Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Hilo la wezekana, lakini kabla ya ku jump kwenye conclusion heba tazama intake na wahitimu wa vyuo vikubwa mfano universities na higher institutions nyingine ni makabila gani yenye watu wengi. Je! wamependelewa kuingia au ni nasibu tu? Kama wana mwamko wakasomesha watoto wao, basi na kwenye ajira ni lazima watakuwa wengi zaidi ya wenzao. Sasa wale wengine watabaki pembeni wakilalamika na kunyoosha vidole. The same applied kwenye udini kama dini fulani ni wachache vyuoni alafu unakuta kwenye ajira wamelundikana, jiuulize wametumia vigezo gani? "Food for thought".
 
naweza toa personal experience, ktk shule zote nilizosoma hapa dar from primary hadi university majority ya wanafunzi ni wa kutoka ktk makabila hayo japo mimi si wa kabila kati ya hayo!!! na cha kushangaza pamoja na wingi wao pia ndio waliokua nashika nafasi za juu darasani, cjawai muona muhaya mjinga ktk shule nilizosoma from primary hadi university kwa hiyo iyo trend kuendelea mbele ya safari kwenye ajira sioni kama ni shida!!!
 
UDSM
PROF MUKANDARA, PROF MULOKOZI,PROFF RUTASHOBYA,PROFF RWEKAZA, PROFF RWAITAMA
IFM
KATO RUGANGILA,PROF TUMWESIGE, PROF
MZUMBE
KABIGIZA,prof kaijage
SAUT, mweiga baregu prof, kwaNINI HAWA TU JAMAN
 
As a Kenyan let me say this

YOU DO NOT WANT THE DEMON THAT IS CALLED TRIBALISM.

I DO NOT WISH TRIBALISM ON ANYONE it will your country social fabric kama mchwa

Stay the f*ck away from tribalism, I beg you
 
mleta hoja ungetaja marina. Namna hii ni majungu. Nadhani makabila nayo watu wamesoma sana na lazima itareflect tu hata kwenye ajira pia. Mbona JK abgejaza wakware!! Pigeni shule jamani
 
Watu wote waliofilisika sera,watataka kujihalalisha,ama kwa udini,ukabila,au ukanda,na hawa ni watu wa kuepuka kama ukoma.
 
Mods hizi threads zingine muwe mnazimaliza wenyewe huko huko, zinatia kinyaa sana hazifai kufika jamvini.
Najua hii topiki haitokuwa poplar na baadhi ya watu humu ndani na hata wenye website lakini potelea mbali

Je ni kweli wizara hizo zimejaa makabila ya Wachagga,Wanyakyusa na wahaya?

mimi nilikuwa siamini mpaka pale NILIPO ambiwa kuwa kuna UKABILA wa hali ya juuu kule Ikulu NA vile vile namba mbili kwa UKABILA ni TRA je kuna ukweli katika haya?

Japo kuna watu wanasema kuwa ni udini lakini sumu ambayo hatuko tayari hata kuijadili ni hii ya ukabila na ndio inayoturudisha nyuma je mnakubaliana nayo?





-JAMBO FORUMS WHERE WE DARE TALK OPENLY
 
samvulechole... hakuna hoja ambayo ni ngeni hapa.. madai ya makabila hayo kupendelewa hayakuanza leo! tangu mara tu baada ya uhuru kulikuwa na tuhuma hizo hizo.. so.. there is nothing there..! Hata hivyo hatari unayoweza kuleta siyo ukabila bali ubaguzi, kuwa kama mtu anatoka kwenye makabila hayo basi asipewe nafasi fulani kwa vile watu fulani wanadhani kuna ukabila! Nitakupa mfano, kuna wanasheria watatu wote ni maprofesa... kuna Prof. Mwakalindile (Sheria, uzoefu miaka 30), Prof. Mtimba (mmakua, uzoefu miaka 10, sheria), na Prof. Chanda (Mzigua, sheria uzoefu miaka 5). Assuming maeneo ya fani zao ni sawa, ceteris paribus Rais anataka kumteua mshauri wa kisheria.. nani apewe kwa haki? Wengi watasema prof. Mwakalindile! Sasa kwa kufanya hivyo hata hivyo kuna wanyakyusa wawili tayari hapo ikulu ambao wameshapata nafasi zao, je tumnyime Mwakalindile kwa vile itaonesha ukabila?

Kabla hatujafikia hapo pa kudai ukabila tujiulize: "Kwanini inaonekana kuna wasomi wengi wa makabila hayo matatu Wachaga, Wahaya, na Wanyakyusa"? Je, tupunguze wanafunzi wanaotoka kwenye makabila hayo na kuwapa nafasi watu wa makabila mengine ili kuleta uwiano (parity)? Je tukiamua kufanya hivyo hatutakuwa tunaanza ubaguzi wa kikabila?

Tarehe 9 Disemba 1968 Nyerere alitumia siku ya Jamhuri kuzungumzia "Vitu ambavyo ni lazima Tuvisahihishe", vitu ambavyo baada ya uhuru havikwenda vilivyotarajiwa. Alizungumzia ukabila; kwanza alisema hivi:

"the man who talks about tribalism being practised without having any evidence for his statement is often a man who wants to stir up tribalism. Even if that is not his purpose, the result can be just the same. People will begin to think that there is tribalism, and, once people begin to think in these terms, then tribalism has begun to enter tinto our society"

Kuhusu Wahaya, Wanyakyusa, na Wachaga kupata nafasi nyingi katika serikali, Mwalimu alisema hivi miaka karibu 30 iliyopita:

"..the work of the civil servants and people in the parastatal organizations does require education..it so happened that the Tanzanians who had the opportunity for higher education under the colonialists were mostly Wahaya, Wachagga, and Wanyakyusa. And because most of the education was provided by missionaries, most of these people are also Christians. That was our inheritance. These conditions will change, but they have not changed yet. And for these reasons, when we get rid of the Europeans who were doing responsible jobs, and give these jobs to Tanzanians, the people who get them come mostly from one or other of these three tribes".

Akaongeza pia,

"Therefore, if you ask me why Wahaya, Wachagga, and Wanyakyusa have most of the jobs which require higher education, the answer is very obvious. They were the ones who received higher education during colonial times. I'd say: investigate the position in politics where a man is not asked about his educational qualifications. Look at the Parliament, the National Executive and Central Committee of TANU, and at the Cabinet. How many Wanyakyusa, Wahaya, or Wachagga are members? You will find that perhaps there aren't any, or there are one or two. This is the truth"

kwa umahiri wake wa maneno JKN akatoboa ukweli huu

"Anyone who refuses to accept a very obvious truth like this, and says that the reason is tribalism, must provide us with the evidence for his statement. If he cannot provide any evidence, we must conclude either that he is a fool, or that he is strirring up tribalism deliberately. He is the sort of (a) person who begs work on a tribal basis, and when he is refused because he does not have the capabilities, he pretends he was refused on tribal grounds."

Akasema pia ni jukumu la serikali kusaidia sehemu ambazo bado ziko nyuma kielimu. Na alimaliza kwa kusema:

".. if a Mchagga, a Mhaya, or a Mnyakyusayoung man were refused work simply because of his tribe - when he is capable and there is no other Tanzanian with the qualifications - then we would be practising a very stupid and very evil kind of tribalism such as that which caused the establishment of Biafra. I beg you, my brothers, avoid ANYTHING WHICH COULD BRING OUR COUNTRY INTO THIS KIND OF DISGRACE" (emphasis mine)
(From: Uhuru na Maendeleo pp 76,77)

so what say you?
Mwanakijiji acha fix, wewe siyo mwanakijiji kwa jinsi ulivyoshusha hii nondo hapa..!
 
As a Kenyan let me say this

YOU DO NOT WANT THE DEMON THAT IS CALLED TRIBALISM.

I DO NOT WISH TRIBALISM ON ANYONE it will your country social fabric kama mchwa

Stay the f*ck away from tribalism, I beg you

You r ----in right baby. Loud and clear. We gonna work on it......

Later: o noooo.... some sht guy cut off my word.....
 
Mkuu usianzishe zengwe jipya, hili la udini linatosha. Unajua hao wakulima wa kahawa walipewa elimu tangu ukoloni ili walime kahawa nzuri. Utamaduni wa kupenda shule ni jadi yao tangu ukoloni, sasa isiwe ugomvi kuwaona wengi kwenye madeski makubwa ya ofisi. Cha msingi kila mtu sasa apende shule na na apewe fulsa kukalia deski kubwa la ofisi. Lakini usisahau kuwahi ndio kupata.
 
Unapozungumzia ukabila unatumia vigezo gani?

Kama utasema Wachaga ni wengi,na wakati huo wewe ni unatokea katika kabila ambalo ni dogo au unatokea katika kabila ambalo watu wake wamechelewa kupata elimu mapema.

Tukizungumzia ukabila tutazame vitu 2. Kwanza ni ukubwa wa kabila husika. Pili ni elimu kama watu wengi katika kabila hilo wamepata.
Sasa ukizungumzia makabila kama Wachaga au Wanyakyusa na hata Wasukuma;utaona kuwa makabila hayo ndio makabila makubwa,kwa maana kuwa yana idadi kubwa ya watu.

Pili ukizungumzia upande wa elimu,utaona kuwa mkoa wa kilimanjaro hususani maeneo wanayotokea Wachaga utakuta elimu ilichukua nafasi tangu kipindi kirefu hususani kabla na hata baada ya kupata uhuru.

Kama watu wanapewa hizo nafasi kwa sababu ya vigezo shule ikiwemo, sioni tatizo. Shida itaanza kama kuna mtu wa kabila lingine mwenye vigezo atanyimwa nafasi/ kazi kutokana na kabila lake.

Wale wenzangu nadhani hoja ingekua kutafuta elimu kwa bidii na sio kulalamika, piga shule, pata vigezo mtu akikunyima kazi kwa kigezo cha kabila hapo una haki ya kulalamika.

Sitoki miongoni mwa hayo makabila ila jamaa wako vizuri.
 
unajua mtu usipojua historia yako.. kuna hatari ya kujaribu kuiandika upya! Ili kuelewa hapa tulipo sometimes we have to look back where we are coming from. Historia yetu haikuanza jana au juzi (kama baadhi wanavyotaka tuamini) matatizo tuliyonayo leo hayakuanza jana (isipokuwa haya ya kina Richmonduli!) lakini mengi yana msingi toka huko nyuma. Binafsi, nitashtuka zaidi kama kwenye nafasi fulani kwenye taasisi kumejaa Wakerewe, Wanyali, au Watindiga.. kwa sababu hakuna jibu zuri la kihistoria linaloweza kuonesha kujaa huko!!

La maana ni kuongeza jitihada ili baadaye hali ielekee uwiano kwani Waha na Wamang'ati na wenyewe watakuwa na shule nyingi na wanapata nafasi nyingi za kusoma.. kwani hata hivi sasa bado Uchagani, Mbeya n.k wanaendelea kuwa na shule nyingi na zenye kutoa wanafunzi wengi (angalia matokeo ya hivi karibuni!)..

Do we need some kind of affirmative action which would not be translated as reverse discrimination?

sure mkuu
 
Ni vyema ukawa na ushahidi kwamba ukabila unaozungumziwa ni wa kupanga au ndio waliopiga shule na kuwa na vigezo. Hatuna nafasi ya Ukabila Bongo. Ona hapo kwa jirani zetu wanavyohaha ka bla ya uchaguzi!!!!
 
Ukabila upo hata John Pombe Magufuli alipokuwa wazili wa ujenzi aling'ang'ana na barabara ya Dar hadi Mwanza. Barabara ya Lindi Dar, Mtwara Songea bado inasuasua kila mwaka fedha hazitoshi. imeanza kujengwa mi hata chekechea zijaanza mpaka leo haijaisha. Hao waliosoma zamani wanahakikisha wakiondoka wanaacha watakaolinda maslahi yao. Si kweli kuwa mpaka leo baada ya miaka 50 na usheu ya uhuru hakuna Wamakonde, Wangoni, Wapemba wasomi wenye uwezo wa kufanya kazi serikalini. Kuna sehemu zinadunishwa makusudi, wacheni wamakonde waje juu na gesi yao. Kwani mitambo ya umeme haiwezi kujengwa huko. hivyo viwanda kwa nini visijengwe mtwara au lindi.
 
UDSM
PROF MUKANDARA, PROF MULOKOZI,PROFF RUTASHOBYA,PROFF RWEKAZA, PROFF RWAITAMA
IFM
KATO RUGANGILA,PROF TUMWESIGE, PROF
MZUMBE
KABIGIZA,prof kaijage
SAUT, mweiga baregu prof, kwaNINI HAWA TU JAMAN

Duh, hivi mtu akiwa Prof kuna ukabila gani? Huyu Baregu alinyimwa mkataba Udsm, SAUT wakamchukua! Ukabila uko wapi hapo?
 
Mwanakijiji.

ina maana hata kabila lako nikutajie mimi?wewe ni mtu maarufu na mwandishi si vyema nikuanike sana. nitakutumia kwenye PM.

Mkandara.

naomba uwasaidie tena hawa waficha ukabila. shule ya Marian girls iko bagamoyo-mkoa wa pwani na hapo bagamoyo ni asilimia kubwa sana ni waislam na makabila ya pwani.

lakini katika vijana waliomaliza kidato cha nne hata cha sita hao waislam au wakwere/wazaramo hawafiki hata watano. tena toka nchi nzima hakuna waislam watano wala usiseme wenye bagamoyo wenyewe kama wapo.


au Nenda ST.Anthony pale mbagala jee kuna wazaramu wangapi wanasoma?au makongo wanaosoma ni watoto wa wanajeshi tu?

kwa hoja za kina Mwanakijiji na YEBO YEBO watasema bagamoyo waislam wamepiga hatua kwani wana shule na wanazidi kusoma.

Kifupi TRA kunatakiwa kumulikwa na hawa wanaopinga wengine ndio wakwepa kodi kwa kutumia ukabila.

nakupa mfano hai Reginald Mengi anadaiwa kodi na TRA zaidi ya billion 5 lakini kutokana na sera za ukabila nani atamshitaki? ukigeuka kuna Kittlya. Laowo, mmanda, salim yusuf, maleko.

Mwanakijiji

najua wewe ni msafiri kuna baadhi ya nchi hasa ulaya unaulizwa utaje wewe ni mtu gani mzungu, mhindi.mwafrika n.k hadi kwenye fomu za vyuo vikuu na wanakwambia tunachukua takwimu hizi ilikuona equal opportunity inachukua nafasi yake.hawa wenzetu wameshtuka, sisi tukisema tuanzishe utaratibu huo Mwanakijiji utakuja juu. na hili suala hata kiusalama wa nchi si zuri. leo jeshini wawe wakurya watupu na itokee professor Sarungi kagombea urais akashindwa ndani ya chama alichoombea halafu aamuwe kuingia msituni kwa kutumia influence ya mkoa wake kuwa na wanajeshi wengi kutakalika?

kwa kila nukta iwe ukabila utafutiwe neno kujuana bado ni jambo baya na la kukemewa sio kufumbiwa macho na kulibatiza majina mengine.

fuatilia Nigeria waliiachia suala hilo leo linawaumiza vichwa.

narua tena Tanzania ya sasa tuna wasomi wengi toka makabila yote, hadi kalani atoke moshi ndio TRA ifanye kazi?

mwaka jana kulitokea nafasi za kazi Hazina zilkuwa 600 na application zaidi ya elfu kumi tena makabila mbalimbali na hata sasa kuna nafasi zingine zimetoa fuatilia kama wanaomba wachagga tu.

pia uliza nafasi 13 zilizotangazwa na mambo ya nje tizama walijaza wangapi? na waliochukuliwa ni kina nani?

na hata miji ya mwanzo kuwa na shule ni Tanga kama wasomi basi wangekuwa waTANGA au hamjui kama wajerumani walianza Tanga?
uliza mkuu wa mwanzoCHUO CHA MZUMBE alikuwa mchagga?ni familia ya mwapachu.

Kama wazaram hawasomi basi tungeona wasukuma, wahaya, wamakonde au wazanzibari. Skuli za Tumekuja, MWanakwerekwe, Jambiani, Tunguu, Makunduchi hakuna mchaga lakini wanyamwezi wapo.
 
MWANAKIJIJI.

Naona unataka kupindisha mada na kuleta upofu sio siri ukabila umetawala sana hivi sasa.
Mama Mkapa alipokuwa Ikulu alifanya kila linalowezekana kuhakikisha anaingiza wachagga kila kona, na hata deal za rada na ndege ni wafanyabiashara wa kichagga wana mikono yao.

chukulia mfano daktari wa mkapa alikuwa dr.Maro mchagga na ni ndugu wa mama Mkapa, mpiga picha wa Mkapa na sasa Rais Kikwete ni mchagga na ndugu wa mama mkapa freddy Maro. na Ikulu imejaa wachagga wengi tu. foreign nako ni hivyo hivyo.

vipi TRA nako imetokea kama ajali? hujui kama ukiwa na jina Kittlya, mrema, mushi, lyimo, tesha, mbowe, Lauo, yaani TRA yote imeshikwa na watu wa moshi. jiulize hadi kituo cha ushuru kilichotakiwa kiwe Tanga lakini kiko Holili.
haya ni masuala ya ukabila ndani ya TRA ambayo ina mahusiano na wizara ya fedha ambako ni ngome ya watu wa kaskazini.

suala la uchagga TRA limefikishwa hadi bungeni. na kama ulifuatilia bajeti ya wizara ya ujenzi ambapo Mramba alihakikisha kila kitu kinakwenda Kilimanjaro na kuzua mtafaruku kwenye bajeti ya mwaka huu.

nchi yetu inakwenda kubaya hivi sasa. wanyakyusa nao wanataka kutawala JKT na Jeshi kwa nguvu hivi sasa labda kwa vile uko nje ya nchi. ndio maana hujui ukabila unavyotafutana nchi.

Mkuu naona una hoja, kiukweli, ukabila unadunda kwa saana tu malangoni mwa taasisi nyingi za selikari hapoa nchini, bt tatizo ni ngumu kuushugulikia coz umeshika pabaya. Ni kama jipu la puani linavyouma lakini gumu kulishugulikia.
Kikubwa tu watu wawe waungwana na wazalendo wa kujali na utaifa na kuacha kutoa kazi kwa kufuata origin, wala itikadi za kiiman.
Tusipoangalia tutafikia pabaya, kuanza kusakana kama ilivyokuwa Rwanda. Tuvumiliane na kumuogopa Mungu kwa kuepuka ubaguzi na upendeleo sehemu yoyote ya kazi au shule!
Hayo yametokea TRA na kwingineko, sasa tuwasaidie kwa kuwaambia waache iyo tabia coz itawahatarishia kizazi chao na nchi kwa ujumla ikitokea watu wakakosa uvumilivu na kulianzisha.

Nahs kichwa kinaniuma kujadili maada yenye uzito hivi na isiyo na suruhisho jepesi, kwani suluhisho lake ni kilio/huzuni kwa watakaoguswa!
 
mhh nahisi hiili suala lina ukweli ndani yake, yani unaweza ingia sehemu ukachek management staff ukabakia kujiuliza maswali na kujijiju mwenyewe tu
 
Back
Top Bottom