Elections 2015 UKAWA na Lowassa unganeni mchukue nchi, wakati ndio huu, mkipuuzia huu ushauri basi tena!

Elections 2015 UKAWA na Lowassa unganeni mchukue nchi, wakati ndio huu, mkipuuzia huu ushauri basi tena!

Siamini kama lowasa akija UKAWA atakuwa na impact tunayodhani. Ukawa wawe makini sana, wanaweza kupotezwa hata kabla uchaguzi haujaanza.
 
Magamba in action.

Kwa kuwa tunajua nchi yetu tunayo TISS ambayo moja ya jukumu lake kubwa ni kuhakikisha kuwa Sisiemu inatawala daima.

Inaelekea hii hoja ambayo imeibuka kwa nguvu sana katika siku 2 hizi humu JF kabla Ukawa hawajamtaja mgombea wao itakuwa ime-originate kutoka huko.

Hivi inawezekanaje Chadema ambayo imejipambanua na agenda yao kuu ya kupambana na ufisadi wa CCM kwa nguvu zote sasa impokee mtu kutoka CCM ambaye anafahamika kama fisadi papa?

Hivi inawezekanaje mtu ambaye hata Chama chake mwenyewe kilimuita kuwa ni fisadi papa na chama hicho kikampa jukumu Nape ambaye alizunguka nchi nzima kuwatangazia wananchi kuwa mafisadi papa watatu (akiwemo Lowassa) wamepewa siku 90 na chama chao ili wajivue gamba sasa ndiyo Chadema kimpokee kama shujaa wao anayetakiwa kuwapeleka Ikulu?

Kwa hiyo huku kupigiwa debe kupita kiasi humu JF siku 2 hizi ili Chadema impokee fisadi Lowassa kwenye chama chao ni mpango madhubuti ulioandaliwa na Sisiemu kupitia kitengo 'chao' cha usalama wa Sisiemu.

Huyo jamaa mahali pekee panapomfaa kama kweli atataka kuondoka CCM si pengine bali ni kwenda kwenye chama cha 'swaiba' wake, chama cha AKTI.



Mkuu,unaona mbali sana,kula like

Hakuna mwanaUKAWA mwenye anatamani Lowasa ahamie CDM seuze kugombea urais

Lowasa ni mchafu,ana taswira mbaya mbele ya wananchi,na nakwambia leo Lowasa akikaribishwa CDM na akapewa nafasi agombee,kwanza hatashinda(goli la mkono litakuwa even more intensive) lakini pia CDM itapoteza voters wengi sana

Ndugu mleta mada na wenzio lazima mtakuwa mnafanya kazi maalum ya kusambaza propaganda ili Lowasa apokelewe CDM mkaishtaki CDM kuwa inafuga majizi na mafisadi
 
Hatufundishwi Maelekezo tulipo toka na tulipo hatukua na Lowasa Asanteni

Chadema Kwanza
 
mchambuzixx

Hata mwalimu Julius alisema Upinzani itatoka ndani ya wanaccm wenyewe. Yani hii ndio chance iliyokuwa inasubiriwa kwa miaka yote. UKAWA mchukueni Lowassa kwani system yenu haitakuwa ya mafisadi na hata lowassa akiwa rais system itamdhibiti ivyo hatakuwa na madhara. Lowassa akihamia Ukawa mjue atakuja na wabunge, hata kama hatakuja nao lkn uwezo wa kuwapata wengi upo. Kumchukua lowassa ndio itakuwa mwisho wa ccm. Kama kweli Mbowe anapigania lowassa kuingia Ukawa basi Mbowe anaona mbali. Nimemkubali
 
Last edited by a moderator:
Atakayebisha hili atakua hana jicho la tatu.Naungana na wewe kwamba kama UKAWA wanataka wabaki kama chama cha upinzani kwa miaka 10 ijayo na waikatae hii golden chance ya Lowassa.
Hata hivyo nasikia mzee wa maamuzi magumu yuko chini ya ulinzi mkali wa TISS sasa sijui itakuwaje.
CCM hawatokubali kirahisi kumuachia Lowassa aje upinzani.

HUYU MTU ANAINFLUENCE KUBWA SANA NA NI DHAHABU KWA CCM /

#MAGUFURI IN OPENLY HEART AMTANGAZE KUWA #LOWASSA NDIYE WAZIRI MKUU WAKE / NADHANI ULE UMCHAKACHAKA WAKE UTAFANYA KAZI VIZURI ZAIDI KAMA MTENDAJI MKUU WA SERIKALI/ii
 
mchambuzixx

Kuna ukweli ktk hii post yako mkuu,kwa kuwa nia ni kumtoa mkoloni mweusi basi hata lowasa atabadilika tu akiwa ukawa na kuwa na mawazo ya kimapinduzi
 
Last edited by a moderator:
Naona thread nyingi sana za kusisitiza Lowasa ahamie ukawa. Hivi akihama, anahamia peke yake? Mnajua rafiki zake lowasa waliokuwa wanamchangia? Huyu abaki huko huko au aende ACT. Kwenda ukawa itakuwa ni sawa na kutia doa kwenye nguo nyeupe..
 
Ukawa haimuhitaji fisadi huwezi kuweka ubovu kwenye gari mpya ukaweka engen mbovu low as a ni engen mbovu
 
mkuu kwani wewe ndo yule mbowe, tafadhali nikumbushe kidogo


Hatuhitaji kuhamisha ufisadi from ccm to ukawa. Na kama wanampitisha Lowasa kugombea maana yake hakutakuwa na mabadiliko tunayoyataka na ni kubadili CHaDEMA kuwa ccm.


Ninachoshauri, Lowasa kama watanzania wengine, akiomba kujiunga na CHaDEMA akaribishwe lakini asipewe uongozi. Anatakiwa asihame na mashart yake ya kugombania uraisi. ahame na mtazamo mpya wa uzalendo kwamba anataka sasa kujenga nchi kwa mtazamo sahihi kwa taifa si ule wa kifirauni ccm.

CHADEMA haiwezi kuzuia mtu kujiunga kwa sababu lengo lake ni kuhakikisha inakua na inabadilisha mitazamo ya Watanzania wenye mawazo ya kifisadi, rushwa na uhayawani wa ccm kuwa Watanzania wazalendo wajenzi wa taifa, Lowasa akiwa mmoja wao. Na baada ya October, Watanzania wote watatakiwa kuwa na uwajibikaji kwa taifa katika m isingi ya UKaWA lowasa akiwe mmoja wao awe ndani ama nje ya ccm.

Suala la uongozi hattutampigia kura kwa kuwa hatutaikomboa nchi kwa kuongozwa na fisadi. Lakini uanachama sidhani kama kuna mtu anamzuia kwa kuwa Milango ya kujiunga nadhani iko wazi kwa Watanzania wote ili kukuza chama na kuondoa itikadi za kifisadi za ccm kwakuwafanya wapya.

Ahsanteni,
 
Mpaka kuwa na vyama vya upinzani wote wametoka CCM hivyo si ajabu kuwa na lowasa na pengine ni kumtumia kupata ushindi ili kuiondoa CCM madarakani.
 
Hatuhitaji kuhamisha ufisadi from ccm to ukawa. Na kama wanampitisha Lowasa kugombea maana yake hakutakuwa na mabadiliko tunayoyataka na ni kubadili CHaDEMA kuwa ccm.


Ninachoshauri, Lowasa kama watanzania wengine, akiomba kujiunga na CHaDEMA akaribishwe lakini asipewe uongozi. Anatakiwa asihame na mashart yake ya kugombania uraisi. ahame na mtazamo mpya wa uzalendo kwamba anataka sasa kujenga nchi kwa mtazamo sahihi kwa taifa si ule wa kifirauni ccm.

CHADEMA haiwezi kuzuia mtu kujiunga kwa sababu lengo lake ni kuhakikisha inakua na inabadilisha mitazamo ya Watanzania wenye mawazo ya kifisadi, rushwa na uhayawani wa ccm kuwa Watanzania wazalendo wajenzi wa taifa, Lowasa akiwa mmoja wao. Na baada ya October, Watanzania wote watatakiwa kuwa na uwajibikaji kwa taifa katika m isingi ya UKaWA lowasa akiwe mmoja wao awe ndani ama nje ya ccm.

Suala la uongozi hattutampigia kura kwa kuwa hatutaikomboa nchi kwa kuongozwa na fisadi. Lakini uanachama sidhani kama kuna mtu anamzuia kwa kuwa Milango ya kujiunga nadhani iko wazi kwa Watanzania wote ili kukuza chama na kuondoa itikadi za kifisadi za ccm kwakuwafanya wapya.

Ahsanteni,

Seen and noted!
 
Wewe siyo UKaWA. Unampa uraisi kwa misingi gani? Kwamba kwa kuhama ccm ufisadi wake umekwisha? Fikiria twice.

Pole sana endapo Lowassa alikufanyia ufisadi wewe na wazazi wako kuliko ufisadi uliofanywa na familia ya JK.
 
Sasa ile kashfa ya ufisadi itahamia kwa nan???dah ama kwel hakuna chama chenye uzalendo wowote vyoooote vinawaza matumbo tuuuu!!
 
Nimezaliwa Na chembechembe za kupenda mabadiliko, na-support UKAWA kwa akili Na imani, lakini sijawahi kuamini hata moja kutoka kwa lowasa, iwapo kweli jamaa ataingia UKAWA Na kupewa walau uanachama wa kawaida Tu, kwa kigezo eti ana watu nyuma yake, basi binafsi tutapishana mlangoni, Kura yangu CCM waihesabie kwao!.
 
Mimi ni mmoja wa watu niliyekuwa nikipinga Lowassa asichaguliwe CCM sababu ni moja tu alikuwa threat kubwa kwa UKAWA. Angepitishwa Lowassa UKAWA ingebaki historia siasa haina rafiki wa kudumu wala adui hata Slaa alivyokatwa CCM alihamia CHADEMA.

Nawaomba CHADEMA na UKAWA msipoteze hii turufu huyu mtu bado yupo vinywani mwa watu wengi.Bado ana influency kubwa kwenye media ambacho ni kitu muhimu wanaomkataa asipokelewe hawaijui siasa.

Kama Lowassa akipokelewa akapeperusha bendera ya UKAWA mtauona mtikisiko wa hii nchi.UKAWA watabeba kila kitu kuanzia Ubunge hadi urais. Lowassa anatakiwa atoke hadharani aeleze uhusika wake wa Richmond naamini akiwa CHADEMA atakua huru kusema.

Ni bora ushirikiane hata na shetani ili mradi uitoe CCM madarakani nyuma ya Lowassa kuna watu wengi sana.Narudia tena kwa wanachadema wenzangu siasa haina rafiki wala adui wa kudumu.

Kama lengo kushika dola shirikiana hata na shetani umalize mchezo, kama lengo ni kupinga ufisadi tutabaki hivi hivi tunapinga ufisadi huku tukiwa wapinzani, vita ni vita tu.

Masikin nchi yangu haina wapinzan bali waganga njaa...a.k.a waroho wa madaraka
 
Wana ccm wapumbavu sana na wanadhani kila mtu mpumbavubkama wao...yaani baada ya kumtosa mwizi mwenzao ndio wampigie chapuo aje ukawa?!!
Hata aibu hamuoni..huku si selo kupokea na kuhifadhi majambazi
 
Back
Top Bottom