Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Mzee Mwanakijiji,

Maelezo yako kuhusu ukabila katika ajira ni mazuri sana. Nimefurahi kwa quotes zako za JKN kuhusu hili. Watu wengi wana mawazo potofu kuhusu ukabila na udini katika ajira. Ukweli ni huo uliouelezea kwa ufasaha. Endelea kuelimisha

Tuangalie.

Kama jina lako linavyosema ilitakiwa uangalie suala la ukabila kwa kina sana. ni sawa na mficha uchi huwa hazai au mficha magonjwa.

Ukabila ni jambo la wazi sana. fuatilia wagombea wa NEC kupitia mkoa wa Mbeya.
Fuatilia mgogoro wa kanisa la KKKT-Same kwa Cleopa Msuya ambapo wapare wanataka wa control kanisa. tizama shirika la Bima kuna kipindi lilikuwa ni Mali ya Wanyakyusa tu.

UKABILA Tanzania upo na watu wa kaskazini wameshika sana na ninakubaliana na watu wanaowashutumu hawa watu.
 
JAMANI NA WAHAYA NA VYOMBO WA HABARI MSIWAHAU.

Hili suala la ukabila ukitizama vyombo vya habari kama gazeti la RAI kuna kundi kubwa la hawa watu wa Bukoba. Kuanzia kwa kina Salva,Muhingo,Bwire, Kamhanda,Balile,n.k

Hawa jamaa wamejipanga na kuna kipindi walikuwa wakimpigia debe Magufuri achukue urais, huku hajafanya chochote na anajulikana kwa ten percent imebidi apelekwe Chenge sehemu ya mabarabara kutokana na rafu alizocheza Magufuri. amejijengea Barabara hadi kijijini kwake.

Naomba muwatizame na wahaya kwenye vyombo vya habari kwa ukabila wao.
 
Mzee Kifimbo, magufuli ni Msukuma (kutokea Biharamulo haimaanishi mkoa wa Kagera wote wahaya), hata kama Wahaya wa Rai walimpigia debe ukabila unaingiaje hapa?
 
Mzee Kifimbo, magufuli ni Msukuma (kutokea Biharamulo haimaanishi mkoa wa Kagera wote wahaya), hata kama Wahaya wa Rai walimpigia debe ukabila unaingiaje hapa?

...kachanganya na suala la chenge kuwa waziri wa miundombinu badala ya magufuli. amesahau kuwa ni awamu tafauti na kabla ya hapo alikuwapo mramba.
 
Ukabila ni jambo la wazi sana. fuatilia wagombea wa NEC kupitia mkoa wa Mbeya.
Fuatilia mgogoro wa kanisa la KKKT-Same kwa Cleopa Msuya ambapo wapare wanataka wa control kanisa. tizama shirika la Bima kuna kipindi lilikuwa ni Mali ya Wanyakyusa tu.

UKABILA Tanzania upo na watu wa kaskazini wameshika sana na ninakubaliana na watu wanaowashutumu hawa watu.

Mzee Kifimbo,

Mgogoro wa KKKT umejikita ktk upinzani wa muda mrefu kati ya South-Pare na North-Pare. South Pare ni maeneo ya wilaya Same, na North Pare ni eneo la Wilaya Mwanga.

Mwanzoni Askofu wa KKKT alikuwa akitokea North-Pare, lakini alipostaafu Askofu mpya ametokea South-Pare.

Nimeelekezwa kwamba tensions kati ya South vs North Pare ziko kwa muda mrefu. Tensions hizo zilianzia na uhasama/upinzani wa kisiasa btn individuals. Naambiwa mambo yalianzia tangu enzi za Chedieli Mgonja wakati huo Mwanga na Same zikiwa wilaya moja.

Huyu Cleopa Msuya tunayemsikia naambiwa alikuwa hawezi kushinda uchaguzi akisimama na mgombea wa South Pare kutokana na South kuwa na wapiga kura wengi. Naambiwa wananchi wa South Pare hawampendi Msuya kwasababu wanaamini aliwanyima maendeleo kwa kumsakama kisiasa Mbunge wa South Pare Chediel Mgonja.

Vilevile inasemekana wasomi wengi wa Kipare[walioko serikalini na mashirika]wanatokea South Pare siyo Mwanga. Ninaambiwa kwamba wale wanaoona kila Mpare wakafikiri amesaidiwa na Msuya wanakosea.
 
Asante JK kwa maelezo yako mazuri. kutokana na uchambuzi wako huu ina maana tunakubaliana kuwa kuna ukabila, na Msuya alikuwa sumu kwenye dhambi hii ya upendeleo serikalini na kwenye mashirika makubwa.

Hawa Wapare nimeona wanalalamikiwa hata na taasisi za waislam, niliwahi kusikia malalamiko makubwa kuwa wanatumia taasisi kwa manufaa yao. kuna taasisi inaitwa Ubungo Islamic Association nasikia imeshikwa na wapare na upendeleo ni kwa muislam Mpare tu.

wamekuwa wakiitumia dini ya Kiislam kama NGO. tujiulize hawa watu wa Kilimanjaro wana nini kuwa wakabila kiasi hiki? ukienda Tanga nao hadi uwe Mtanga ndio washirikiane na wewe.
 
Hawa Wapare nimeona wanalalamikiwa hata na taasisi za waislam, niliwahi kusikia malalamiko makubwa kuwa wanatumia taasisi kwa manufaa yao. kuna taasisi inaitwa Ubungo Islamic Association nasikia imeshikwa na wapare na upendeleo ni kwa muislam Mpare tu.

Uzushi!!!
🙄
 
Ukabila,
Hauko tu kwa Wapare- uko sehemu nyingi tu! Tz serikali haisemi wazi kuna ukabila- MFICHA UCHI HAZAI! Nchi nyingine zimechukua hatua mbali mbali kukabiliana na mambo hayo- ktk elimu, kazi, n.k
Ni ukweli usiofichika sasa kuw tofauti inazidi kuwa kubwa jinsi tunavyoenda mbele. Ila lazma serikali iliongelee kwanza kisera. Kuna tofauti za kidini, kanda, mikoa, kikabila n.k. Sababu za kuwepo na haya mambo nyingine ni za Kihistoria. Ila nyingi zimeendelezwa na upendeleo wa kikabila unaoendelea kwa sasa!
 
....ukabila haufai waulizeni wanywarwanda mtapata jibu!
 
Uzushi!!!
🙄

Bokassa.

Issue ya Upare-Taasisi za kiislam sio uzushi. mimi nimewahi kutumiwa email kuwekewa wazi jambo hilo na au muulize Mwandishi Balile atakupa ukweli na hisia za upare Ubungo. naomba nitumie PM email yako nikutumie habari ya upare taasisi za kiislam.

inawezekana wewe ni muislam lakini kuficha mapungufu si dawa suala ni kujadili. kuna watu wanaamini kuna udini nchini na vitabu vimeandikwa. pia usitakae ukabila upo na uislam unasumbuliwa na wapare ambao ni jadi yao ukabila wameridhishwa toka kwa Mgonja na Msuya.

mfano Mzuri Cleopa Msuya amechangia sana misikiti kwa waislam wa huko kwao. sasa muislam aliyesaidiwa na Msuya atakuwa na hisia za kuwa upare ni zaidi ya uislam.

Bokassa endeleeni kuficha uchi tu. maadui zenu si wasio waislam kama baadhi ya watu wanavyoamini ni ukabila tena upare.

nakuuliza kijadirida za Annur umewahi kuona kimeeleza matatizo ya sehemu nyingine ya waislam kuliko ya huko Upare? viongozi wote wanatukanwa na kijarida hicho lakini haijawahi kutokea Msuya au Gladdness Mziray ukasikia wametukanwa anatukanwa JK na ruksa. kisa mhariri na waongozaji wa kijarida hicho ni wapare.

Ndugu zangu Waislam kama mnataka maendeleo ya kweli tatueni matatizo yenu kwanza. na pambaneni na wanaoleta ukabila kwa kwenye dini yenu.

nakupa homework Bokassa. fuatilia miradi ya shule za Ubungo, kirinjiko, mudio, Kibohehe,na zingine mbili zote za kiislam ziko Kilimanjaro kwanini msizipeleke Bagamoyo. kilwa ,pangani, Mtwara au Lindi?

na mnapokuwa na watendaji waliokosa busara kama Saiboko ambaye mnadai ni kiongozi wenu huku hana busara hata chembe mnategemea nini? Saiboko ni mpare na product ya Msuya, jee atakuwa na mapenzi na waislam au wapare? nakupa homework.
 
Ukabila ni sumu kali. naona tumekuwa wasiri kwenye ukabila kama tulivyo kwenye kwenda kwa waganga wa jadi. kila mtu atakwambia hakuna ushirikina lakini waganga wa jadi wanajitangaza kwa wingi kwenye magazeti. na ukienda mlingotini unakutana na John, Bakari Mwakipesile wote wako kwenye foleni ya kusubiri ndumba toka kwa Tekero.mkikutana ofisini mnasema hakuna imani hizi.
tuwe wakweli kwenye hili la Ukabila na juhudi za maksudi zichukuliwe.
 
Mtalii,
Tatizo la Waislamu wa Pwani ni kutokuwaelewa watu wa Bara. Kwa watu wa Bara dini ni suala secondary tu. Watu wa Bara wanathamini Mila na Tamaduni zao kuliko masuala ya Dini[Ukristo na Uislamu].

Unaweza ukakuta mtu wa bara ni Mkristo lakini ana wake wawili kwasababu mila za kabila lake zinamruhusu. Vilevile unaweza ukakuta Muislamu anakunywa pombe kwasababu ni utamaduni wa mababu zake.
 
Bokassa.

Issue ya Upare-Taasisi za kiislam sio uzushi. mimi nimewahi kutumiwa email kuwekewa wazi jambo hilo na au muulize Mwandishi Balile atakupa ukweli na hisia za upare Ubungo. naomba nitumie PM email yako nikutumie habari ya upare taasisi za kiislam.

inawezekana wewe ni muislam lakini kuficha mapungufu si dawa suala ni kujadili. kuna watu wanaamini kuna udini nchini na vitabu vimeandikwa. pia usitakae ukabila upo na uislam unasumbuliwa na wapare ambao ni jadi yao ukabila wameridhishwa toka kwa Mgonja na Msuya.

mfano Mzuri Cleopa Msuya amechangia sana misikiti kwa waislam wa huko kwao. sasa muislam aliyesaidiwa na Msuya atakuwa na hisia za kuwa upare ni zaidi ya uislam.

Bokassa endeleeni kuficha uchi tu. maadui zenu si wasio waislam kama baadhi ya watu wanavyoamini ni ukabila tena upare.

nakuuliza kijadirida za Annur umewahi kuona kimeeleza matatizo ya sehemu nyingine ya waislam kuliko ya huko Upare? viongozi wote wanatukanwa na kijarida hicho lakini haijawahi kutokea Msuya au Gladdness Mziray ukasikia wametukanwa anatukanwa JK na ruksa. kisa mhariri na waongozaji wa kijarida hicho ni wapare.

Ndugu zangu Waislam kama mnataka maendeleo ya kweli tatueni matatizo yenu kwanza. na pambaneni na wanaoleta ukabila kwa kwenye dini yenu.

nakupa homework Bokassa. fuatilia miradi ya shule za Ubungo, kirinjiko, mudio, Kibohehe,na zingine mbili zote za kiislam ziko Kilimanjaro kwanini msizipeleke Bagamoyo. kilwa ,pangani, Mtwara au Lindi?

na mnapokuwa na watendaji waliokosa busara kama Saiboko ambaye mnadai ni kiongozi wenu huku hana busara hata chembe mnategemea nini? Saiboko ni mpare na product ya Msuya, jee atakuwa na mapenzi na waislam au wapare? nakupa homework.

Mtalii.

Somo zito umempa Bokassa, mie niliambiwa Mzushi jee haya ya Mtalii nayo uzushi? Bokassa uko wapi?

Tena hao Wapare wa Ubungo nasikia wanakula hadi ada za wanafunzi wale waliofaulu kwenda serikalini. nimebahatika kuona joining instruction yao inasema wazi " PESA IKILIPWA HAIRUDI KWA SABABU YEYOTE ILE" bwana Bokassa katika sheria zetu hizi common Law na hasa Law of Contract kuna nafasi za mtu kuwa refunded always kuna general law ikifuatiwa na exceptional law.

Huwezi kuchukua pesa ya mtu bure bure. sheria ya uislam sijui inasema nini? lakini naamini haikubali mtu kumdhulumu mwenzie kienyeji kiasi hicho cha wapare wa Ubungo wanavyowaibia waislam.

Naamini wanachokifanya Ubungo ni unyama na wizi wasitumie dini.
nakaribisha maoni yako Bokassa.
 
nungwi,mtalii,
mimi naona nyinyi pia ni wabaguzi. hivi hao wapare wasingedhulumu mngewataja kwa kabila lao? i doubt it. kwani ktk wanaodhulumiwa hakuna wapare? hao pia mtawataja kwa makabila yao?
 
nungwi,mtalii,babu: mwanangu hii gari na dereva anayekuendesha ni ya nani?
kijana: babu hiyo ni gari ya serikali na huyo ni dereva wamenipatia.
babu: mwanangu umepanda cheo siku hizi mpaka una gari na dereva?
kijana: ndiyo babu, namshukuru Mungu. nimekuwa mkurugenzi wa shule za msingi.
babu: mkurugenzi wa shule za msingi za daresalamu au hata hizi za hapa kijijini kwetu?
kijana: mkurugenzi wa shule za msingi tanzania nzima.
babu: basi mwanangu huu ni mwezi wa 3 waalimu hawana chaki ktk shule yetu. hebu chunguza huko kwa wakubwa wenzako maana itakuwa aibu wewe kuwa mkurugenzi na kijijini kwenu shule hazina chaki.

....sasa huyu Mkurugenzi akirudi mjini basi atahakikisha kwamba anajuana na afisa ugavi na kwamba shule ya kijijini kwao haikosi mgao wa chaki. hata ikibidi kumhonga kwa pesa yake mwenyewe au kumnunulia pombe.

...ningefanya hivyo hivyo.

...labda kama tatizo hilo lingekuwa la nchi/nnji nzima!

...ni aibu haswa!mkurugenzi mzima kwenu hamna hata chaki!

...charity begins at home!
 
...ningefanya hivyo hivyo.

...labda kama tatizo hilo lingekuwa la nchi/nnji nzima!

...ni aibu haswa!mkurugenzi mzima kwenu hamna hata chaki!

...charity begins at home!

Ni wale wale wanaofaidika.hata ukabila unaanza nyumbani kwani ukabila unaanza wapi?.Acheni hizo sasa mtu asiyekuwa na ndugu au mtu wa kabila lake afanye?.kwa hiyo hasitaili kufanya kazi katika nchi yake.Ninani katika wanamtandao atakayesema kikwete si kiongozi mzuri wakati anafaidika?.hata wewe huwezi kusema ukabila mbaya kwa sababu ndipo unapofaidikia.
acheni hizo kuwa watetezi wa ubaguzi.uko siku mtaona ukweli wake kwani watu watawachoka!
 
..we utasema sana,ukweli ni kwamba ukabila upo,ulikuwapo na utaendelea kuwapo.

..point is,huo ukabila ni wa ubinafsi au wa kuleta maendeleo?

..kwa mfano,siye watu wa mkuranga tukiamua kuitishana na kuchangishana kwa ajili ya maendeleo yetu,halafu kiongozi wa serikali aliyetoka huku naye akijachangia[tena fedha nono],utasema huo ni ukabila!

..sasa,si tusonge!tuache maneno maneno,tujenge nchi!

..charity begins at home!
 
DAR_si_LAMU,
huu utaratibu wa "kujuana" hauwezi kuisha as long as kuna uchache wa nafasi za ajira nchi nzima. yaani mimi nimeshangaa waTanzania tunatoana macho kwa ajira za TRA,BOT,na IKULU.

Halafu ajira zenyewe za Uhasibu,Economist, Wanasheria, taaluma ambazo kwa kweli hazijengi nchi. Bora zingekuwa ajira za Uhandisi,Udaktari,...

Katika nchi za wenzetu vijana wanazikimbia hizi kazi za serikali kwasababu malipo yake siyo mazuri. sisi waTanzania tumekabana makoo. Kwenye nchi za wenzetu sekta binafsi ndiyo inalipa.

Anyway, kama humjui mtu Tanzania basi kupata ajira ni taabu kweli kweli. Tuukubali tu ukweli huo na tujenge nchi. Kulalamika peke yake haitoshi.

Sasa hao wanaotoa ajira kwa kujuana hawafanyi hivyo kutokana na roho mbaya. Ndiyo mazingira yaliyopo. Lakini in a long run mambo mengi yanakuwa balanced na maisha yanaendelea.

Mkubwa anayetokea Mkuranga[Pwani] anamtumia anayetoka Kagera, na wa Kagera naye anamtumia anayetoka Mbeya, wa Mbeya anamtumia anayetoka Mtwara etc etc....life goes on.....could be our way of life!!!

Pamoja na kusema hayo haimaanishi kwamba hakuna watu wabaya ktk jamii yetu. Lakini mimi nitawatofautisha watu wabaya wa Mkuranga na wale wa Rombo.

THIS IS MY OBSERVATION: Mwenyeji wa Rombo akipewa umeneja wa Benki basi atajitahidi baadhi ya mikopo wapate wa Rombo wenzake. Mwenyeji wa Mkuranga,Bwagamoyo,Newala,Songea, akipewa ulaji Benki basi anakula na Wahindi tu, watu wa kwao hawapi kitu.

Halafu baadaye wananchi wa Mkuranga,Bagamoyo,Newala... wanaanza kuwazomea wa Rombo kwamba wamebebwa na Ukabila.
 
Back
Top Bottom