Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Nawaomba sana wakuu wangu kwa heshima na taadhima , Michango yenu bado ni muhimu mno , toeni kusaidia wahanga pamoja na familia za marehemu na Mungu atawalipa , natambua changamoto zilizotokea kwenye michango ya Tetemeko la Kagera lakini ni vema tukakubali kwamba YALIYOPITA SI NDWELE , tuendelee kuiamini serikali .

Natanguliza shukrani .
 
Misiba ya kaskazini wanavyoivalia njuga Chadema lazima iwe ya kichama.Angalia msiba ule wa watoto ambao basi lilitumbukia mtoni Na wa ndesamburo Chadema walikuwa kutwa wako msitari wa mbele .Mbwa wa Nassari aliyepigwa risasi alizikwa kwa heshima zote za Chama wabunge wa Chadema Na viongozi wa Chama walihudhuria msiba ule.Mbwa wa Nassari mbunge wa Arumeru iliyo mikoa ya kaskazini ana heshima na hadhi kwao kuliko hao wakerewe waliokufa na kivuko sababu huyo mbwa ni wa kaskazini wakati hao wakerewe waliokufa Kwenye kivuko si wa kaskazini
Nakuonea Sana huruma, unataka Kusema katika watu 209 waliopoteza Maisha hakukuwa na mwanaccm? Jamani hizi siasa nyepesi mnazofanya awamu hii zitatuharibia nchi
 
Ndio maana wananchi wameanza kuwapuuza wanajaa kumsikiliza mdee siku ya kura wanaipigia ccm!
 
Lile ni jimbo la Chadema toka 2010, na ni ngome yao kuu kanda ya Ziwa, hawa viongozi waliokufa maji leo ndio waliowezesha Chadema kuongoza jimbo kwa awamu Mbili, kifupi jimbo zima la Ukerewe ni Chadema.

Naomba Chadema kitoe sababu za msingi kwa nini hakijashiriki mazishi ya viongizi wake.....au mnawathamini nyakati za uchaguzi tu...
===========================

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Ukerewe kimepata pigo baada ya viongozi wake kufariki dunia katika ajali hiyo.
Katibu wa Chadema wilayani humo, Deodatus Makalanga alisema viongozi waliopoteza maisha ni wa ngazi ya shina, vitongoji, vijiji na kata.
“Viongozi hawa wanatoka katika kata nne za Bwisya, Nyamanga, Bukiko zinazounda tarafa ya Ukara,” alisema Makalanga.
Tarafa ya Ukara ni kati ya ngome muhimu za Chadema wilayani Ukerewe. Chama hicho kinaongoza kata tatu kati ya nne zinazounda tarafa hiyo tangu 2015.
Jimbo la Ukerewe pia linaongozwa na Chadema tangu uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Chanzo Mwananchi.

Uko sahihi sana kwa huu uzi wako. Sasa twende pamoja, wakati wa janga la tetemeko la kagera viongozi wa cdm na wa upinzani tuliona kabisa wakifanyiwa figisu figisu zisizo na tija, ilifikia mahali mganga mkuu kukimbia msaada kwa wahanga uliopoelekwa na Mbunge wao kwa maagizo toka juu. Ikaja msiba wa vifo vya wanafunzi wa luck Vincent Arusha. Tuliona kabisa viongozi wa cdm wakifanyiwa udhalilishaji usio na sababu. Kwenye ziara za Magufuli tunaona wazi viongozi wa cdm wakidhalilishwa. Katika mazingira haya unahitaji kushiriki ili udhalilishwe?

Huu msiba bado una muda, nawashauri viongozi wa cdm waende baada ya msiba ili kutoa pole ya kweli ya kibinadamu na sio hiyo pole yenye lengo la kusaka mtaji wa kisiasa. Na pia ili kutaka kuonyesha kwamba hakuna mshikamano bali ni unafiki, ni bora viongozi wa cdm na wanacdm kutokushiriki msiba wa mwanaccm na kinyume chake. Bila kuchukua hatua stahiki huu ukatili hautapatiwa ufumbuzi. Sioni haja ya kuonyesha mshikamano huku udhalilishaji wa wazi wakifanyiwa hao cdm. Mtu mmoja ndio anaratibu hii tabia na watu wananyamazia, ni vyema kuchukua hatua za amani kwani nyingine za kikatiba kama kuandamana inaonekana nguvu ya dola inatumika vibaya. Ngoja sasa watu wahamishie kwenye hiyo misiba na itangazwe waziwazi. Huenda hatua hizo zitasababisha wanaofumbia macho huu mwenendo wa kuligawa taifa letu watataka suluhu.
 
Nawaomba sana wakuu wangu kwa heshima na taadhima , Michango yenu bado ni muhimu mno , toeni kusaidia wahanga pamoja na familia za marehemu na Mungu atawalipa , natambua changamoto zilizotokea kwenye michango ya Tetemeko la Kagera lakini n vema tukakubali kwamba YALIYOPITA SI NDWELE , tuendelee kuiamini serikali .

Natanguliza shukrani .
Matajiri tena? si ndio maadui wa baba yangu!
 
Sasa kwa nini wana Ukerewe wanakejeliwa na wana CDM, hata huu uzi kuna kila aina ya kejeli kutoka kwa nyumbxxx wa CDM kwenda kwa wana Ukerewe. Wengine wamefikia kusema acha wafu wazikane, wengine wana kejeli waliowaua ndio wawazike wengine hata kuona CDM haina jukumu la kufariji wana Ukerewe. Hizi dharau na kejeli zitawarudia tu, tutakumbushana hapa 2020.
Jukumu namba moja lipo kwa rais, ukiacha habari ya siasa zenu nyepesi wale ni watanzania,rais alitakiwa kwenda huko maana yeye ndiye mfariji namba moja katika Taiga, siasa zenu nyepesi ndo zinapelekea ninyi kuhoji ujinga wenu huu
 
Kuuliza ushiriki wa CDM ni upumbavu? Kuuliza kwa nini CDM wanatoa maneno ya kejeli na uzushi ni upumbavu? Jimbo lipo chini ya CDM tena tangu 2010 kuzidi majimbo mengi tu ya Arusha na Moshi ila mmewadharau sana wana Ukerewe. 2020 CDM yyte akiniomba kura nitamtemea mate kuonyesha dharau yangu kwake pia.
Umeshupaa shingo utafikiri ni mpiga kura kweli. Nani aombe kura kwa ma.ng'aa kama wewe? Wacha kutokwa povu wewe na hilo YEHODAYA . JF wanawajua kwa fitna.
Nani asiyejua viongozi wa chadema wana u salama mdogo nchi hii? Mlipanga kuwazamisha kwenye maji? Mbona mnawalilia sana huko kuliko mnavyolilia uwepo wa mwenyekiti wa ccm Taifa kwenye msiba huo? Kuna kitu, siyo bure.
 
Wengine hatupendi kwenda kwenye ubaguzi na ukanda lakini kwa hali hii inatufanya tufike huko.

Ni hivi idawa wewe nakuheshimu, lakini kuna mwenendo ambao sio mzuri unaoendelea hapa nchini na kila mtu anaufumbia macho. Ni nani asiyeona viongozi wa cdm wakidhalilishwa na bado wanakaa kimya? Wewe huoni mwenendo wa uchaguzi unavyofanyika? Watu wakitaka kuandamana kuonyesha kuna shida nguvu ya dola inatumika badala ya kusawazisha hayo mambo. Juzi tumeona watu wamesusia uchaguzi na idadi imekuwa ndogo kupita kiasi. Idadi ikapikwa na watu bado wako kimya. Kwanini hao wapinzani wasitumie njia nyingine kuonyesha kwamba hali sio shwari na mtu mmoja ndio tatizo? Ngoja itumike njia ya amani ya kuvunja huo umoja wakitaifa tuone kama hao wananchi waliokalia kimya huu mwenendo hawatatokea. Hao viongozi wa cdm watangaze kiwazi wazi hakuna kushiriki msiba wa upande wa pili au wa kiongozi wa serekali. Wahamasishe bila woga. Nadhani umeona michango wa huo msiba unavyosua sua na uhamisishaji wa kwamba watu wasichango uko wazi. Iwapo tutakalia kimya mwenendo mbovu tutaliangamiza taifa letu. Mimi naunga mkono hii njia ya kusisiana misiba na sherehe ili tupate ufumbuzi wa huu mwenendo.
 
Mkuu tindo huenda uko sahihi kiasi, lakini wananchi tunaona kila kinachoendelea ndani ya nchi yetu kuhusu vyama vya upinzani hasa chadema jinsi ya wanavyofanyiwa figisu.

Lakini kwa kuweka kumbukumbu sawa ni vyema wengeshiriki halafu wazuiwe Watanzania wengi tungekuwa nyuma yao na hansadi zingetunzwa.

Lakini kitendo cha Kumwacha mbunge husika peke yake mbele ya kundi la viongozi wa CCM ni usaliti mkubwa sana.

Kwa hili viongozi inabidi wajitafakari.
 
Tatizo pesa haiendi kwa watu moja kwa moja kwanini kila mtu asiwekewe kwenye account zao za wafiwa badala ya kujenga minara
 
Mazishi yalishafanyika rambi rambi Na kuwa karibu Na wafiwa zoezi hilo huwa la maana Na kuthaminiwa hutakiwa kufanyika kabla ya Mazishi
Kiongozi Mkuu wa Nchi Mh.Magufuli anafahamu hili?
 
Back
Top Bottom