Ukatili kwa watoto: kwanini madrasa huwa ni kawaida kuambatana na vipigo kwa watoto, walimu hawana mbinu mbadala kuwafunza?

Ukatili kwa watoto: kwanini madrasa huwa ni kawaida kuambatana na vipigo kwa watoto, walimu hawana mbinu mbadala kuwafunza?

R-K-O

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2023
Posts
482
Reaction score
2,178
Post hii sio ya ligi ya ukristo vs uislam, Tupeane elimu na ushauri namna ya kujenga awareness kwamba kinachofanyika ni ukatili na tushauriane mbinu nzuri mbadala.

Hii ni video ikionyesha mfano wa hali iliyozoeleka katika baadhi ya madrasa na wala si jambo geni, adhabu wanayopata watoto ni ukatili kwao hasa ukizingatia bado wana speed ndogo ya kujifunza ila mwalimu hatilii maanani anatoa kipondo heavy.


Na mbaya zaidi unakuta wazazi wala hawana tatizo na walimu kufanya haya, hii hupelekea hata watoto kuogopa kusema kwa wazazi wao endapo mwalimu akivuka mipaka.

Hii ni mbinu mbaya kufundisha ndio maana wengi huishia kukariri badala ya kuelewa, hata mtu akiwa mtu mzima unakuta kashasahau vingi alivyojifunza madrasa.

Pendekezo langu ni kwamba kwanini kusiwe na mbinu ambazo zipo balanced kufundisha watoto kwa namna ambayo itawafanya wapende kujifunza kwa hiari na si kwa vitisho?

Kuna kujifunza kwa michezo, kujifunza kwa kuimba, kujifunza kwa zawadi, n.k. vitu hivi ndivyo wanavyopenda zaidi watoto.
 
Na mbaya zaidi unakuta wazazi wala hawana tatizo nao husema "na sisi tulipitia huko huko tena nyoe mna nafuu", wanaruhusu, hii hupelekea hata watoto kuogopa kusema kwa wazazi wao endapo mwalimu akivuka mipaka.
Mbinu mbadala ni zipi?
 
Hata upapai huanzia huko, sijui huwapa nini watoto wanaficha matendo ya ukatili na unyanyasaji wanayofanyiwa...
 
Kiukweli wale ma ustadh hua ni wakatili Sana Wana piga watoto kupita kiasi, ukiwa unatazama wanavyo wachapa utashindwa kuvumilia
 
Weka matukio mawili ya kesi za ulawiti kutokea kanisa la RC Tanzania, na mimi niweke hapa kesi za ulawiti MADRASA hapa tz
Umeisahau ya mpanda? Vipi kuhusu padri kimario tuliyeamini yupo gerezani kumbe mfumo kristo ulimkimbuzia msumbiji hadi umauti kumkuta. Zipo kibao tu
 
sehemu yoyote ya kujifunza lazima iambatane na mateso(adhabu)
 
Weka matukio mawili ya kesi za ulawiti kutokea kanisa la RC Tanzania, na mimi niweke hapa kesi za ulawiti MADRASA hapa tz
Kula chuma hicho na ukitaka nyingine naongeza.
 
Tafadhalini hii post inahusu uislam, sio ligi ya uislam na ukristo, mkitaka ligi hizi naombeni mfungue uzi maalum.

Naombeni tujadili positively kulingana na maada tujadiliane namna hili tatizo linavoweza kupunguzwa na si kuanza kucharuana.
TZ kila kitu ni ligi tu, simba vs yanga, katarama vs ally's star
 
Kula chuma hicho na ukitaka nyingine naongeza.

Hapo vipi...?
 
Pain will make you a believer...
pain makes you beleive even without your will,

Maumivu yanaweza kukufanya uamini hata bila ridhaa yako,

Naamini kuna mbinu nzuri zaidi ya kufunza haya mambo.

Hata mnyama ukimfunza kwa zawadi kama chakula na kumjali anajifunza haraka kuzidi kwa viboko.
 

Hapo vipi...?
Hapo sawa.
 
Wewe mwalimu wa mchongo tuendeleze ligi hadi mmoja asande
 
Back
Top Bottom