Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

DW: Idadi ya waliokufa baada ya kuvuko cha MV Nyerere kuzama katika eneo la Ziwa Victoria mkoani Mwanza nchini Tanzania imeongezeka na kufikia zaidi ya 100. Jitihada ya uokoaji zimeendelea tena leo baada ya kusitishwa kwa muda jana usiku. Kutoka katika eneo la Busia. Mwenzetu Sudi Mnette amezungumza na mwandishi wa habari Jovitha Kaijage aliyesema kuna wasiwasi wa kuongezeka kwa idadi ya vifo.
 
Huko ni kwetu na nilipanda kivuko hicho mwaka Jana mwezi wa 9. Tulikua abiria zaidi ya uwezo wa meli. Niliongea na captain na tukajenga urafiki huku nikimweleza juu ya jambo hili. Kibaya zaidi nimesoma karibu na Bugolora Alhamisi abiria na mizigo kuelekea Ukara huwa utitili. Serikali inajua vyema lakini wao hujikita kwenye mapato kuliko tahadhali ya kupoteza maisha ya watu. Mungu iumbe upya Tz. CCM inatumaliza na kututeketeza bila mapenzi yako.
 
Yaani hata mm nimeshangaa sana hii nchi sjui tulilogwa na nani??
 
Mkuu kumbuka pia na habari ya mbunge aliyetolea ufafanuzi bungeni swala la hicho kivuko
Acheni hizo chanzo cha ajali ni kuelemewa kwa kivuko kivuko cha watu 100 kikabebe zaidi ya watu 200 na mizigo unategemea nini?
 
Watu wanacheza Mpira usiku we unasema hamuwezi kuokoa watu wana kufa na maji uck kucheza mpira na kuokoa maisha ya watu bora nn
 
Funny Enough mwezi huu wakaji Magufuli anazindua ujenzi wa meli mpya nilimsikiliza mwanzo mwisho.

Yule mkurugenZi wa mambo ya usafiri majini alikuwa kaimu na rais kamfanya awe kamili hapo hapo.

Rais aliwalaumu sana kwa uzembe na aka quote ule uzembe wa mv bukoba.

Rais alikuwa anaongea kwa uchungu sana tena sana.

Na akawaagiza waanzishe tiketi za electronics.
Aliwaambia anajua wanayoyafanya na aliwaasa waache upuZi na ujanja ujanja.

Nina uhakika kwa research yangu niliyoifanya. Tiketi zilizouzwa kihalali zilikuwa ni 70. Na magari mawili na mizigo basi.

Ila kivuko kilibeba watu zaidi ya mia nne.(imagine kivuko kina uwezo wa kubeba watu 101 ila wamezidi watu miatatu).

Tiketi zingine wahudumu walipiga pesa kwa ujanja ujana pamoja na kwamba rais mwezi huu aliidhinisha pesa za mishahara yao.

Jiulizeni walikaa zaidi ya miezi kumi hawalipwi mishahara sasa walikuwa wanaishije?

Ndio upumbavu kama huu.

Nashauri hawa jamaa wanyongwe.


Uzembe unaanzia kwa mkuu wa mkoa kushuka chini.
Wote ni wazembe askari wote walikuwa wanaona jinsi wananchi wanavyojazwa kwenye kivuko.

Shiriki la usafiri majini linasema eti haijulikani watu wangapi walikuwa kwenyw kivuko hicho.
Hili ni jibu kutoka kwa wataalamu ambao wamesoma na wanasimamia rasilimali zetu.
 
Kwa kweli hawa wahusika wa kivuko ni wahuni sana.

Haiwezekani meli yenye capacity ya watu 100 ibebe watu zaidi ya 400.

Ukijaribu kuwaelimisha watakwambia katengeneze meli yako upande ujinafasi.

Hata kwenye madaladala watu wanajazwa nyomi kama siafu.

Kila kitu shithole.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…