Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

serikali ya ccm haiwezi kujitenga na uzembe uliofanyika. si mara ya kwanza kwa vyombo vya majini kuzama kwa kuzidisha ujazo, lakini wanaacha makosa yanajirudia.
Kwa jinsi nilivyopoteza ndugu zangu nitakuwa wa mwisho kuwaondoa hao nyang'au kwenye lawama. Lakini mleta mada anapowaingiza viongozi wa dini na wanasiasa wa upinzani kwenye lawama ETI wao walipaswa kuendelea na zoezi la uokozi hata kama serikali ilijiondoa sababu ya Giza ni kutowatendea hali. Tukio kama lile linakuwa na kamati ya uokozi na tumetangaziwa na asiye na aibu Mongela kuwa Mwenyekiti na waziri Kamwelwe hivyo huwezi kuendelea na uokoaji kwenye eneo linaloendeshwa na serikali maana chochote kitakachotokea utakuwa liable. Halafu wangefanya hivyo ndo ungeona nguvu ya FFU kuwasambaratisha. Mongela anasitisha zoezi kwa kisingizio cha Giza na kujiaminisha hakuna mtu aliye hai, siku ya tatu MTU anatolewa akiwa hai!! Halafu bado anaitwa Mkuu wa Mkoa?
 
Kama leo ameokolewa mtu akiwa hai japo hali yake ni mbaya.
Basi wangeokolewa wengine wengi usiku ule.
Yalikuwa ni maamuzi ya........... sana
 
Tatizo lipo na Raia namba moja,watu wakianzisha harambee utasikia wanatafuta kiki..

Kama viongozi wenyewe wanapata matatizo lakini hawajuliani unategemea sisi wananchi wa kawaida tufanyeje.?

Kiongozi wetu anakipenda zaidi chama chake kuliko Taifa, ndio maana yupo tayari kufanya lolote ilimradi chama chake kiendelea kuwa juu.

Hahubiri upendo,amani na utulivu ambayo ndio tunu ya Taifa letu yeye anahubiri Majigambo na ujivuni kana kwamba yeye ndio wa kwanza na wa mwisho kuongoza Taifa hili...

Sifa ya kiongozi ni kuwaunganisha watu sio kuwagawa kwa itikadi,Rangi,Kabila ama jinsia.

Tanzania ni yetu sote lazima tuifurahie kwa pamoja bila kujali tofauti zetu za kimtazamo

Leo hata angejitokeza mfanyabiashara aseme nipo tayari kufunga jenereta uokozi uendelee, kesho yake TRA wangehamishia ofisi kwake...uraia wake ungekuwa shakani...vitu kama ndio vinachangia utengano wa Kitaifa.

Zamani CCM na Chadema utani ilikuwa kama Yanga na Simba....Siku hizi CCM na Chadema ni kama Simba na Swala.
 
Kwa maxudi,japo walizuiliwa na mmiliki wa feri za kamanga feri,ni mzungu anaeitwa Gej,
Alilia kwa machungu huyo mzungu walivokaidi ushauri wake,wakaanza kuipasua kwa gesi.baada ya kutoboa tu,walitoka watu kama watatu tu na ikaanza kuzama kwa speed saana
Feri za huyo mzungu ndio zilikuwa zimeipiga cheni mv bukoba ili isizidi kuzama.walivotoboa tu na jamaa akatoa minyororo yake iliokuwa inaizuia isizame
Yaani fery mbili ndio zilikua zimeizuiwa,sasa akahofu kuwa na feri zitazama baada ya mv bukoba kutobolewa na kuingiza hewa na kuzidi kuzama kwa kasi
Asante sikuwahi jua,nahisi na wengi hawajui kama mm kuwa ilizamishwa makusudi,Nilijua ni ajali ya kawaida .

Tupia Uzi wake mkuu kama wajua kwa undani.
Asante
 
Amekaa majini masaa zaid ya 40 hakuna oxygen ameishije wataalamu nawaomba msaada Ila hapa kuna maswal mengi
 
Ukishaona mambo yapo hivyo,ndio ujue kuwa nchi hii ndio maana ikawa na amani maisha yake
Na mungu azidi kutujaalia amani nchini kwetu

Usiombe watu tuamke,patatokea machafuko fasta Mkuu
 
Mgawanyiko ulianza mara baada ya uchaguzi wa mwaka 2015. Sasa hivi Taifa liko vipande vipande.
Labda familia yako ndio mko vipande vipande walahi!
18F2A122-763B-44B2-A384-FC5A0E6656B9.jpeg
 
Fundi wa mkuu wa Mv NYERERE Alphonce Cherehani amepatikana akiwa hai na kuokolewa muda huu, hadi sasa idadi ya miili iliyoopolewa ni 163 kwa mjibu wa Waziri wa Uchukuzi ambapo miili 116 tayari imetambuliwa.

Inasemekana kuwa Fundi Mkuu wa MV Nyerere, Mhandisi Agustino Cherehani ambae ameokolewa leo akiwa hai alikuwa amejifungia ktk chumba maalumu ndani ya kivuko hicho tangu kilipozama.
 
Back
Top Bottom