Mmawia
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 122,494
- 96,074
Hapana ndiye mmiliki wa hicho kivuko
Kumbe yeye ndio alikuwa mkata tiketi?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kumbe yeye ndio alikuwa mkata tiketi?
huyu mbunge awe makini. wanaccm sio watu wazuri hawakawii kumdhalilisha....
Chadema ndio walivyo hivyo, haswa huyu Mwanahabari Huru ndio mchezo wake huu. Wameishiwa mbinu za propaganda wamebaki kuparamia kila wanaloliona bila ya kutafakari.
mkuu naona watu wengine hapa wanaongea tu ila hata hawajui nini cha kujadili, hio ni swali sawa kabisa ambalo umemuuliza, wacha tusubiri jibu lakeUlitaka aongee vipi ili aonekane kaongea kiuongozi?
Actually, ndo matarajio ya wengi. Amepyaya sana. Nilimuonea huruma alivyokuwa akitoa taarifa yake; angalau RC alikuwa stable.Lawama zote ziende kwa waziri husika na ikibidi atumbuliwe maana kama angekuwa mkali wizarani kwake watu wangekuwa wanafuata taratibu walizo jiwekea
Wenzetu wanaojitambua wanachukua hatua sisi haohao wanaopaswa wasulubiwe ndio wanatutisha namna ya kulia iweje.Na kuna watu walikuwa wanalipwa kuzuia uzembe huo lakini hakuna walichokuwa wanafanya!!
Hili ndio kilitakiwa bla bla zenu tupa kule!Chadema ndio walivyo hivyo, haswa huyu Mwanahabari Huru ndio mchezo wake huu. Wameishiwa mbinu za propaganda wamebaki kuparamia kila wanaloliona bila ya kutafakari.
Kwenda zako, kukaa nyuma ya TV na kuangalia tibisi ndio kuwa Ukara?Mbona na mimi nilikuwepo, unafikiri ulikuwepo peke yako?
Unaona Waziri anahitimisha hesabu kisha analetewa hesabu mpya kuwa kuna maiti nyingine imeibuliwa!Yeye ndio alikatisha Tiketi?
Je yeye anauakika gani kuwa waliopanda ni zaidi ya 300wamemlishaje mkuu? mbona sijakuelewa?
"nataka waishi kama mashetani?"
Unadhani ni wasahaulifu kiasi hicho..?
Huyu ndo kasababisha mpaka yanga tunahaha.
Kikubwa ni serikali imekiri kuwa kivuko kilizidisha uzito.
Au kuna miili imefichwa?
Kwani ile michango ya Msiba wa Mbwa wa Nassari mliiipeleka wapi mkuuu, hebu leta mchanganuo basi.Sawa lakini hiyo huwa si kazi ya rambi rambi. Au nyie watu wa CCM hamjawahi kufiwa nini au pia mkifiwa huwa hampewi rambirambi?
Mkuu serikali imesema waliookolewa na kuopolewa jumla ni 265 na imesema inaendelea kutafuta miili mingine mpaka yote ipatikane kwa maana hiyo inaweza kufika 300 na ama zaidi.
Na mbunge amesema walikuwa zaidi ya abiria miatatu, japo sina hakika na takwimu zake.
Lakini ukiangalia kauli zote mbili hazipingani.....
Ila chadema wanaripotiwa kama mbunge na serikali wanapingana...
Hiyo ni idadi ya marehemu tu, waziri hakujumlisha na idadi ya waliotoka hai(wazima) au umesahau pia kuna wailookoka humo ambao wanaweza kufikisha idadi ya watu 300Wakati Serikali ikisema miili 224 imeopolewa baada ya kivuko cha MV Nyerere kuzama, mbunge wa Ukerewe (Chadema) Joseph Mukundi amedai idadi ya abiria waliokuwa kwenye kivuko hicho ni zaidi ya 300.
Kivuko hicho kilizama Septemba 20, 2018 mita 50 kabla ya kutia nanga kwenye gati la Bwisya kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe.
Mkundi ametoa kauli hiyo leo Jumapili Septemba 23, 2018, saa chache baada ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe kusema kuwa kivuko hicho kilikuwa kimepakia abiria 265 wakati kina uwezo wa kubeba watu 101.
Akitoa mchanganuo wa vifo, Waziri Kamwelwe amesema wanawake 126, wanaume 71, watoto wa kike 17, watoto wa kiume 10 na kufanya jumla ya maiti 224.
Akizungumza na MCL Digital leo mbunge huyo amesema kulingana na mazingira na changamoto za usafiri kati ya Bugolora na Ukara, ni wazi kuwa abiria katika kivuko hicho walikuwa zaidi ya 300.
"Hili suala niliwahi kuliwasilisha bungeni lakini kilichofanyika ni ununuzi tu wa injini mpya," amesema Mkundi.
“Serikali ina majukumu mawili, la kwanza ni kununua kivuko kikubwa na pili ni kuongeza safari za kivuko kutoka safari mbili kwa siku hadi nne ili kuzuia upakiaji wa abiria kupita kiasi.”
Mkundi amesema Ukara ni kata kubwa ambayo inahitaji siku maalum ya gulio, si wananchi wake kwenda Bugolora kila wakati kwa ajili ya kununua bidhaa.
Mbunge huyo ameungwa mkono na mwenyekiti wa kijiji cha Bwisya, Oru Magero aliyesema kuwa ni kawaida kushuhudia kivuko cha Mv Nyerere kikiwa kimepakia mizigo na abiria kupita kiasi.
"Serikali isaidie wananchi wa Ukara kuwaboreshea usafiri kama sehemu nyingine za nchi yetu," amesemaMagero.
Hahahaaaa........ Chadema yawatelekeza wapiga kura wake!Acha unafiki,wewe kiongozi wako mkuu ameenda mazishini?Nyie watu mmeumbwaje vichwani mwenu?
Nimejiuliza sana ili swali hasa baada ya kusoma katika gazeti la Chadema liitwalo Tanzania Daima kwamba uongozi unakaribia kumsajili maalim Seif katika chama chao. Ndiposa najiuliza mgombea urais mtarajiwa ndio kipaumbele cha Chadema kiasi cha kumtelekeza mbunge wa Ukerewe my Joseph Mkundi?!!!