Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ulitaka iweje, kwani nani aliyekuambia mfuko wa maafa kazi yake ni kujenga mnara wa kumbukumbu! Tanzania kwani tuna wapinzani…tuna wapinga yote…aibu yao! Hao wahanga watapewa mkono wa pole!

Mkuu umepaniki, serikali yako linapokuja swala la rambirambi aiaminiki kumbuka kilichotokea Kagera. Kumtetea mwizi kunahitaji ujasiri mkubwa!
 
matumizi ya rambirambi ni kutatua yatokanayo na msiba, na kama mnara ni moja wapo ya yatokanayo basi itatumika pia kwa hilo.
Lakin hero mnara utasaidiaje familia za wafiwa maana wengine wameondokewa na watu ambao ndio tegemezi kwa familia?
 
mawazo yako yashaanza kufanyiwa kazi

index.jpg
 
Nimejiuliza sana ili swali hasa baada ya kusoma katika gazeti la Chadema liitwalo Tanzania Daima kwamba uongozi unakaribia kumsajili maalim Seif katika chama chao. Ndiposa najiuliza mgombea urais mtarajiwa ndio kipaumbele cha Chadema kiasi cha kumtelekeza mbunge wa Ukerewe my Joseph Mkundi?!!!
Alipokufa mbwa wa Nasari walimzika kitaifa na makamanda walihudhuria. Lakini hawa wapiga kura wao hayawahusu. Kwao mbwa ana thamani kuliko wapiga kura wao
 
Kwa hiyo unataka usemeje?? Acha ujuaji..watu wameingia chini wametafuta..unadhani wangewaacha tu kama wameonekana..au wangekuwa na nia mbaya si wangeacha hicho kivuko hata mwezi..
Kwani walipoahirisha zoezi la uokozi kwa sababu ya giza walikuwa na nia nzuri?
 
Kumtumbua Waziri,Naibu Waziri,katibu si vyema kabisa na naamini serikali haitafanya hivyo..Hili swala litawakaanga SUMATRA na watu wa OSHA na wakuu vitengo vya uendeshaji wa Meli na Vivuko Ziwa Victoria.Tayari Serikali imeamka na jamaa wa SUMATRA.
Kitu mi napenda Serikali itazame ni kuwepo Afisa wa Polisi katika kila kituo cha Kivuko Mwenye dhamana ya kuweza kuzuia Meli au Kivuko kufanya safari atakayepiga simu Direct kwa Waziri anapobaini tatizo kama hili na ukiukwaji wa sheria ya usalama katika vyombo.Kujenga Ofisi za uhakika na watendaji making, kuweka kitengo cha Uokoaji na dharura katika kila eneo Vivuko vinafanya kazi hii itaongeza ufanisi
 
Jana nimeota nilizama kwenye MV Nyerere nashangaa Asubui Leo Niko mzm hapa Mbeya ndoto zingine bwana
 
Wewe Sababu ya ajali umeijuaje kama unasema tusubiri tume tupate majibu kwa nini kivuko kimezama?
Hivi wewe umeenda shule wewe?Unaelewa kwanini kivuko kinaelea na shilingi inazama?kama kinabeba watu mia na walikuwa zaidi ya 400 unategemea nini?Au unasubiri Tume ya polisi na wanajeshi was daresay la 7 wakupe ripoti?
 
Serikali ya kipuuzi hi acha kabisa, hayo makaburi yalitakiwa yajengwe na serikali, mi nashangaa serikali inayo jitapa kuwa inakusanya kodi wakati maafa yakitokea wanatembeza bakuli, hizo kodi zinaenda wapi? Leo badala ya waziri mkuu tena msomi kuja na mawazo ya kuepusha maafa mengine hapo ziwani anakuja na mawazo ya kijijini. Na hiyo ferry haina insurance? Hao wafiwa ni lazima walipwe fidia lakini utakuja kusikia Magufuli anaropoka kuwa "Kwani waliambiwa na serikali wapande ferry? Mimi sitoi hela"
 
Hasira za kukosa nafasi ya kuwadhalilisha.
How often wakiwa katika maeneo yao (kama mlivyowaamulia) mmewadhalilisha na kutowapa heshima zao?! Sembuse huko mbali na maeneo yao ya kibunge??
Wote tunajua kuwa the moment wangetia team lazima hata gathering ndogo tu ya kusalimiana yangeitwa maandamano.
Kila mzt aliyeguswa na msiba huu amekuwa na MTU wa kulaumu au kunyooshea kidole kama mzembe- ndio maana mkuu sana kavunja bodi ya temesa- but viongozi wa upinzani walipotoa mtazamo wao immediately imeonekana ni kutafuta kick za kipolitic, sasa ulitaka waje mseme zaidi??!!. Kuhani msiba huwa hakuishi- watakuja siku nyingine na wengine.
Au watamsindikiza mkuu sana atakapoenda kuwasalim na kuwapa kivuko kingine.

Above all, ukerewe wala samaki- akili kubwa wale. Hawana utapia mlo, hizi propaganda za ovyo haziwafanyi kitu.
Wana uwezo was kudeal nazo na kujua pumba ni IPI na mchele ni UPI.
Mbwa wa Nassari ana thamani zaidi ya wala samaki?!!
 
Kwani walipoahirisha zoezi la uokozi kwa sababu ya giza walikuwa na nia nzuri?
Kuna binadamu anaweza ishi chini ya maji bila vifaa vyovyote vya upumuaji?Kivuko kilipinduka saa 8,unafikir masaa manne mbele bado kulikua na kitu kinachoitwa UOKOAJI?Au zoezi lilikua UOPOAJI?
 
Pia na sisi Raia tubadilike jamani! Meli au Kivuko kimejaa usilazimishe kupanda..Pale mwendokasi pia inabidi serikali itoe tamko la msisitizo Basi moja abiria wangapi wa kusimama maana majanga yapo tu huwa yanatokea. Idadi ya watu ikizidi katika chombo lawama itaangukia serikali..kila mamlaka ijitahidi kuwajibika..pressure zote zinaelekezwa ikulu, Hayati Mwl JKN aliwahi sema ikulu sio mahali rahisi kama raia ambavyo huwa tunafikiri
 
Kumtumbua Waziri,Naibu Waziri,katibu si vyema kabisa na naamini serikali haitafanya hivyo..Hili swala litawakaanga SUMATRA na watu wa OSHA na wakuu vitengo vya uendeshaji wa Meli na Vivuko Ziwa Victoria.Tayari Serikali imeamka na jamaa wa SUMATRA.
Kitu mi napenda Serikali itazame ni kuwepo Afisa wa Polisi katika kila kituo cha Kivuko Mwenye dhamana ya kuweza kuzuia Meli au Kivuko kufanya safari atakayepiga simu Direct kwa Waziri anapobaini tatizo kama hili na ukiukwaji wa sheria ya usalama katika vyombo.Kujenga Ofisi za uhakika na watendaji making, kuweka kitengo cha Uokoaji na dharura katika kila eneo Vivuko vinafanya kazi hii itaongeza ufanisi
Porojo hizi, responsibility inaanza kwa waziri, kwa tanzania ya sasa ukanda una priority kila mtu anajua
 
Back
Top Bottom