Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

We upo kwenye point
Yaani sasa hivi kila mtu anasema lake
huyu jamaa anasema alimuona Nahodha akikata kona kali, mara anadai alikuwachooni hakuona ikiyumba ila tu akiwa chooni juu alishtuka yuko chini na kwa uzoefu akaogelea MUONGO
ukweli kuokoka ni majaliwa hichi kivuko kilipinduka up side down
 
Hawachelewi kumuita msaliti, kwa jinsi walivyo waduanzi.
 
Ngoja tungojee ITV Habari saa mbili maana wewe umeshindwa kuweka hata kaklip!
 
Endeleeni na umbea wenu. Diwani wa kata ya Matarawe (chadema), Manispaa ya Songea leo amejiuzulu nyadhifa zake zote kuunga mkono juhudi. Mnajitoa ufahamu sio?

Chanzo:
mkuu. hata wakiunga mkono hali inazidi kuwa ngumu tu. kule ruvuma bei ya kahawa na mahindi haieleweki bado...
 
Mh Kasim Majaliwa ameongea na akasema hilo sawala la injini lilitekelezwa kama mbunge alivyo omba, kiukweli ni kwamba ajali haijasababishwa na ubovu au uchakavu hili limetokana na uzembe wa kujitakia. Tusimtafute mchawi ni nani tu ungane pamoja kuomboleza tuwafariji wafiwa tuache siasa kwenye hili.
 
Kulikuwa na kitabu?
Hivi pale Ferry au Kivukoni kuna orodha mnapopanda kivuko?
Pale ferry hamna orodha we unachukua tiketi yako ukishaingia ndani pale hamna hata hesabu ya kujua watu ni wangapi mnasubiri kupanda tu si ajabu hiyo idadi ya makadirio ya watu kama 400 inafichwa bado idadi inaweza ikawa zaidi ya watu 500.
 
Video muhimu Sana hiki kipindi hatuwezi kuaminiana kimaandishi hivi,
 
Tunazungumzia bima wewe umeleta kudaiwa fidia hiyo ni issue nyingine!

..sasa bima si inakatwa ili kurahisisha masuala ya fidia ikiwa kutatokea ajali?

..Je, kwasababu magari na vyombo vya serekali havina bima maana yake ni kuwa serekali haipaswi kudaiwa fidia ikiwa gari au chombo cha serekali kimesababisha ajali?
 
Hata Mimi siwezi kukabidhi Nyaraka itakayotumiwa kuniangamiza Mahakamani Na kazini

Bora kushtakiwa Kwa Kosa la kupoteza Nyaraka kuliko la kuua bila ya kukusudia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…