Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Dalili zimeanza kuonesha, baadhi ya Wanasiasa kudai watu flani wawajibike,wajiudhuru, mawazo ambayo yako kisiasa zaidi, ni kweli ipo sababu iliyopelekea kutokea ajali hiyo mbaya, sababu zinaweza kuwa ni za uzembe wa kibinadamu,au za kitaalamu(mechanical problems), hivyo kwenda moja kwa moja kwenye(human error) tutakuwa hatuwatendei haki wataokumbwa na sakata.

Itakuwa kisiasa zaidi, hivyo kabla ya yote Mashauri uchunguzi wakina ufanyike, isije kutokea kama ile ya Muhimbili kupasua kichwa badala ya mguu na mguu badala ya kichwa, maamzi ambayo yalipelekea kuwapoteza !adakitari bingwa wa mifupa na wenye uwezo mkubwa, ambao Mara moja Botswana iliwachukua hadi leo wanafanya maajabu huko.

Ikumbukwe mfano Prof. Kinasha alieleza kwamba alikuwa ameshafanya upasuaji wa kichwa kwa watu 1,008 na wote walipona, na huyu ambaye ni bahati mbaya alikuwa wa 1,009. Sasa akahukumiwa kwa kosa moja tu !!!!

Hii ilikuwa kisiasa zaidi ikiongozwa na Prof. Mwakyusa, Sikatai kuwa uzembe ni mbaya na unaweza kugharimu maisha ya watu, jambo ambalo kamwe halikubaliki wala kuvumilika.

Lakini pia sikubaliani kuona kuwa watu wanaadhibiwa kwa mintarafu ya kisiasa, watu kutafuta kiki za kuonekana na jamii kwamba wamechukua hatua. Ajali hutokea kokote kule hata Ulaya na marekani, mfano Nyambizi ilizama, je nani aliwajibishwa?

Ndege aina ya Conctord iliua watu kibao je nani alifukuzwa kazi? Tusilione limetokea hapa kwetu, sasa ukawa muda wa wanasiasa kuishutumu Serikali nakuitaka kufukuza watumishi wake kwa madai kwamba wamefanya uzembe.

Kikubwa hapa ili Wanasiasa waoneshe kukomaa kwao wanatakiwa kuitaka Serikali kufanya uchunguzi wa kina juu ya sababu zilizopelekea ajali hii mbaya. Huu ni Ushauri tu na si vinginevyo.

Unahitaji uchunguzi gani kwa sababu ambazo ziko very clear mkubwa??

Capacity ya kivuko ni kubeba:

• Abiria wasiozidi 100 tu

• Tani za mizigo zisizozidi 25 tu

• Magari madogo yasiyozidi matatu 3 tu

Hebu cheki sasa kinachoripotiwa:

- Eti kivuko kilibeba abiria zaidi ya 500!!!
- Mizigo zaidi ya tani hizo za uwezo wake!!
- Magari makubwa badala ya madogo!!

Sasa ni uchunguzi gani zaidi unaohitajika hata kutumia pesa kwa mambo ambayo yako so open?

Hivi ktk mazingira kama haya utawezaje kuzuia watu kuusema ukweli kama huu ulio wazi kabisa?

Utawezaje kuzuia watu kusema kuwa ilishindwa kuokoa uhai wa watu waliokuwa wakizama mita zisizo zidi 200 kutoka nchi kavu eti kwa sababu ya Giza??

Kuna siasa gani hapa?? Hakuna siasa lakini hii ndiyo reality kuwa kama taifa kuna shida ktk eneo la uokozi na hatujajifunza na nadhani kuna tatizo ktk priorities zetu!!

Whether we like it or not, serikali na viongozi wake ndiyo hasa wanaotaka kulifanyia siasa jambo hili eti kwa kuzuia watu wengine tusiseme kuwa kuna tatizo somewhere!!
 
Yaani hadi leo eti bado wameendelea kukaa kwenye ofisi za umma wakijiita watumishi, sijui wanamtumikia nani hadi leo raisi anatoa agizo bado wako tu kimya. Wahukumiwe kuua hawa watu
 
Mwanza kuna polisi wanamaji, walikuwa wapi wakati chombo kinajaza kuliko uwezo wake. Ninja Lugola anapaswa kumwajibisha RPC au ajiuzulu.
 
Nilitegemea kwa wakati huu KUB Mbowe angekuwa kisiwani Ukerewe kujumuika na mbunge wa jumbo hill ambaye ni wa Chadema pamoja na timu nzima ya viongozi wa serikali na vyombo vya dola. Kwanini Mbowe kamuacha mbunge wake akiwa mpweke katika wakati huu mgumu!
Kwani ndiye wliyekuwa anasubiliwa kupeleka mwanga ili zoezi la uokoaji liendelee?
 
POLE MIMI MTANZANIA POLE WATANZANIA WENZANGU POLE UKARA .
 

Attachments

  • tanzania.jpg
    tanzania.jpg
    1.1 KB · Views: 20
Mmeambiwa msiba huu usitumike kisiasa na rais so tuomboleze kwanza kwa ajili ya ndugu zetu waliokufa kwenye msiba
 
INAUMA SANA SANA SANA ! Ilishindikana kuleta diving equipment kutoka Dar na Zanzibar ziletwe kwa ndege na zipelekwe Ukara kwa helikopta? Mawaziri na viongozi wengine akiwemo IGP wapo eneo la tukio. Hizo ndege zilizowaleta zingeshindwa kupeleka vifaa vya uokozi kwenye eneo la tukio? Na kama mchangiaji mwingine alivyosema ni kweli ilishindikana kutafuta taa ili uokoaji uendelee usiku?
Tanzania ina viongozi vichwa pumbu sana" kwa hiyo walipanda ndege na kwenda wao kama wao kwenye tukio pasipo kujiongeza kubeba vifaa " .... walikuwa wanataka kwenda kuwa shuhudia watu wanavyozama" sindio tunavyoweza kusema au ""?
 
Ndugu wanabodi:
Hivi sisi Watanzania nano katuloga? TBC na vyombo binafsi vimeshindwa kujiunga mubashara kwenye shughuli ya uopoaji maiti lakini hats kupiga nyimbo za maombolezo imeshindikana kweli?

Nimesema shughuli ya uopoaji kwa sababu serikali ingekuwa serious na maisha ya Watanzania wenzetu ingepeleka jenereta jana ili shughuli ya uokoaji iendelee Jana usiku.

Watanzania zaidi ya 126 ni msiba mkubwa wa taifa lakini radio na luninga ya taifa wameshindwa kujiunga mubashara hatua kwa hatua badala yake wanaendelea na mambo yao yasio na maslahi kwa Taifa.

Naamin kwa Wazungu habari ingekuwa ndio hiyo kuwa mubashara muda wote kwa kila kituo cha luninga na redio.Na wasingekubali kusitisha shughuli ya uokoaji eti kisa giza

Tumeshindwa kuthamini uhai wa wenzetu, kweli ngozi nyeusi ni wabinafsi haijapata kutokea
Kaka kabla ya yote kulaumu emb angalia ishu ya kufungia Local channels kutoonyeshwa kataika hizi decoder za AZAM na DSTV.. imeathiri vip matangazo yao? na hapo naona ni figisu tu,,, ili TBC wapate tenda za kutangaza matangazo ya private broadcasters mie naona kama WAMESUSA tu

MTAZAMO binafsi
 
Eti nchi iko salama,

Makonda na jamaa zake wameruka juzi kwa waitara na kura feki wee!!

Kisa wao kwa akili zao chadema ndio inahatarisha uhai wa watanzania....

Kisingizio cha hovyo kabisa na mibunduki yao,

Amani gani watu 400 wanapanda meli ya kubeba watu 100?

Walikuwa wapi? Mbona taarifa za kuzuwia mikutano ya maalimu sefu huwa wanahabarika siku moja kabla nakuzuwia????????? Vipi wasitumie intelijensia hiyo hiyo kubaini hilo tatizo!
 
Back
Top Bottom