Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Walisema kina uwezo wa watu 100
Sasa maiti 126 + zaidi ya 40 waliookolewa
 
Mtu anasemwa live na mkuu wake lakini kagoma kujiuzulu; sasa itakuwa hili ambalo halimhusu mtu directly.

Kujiuzulu ni utamaduni wa watu waliostarabika; sisi bora kumekucha.!!
Sisi bora kumekucha ni kweli. Lakini ni lini Tanznaia tutakapostaarabika?
 
Kuhusu TBC kujiunga mubashara waoneshe nini sasa ? Ki ubinadamu sio sahihi.mi nimeona clip za ile miili whatsapp sio busara kuionesha kwenye TV
 
Haya ni maajabu sana, kwa hiyo mkata tiketi naye alikuwa ndani na kaefd machine yake. Huku nchi kavu hakuna data iliyobaki?? Kweli tunaishi stone ages..


Imagine dunia ya sasa with all up to date techno, sisi bado hata kuweka data za namba ya idadi ya wasafiri hatujaweza.

Halafu usafiri kama huu usiokuwa na uhakika wa usalama wa maisha ya watu.
We're talking about human lives, kitu kilichotakiwa first priority.
Lakini ona jinsi mpaka mkuu wa mkoa ana jikanyaga tu. He has no idea about anything.
 
Wanaoleta siasa ni ccccccm, unawezaje kusitisha uokoaji eti kwa sababu ya giza, halafu mnategemea watu wanyamaze, Nyambafu.
 
Lowassa hakujiuzulu kwa sababu ya MIKASA katika utendaji wake bali utofauti WA kiituikadi na chama chake cha zamani cha CCM.
Ukweli ni vizuri usemwe.
Huwezi kulinganisha janga hili na KUJIUZULU kwa Mh, Lowassa
 
Uzembe wa kusitisha uokoaji jana japo inasemekana iligubikwa na ukosefu wa vitendea kazi umenisikitisha sana.

Nina imani kuna wapo wangeokolewa wakiwa hai hata kama wangekuwa mahututi.

So sad!!
 
Kwa Wamarekani kukitokea janga kama hili huwa muda wote vyombo vya habari vinatumia muda mwingi kutoa upadate ya tukio na sio kupiga KIOKOTE!
 
Yuko live.
-Anasema taarifa aliyopewa ni kuwa hiyo meli inaweza beba watu 100 na tani 25. Ila ilizidisha watu.

-Pia ilipakia mahindi magunia mengi na makreti ya bia na soda na vifaa vya umeme pamoja na gari/ magari.

-Ilikiwa ni siku ya soko alhamis hivyo na abiria walikuwa wamebeba mizigo, hivyo ni wazi ilizidisha uzito.

-Pia anasema inasemekana aliyekuwa anaendesha yawezekana sio kapteni mwenyewe, hivyo ameagiza wote wakamatwe. Pamoja na kapteni na watendaji wa kivuko wakamatwe na shughuli za upelelezi ziendelee.

-Pia amemuagiza waziri mkuu kuunda tume ya uchunguzi juu ya hii ajali.
Ataka wanasiasa wasichukulie hii kitu kisiasa.

Mwisho ametoa pole kwa wafiwa wote.
 
Serikali haikuleta tetemeko/kuzama kivuko! Huyo eti ni kiongozi. Ilibidi kuomboleza angalau kwa leo!
 
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, naangalia TBC leo wameweka ni maombolezo wakitupa habari ya kinachoendelea. Sasa hivi saa moja na dakika tisa Raisi anaongea kuhusu ajali
 
TBC wameweka nyimbo za maombolezo kwenye hili usiwaonee.
Hapa nipo namtazama Rais, anasema miili ni 130+ kwa sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…