laki si pesa.
JF-Expert Member
- Jul 14, 2015
- 10,003
- 9,755
Inawezekana...Meli zote zinakuwa na mstari wa usalama.ambao maji hayatakiwi yauguse huo mstari...maji yakiugusa inamaanisha uzito umezidi.. Tatizo ni stability.,,Meli ilikata kona vibaya/ ghafla hivyo mizigo ikahamia upande mmoja, ikakosa balance ikapinduka...1. Inasemekana kivuko kimefanyiwa ukarabati miezi kama miwili iliyopita kwa kuwekewa injini mpya za thamani ya milioni 190 ( kama sijakosea).
2.Tahadhari nadhani ambayo haijazingatiwa itakuwa ni uwezo halisi wa kivuko kubeba mzigo na mzigo halisi uliobebwa. Hata hivyo kuhusu uwezo wa kivuko unaweza kutupa elimu maana kwa jinsi ulivyokokotoa uwezo wa vivuko unaweza kutusaidia kivuko hiki kilikuwa na uwezo kiasi gani. Kwani kwenye pointi hii ulikazia kabisa kuwa " haiwezekani"!
3.Pia kitendo cha kutojua idadi kamili ya abiri haikubariki wakati siku hizi naona wanatoza nauli na kutoa tiketi za electronic. Lazima kumbukumbu ziwepo vinginevyo kuna udanganyifu mkubwa unafanyika.
4.Kuna uwezekano wa kuwa labda ni majanga ya asili, kwani kipindi hiki kumekuwa na upepo wenye kasi kubwa na wa kushtukiza. Hata hivyo(kama ajali hii imetokana na upepo) hii inaonyesha yawezekana hakuna ushirikiano wa kutosha kati Mamlaka ya hali ya hewa na wamiliki wa vivuko(TEMESA) ama wamiliki na makapteni wanapuuzia taarifa wanazopewa na wataalamu wa hali ya hewa.
6. Nimakosa kuingiza masuala ya kisiasa tena ambayo hayana ushahidi kwenye masuala ya majanga kama haya. Vinginevyo, ieleweke kuwa unakusudia kuhujumu utawala sa serikali ya sasa kwa kuigombanisha na wananchi kwa malengo " maalumu". Kama huna lengo hilo jitahidi kukwepa kutumia maneno yanayoweza kuashiria hilo.
===
Inauma sana taifa kupoteza watu wake kwa namna hii.