala hili lilizungumziwa bungeni kuhusu ukabila pale TRA. Je unaweza kufuta usemi wako kwangu, Mswahili na wengineo wa maneno yako haya:

Hii ni kampeni ya kuwachonganisha wachaga na makabila mengine ya Tanzania. Jamboforums imekuwa kama gazeti la kihutu kangura lilokuwa likihamisha chuki dhidi ya watutsi.
bwana mswahili,
CHUKI yako na wenyeji wa mkoa wa kilimanjaro
Dua,
shutuma unazozielekeza kwa wachaga hazina tofauti na makala za chuki gazeti kihutu, kanguru.

Hili swala ambalo limezungumzwa kwa kirefu katika bunge la Tanzania haliwezi kuwa sawa na maneno uliyoandika hapo juu kwa wanabodi.

2.) Je kama TRA hawakuwa na makosa ni kwa nini walilipa 'compensation'?

3.) Je wewe ni kati ya wale wanaofaidi na uendekezaji wa ukabila pale TRA?

Only in Tanzania maamuzi ya waziri yanaweza kupuuzwa na viongozi wa ngazi ya chini yake, iko siku tutapata wasafishaji wa hii system iliyooza.
 
Back
Top Bottom