Elections 2015 UKAWA kusimamisha mgombea Urais 2015

Elections 2015 UKAWA kusimamisha mgombea Urais 2015

Umakini unahitajika sana. Wakikurupuka kwa matamanio ya kuingia Ikulu utakua ndio mwisho wa upinzani. Kinachofanyika Kenya ni recycling, na watanzania tunapaswa kujiepusha kabisa na siasa za kilaghai kama hizo za Kenya.
 
pia kwenye ubunge vyama vyote kusimamisha mgombea mmoja sehemu ambapo chama kinakubalika mfano kigoma nccr.mwanza chadema na lindi mtwara na lengo ni kuitoa ccm marakani. my take.ccm mwisho wao hatimaye umefika source.mwananchi

Hata maneno yako mwenyewe source yake ni mwanachi? Du!
 
Ni wachache sana watakaopuuza na kubeza mipango hiyo mikubwa ya UNCC ila ukweli nikwamba hata babu yangu kijijini kwetu alikuwa analilia kuungana kwa upinzani ili kuitoa CCM kwenye utawala na kwa taarifa hizi zimempa faraja sana hivyo wanaobeza waendelee ila kwenye nafsi zao hakuna furaha tena!


Sent from my iPad using JamiiForums app
 
Itakuwa bonge la wimbo hili lakini nani atamshirikisha mwengine?? itakuwa Chadema ft.CUF au CUF ft Chadema??,Hapo ndo mbinde itakapoanzia wakubwa ila wakiweza mbona ni bonge la kolabo!
 
Hapo ndipo utaona unafiki wa wanasiasa,Mbowe alisema hawez ungana na chama chochote hapa nchn maana chadema inajitosheleza.

Usiongope, ninakumbukumbu, Mbowe mara baada ya kuingia bungeni, kulikuwa na mtafaruku fulani uliosababishwa na Rashid Hamad, alisema kwa sasa tutaunda peke yetu hadi majeraha yaliyotokea kipindi cha uchaguzi yapone kisha tutaangalia uwezekano wa kuunganisha kambi ya upinzani. Umeyasahau haya maneno?
 
hivi unafikiri ni mara ya kwanza vyama pinzani kufikiria kujiunga ?from 2000 hizo stori zao nasikia Lyatonga Mrema aliwaambia anataka awe Mwenyekiti wao so far ,mgomo wa juzi tu huu kuna wengine walirudi kimya kimya kwenda kuvuta posho bungeni......usisikie zinc njaa mbaya sana inaua umoja

Thibitisha nani aliyerudi bungeni. Mapalala!!!
 
Last edited by a moderator:
Nawatabilia changamoto hasa kwenye kuamua nani agombee jimbo gani hasa ikizingatiwa chadema walikuwa na lengo la kukabiliana na ccm tanzania yote so ukiruhusu kugawana majimbo ujue unavifufua CUF na NCCr.
 
Ni wazo zuri sana na ndicho watanzania tulikuwa tunahitaji. Ila mnahitaji kuweka mipango mikakati mizuri ili kuepuka migogoro hapo mbeleni. ALL THE BEST!
 
Chadema mwisho wenu umefika, toka lini Mbatia na Lipumba wakawa ndugu zenu?? Muwe makini sana
 
Naunga mkono muungano wa vyama pinzani kwa asilimia mia moja kwa 7bu umoja ni nguvu pia itakuwa kazi rahsi kuidondosha ccm pia makubaliano na utekelezaji ndo jambo la mcng wanaobeza kwamba muungano autakuwa na manufaa uyo ni muongo na mnafika kwa 7bu hakuna muungan uco kuwa na makubaliano......
 
kwahiyo kama babu yako alikuwa analilia hayo ulitaka iweje,kwamba hao wapinzani wakipata nchi watampa uDC,They have long and wrong way to go kwasababu wote wamejaa wenyemaslahi binafsi
Ni wachache sana
watakaopuuza na kubeza mipango hiyo mikubwa ya UNCC ila ukweli nikwamba
hata babu yangu kijijini kwetu alikuwa analilia kuungana kwa upinzani
ili kuitoa CCM kwenye utawala na kwa taarifa hizi zimempa faraja sana
hivyo wanaobeza waendelee ila kwenye nafsi zao hakuna furaha tena!


Sent from my iPad using JamiiForums app
 
Back
Top Bottom