Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Bora wangeonesha ukakamavu kama ule walionesha wakati wa kuzuia ukuta, walituonesha uwezo mkubwa walionao ktk kulinda usalama na maisha ya watanzania, kumbe kuokoa maisha yetu wakati wa majanga hawawezi. Ombi kwao, wajenge haraka daraja la wami wasije kusingizia giza siku maafa yakitufika.
 
Hawa vijana wa kijani ndio wanawasafisha mabosi wao mkuu wa mkoa na mkuru na count
 
Naomba mnijibu, nataka kujuwa hao divers are they professional trained and awarded certificates na wana utaalamu kiasi gani au ni divers wa mtaani tu wamejitolea kuokoa
Hamna wataalam anaependa kuona watu wanaangamia akasema tusitishe zoezi la uokozi hao ni wahuni kama wahuni wengine ambal hawana utu kabisa .
 


Wewe badilisha id yako badala ya etwegw anza kutumia Ebwege maana huko upstairs ni empty set!
 
Pole mkuu umesema ukweli ambao wote tunausema maana wnatupa sababu zisizo mashiko kabisa
 
Maagizo ya serikali hayawaruhusu viongozi wa upinzani kufanya shughuri zozote kwenye majimbo ambayo si yao, tukumbuke mhe. Zitto licha ya kuwa mwenyekiti wa taifa wa ACT lakini alikamatwa Morogoro kwa kufanya siasa eneo ambalo si mbunge!
Hapa ndipo kama nchi tunapokuwa wapumbavu kwa ujumla wetu.
Siku ya alhamis SAA 1.22 jioni nikiwa eneo la tukio nilimuona na kumsikia Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela akitangaza kusitisha zoezi la uokozi kwa sababu ya giza. Na nikiri wazi sikumsikia akisema ameshauriwa na wataalamu au yalikuwa mawazo yake. Wakati anatoa tangazo lake kulikuwa na divers ndani ya kivuko ambao walitoka na miili kadhaa saa mbili kasoro hivi. Mara baada ya kutangaza kusitishwa kwa zoezi vilio vilisikika mwaloni toka kwa ndugu waliokuwa na matumaini labda kuna watu wako hai ndani. Baada ya kusoma mawazo ya waombolezaji Mkuu wa wilaya ya Ukerewe akalazimika kutuliza hali ya hewa kwa kusema, namnukuu; Ndugu zangu katika hali ya kawaida mtu hawezi kukaa ndani ya maji kwa masaa zaidi ya manne bado akawa hai kama hana vifaa vya kumsaidia kupumua, Sisi viongozi wenu tuna huzuni kama ninyi lakini kazi hii haiwezi kufanyika gizani, mwisho wa kunukuu". Kwa vile watanzania huwa tunaona kauli za viongozi ni kauli za mbingu wengi walitii lakini wachache wenye uchungu walitoa hoja wakaonekana wabishi mbele ya viongozi. Hilo ziwa lililochafuka SAA 1 jioni hapa Ukara ni lipi? Au waliondoka nalo sisi hatukuliona? Kivuko kimezama chini ya mita 100 toka ufukweni, wazoefu wa ziwa mnajua vizuri, hivi hata ziwa likichafuka kwa umbali huo na kwa watu wenye vifaa watashindwa kuendelea na kazi?
Kesho yake baada ya kelele za wananchi na mitandaoni zoezi lilifanyika hadi usiku siku ya Ijumaa. Hizi sababu za ziwa kuchafuka tumeanza kuzisikiaIjumaa jioni baada ya Waziri Mkuu kuwepo na walikuwa wanaongea kama kujikosha tu na Leo ndo zimeletwa hapa kama sababu rasmi.
Siasa zinatufanya watanzania tukose mawazo ya kuhoji hata vitu vya msingi. Nawashangaa vijana wa ccm mitandaoni mnavyokosa utu na kushabikia makosa ya kiutendaji kwa vile tu aliyekosea ni wa Chama chenu. Sidhani kama kuna mwanaccm mwenye uchungu na aliyepotelewa na ndugu/jamaaa/rafiki kama ilivyonitokea Mimi anayeweza kuunga mkono mawazo yenu. Mimi nilisafiri Jumanne na kivuko hicho hicho na alhamis kikapata ajali, lakini maneno ya usalama mdogo ndani ya kivuko yalikuwepo, na bado tulijaa ingawaje si kama siku ya gulio Bugolora. Siku za Gulio mpaka mitumbwi toka Chifule na Chibasi huwa inasadia kutokana na wingi wa watu.
Mbunge wa Ukerewe kawa mkweli kwamba kivuko kilifanyiwa ukarabati, napo ni kuwekewa injini mpya tu na hoja kuu hata kwenye baraza za madiwani ni kupatiwa kivuko kipya na kikubwa zaidi.
Acha nikae kimya Nina majonzi.
 
Mkuu hata OSHA,SUMATRA nao wana mkanganyiko baadhi ya majukumu na mamlaka.
 
Huyo RC na timu yake hawajali maisha ya wanyonge. Wavuvi wa dagaa wanavua usiku japo kuna giza inakuwaje kuvua watu (kuokoa) kusitishishwe kutokana na giza.
 
Hivi mbona mnatumia nguvu nyingi kukanusha uzembe huu, nadhani tunahitaji kujieleza kwa vitendo zaidi ya matamko yasiyo na tija
 
We jinga kweli ndio majibu gani ya kumjibu mtu aisee we huna hata huruma unchojali ni kuwasafisha mafiem wwnzako tu
 
Kwa hiyo waokoaji hawaruhusiwi hata kula?
unajua maana ya kiongozi kuhamasisha watu kufanya kazi pratically! umewahi kuzijua au kuzisoma principles za kiongozi makini...

umewahi kufanya kazi sehemu yenye kiongozi smart automatically ukajiona unafafanya kazi mpaka unasahau kula?

umewahi kupata uzalendo wa japo kujiuliza wale waliopo majini ni watanzania wenzangu na hawajala...mimi njaa kitu gani?

ukipata majibu ya hayo maswali utajielewa what is on your mind...
 
Wataalamu ndio wenye uwezo wa kujua , vipi wanaweza fanya, NA ushauri wao ni muhimu sana. Tukumbushane wale watoto 11 waliopotea ndani ya pango Thailand 2017, ili hukua karibia wiki nzima, mikakati kuwekwa sawa ili kuwaokoa, hata ile Submarine ndogo iliyotolewa na tajiri wa magari ya Tesla, ilikataliwa, NA waokowaji wakaonekana wana nia mbaya, mwishowe Bw Elon Musk aliabika kwa propaganda alizozifanya.

Mogela yuko sawa kama ayasemayo ni ya kweli.

Akina Mbowe NA Zitto hapa wamejiabisha, si tungeona hata kwenye hizo press conference zao wakianzisha michango .
 
Ndio mkuu uko sahihi kabisa Harafu wao wana kuja na hoja nyepesi eti mtu hawezu kuaa majini kw zaidi ya masaa 3 akawa hai mbona huyo yy amepona sasa aibu yao hao mafiem na roho zao mbaya.
 
Wanachoju ni ufisadi tu hamna lingine wanaleta masihara na maisha ya watu ingekuwa kuna ndugu zao mule wangestisha !!??[emoji26][emoji26]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…