"TUJITEGEMEE, post: 28457702, member: 31026"]1.
Tahadhari nadhani ambayo haijazingatiwa itakuwa ni uwezo halisi wa kivuko kubeba mzigo na mzigo halisi uliobebwa. Hata hivyo kuhusu uwezo wa kivuko unaweza kutupa elimu maana kwa jinsi ulivyokokotoa uwezo wa vivuko unaweza kutusaidia kivuko hiki kilikuwa na uwezo kiasi gani. Kwani kwenye pointi hii ulikazia kabisa kuwa " haiwezekani"!
Mkuu ninajitahidi sana kuepusha malumbano na wewe , kwa hili naomba kwanza usome habari nii
"sifi leo, post: 28448625, member: 75839 ;Kivuko cha MV. NYERERE kilinunuliwa na kuanza kutoa huduma mwaka 2004. Kilifungwa injini mbili mpya zenye thamani ya shilingi milioni 191 JULY 2018. Kivuko cha MV. Nyerere kina uwezo wa kubeba tani 25 sawa na abiria 100 na magari 3 kwa wakati mmoja.
[Habari ipo mwanzoni kabisa mwa bandiko(rejea bandiko namba 1), sijaitafuta mahali na wala sijasema imetoka mamlaka yoyote.Nimeangalia uhalisia wa mtoa taarifa hiyo
Nikasema hivi, kivuko kina uwezo wa tani 25 kwa mujibu wa mtoa mada hapo juu
Kina uwezo wa kuchukua watu 100 na magari 3, kwa mujibu wa mtoa mada hapo juu
Kisha nikafanya tathmini yangu kwa kutumia namba hizo.
Nikakifanya assumptions,wastani wa uzito wa abiria ni Kg 70,abiria 100 ni kilo 7,000 au tani 7
Nikauliza, magari 3 yenye uzito gani?uzito wa saloon, Van, truck n.k. vinatofautiana.
Kisha nikafanya assumption ya tani 4 kwa magari 3 ni sawa na tani 12
Ukijumlisha ni sawa na 7+12 ambazo ni tani 19, chini ya tani 25
Namba alizoweka mleta mada(bandiko 1) kauli ya `tani 25 ni sawa na watu 100 na magari 3 ina waakini, ndipo asili ya neno haiwezekani, namba hazikubali nikimjibu mleta mada
Soma bila prejudice uelewe nini kinazungumziwa.Nasema prejudice kwa sababu hii uliyoandika
Nimakosa kuingiza masuala ya kisiasa tena ambayo hayana ushahidi kwenye masuala ya majanga kama haya. Vinginevyo, ieleweke kuwa unakusudia kuhujumu utawala sa serikali ya sasa kwa kuigombanisha na wananchi kwa malengo " maalumu"
Wapi kuna siasa katika hayo niliyoeleza hapo juu?
Kama tathmini yangu kwa mleta mada si sahihi mambo unayosema yanaingiaje?
Unaposema ninahujumu una maana gani, sijasema lolote kuhusu mamlaka yoyote kutoka namba zilizowekwa na mleta mada. Nilichofanya ni kumjibu mleta mada
Dhamira yako si nzuri hasa unaposema kuna lengo la kuchonganisha wananchi au malengo maalumu, umenisikitisha. Unaeleza kitu kisichokuwepo kwa prejudice.
Unachukua maneno ``out of contents and context just to suit you ill intention``
Chuki hii inaletwa na nini! Kwa asiyefuatilia au kusoma details za hii mada, kauli zako ni za hatari,naichukulia serious. Nimejifunza ,ume clear doubt.Nimethibitisha shaka niliyokuwa nayo
Kwa muda nimejiepusha katika mijadala na wewe,naomba radhi kukujibu nimelazimika kutokana na kauli zako hatarishi kwa maisha ya mtu.
Hata hivyo nashukuru kwa kunitahadharisha,wachache wanapata bahati hii ya kuonywa
Kama una reservations nyingine it's ok usitumie hili ku infiltrate na kutengeneza `mazingira` Nadhani utafurahi sana nikipatwa na majanga ya aina yoyote ile. Hii ni serious