Uchaguzi 2020 Ukara: Wananchi wamuua mtu aliyetaka kumteka mgombea udiwani wa kata ya Bwisya kwa tiketi ya CHADEMA

Mpwa, Mpwa, Mpwa ngoja nikae kimya tu! Niko JF miaka mingi kuna tarifa nyingi sana zimewahi kuwekwa hapa with vivid evidence lakini tuishie hapa
 
Hii roho mbaya ya kutekana inaonekana kushamiri. Kama waliweza kumthibiti wasingemua ili tujue ni akina nani waliowatuma.....
Kinachotafutwa ndicho hicho ili "watu" wakamatwe kwa makosa ya jinai kama mauaji nk pindi watakapojihami dhidi ya watesi wao.
Khofu itatamalaki, upedo na kuaminiana baina ya watanzania KWAHERI!
 
Wale wa Hai - Kilimanjaro waliorusha mawe ni chama gani?

Hapa ndio upate majibu kuwa CCM inahusika katika haya matukio na ndio wanaratibu 100%
 
Kwahiyo yanafanywa na nani ?
 
Mpwa, Mpwa, Mpwa ngoja nikae kimya tu! Niko JF miaka mingi kuna tarifa nyingi sana zimewahi kuwekwa hapa with vivid evidence lakini tuishie hapa
Sawa mkuu, lakini nikuachie swali wakati kule kibiti wanaccm walivyokuwa wakiuawa kila kukicha vipi ni CHADEMA wale ndio walikuwa wakifanya yale mauaji? Ulisikia tuhuma zozote kutupiwa CHADEMA kuwa ndio wahusika? Na ingekuwaje Kama wale waliokuwa wanauawa wangekuwa Wana CHADEMA hali ingekuwaje tuhuma angetupiwa nani?
 
Wang'olewe na kucha kabisaaa, wametuonea vya kutosha acha wananchi wajilinde wenyewe maana polisi wanailinda ccm, sasa wananchi wawalinde wapinzani...patamu hapooooo
Kweli kabisa uchaguzi huu ni jino kwa jino, ukipigwa shavu la kushoto hakuna kugeuza la kulia, nawe unapiga mambata na mitama!
 
Na serikali ya ccm na wanachama wake sasa wameshafikia hiyo hali sasa wao wanajiona ni watu zaidi kuliko wengine.

Pia wao wameshafikia hatua ya kujiona ni first class citizens na wanahaki ya kufanya chochote kwa wengine bila kuguswa.

Nchi iko kwenye mtanziko wa uongozi, hatuna viongozi wenye utu tena.
 
Dah jamani wengine tufanye kazi za kawaida tu siasa gani hizi za kuuana ni kwa sababu ya ukereketwa wa kwenda kutumikia watu au kuna sababu nyingine ambazo swala la kuchaguliwa ni kufa na kupona kwa baaadhi ya watu.
 
Mauwaji ya MKIRU yalikua ya tofauti sana sana na ndio maana jeshi liliingilia kati, huenda ilikua ni zaidi ya yale tuliyokua yunayajua, all in all tupendane na kuheshimiana maana chaguzi zitapita ila maisha yatakuepo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…