Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Inawezekana...Meli zote zinakuwa na mstari wa usalama.ambao maji hayatakiwi yauguse huo mstari...maji yakiugusa inamaanisha uzito umezidi.. Tatizo ni stability.,,Meli ilikata kona vibaya/ ghafla hivyo mizigo ikahamia upande mmoja, ikakosa balance ikapinduka...
 
Imagine doesn’t count!
Grow up kido!
hata sayansi iliyopelekea tukawa na dreamliner ilianza na assumption mkuu.
ninasema hivyo maana kwenye matukio kama haya ukifanikiwa kukutana na waanga huwa kuna story nyingi. Hata ninachokisema kinawezekana. Labda kama wahusika walijiridhisha hakuna aliyehai ambaye amebaki hivyo watakuja kuokoa kesho tu taratibu kwenye mwanga. Ila maoni Yangu Bora wangefanya kimyakimya, maana siku meli ikipinduka na giza likianza kuingia nitajua sitegemei kuokolewa hadi asubuhi.
 
Hivi RC, Msimamizi wa bandari Mwanza, RPC, DC, Kiongozi wa Zimamoto leo walipata usingizi kweli? huku roho za Watanzania zikiteketea ziwani? I cant imagine uongozi wa dizaini hii, na utasikia hakuna atakayewajibika.
Unajiuliza swali ambalo hauna jibu alafu unahitimisha kuonyesha walilala.
Unapojaribu kutafuta upenyo hapa ili uongeze political mileage lazima utakuwa na mtazamo kama wako.
 
Hapa kwetu wanakesha kwa mambo ya hovyo kama
Mkesha wa mwenge, Uchaguzi dhidi ya vyama pinzani wanakesha nk.
Uokozi wanataka break!!
 
Tuna helkopta zinaruka juu kulinda wateule,nchi jirani zina vifaa kedekede mf. Kenya. In a matter of hour or two, watakuwa wamefika site!! Kipindi cha Mkapa na MV Bukoba, kuna kikosi kilitoka Zenj na SA walifanya kazi day& night. Nashauri, pamoja na juhudi zote, tusitangulize visingizio vya giza!! Tuongeze juhudi na tuimarishe mahusiano mema na majirani zetu ili tunakotindikiwa tupate msaada. Mungu weka mkono wako katika hili.
 
Hapo wanebugi
 
Huyu RC angekuwepo mama yake miongoni mwa abiria sizan kama wangesitisha zoezi,,,,,,,na bado kile cha kigambon maana geti linafunguliwa watu wanaenda tu wote hakuna idad maalum
 
Hivi kwamfano malaika mkuu Gabriel Makufuli angekuwepo ndani ya hiyo meli sipati picha wale vikaragosi wake venye wangehangaika kumuokoa.
 
Tatizo zinajaza sana mkuu... Kuna siku nilipanda Mv Victoria kutoka Mwanza kwenda Bukoba...Ile meli ilikuwa imejaza hatari hata sehemu ya kukaa hamna.....
 
Kwa hiyo mtu akifa basi hana thamani? Yaani sijakuelewa kabisaaa!
 
Kuna kipindi wajukuu zetu watatamani kufukua makaburi yetu wapime hivi vichwa vya karne hii vinawaza nini...
 
Kwa hiyo mtu akifa basi hana thamani? Yaani sijakuelewa kabisaaa!
Sijamaanisha hivyo. Ila ktk zoezi lolote la uokoaji, maisha ya muokoaji ndio kipaumbele cha kwanza. Namaanisha mazingira ya shughuli hiyo ya uokoaji. Ilifika wakati kilichokuwa kinatolewa ni miili tu na sio watu walio na pumzi. Hivyo kama itafika muda zoezi likawa gumu kulisitisha ni wazo zuri. Halihusiani na wewe unavyosema uthamani wa mwili. Thamani iko pale pale. Hapa ishu ni zoezi la utoaji wa miili na sio uokoaji tena. Kuokoa binadamu maana yake baada ya kuokolewa basi bado ana pumzi. Mtu asiye na pumzi haokolewi. Unaokoa maisha.

Kuna kitu kwenye hii shughuli kinaitwa;
RESCUE vs RECOVERY.

In rescue, the team puts all efforts in hope that there is still life left AND in recovery, the team concludes that there is no life so even the mode of 'rescuing' is different.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…