Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Siasa zile zile za kiafrika, zilizojaa malalamiko. Inapopitishwa bajeti ya mawasiliano na miundo mbinu wabunge wanatoka nje na kupinga.

Mungu kwa unyenyekevu mkubwa liondolee ujinga bara la Afrika, limeteseka na kuendelea kuteseka.
 
Ndio maana Waafrika tunazarauriwa sana na kuonekana ni Binadamu wa ajabu katika karne hii. Pole sana.
Pole jipe wewe kila jambo ujuaji tu,acheni watu wafanye kazi, report itolewe kuhusu source ya ajali ndo tuisurubu,sasa uokozi unaendelea mnaiiimba ka kasuku
 
Siasa tu hapa unafanya ,lisingetokea hili ungesema nn!.ujuaji for nothing
Sio hili tu, yapo mengi yanakuja na yataendelea kuja kwa sababu maisha yetu yanafanyiwa maamuzi na wanasiasa. Hivi ni leo wewe umesikia watu wakipigia kelele suala la vipaumbele vya nchi? Hakika wewe ni mwanasiasa ama mnufaika wa kisiasa, Huna hata chembe ya huruma.
 
Pole jipe wewe kila jambo ujuaji tu,acheni watu wafanye kazi, report itolewe kuhusu source ya ajali ndo tuisurubu,sasa uokozi unaendelea mnaiiimba ka kasuku
Nahisi upo kitengo cha maafa wewe, muda mrefu hamjabeba maiti, naona umefurahia kweli kweli. Unaona raha kuokoa maiti hee! Hizo huopolewa ndugu
 
Siasa zile zile za kiafrika, zilizojaa malalamiko. Inapopitishwa bajeti ya mawasiliano na miundo mbinu wabunge wanatoka nje na kupinga.

Mungu kwa unyenyekevu mkubwa liondolee ujinga bara la Afrika, limeteseka na kuendelea kuteseka.
Asnte Bukililo kwa maelezo mafupi fasaha,wamekazana na tu thread mwanzo mwisho,wanaishi kwa matukio,ama kweli ukistaajabu ya musa ,ya firauni........
 
Hivi hatuna Jeshi la majini (Navy)?? Inamaana tungevamiwa na mmoja wa majirani zetu kwa upande wa ziwa victoria tungeambiwa hivyo?? Yaani giza na vifaa maalum?? Kwa kifupi serikali yangu imechoka wamebakiza nguvu kidogo kwajili yakupambana nq wanasiasa wa ndani hasa wapinzani wa jiwe.
 
Nimesikiliza clouds fm jioni....nimekuta ile songi lao. "Do you want the beer" yees....

Afu kuna ile......acha safari iendelee kwa buku hizi tu....kwa buku mbili tu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Makada wa CCM humu JF huwa mnatia huruma, yaani mpo busy kusifia rambirambi za Putin badala ya kufunika uso kwa aibu ya utendaji kazi mbovu wa serikali yenu. Mbunge wa Ukerewe alishatabiri haya na kuomba kivukio kirekebishwe lakini mkaziba maskio....

Mm sio kada wa ccm.. But alivyoongea huyo kivuko kilirekebishwa.. Hapo maybe hawajarekebisha vizur.. Au watu walizid sana kweli.. Ambayo pia ni uongozi mbovu wa meli.. But overall serikali imezngua ..on tht picture u can see new engines.. So myb waliweka vibaya.. Au watu walizid.. Kuna uzembe flan. Inabid tusiufungie macho
IMG_20180921_172452.jpg
 
Poleni wana Mwanza , Poleni ndugu na jamaa.

Raisi ametoa salamu za pole na kutangaza siku nne za maombolezo ikiwa ni pamoja na kupeperusha bendera nusu mlingoti.
Watu wengi wamekua wakiuliza kama siku hizo nne ni mapumziko ya kazi ?
Kama kuna mwnye ufafanuzi juu ya hilo basi awasaidie wadau.
 
Sijafurahishwa kabisa na lugha unayoitumia;
Eti viongozi wetu wanafurahi watu kufa ukisema eti waamuru bendera kukpepea nusu mlingoti na maneno mengine machafu machafu ambayo hayafai kamwe kuandikwa mitandaoni, nikudhauri kuacha Mara moja kufanya dhihaka kwenye mambo yenye kutia uchungu kwa Jamii ya Watanzania. Vinginevyo kama tabia hii itaendekea kwa yeyote yule basi TCRA na mamlaka nyingine zinazohusiana na mitandaoni, basi zichukuwe hatua kali na haraka kudhibiti hali hii, na hili nashauri kwa dhati na siyo kutishia mtu.
 
WAZIRI huwa anachukuwa jukumu la KUJIUZULU.
Si kwa sababu YEYE ALIHUSIKA DIRECTLY bali kama kuchukuwa POLITICAL RESPONSIBILITY la uzembe WOWOTE uliotokea wizarani mwake.

Je hili linaweza kutokea Tanzania?
Jibu ni ndiyo ikiwa mioyo yetu itajielewa.
Picha hii ya kujiuzulu huonyesha nchi kuwa hata mkuu wa nchi huwa naye AMEKERWA.

Nawaachia WAHUSIKA wajihoji NAFSI zao!!
Wakiamua kuwa "HAMNA" na ni business as usual basi bado ni sawa tu hata hivyo I have given out my mind!/Nimetoa maoni yangu.


Tunaambiwa uwezo wa kivuko ni abiria 100, wakizidi sana 101, mizigo tani 25 na magari 3, hii inatupatia picha kwamba collections kwa siku zinaweza kuwa fixed au zikashuka au kuzidi kidogo kulingana na idadi ya watu wanaosafiri kwa siku husika.

Najiuliza swali, je mamlaka husika hazikuwa zinafanya monitoring kuona mauzo yakiwa juu sana ambayo ni kama mara nne zaidi ya kawaida, ikiwa na maana kwamba kama one way kivuko kilitakiwa kuingiza shilingi 100, kikaonekana kinaingiza shilingi 400 ka abiria peke yake ukiacha mizigo? hii ingewapa picha kuwa kuna mahali mambo hayako sawa na walitakiwa kuchukua hatua.
 
Ni rahisi kusema ni mapenzi ya Mungu lakini, binafsi hiyo itakuwa ni sababu ya kijinga. Vyombo vya usafiri vimetengenezwa kitaalamu. Vinatakiwa kuendeshwa kitaalamu kwa kufuata utaratibu au sheria zilizojalibiwa na kuonyesha mafanikio. Wanaoviendesha ni watu waliofunzwa na kusomea taratibu za kuviendesha. Ndivyo ilivyo kwa Ndege, magari pamoja na meli kama hii MV Nyerere iliyozama.

Tatizo liko wapi hadi tuwe na ajali za aina hii? Tujiulize kwa nguvu sana kwa ajali kama hii ya meli ambayo siyo mara ya kwanza. Ilikuwa hivyo na MV Butiama, MV Kipepeo, MV spice sasa ni MV Nyerere! Napenda niseme haya yote yanatokana na ujinga wa waliosomea kuendesha vyombo hivyo. Kila wakati sababu inayotolewa ni kuzidisha uwezo wa vyombo hivyo. Sisi ni watu wa aina gani tusiweza kujifunza kutokana na makosa ya nyuma? manahodha hawa ni wajinga kiasi gani kuliko wanayama wa kufugwa wanaoweza kujifunza kutokana na matendo?

Ni aibu kuona mtu amesoma na kuelewa idadi ya abiria pamoja na uzito wa mizigo unaostahili kubebwa na vyombo hivyo. Nahodha anafahamu zana za uokoaji zilizoandaliwa kutokana na idadi ya abiria wanaobebwa na vyombo hivyo. Nahodha anafahamu uwezo na madaraka aliyonayo kuzuia abiria walio nje ya uwezo wa chombo chake. Sasa tuseme wazi kwamba watu hawa wanasomea unahodha lakini, wana viendesha kwa ujinga wao. Yaonekana wanashindwa kufuata mafunzo yao badala yake wanaongeza vipaji vyao vya kijinga na kuleta ajali kama hizi. Hii ni kwa wote. Hata magari yanaendeshwa kwa ujinga huo na wakati mwingine kujaribu kuonyesha kwamba watengenezaji hawakuelewa uwezo wa vyombo. Ukiwaangalia wakiwa kwenye kazi zao hizi, wanaonyesha umwamba wa kijinga na ufahamu wa kijinga, na mikogo ya kijinga kabisa kiasi kwamba wangeelimika, tusingekuwa na ajali kama hizi zambazo wakati mwingine, tunalazimisha kutoa majibu ya kiroho, eti ni mapenzi ya Mungu. Ajali hizi hazitokani na mambo ya kiroho!
 
Back
Top Bottom