Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Nackia leo nisiku ya mnada huko kwaiyo itakua ilijaza sana
 
Hawajapata idadi kamili ya watu waliokuwemo?kwani hicho kivuko ni sawa na daladala la kariakoo ambalo watu hupanda tu?
 
Ukerewe wanahitaji meli kubwa bajeti ya kurudia uchaguzi ielekezwe huko katika miundombinu
Kwani kurudia uchaguzi ni bei gani.na kununua kivuko kipya ni bei gani?
Mbona unatuchanganya.tuache kwanza tuna huzuni.[emoji30] [emoji30] [emoji30]
 
Unaambiwa wamezama halafu unasema Mungu awanusu

Ingawa haturidhishwi na hizichaguzi bado hii inabaki kuwa ajali kama ajali zinginelabda tupewe taarifa tofauti ya uzembe
Kwanza Muulize kwa nini anamtaja taja Mungu kwa sababu ya uzembe wa watu
 
Taarifa nilizozipata haraka sasa hivi ni kuwa watu wengi sana wanahisiwa kufa maji baada ya kivuko kubinuka juu chini, chini juu katika kisiwa cha UKALA wilayani Ukerewe.

====
Taarifa Kwa Umma Kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme-TEMESA Kuhusu Kuzama Kwa Kivuko Cha MV.Nyerere

View attachment 872340

Kivuko cha MV Nyerere kinachofanya safari zake kati ya Bugorara na kisiwa cha Ukala katika ziwa Victoria kimezama huku taarifa za idadi ya watu waliokuwemo ndani ya kivuko hazijajulikana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jonathan Shana amesema kivuko hicho kimezama wakati kikielekea katika Kisiwa cha Ukara. Kiliondoka saa 6 mchana na ilipofika saa nane kamili mchana kilipinduka.

Amesema bado hawajapata idadi kamili ya waliokuwemo kwenye kivuko hicho.

Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa), Hassan Karonda amekiri kuzama kwa kivuko hicho na yuko njiani kulekea huko na watatoa taarifa baadaye.

Kivuko cha MV. NYERERE kilinunuliwa na kuanza kutoa huduma mwaka 2004. Kilifungwa injini mbili mpya zenye thamani ya shilingi milioni 191 JULY 2018. Kivuko cha MV. Nyerere kina uwezo wa kubeba tani 25 sawa na abiria 100 na magari 3 kwa wakati mmoja.

View attachment 872299
Wanajeshi na raia wakitoa msaada wa uokoaji​
Hiki kivuko ni kidogo, wapeleke vivuko vikubwa kama mv.Sengerema , hako lazima kayumbe kwenye dhoruba
 
Kwa taarifa za mtu wangu wa karibu ananiambia kivuko hubeba watu zaidi ya 500 pamoja na magari ...
najaribu kuimagine
 
ni serikali ndugu sio ya mtu binafsi, sasa utamfunga nani hapo

U ndumila kuwili ndiyo tunaoupigia kelele tunapokuwa tunaomboleza matukio kama haya.

Haki bin haki pekee ndiyo inapaswa kutamalaki. S
ni serikali ndugu sio ya mtu binafsi, sasa utamfunga nani hapo

Mkuu kinachogomba ni huu u ndumila kuwili tunapokuwa tunaomboleza matukio kama haya.

Kinachopaswa ni haki bin haki hakuna mtu anataka au kuombea ajali si serikali wala mtu binafsi. Ikitokea hivi mtu binafsi korokoroni, serikali aah aah makengeza yanaingia.

Haki si mpaka mbinguni tu hata hapa duniani yawezekana. Onyesheni japo utashi basi tuone mko pro haki?

Cc: massabuni
 
Idadi kwanini isijulikane ina maana hao Abiria huwa hakuna record yoyote inayobaki ofisin wakati kivuko kikiwa safarin?
je hakuna tikets? Africa kila siku uzembe uzembe
 
Kwanini watu wafe?? Wakati kuna maboyance?
Mungu awapumzishe wote waliopoteza maisha yao.
 
Mungu awape pumziko la amani wale alioona inafaa kutangulia, nao majeruhi Mungu awafanyie wepesi wapone haraka ili warudi kuendelea na majukumu yao ya kila cku
 
Taarifa nilizozipata haraka sasa hivi ni kuwa watu wengi sana wanahisiwa kufa maji baada ya kivuko kubinuka juu chini, chini juu katika kisiwa cha UKALA wilayani Ukerewe.

====
Taarifa Kwa Umma Kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme-TEMESA Kuhusu Kuzama Kwa Kivuko Cha MV.Nyerere

View attachment 872340

Kivuko cha MV Nyerere kinachofanya safari zake kati ya Bugorara na kisiwa cha Ukala katika ziwa Victoria kimezama huku taarifa za idadi ya watu waliokuwemo ndani ya kivuko hazijajulikana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jonathan Shana amesema kivuko hicho kimezama wakati kikielekea katika Kisiwa cha Ukara. Kiliondoka saa 6 mchana na ilipofika saa nane kamili mchana kilipinduka.

Amesema bado hawajapata idadi kamili ya waliokuwemo kwenye kivuko hicho.

Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa), Hassan Karonda amekiri kuzama kwa kivuko hicho na yuko njiani kulekea huko na watatoa taarifa baadaye.

Kivuko cha MV. NYERERE kilinunuliwa na kuanza kutoa huduma mwaka 2004. Kilifungwa injini mbili mpya zenye thamani ya shilingi milioni 191 JULY 2018. Kivuko cha MV. Nyerere kina uwezo wa kubeba tani 25 sawa na abiria 100 na magari 3 kwa wakati mmoja.

View attachment 872299
Wanajeshi na raia wakitoa msaada wa uokoaji​
Hapa naona nikatika hali ya kutoa watu kwenye mada ya uchanguz sasa aya matukio sielewi elewi iv maana du bt poleni watanzania wenzangu
 
Back
Top Bottom