Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Lawama zote ziende kwa waziri husika na ikibidi atumbuliwe maana kama angekuwa mkali wizarani kwake watu wangekuwa wanafuata taratibu walizo jiwekea
Actually, ndo matarajio ya wengi. Amepyaya sana. Nilimuonea huruma alivyokuwa akitoa taarifa yake; angalau RC alikuwa stable.
 
Na kuna watu walikuwa wanalipwa kuzuia uzembe huo lakini hakuna walichokuwa wanafanya!!
Wenzetu wanaojitambua wanachukua hatua sisi haohao wanaopaswa wasulubiwe ndio wanatutisha namna ya kulia iweje.
yerickonyerere___BoFFp6qBls3___.jpg
 
Yeye ndio alikatisha Tiketi?
Unaona Waziri anahitimisha hesabu kisha analetewa hesabu mpya kuwa kuna maiti nyingine imeibuliwa!
Sheria ya takwimu ianzie kwa waziri kumlamba kama lile LA kufukuzwa limeshindikana
 
Acha unafiki,wewe kiongozi wako mkuu ameenda mazishini?Nyie watu mmeumbwaje vichwani mwenu?
 
Sawa lakini hiyo huwa si kazi ya rambi rambi. Au nyie watu wa CCM hamjawahi kufiwa nini au pia mkifiwa huwa hampewi rambirambi?
Kwani ile michango ya Msiba wa Mbwa wa Nassari mliiipeleka wapi mkuuu, hebu leta mchanganuo basi.
 
Mkuu serikali imesema waliookolewa na kuopolewa jumla ni 265 na imesema inaendelea kutafuta miili mingine mpaka yote ipatikane kwa maana hiyo inaweza kufika 300 na ama zaidi.

Na mbunge amesema walikuwa zaidi ya abiria miatatu, japo sina hakika na takwimu zake.

Lakini ukiangalia kauli zote mbili hazipingani.....

Ila chadema wanaripotiwa kama mbunge na serikali wanapingana...

Mkuu Idawa kuna jambo la kujiuliza hapa kuhusu serekali. Inakuwaje serekali ilikuwa inakusanya hela nyingi kuliko kiwango inachopaswa kwa trip na haichukui hatua kujua kwamba inazidisha abiria? Huoni hapa serekali ilibariki hii overload kwa kukusanya mapato zaidi?
 
Wakati Serikali ikisema miili 224 imeopolewa baada ya kivuko cha MV Nyerere kuzama, mbunge wa Ukerewe (Chadema) Joseph Mukundi amedai idadi ya abiria waliokuwa kwenye kivuko hicho ni zaidi ya 300.
Kivuko hicho kilizama Septemba 20, 2018 mita 50 kabla ya kutia nanga kwenye gati la Bwisya kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe.


Mkundi ametoa kauli hiyo leo Jumapili Septemba 23, 2018, saa chache baada ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe kusema kuwa kivuko hicho kilikuwa kimepakia abiria 265 wakati kina uwezo wa kubeba watu 101.



Akitoa mchanganuo wa vifo, Waziri Kamwelwe amesema wanawake 126, wanaume 71, watoto wa kike 17, watoto wa kiume 10 na kufanya jumla ya maiti 224.



Akizungumza na MCL Digital leo mbunge huyo amesema kulingana na mazingira na changamoto za usafiri kati ya Bugolora na Ukara, ni wazi kuwa abiria katika kivuko hicho walikuwa zaidi ya 300.



"Hili suala niliwahi kuliwasilisha bungeni lakini kilichofanyika ni ununuzi tu wa injini mpya," amesema Mkundi.



“Serikali ina majukumu mawili, la kwanza ni kununua kivuko kikubwa na pili ni kuongeza safari za kivuko kutoka safari mbili kwa siku hadi nne ili kuzuia upakiaji wa abiria kupita kiasi.”
Mkundi amesema Ukara ni kata kubwa ambayo inahitaji siku maalum ya gulio, si wananchi wake kwenda Bugolora kila wakati kwa ajili ya kununua bidhaa.


Mbunge huyo ameungwa mkono na mwenyekiti wa kijiji cha Bwisya, Oru Magero aliyesema kuwa ni kawaida kushuhudia kivuko cha Mv Nyerere kikiwa kimepakia mizigo na abiria kupita kiasi.



"Serikali isaidie wananchi wa Ukara kuwaboreshea usafiri kama sehemu nyingine za nchi yetu," amesemaMagero.
Hiyo ni idadi ya marehemu tu, waziri hakujumlisha na idadi ya waliotoka hai(wazima) au umesahau pia kuna wailookoka humo ambao wanaweza kufikisha idadi ya watu 300
 
Nimejiuliza sana ili swali hasa baada ya kusoma katika gazeti la Chadema liitwalo Tanzania Daima kwamba uongozi unakaribia kumsajili maalim Seif katika chama chao. Ndiposa najiuliza mgombea urais mtarajiwa ndio kipaumbele cha Chadema kiasi cha kumtelekeza mbunge wa Ukerewe my Joseph Mkundi?!!!


Hasira za kukosa nafasi ya kuwadhalilisha.
How often wakiwa katika maeneo yao (kama mlivyowaamulia) mmewadhalilisha na kutowapa heshima zao?! Sembuse huko mbali na maeneo yao ya kibunge??
Wote tunajua kuwa the moment wangetia team lazima hata gathering ndogo tu ya kusalimiana yangeitwa maandamano.
Kila mzt aliyeguswa na msiba huu amekuwa na MTU wa kulaumu au kunyooshea kidole kama mzembe- ndio maana mkuu sana kavunja bodi ya temesa- but viongozi wa upinzani walipotoa mtazamo wao immediately imeonekana ni kutafuta kick za kipolitic, sasa ulitaka waje mseme zaidi??!!. Kuhani msiba huwa hakuishi- watakuja siku nyingine na wengine.
Au watamsindikiza mkuu sana atakapoenda kuwasalim na kuwapa kivuko kingine.

Above all, ukerewe wala samaki- akili kubwa wale. Hawana utapia mlo, hizi propaganda za ovyo haziwafanyi kitu.
Wana uwezo was kudeal nazo na kujua pumba ni IPI na mchele ni UPI.
 
Back
Top Bottom