Ukabila ni jambo lisilo semwa sana nchini lakini lipo sana kazini/maofisini

Ukabila ni jambo lisilo semwa sana nchini lakini lipo sana kazini/maofisini

Kuna wakati MSD ilikua kama uko Rio De Janeiro. Sijui siku hizi kama haya mambo hayapo. Lakini ukweli ni kwamba kujuana kupo sana tu na hakuzingatii kabila peke yake. Kuna vigezo vingi sana wanavyovitumia watu katika kujuana na ndio maana tuna kitu kinaitwa connection.

Tell me why, kuna PSRS lakini Bunge, BOT, TRA, JSC etc wanajiundia vimfumo vyao amabvyo ni non transparent kwa ajili ya kuajiri wakati ajira kwenye utumishi ni HAKI ya watanzania wote. Tena wanasema pale "only succesful candidates will be contacted". Lengo ni kwamba, it is easy to temper when the system is not transparent. Huko utumishi ilikua ni rahisi kwa competent people ambao hawamjui meneja rasilimali watu waingie kwenye ajira.

Mwisho wa siku yanakua kama yale yale ya USAID. Baada ya kusimamishwa kazi, familia nzima wako jobless 😁 😁 😁​
 
Tumlaumu mkoloni aliyependa kuishi maeneo ya miinuko na baridi hapa nchini na kuanzisha shule na makanisa huko.Jambo hili lilipelekea maeneo hayo kupata elimu kuliko maeneo mengine nchini.Matokeo yake yalionekana kwenye ajira yakitawaliwa na hao uliowataja.Tunamshukuru Mwalimu kuliona tatizo na kuanzisha shule zilizosomesha hata wabarabeid hata kwa maksi ndogo walipelekwa sekondari.Philosofia ya mwalimu ilianza kuondoa ukabila ktk ajira taratibu kwa sababu elimu iliwafikia makabila yote nchini.Haya unayosimulia ni matokeo ya ukoloni kwamba hao uliowataja walikutangulia lakini sio nyakati hizi.
Chunguza tena mkuu. Yani watu waajiriwe 2022 useme habari za nyerere wengi wanao ajiliwa wana msoma tu kwenye historia?
 
Jambo moja tu huwa linanikela nalo ni hili "mtu moja anayefahamika kwa jina la holoholo mkazi wa manispaa ya bukoba msukuma na mkulima wa tumbaku anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za....." hilo kabila ni la nini hapo wakuu?
 
Ila Wahaya wamezidi, kuna shule nilienda kuanzia mlinzi mfanya usafi, walimu mpaka secretary ni wahaya. Hadi madereva wa school bus.

Yani ukiingia ni kama upo Bukoba, mwendo wa kihaya tu. Mmiliki wa shule ni Muhaya.
 
Sio tu huko wachaga ,wahaya waha ,wamejazana pia ulaya na America hasa Downton D.c.
Huwa najiuliza hata ukiwa kiongozi unaweza kupambana vipi na ukabila maofisini?
Maana kwenye usaili unaweza usiitwe kabila na mbaya zaidi majina yetu hasa surname ndo kielelezo cha makabila yetu.Boss akiona cv yako tu na kisha akaona cv ya kaijage basi mchezo umeisha inatupwa kabisa na haitaoneana.

Je wewe kama mdau unaweza pambana nalo vipi jambo hili?
 
Binafsi nimeona kitu wakati najenga.

Ukipata fundi kabila fulani basi atakuwa akikushawishi vifaa mkanunue duka la mtu wa kabila lake kwa hoja ya bei nzuri au ubora wa bidhaa ila ukifuatilia hutoona utofauti wa bei/ubora na maduka mengine.

Ukienda Hardware moja ukakosa bidhaa husika hasa kama ni mzigo mkubwa eg tiles basi,muuzaji atakuunganisha na duka la mtu wa kabila lake hata kama duka jirani yake linauza bidhaa hiyohiyo.

Hizi jumuiya/vikundi vya watu wa kabila fulani wanaoishi mkoa/mji fulani vimefanya watu wa kabila moja watambuane na mambo ndiyo hayo.
 
Huwa najiuliza hata ukiwa kiongozi unaweza kupambana vipi na ukabila maofisini?
Maana kwenye usaili unaweza usiitwe kabila na mbaya zaidi majina yetu hasa surname ndo kielelezo cha makabila yetu.Boss akiona cv yako tu na kisha akaona cv ya kaijage basi mchezo umeisha inatupwa kabisa na haitaoneana.

Je wewe kama mdau unaweza pambana nalo vipi jambo hili?
Kiukweli kumnyima mtu mwenye sifa nzuri nafasi kwa sababu za kikabila ni ushamba, japo jambo kama hili sio rahisi kulimaliza, hata ukisema tuache tumia majina ya koo kuna lafudhi pia 🤔
 
Back
Top Bottom