Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
I agree with you! Lowassa is a gold for system change in the Country.
Magamba in action.
Kwa kuwa tunajua nchi yetu tunayo TISS ambayo moja ya jukumu lake kubwa ni kuhakikisha kuwa Sisiemu inatawala daima.
Inaelekea hii hoja ambayo imeibuka kwa nguvu sana katika siku 2 hizi humu JF kabla Ukawa hawajamtaja mgombea wao itakuwa ime-originate kutoka huko.
Hivi inawezekanaje Chadema ambayo imejipambanua na agenda yao kuu ya kupambana na ufisadi wa CCM kwa nguvu zote sasa impokee mtu kutoka CCM ambaye anafahamika kama fisadi papa?
Hivi inawezekanaje mtu ambaye hata Chama chake mwenyewe kilimuita kuwa ni fisadi papa na chama hicho kikampa jukumu Nape ambaye alizunguka nchi nzima kuwatangazia wananchi kuwa mafisadi papa watatu (akiwemo Lowassa) wamepewa siku 90 na chama chao ili wajivue gamba sasa ndiyo Chadema kimpokee kama shujaa wao anayetakiwa kuwapeleka Ikulu?
Kwa hiyo huku kupigiwa debe kupita kiasi humu JF siku 2 hizi ili Chadema impokee fisadi Lowassa kwenye chama chao ni mpango madhubuti ulioandaliwa na Sisiemu kupitia kitengo 'chao' cha usalama wa Sisiemu.
Huyo jamaa mahali pekee panapomfaa kama kweli atataka kuondoka CCM si pengine bali ni kwenda kwenye chama cha 'swaiba' wake, chama cha AKTI.
Atakayebisha hili atakua hana jicho la tatu.Naungana na wewe kwamba kama UKAWA wanataka wabaki kama chama cha upinzani kwa miaka 10 ijayo na waikatae hii golden chance ya Lowassa.
Hata hivyo nasikia mzee wa maamuzi magumu yuko chini ya ulinzi mkali wa TISS sasa sijui itakuwaje.
CCM hawatokubali kirahisi kumuachia Lowassa aje upinzani.
Hatuhitaji kuhamisha ufisadi from ccm to ukawa. Na kama wanampitisha Lowasa kugombea maana yake hakutakuwa na mabadiliko tunayoyataka na ni kubadili CHaDEMA kuwa ccm.
Ninachoshauri, Lowasa kama watanzania wengine, akiomba kujiunga na CHaDEMA akaribishwe lakini asipewe uongozi. Anatakiwa asihame na mashart yake ya kugombania uraisi. ahame na mtazamo mpya wa uzalendo kwamba anataka sasa kujenga nchi kwa mtazamo sahihi kwa taifa si ule wa kifirauni ccm.
CHADEMA haiwezi kuzuia mtu kujiunga kwa sababu lengo lake ni kuhakikisha inakua na inabadilisha mitazamo ya Watanzania wenye mawazo ya kifisadi, rushwa na uhayawani wa ccm kuwa Watanzania wazalendo wajenzi wa taifa, Lowasa akiwa mmoja wao. Na baada ya October, Watanzania wote watatakiwa kuwa na uwajibikaji kwa taifa katika m isingi ya UKaWA lowasa akiwe mmoja wao awe ndani ama nje ya ccm.
Suala la uongozi hattutampigia kura kwa kuwa hatutaikomboa nchi kwa kuongozwa na fisadi. Lakini uanachama sidhani kama kuna mtu anamzuia kwa kuwa Milango ya kujiunga nadhani iko wazi kwa Watanzania wote ili kukuza chama na kuondoa itikadi za kifisadi za ccm kwakuwafanya wapya.
Ahsanteni,

Wewe siyo UKaWA. Unampa uraisi kwa misingi gani? Kwamba kwa kuhama ccm ufisadi wake umekwisha? Fikiria twice.
Mimi ni mmoja wa watu niliyekuwa nikipinga Lowassa asichaguliwe CCM sababu ni moja tu alikuwa threat kubwa kwa UKAWA. Angepitishwa Lowassa UKAWA ingebaki historia siasa haina rafiki wa kudumu wala adui hata Slaa alivyokatwa CCM alihamia CHADEMA.
Nawaomba CHADEMA na UKAWA msipoteze hii turufu huyu mtu bado yupo vinywani mwa watu wengi.Bado ana influency kubwa kwenye media ambacho ni kitu muhimu wanaomkataa asipokelewe hawaijui siasa.
Kama Lowassa akipokelewa akapeperusha bendera ya UKAWA mtauona mtikisiko wa hii nchi.UKAWA watabeba kila kitu kuanzia Ubunge hadi urais. Lowassa anatakiwa atoke hadharani aeleze uhusika wake wa Richmond naamini akiwa CHADEMA atakua huru kusema.
Ni bora ushirikiane hata na shetani ili mradi uitoe CCM madarakani nyuma ya Lowassa kuna watu wengi sana.Narudia tena kwa wanachadema wenzangu siasa haina rafiki wala adui wa kudumu.
Kama lengo kushika dola shirikiana hata na shetani umalize mchezo, kama lengo ni kupinga ufisadi tutabaki hivi hivi tunapinga ufisadi huku tukiwa wapinzani, vita ni vita tu.