Upepo wa Pesa
JF-Expert Member
- Aug 8, 2015
- 21,600
- 35,158
Kwa hiyo watu wasipochanga huo ukuta hautajengwa?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbwa wa kaskazini ni bora kuliko......!!!Vijana wa Lumumba mtaacha link kutumia vijambio kufikiri?
Kwa hiyo wajane watakula mnara .ficha ujinga wako mara moja mojaMnara wa kumbukumbu ni sehemu ya heshima kwa marehemu na faraja kwa ndugu
Kama Pombe ni faraja wacha wafiwa wanywe wapoteze mawazo. Kama mtu kafiwa na baba yake halafu awaze kuwa kama kungekuwa na mwanga labda baba yake angeokolewa, huyu akinywa pombe tatizo liko wapi?Mlitaka rambi rambi ikanunulie pombe?
Kwa maana hiyo mngemshauri na mbunge wenu akasusia maziko basi halafu tuone 2020 kama mtakuwa na hadhi hata ya UDP. Acha kujidanganya eti CDM ndo nini sijui. CHADEMA inaweza kuwa kama NCCR, CUF UDP au PPT MAENDELEO! mda utatupa majibu na tutakutana hapahapa na vijisababu vya kwenye vijiwe vya kahawa na maisha yataendelea kuwepo.
Naomba niulize swali, rambi rambi kwa upeo wako unajua ni nini? Je kazi yake ni ipi?Mlitaka rambi rambi ikanunulie pombe?
"...baadhi ya fedha zitazopatikana zitajenga uzio na mnara..." means zitakazobaki zitapelekwa wapi? Au ndio zitafidia huo ubani wa laki5 uliotolewa?Umeisoma kauli ya PM?
Well said mkuu!Matangwa wewe acha tu, kuna watu wameamua kutetea huu ujinga. Binafsi sina tatizo na kejeli za siasa ila kejeli za msiba, si sahihi kabisa. Tutafundishana adabu 2020. Zinatolewa sababu za kitoto sana za kwa nini CDM wameamua kutoshiriki huu msiba wa Taifa, tena kwenye jimbo lililo chini ya CDM.
CDM wana amini wanapendwa sana wasichojua kinachopendwa si CDM ila ni matendo ya CDM. Nakumbuka Dr Slaa aliongoza mazishi ya Arusha baada ya lile bomu la Olesetini mbele ya mtutu wa bunduki, CDM wa 2012 walikuwa hawaogopi bunduki ila CDM 2018 wanaogopa maneno ya kudhalilishwa na hapo hapo wanategemea wananchi tutakuja kuwasaidia wakiwekwa angle. Muda utatoa somo tu kwa hizi kejeli na dharau.
Kingine ambacho viongozi wa CDM hawajifunzi ni wananchi ambao ni wapenzi wa upinzani wapo loyal kwa malengo yao na si kwa chama. NCCR Mageuzi ilidondoka ikaja CUF, CUF ikadondoka ikaja CDM na CDM kwa hichi kibri inabidi idondoke tupata chama bora zaidi.
Naona hata Shivji kesha choka sasa analikalia jiwe na kulij...... kimya kimya.Vijana wa Lumumba mtaacha link kutumia vijambio kufikiri?
Mngekua mnawaheshimu mngewajali kwa kivuko boraMnara wa kumbukumbu ni sehemu ya heshima kwa marehemu na faraja kwa ndugu
Kikubwa ni serikali imekiri kuwa kivuko kilizidisha uzito.Wakati Serikali ikisema miili 224 imeopolewa baada ya kivuko cha MV Nyerere kuzama, mbunge wa Ukerewe (Chadema) Joseph Mukundi amedai idadi ya abiria waliokuwa kwenye kivuko hicho ni zaidi ya 300.
Kivuko hicho kilizama Septemba 20, 2018 mita 50 kabla ya kutia nanga kwenye gati la Bwisya kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe.
Mkundi ametoa kauli hiyo leo Jumapili Septemba 23, 2018, saa chache baada ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe kusema kuwa kivuko hicho kilikuwa kimepakia abiria 265 wakati kina uwezo wa kubeba watu 101.
Akitoa mchanganuo wa vifo, Waziri Kamwelwe amesema wanawake 126, wanaume 71, watoto wa kike 17, watoto wa kiume 10 na kufanya jumla ya maiti 224.
Akizungumza na MCL Digital leo mbunge huyo amesema kulingana na mazingira na changamoto za usafiri kati ya Bugolora na Ukara, ni wazi kuwa abiria katika kivuko hicho walikuwa zaidi ya 300.
"Hili suala niliwahi kuliwasilisha bungeni lakini kilichofanyika ni ununuzi tu wa injini mpya," amesema Mkundi.
“Serikali ina majukumu mawili, la kwanza ni kununua kivuko kikubwa na pili ni kuongeza safari za kivuko kutoka safari mbili kwa siku hadi nne ili kuzuia upakiaji wa abiria kupita kiasi.”
Mkundi amesema Ukara ni kata kubwa ambayo inahitaji siku maalum ya gulio, si wananchi wake kwenda Bugolora kila wakati kwa ajili ya kununua bidhaa.
Mbunge huyo ameungwa mkono na mwenyekiti wa kijiji cha Bwisya, Oru Magero aliyesema kuwa ni kawaida kushuhudia kivuko cha Mv Nyerere kikiwa kimepakia mizigo na abiria kupita kiasi.
"Serikali isaidie wananchi wa Ukara kuwaboreshea usafiri kama sehemu nyingine za nchi yetu," amesemaMagero.