Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Yaani tunasikitisha kama taifa na bahati mbaya sana hatua zozote za tahadhari huwa ni za muda mfupi tu baadaye zinaisha mfano baada ya ile meli iliyokuwa inaenda zenji kuzama kuna baadhi ya vitu vilivyofanyika kama kutoa elimu kupitia TBC na vyombo mbalimbali vya habari juu ya nini cha kufanya ikitokea ajali pamoja na kuvaa life jacket lkn baada ya muda hatukuoni tena, la pili baada ya chuo cha Kenya kuvamiwa na alshabab kuna hatua za kiusalama zilichukuliwa kwenye baadhi ya vyuo za ukaguzi kwa wanaoingia na kutoka na tahadhari kadhaa lkn Leo hazipo unaweza kuingia na kutoka bila kuulizwa chochote

Yaani mipango yetu siyo endelevu kana kwamba janga likitokea ndiyo halirudi tena nadhani ni wakati viongozi wakabadilika na kuweka mipango ya kudumu ya namna ya kukabiliana na majanga na siyo kuwa na mipango ya muda mfupi tu maana tunapoteza watanzania wenzetu wengi sana watu 100+ ni wengi sanaa
 
Pia alie kuwa kiongozi wa bunge siku mbunge wa Ukerewe alipo uliza swali akajibiwa utumbo kwa sababu za ijinga na ushabiki wa kipimbavu wa wabunge wa Ccm nae aachie ngazi.
Ki uhalisia Ccm na serikali yake wanatakiwa kulaaniwa kwa hili tatizo
Kila ALIYESHIRIKI,kamaule mfano wako wa mbunge kujibiwa kipumbavu katika hali ya kishabiki aliyekuwa kiongozi naye pia AWAJIBISHWE.
Nchi hii si nchi ya CHAMA fulani bali ni Watanzainia wote pasipo kujali vyama vyao.
Nakubalianan nawe kuwa kila mtu na msalaba wake.
 
Sii ajabu ukakuta Maccm wamevaa ma nhuo yao ya kijani kwenye uokoaji ili hali mbunge alisha piga kelele kuhusu hili jambo akajibiwa walivyo weza kujibu.. Mungu ana waona Ccm
 
Ni sawa ila unapokuwa na mfumo ambao watu wake hawajajiandaa na majanga, pindi linapotokea hata akili ya kujiongeza hawana!! Na tatizo kubwa pia ni kutegemea vivuko vya abiria ndio vitumike, kwani vingi viko mwanza na kutoka mwanza hadi huko ni parefu na vingi unakuta viko kwenye safari zake!!! Ila waambiwe kuna magendo ziwani, utaziona zile boti za kwenye movie
 
Eti macho yake yako Hulu ..!?
Mpka leo ningetarajia ameshafika huko
 
Ni kawaida maraisi kutoa pole

Lakini kwanini hatujifunzi kutokana na makosa
Doria kwenye maji hakuna? Na uokoaji hakuna
Ajali za barabara zisizoisha na majini tukio linatokea hatujiulizi tunakosea wapi na hatua stahiki hazifuatwi

Hao waliofiwa hata wapewe nini haitasaidia
Maadamu bado wasimamizi wetu wapo ofisini bila kufukuzwa au kujiuzuru bado napinga kuwa our system stinks
 
Hakuna kujiuzulu Bashite kashindwa kujiuzulu itakuwa wa Uchukuzi mtakuwa mnamwonea jamani
Hapa hamna cha Bashite ama ndugu ya Bashite tunachokizungumzia hapa ni KIKUU sana kuliko hicho unachokizungimza.
Haya ni MAISHA ya watu mamia WALIOKUFA sababu ya UZEMBE!.
Watu wakae ofisini wakifanya nini?
 
Ilizama Mv Bukoba,Spice Island na vyombo vingine vingi,mawaziri hawakujiuzulu au kufukuzwa kazi,kwani wafukuzwe sasa?.
Tusitafute short cut,tatizo la ajari za majini ni kubwa mno linataka ufumbuzi wa kudumu.
Ukiangalia kwa undani linaanzia ubora wa chombo tokea michoro yake,usimamizi wa ujenzi wa chombo,utoaji wa leseni ya chombo na leseni za waendesha chombo.
Hili jambo ni la kitaalamu zaidi,tuwape wataalamu wenye vigezo na uzoefu uliotukuka walishughulikie kwa kina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…