Binafsi nimeona kitu wakati najenga.
Ukipata fundi kabila fulani basi atakuwa akikushawishi vifaa mkanunue duka la mtu wa kabila lake kwa hoja ya bei nzuri au ubora wa bidhaa ila ukifuatilia hutoona utofauti wa bei/ubora na maduka mengine.
Ukienda Hardware moja ukakosa bidhaa husika hasa kama ni mzigo mkubwa eg tiles basi,muuzaji atakuunganisha na duka la mtu wa kabila lake hata kama duka jirani yake linauza bidhaa hiyohiyo.
Hizi jumuiya/vikundi vya watu wa kabila fulani wanaoishi mkoa/mji fulani vimefanya watu wa kabila moja watambuane na mambo ndiyo hayo.