Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Hivi boti za doria za polisi na JWTZ hazina taa, mbona zina tochi kubwa kwa juu zenye uwezo wa kumlika zaidi ya mita 200.

Hizo boti zipo ni juzi tu tulitangaziwa kuwa serikali imenunua boti za doria za kisasa na kupelekwa ziwa Vitoria na zanzibar.

Kuwa na hizo boti (kuzimiliki) ni jambo moja, ni jambo jema. Lakini je, hiyo jana zilikuwepo site ? Kama hazikuwepo (kwa sababu yoyote ile) zoezi lisingeweza kuendelea. Uwezo wetu wa kukabiliana na majanga bado uko chini, Mungu saidia leo kiza isiwe ni kikwazo maana bado muda upo wa kupeleka kila aina ya vifaa ili ku "improve the methods"
 
Hatukujifunza kwa MV Bukoba kosa lilelile linajirudia, vikosi vyetu havina maandalizi mazuri. Sisi tuna maziwa tuna bahari tuna mito, tunajua ajari kama hizi lazima zitatokea kwanini tusiimarishe vikosi vyetu vya uokozi?

Katika karne hii bado tunasingizia giza, ingekuwa vita tungesitisha sababu ya giza, siku hizi kuna vifaa vya kuona gizani (night vision goggles) nafikiri lazima jeshi linazo.
 
Tunaachaje kuilaumu serikali ?!, pale kuna wasimamizi ambao ni watumishi wa hiyo serikali, na wanalipwa mishahara ambayo ni kodi zetu, kama wamekaa tu wanaangalia watu wanapanda bila Control hii ni failure government, Bernard Membe alisema hii serikali imefeli mapema kabisa, serikali ndio msimamizi na ina vyombo vya ulinzi, (Polisi na migambo ambao kazi yao huwa ni kupiga wapinzani)
 
Ila watanzania lazima ukubali uzembe wetu sisi kama raia. Nimeshangazwa ma picha hiyo hapo juu ya raia waliangalia na caption yake inasema RAIA WAKIWA MITA CHACHE TOKA ILIPOZAMA BOTI. Tujifunze kuogelea, idadi zitapungua ingawa najua kuna mida kunakuwa ma panick ktk ajali.
 
Hata enzi za serikali ya akina Benard Membe, kivuko hiki kilikuwapo na kilijaza watu.
 

Mkuu naomba nikujibu kwa ufupi tuu uelewe majanga yote yanatokea katika mazingira magumu na ndio maana waokoaji wanasomea sio kila mtu anaweza kuokoa iwe majanga ya maji au moto.

pili umeongelea huwezi kuhatarisha maisha ya walio hai kwa ajili ya uokoaji hiyo haipo na umezungumzia duniani sijui ya wapi hiyo dunia...waokoaji wengi wanahatarisha maisha ndio maana hata unaona wanafanya kazi ya hatari ili kuokoa maisha ya walioathirika huko wiki iliyopita waokoaji wawili walikufa SA gorofa ya nane baada ya kwenda kumuokoa mtoto ambae alipona kule Thailand waokoaji waliwaokoa wale watoto kwenye mazingira magumu muokoaji mmoja alifariki kwa kukosa hewa ya oxygen ila watoto wote walipona na ndio maana waokoaji wapo katika jeshi la Zimamoto katika Nchi zilizoendelea...
 
Yani wewe jamaa
Yan kuku tu vitoto wake wakinyeshea mvua atawafunika kwa mbawa zake hata anaeeza asitoke kwenda bandani
Je binadam
Unaanzisha usafiri wa majin afu hujui kama kuna majanga?
 
Kweli inasikitisha vyombo vya usalama kwenda kulala huku watanzania wanaangamia wameshindwa kufanya kazi hata kwa shift?? Kwa technolojia ya Leo ni aibu kusema eti kuna Giza , so sorry kwa wafiwa
 
Daah afu linatokea lijitu ambalo vivu la kufikia na kusema wanaoishi Dsm wanapoteza muda wakati maisha ya mikoani yana risk sn hasa inapotokea maafa makubwa
 
Ndiyo matunda ya Absolute power, Tume kufuru ya uchaguzi, kufurahia uonevu na ukatili wa vyombo vya Dola dhidi ya raia wasio na hatia.
 
Hakika wewe ni mwendawazimu kuu walahi
 
Vifaa vya uokozi lazima ziwe standby hujui ajari itatokea lini na wapi, boti za doria zinafanya kazi 24hrs, nyingi ziko Mwanza jijini, kwa speed za boti hizo kutoka Mwanza hadi kisiwa cha Ukara sidhani itatumia hata nusu saa, afterall ajari imetokea saa 8 kulikuwa na uwezekano mkubwa wa kufika pale mapema na kuanza maandalizi ya kukabiliana na giza kwa kuandaa taa.

Mbali na boti za polisi za doria kuna helikopta za polisi na jeshi zisingeshindwa kufika pale na kumulika wakati zoezi likiendelea. Ni uzembe fulani tu umefanyika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…