Elections 2015 UKAWA na Lowassa unganeni mchukue nchi, wakati ndio huu, mkipuuzia huu ushauri basi tena!

Elections 2015 UKAWA na Lowassa unganeni mchukue nchi, wakati ndio huu, mkipuuzia huu ushauri basi tena!

Mimi ni mmoja wa watu niliyekuwa nikipinga Lowassa asichaguliwe CCM sababu ni moja tu alikuwa threat kubwa kwa UKAWA. Angepitishwa Lowassa UKAWA ingebaki historia siasa haina rafiki wa kudumu wala adui hata Slaa alivyokatwa CCM alihamia CHADEMA.

Nawaomba CHADEMA na UKAWA msipoteze hii turufu huyu mtu bado yupo vinywani mwa watu wengi.Bado ana influency kubwa kwenye media ambacho ni kitu muhimu wanaomkataa asipokelewe hawaijui siasa.

Kama Lowassa akipokelewa akapeperusha bendera ya UKAWA mtauona mtikisiko wa hii nchi.UKAWA watabeba kila kitu kuanzia Ubunge hadi urais. Lowassa anatakiwa atoke hadharani aeleze uhusika wake wa Richmond naamini akiwa CHADEMA atakua huru kusema.

Ni bora ushirikiane hata na shetani ili mradi uitoe CCM madarakani nyuma ya Lowassa kuna watu wengi sana.Narudia tena kwa wanachadema wenzangu siasa haina rafiki wala adui wa kudumu.

Kama lengo kushika dola shirikiana hata na shetani umalize mchezo, kama lengo ni kupinga ufisadi tutabaki hivi hivi tunapinga ufisadi huku tukiwa wapinzani, vita ni vita tu.

Kwanini nyinyi wa ACT msimchukue?
 
Uzi wako una mantiki nzuri sana, sema UKAWA wanaanzaje kumsafisha kwa wananchi ili aeleweke vizuri?

Ndio Sasa Yeye Mwenyewe Itabidi Aseme A 2 Z Nini Kilitokea Na Nani Mchafu Kwenye Kashfa Zakee...

Akijielezea Ataeleweka Akimua Kukaa Kimya Kazi Anayo
 
Nimezaliwa Na chembechembe za kupenda mabadiliko, na-support UKAWA kwa akili Na imani, lakini sijawahi kuamini hata moja kutoka kwa lowasa, iwapo kweli jamaa ataingia UKAWA Na kupewa walau uanachama wa kawaida Tu, kwa kigezo eti ana watu nyuma yake, basi binafsi tutapishana mlangoni, Kura yangu CCM waihesabie kwao!.
 
Kumpokea Lowasa kwenu haita jalisha hata CUF mlio wadhihaki leo mmeungana nao, CUF mlikuwa mnawaita majina yote yasiofaa leo mmeungana nao, haita shangaza kwenye kusaka maslahi mnakula matapishi yenu.

kwani kuelewana ni vibayaa?? NDOOOORRRRROBBOOOOweee!!!
 
Naona huna nia njema na Lowasa.
Kwa maoni yangu UKAWA yatosha.
Ushauri wa bure kwa Lowasa: akapunzike, siasa kwake basi. Ya CCM ikimshinda kwenda kutangatanga uzeeni hakutamfikisha popote isipokuwa atajizolea aibu na kuporomoshwa zaidi.

Hata hivyo joto la umaarufu wa lowasa limeshapungua. Angefanya maamuzi ya kuhama palepale alipofahamu jina lake limekatwa. It is now too late. Ukawa waendelee wenyewe.
 
Kwani Lowasa naye alitoka nje ya Bunge la Katiba?.... Kwa nini sasa asimame kwa tiketi ya Ukawa?

swali zuri kwa UKAWA. PIA lowasa na team yake ni
mafisadi au sio. je akija ukawa atakuwa msafi??
au mnaangalia pesa.KWA STAILY HIYO TUELEWEJE MKIFIKA IKULU. Yeye kamq sio fisadi kaonewa na KWANZA AJISAFISHE AFUNGUKE WAZI TUMUELEWE NDIO AOMBE KUJIUNGA.
KAMA YUPO KIMYA AKAE HUKO HUKO CCM
 
Lowasa angetusaidia kuleta majimbo mengi ya wabunge kwenda upinzani...slaa hawezi kupambana na magufuli akipata hata 25percent, lakini lowasa anaweza kupata hata 35percent..lowasa hawezi shinda nje ya ccm hilo lipo wazi lakini lazima apate zaidi ya 35percent, ambaye atatusaifia kupata wabunge wengi...
Uzuri wa lowasa ana pesa na ana influence kwenye vyombo vya habari, hivyo tutapata coverage kubwa sana..
Ukweli ambao hsusemwi dr slaa ameshuka sana kisiasa,
 
kama chadema au ukawa wakimchukua lowassa nachana kadi na ktk maombi yangu kwa mungu nitaomba wasipate hata kula moja
coz hivi leo unamteteaje lowassa jukwaan wakati nyinyi mlikuwa mnasema ni fisadi leo mtawambia nini wananchi?
kumbukeni Mwakyembe anazo kalatasi 5 ambazo akuzisoma bungeni kwa kumtunzia Heshima Lowassa sasa zitasemwa ktk kampeni.
ccm watasema cc tumemfukuza fisadi wao wamempokea fisadi sasa kati ya baba na jiran nani anajua mtoto vizuri mtajibu nini?
kingine itakuwa fedhea kwa Dr slaa ambae alikuwa padre leo kuonekana jukwaan na lowassa akimnadi yule aliesemekana fisadi papa.
someni alama za nyakati lowasa kwa sasa ni kama gari sasa kila mda linashuka thamani unaweza kulinunia million 100 ukaja ukaliuza million 1
wafwasi wake now wako busy kujipendeza kwa magufuli ni bora kumsimamisha kugombea urais mzee mtei ili kulinda heshima ya chama kuliko kumsimamisha lowassa mkaenda kukiuwa chama
wananchi wa leo sio wa mwaka 47 lowassa is so yesterday compare to magufuli for now
 
Haya ndo maneno.lowasa amechelewa kujiunga na ukawa asinngesubiri kukatwa,angekuja mapema hatakabla ya kutia nia ccm.tungemkubali,na ukwa tungemsafisha kwa mchanga wa ziwa victoria
 
Lwasa akienda chadema nitaamini kwamba sisiemu itatawala kwa muda mrefu sana, maana yake HAMNA upinzani.
Wanapanga na kupangua wenyewe!
 
Ndio Sasa Yeye Mwenyewe Itabidi Aseme A 2 Z Nini Kilitokea Na Nani Mchafu Kwenye Kashfa Zakee...

Akijielezea Ataeleweka Akimua Kukaa Kimya Kazi Anayo


Wee acha kuwa kama mchawi... think forward mmanina...unaudhi sana..!!

Watu tunafikiria KUUNGANISHA NGUVU KUITOA CCM MADARAKANI, KULETA MAENDELEO KWA KILA MMOJA NA TAIFA KWA HARAKA, sbb system ya CCM has proven FAILURE, ww unaongelea mambo ya Richmond of which Lowassa hahusiki, pili hayo yameshapita, hayatusaidii kwa sasa, sasa ni wakati wa ukombozi, akili za haraka na kuwa very active with time, ili KUHAKIKISHA Muungano wa UKAWA na Lowassa unaitoa CCM madarakani..

Acha upuuzi bana, plz, we hv 2 days only kuumua hatima ya nchi yetu, which is Muungano wa UKAWA + Lowassa..

Sasa ww unafikiria kichawi humu, kitu ambacho hakitusaidii kwa sasa hakitakiwi kufikiria, the main aim ni USHINDI, kuwaokoa watanzania... sio unaongelea mambo ya miaka kadhaa huko nyuma kwa sasa of which HAYATATULETEA USHINDI.. acha akili za kichawi...😨😨😨😨😨😨😨👿👿👿
 
Kwangu Mimi swali kubwa bado ni kuhusu scandal ya kampuni ya kufua umeme ya Richmond.

Kwamba, laiti umma ukipata Maelezo sahihi ya nani hasa muhusika mkuu wa kashfa hii kama si yeye, sioni tatizo la EL la kuhamia chama chochote cha upinzani!

Lakini kama EL hatatueleza ni ukweli upi hasa haukusemwa kuhusu Richmond na huo ukweli ukamtenga yeye na kashfa hiyo, bado EL ni tatizo ktk chama chochote atakachojiunga nacho sasa!.

Na option nzuri zaidi niionayo mimi ni kwa huyu bwana kupambana akiwa humohumo ndani ya chama chake, kusema kila alichonacho kuhusu kashfa anazodai anasingiziwa ili wenzake wamuamini na wamwelewe hukohuko.

Ni kwa kufanya hivi atajenga taswira ndani ya chama na wanachama wa CCM kuwa mtu wao kumbe ameonewa kwa sababu ambazo kiukweli hazipo na kutoka hapo sasa tutashuhudia mtafaruku mkubwa ndani ya CCM na hii automatic itakuwa faida kwa upinzani!

Kwa hili atabaki kuwa na heshima yake na kwa hakika atakuwa amesaidia upinzani hukohuko aliko pasipo na ulazima wa kuhama chama. Si atakuwa ameamua kumwaga ugali baada ya wao kuwa wamemwaga mboga bwana, au siyo?
 
Siamini kama lowasa akija UKAWA atakuwa na impact tunayodhani. Ukawa wawe makini sana, wanaweza kupotezwa hata kabla uchaguzi haujaanza.

UKAWA should not buy the idea of coopting Lowassa and then picking him as their presidential candidate as suggested by some of his followers; to do that will be contrary to UKAWA"S fight against impunity and hence its own contradiction!! If Chadema agrees with MBOWE"s dictatorial tendencies of forcing his wishes, then that will sound the demise of Chadema as a viable political party.
 
Very objective!. Tatizo la UKAWA ni kukosekana kwa watu wenye uelewa wa level hii!

Pasco

Pasco, UKAWA wakiachia opportunity hii kwa sababu yoyote ile, then, tusahau mabadiliko ya hivi karibuni.
 
Lowassa ni backup nzuri kwa ukawa, uongozi ni mfumo siyo rais! Fikra zenu sasa zilenge kuondoa mfumo mmoja na kuweka mfumo mwingine kama USA na siyo kujikita tu kwenye agender ya urais.

Wazo zuri sana.
 
Wee acha kuwa kama mchawi... think forward mmanina...unaudhi sana..!!

Watu tunafikiria KUUNGANISHA NGUVU KUITOA CCM MADARAKANI, KULETA MAENDELEO KWA KILA MMOJA NA TAIFA KWA HARAKA, sbb system ya CCM has proven FAILURE, ww unaongelea mambo ya Richmond of which Lowassa hahusiki, pili hayo yameshapita, hayatusaidii kwa sasa, sasa ni wakati wa ukombozi, akili za haraka na kuwa very active with time, ili KUHAKIKISHA Muungano wa UKAWA na Lowassa unaitoa CCM madarakani..

Acha upuuzi bana, plz, we hv 2 days only kuumua hatima ya nchi yetu, which is Muungano wa UKAWA + Lowassa..

Sasa ww unafikiria kichawi humu, kitu ambacho hakitusaidii kwa sasa hakitakiwi kufikiria, the main aim ni USHINDI, kuwaokoa watanzania... sio unaongelea mambo ya miaka kadhaa huko nyuma kwa sasa of which HAYATATULETEA USHINDI.. acha akili za kichawi...😨😨😨😨😨😨😨👿👿👿

Kwa mawazo yako uliyoandika hapa inaonyesha ni jinsi gani inaonyesha unashindwa kuandika points za kueleweka zaidi ya kupayuka na kumkashifu mwenzio. Eti Lowassa hausiki kabisa na Richmond, eti Lowassa akiungana na UKAWA basi CCM watatoka madarakani, hivi wewe unafikiri wana UKAWA wote wana akili mgando na vichwa vya kuku kusahau aliyofanya huyo mheshimiwa wako akiwa kiongozi? Hivi haujui kwamba UKAWA itateteleka endapo huyo bwana atajiunga nao? Hivi haujui kwamba ndani ya UKAWA wapo watu makini ambao hawapo tayari kuona muungano wao unasabaratika. Huyo bwana akienda UKAWA basi watu wengi tu makini wa muungano huu nikiwemo mimi mwenyewe nitajitoa kabisa na sitoweza kumsupport.
Unajua ni kwanini CCM walimkata huyo bwana?
Kaa chini fikiria kwanza kabla ya kutoa maneno makali.
Unajua who is behind Lowassa? Na unajua ametoa ahadi gani kwao akikamata urais anaoutaka kwa udi na uvumba?
Hivi kwanza tumia akili kidogo fikiria tu utajiri alionao huyo bwana yeye na familia yake kaupata vipi na wapi. UKAWA imeshakuwa stable we don't need anyone from CCM.
Lakini swali la mwisho homework kwako, nenda kafikirie upya je kweli waliokuwa wanajazana kwenye mikutano ya huyo bwana wote walikuwa serious wanamsupport? Mwisho usisahau kuna friends of Lowassa, Team Lowassa hao wote sijui UKAWA watawaacomodate vipi kwenye utawala endapo kweli ndoto zako zitatimia.
Go home and think twice, ila jamaa yako hatumtaki.
 
UKAWA should not buy the idea of coopting Lowassa and then picking him as their presidential candidate as suggested by some of his followers; to do that will be contrary to UKAWA"S fight against impunity and hence its own contradiction!! If Chadema agrees with MBOWE"s dictatorial tendencies of forcing his wishes, then that will sound the demise of Chadema as a viable political party.

No such a thing bro!

And if there is, then we should understand, this is not a coincidence and despite it is something which was professionally planned long, long time ago!!

However, to make it work thoroughly and to clear all benefit of doubts among opposition members and supporters in order to understand and believe, there must be a viable explanation why this man!

Contrary to that, I agree with you.
 
Back
Top Bottom