Nguvu, ari na kasi ya UKAWA kuelekea magogoni mwaka 2015 inazidi kukua kila kukicha. Kasi hii ndio inayowafanya CCM kuweweseka kila siku kutaka kuwadhibiti UKAWA lakini jitihada zao ovu zimeshindwa kuzaa matunda. Juzi CC ya CCM iliketi ikulu jijini Dar na ajenda yao kubwa ilikuwa kutafuta mbinu mpya za kuhujumu UKAWA.
Pamoja na njama zote zinazofanywa na CCM kupitia vitengo vyake kama polisi, mahakama, usalama wa CCM (sio Taifa), TBC, nk, UKAWA imezidi kuchanja mbuga na kupasua mawimbi kama kawaida. Hakuna kurudi nyuma.
Ili kuididimiza kabisa CCM, nashauri UKAWA wafanye hivi:
Mosi, wateue mgombe mmoja wa urais na kuachiana majimbo ya uchaguzi, na kata. Napendekeza Dr Slaa awe mgombea urais wa UKAWA, Prof Lipumba mgombea mwenza na Mbatia ateuliwe kuwa Waziri Mkuu baada ya ushindi. Hapa lazima magamba wakae.
Pili, ktk majimbo, kila chama kisimamishe mgombea pale tu kiliposhinda mwaka 2010 na pale iliposhinda CCM, TLP au DP, chama kilichoshika nafasi ya 2 kisimamishe mgombea wake.
Nawasilisha.
:israel: