Elections 2015 UKAWA kusimamisha mgombea Urais 2015

Elections 2015 UKAWA kusimamisha mgombea Urais 2015

Kila mtu ametumbulia mijicho yake kwenye hicho kiti.
 
Nguvu, ari na kasi ya UKAWA kuelekea magogoni mwaka 2015 inazidi kukua kila kukicha. Kasi hii ndio inayowafanya CCM kuweweseka kila siku kutaka kuwadhibiti UKAWA lakini jitihada zao ovu zimeshindwa kuzaa matunda. Juzi CC ya CCM iliketi ikulu jijini Dar na ajenda yao kubwa ilikuwa kutafuta mbinu mpya za kuhujumu UKAWA.

Pamoja na njama zote zinazofanywa na CCM kupitia vitengo vyake kama polisi, mahakama, usalama wa CCM (sio Taifa), TBC, nk, UKAWA imezidi kuchanja mbuga na kupasua mawimbi kama kawaida. Hakuna kurudi nyuma.

Ili kuididimiza kabisa CCM, nashauri UKAWA wafanye hivi:
Mosi, wateue mgombe mmoja wa urais na kuachiana majimbo ya uchaguzi, na kata. Napendekeza Dr Slaa awe mgombea urais wa UKAWA, Prof Lipumba mgombea mwenza na Mbatia ateuliwe kuwa Waziri Mkuu baada ya ushindi. Hapa lazima magamba wakae.

Pili, ktk majimbo, kila chama kisimamishe mgombea pale tu kiliposhinda mwaka 2010 na pale iliposhinda CCM, TLP au DP, chama kilichoshika nafasi ya 2 kisimamishe mgombea wake.

Nawasilisha.

:israel:
 
wazo zuri lakni amini nakwambia chadema na uroho wao hawawez kukubaliana na wewe. Eti waachiane majimbo, na mgombea mwenza atoke cuf! Cdm hawatakubal. Alaf wilbrod slaa hawez tena kuongoza tanzania weledi wake ushashuka sana amebaki kutangatanga tu na kutembelea kwenye kivuli cha UKAWA
 
tpaul, Umenichekesha kwelikweli!!!!!!
Nadhani utakuwa upo mitaa ya unga limited Arusha!

Hivi kwa akili yako na maono yako kichwani, unadhani kuna Watanzania wengine wanaoweza kuongozwa na babu Slaa; mwongo, mnafiki, mhafidhina, mtafuna mali za chama na mkabila!

Watanzania wa kaskazini pekee ndio wanaweza kuongozwa na Slaa na siyo vinginevyo!

CCM chama cha mafisadi, acha waendelee kuongoza! Tanzania bado hakuna wapinzani bali wenye njaa kali na wachumia tumbo ambao hata wakibahatisha wakapata kuongoza nchi wataishia kupigana na kuuwana.
 
Last edited by a moderator:
tpaul, Lipumba ni Mzanzibar ili awe mgombea mwenza?
 
Last edited by a moderator:
tpaul, Mengine umesema vema isipokuwa umeteleza kwenye mgombea mwenza, huyu sharti atoke Zanzibar! Pia Rais anafaa agombee Lipumba, Waziri Mkuu Dr. Slaa, Mbatia apewe Wizara ya fedha!
 
Last edited by a moderator:
Wana JF,
Nani anafaa kugombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA / UKAWA mwaka 2015???

Mandla,
 
Unauliza lakini jibu unalo sana,na usiposikia hili jina unalolifikiria kichwani kwako sijui utafurahi au utanuna?
 
Wana JF,
Nani anafaa kugombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA / UKAWA mwaka 2015???

Mandla,
kwa Tanzania hakuna mwenye sifa zaidi ya Dr.Slaa,sb ni kuwa anajua tatizo la nchi,hana usasi,ni msomi,ana ujasiri,ni mfuatiliaji,anapenda kusoma,anapenda demokrasia,anapenda kuona mali asili yetu inatunufaisha...waziri wake wa fedha awe lipumba,waziri wa mambo ya ndani lema....
 
Back
Top Bottom