Hatuhitaji kuhamisha ufisadi from ccm to ukawa. Na kama wanampitisha Lowasa kugombea maana yake hakutakuwa na mabadiliko tunayoyataka na ni kubadili CHaDEMA kuwa ccm.
Ninachoshauri, Lowasa kama watanzania wengine, akiomba kujiunga na CHaDEMA akaribishwe lakini asipewe uongozi. Anatakiwa asihame na mashart yake ya kugombania uraisi. ahame na mtazamo mpya wa uzalendo kwamba anataka sasa kujenga nchi kwa mtazamo sahihi kwa taifa si ule wa kifirauni ccm.
CHADEMA haiwezi kuzuia mtu kujiunga kwa sababu lengo lake ni kuhakikisha inakua na inabadilisha mitazamo ya Watanzania wenye mawazo ya kifisadi, rushwa na uhayawani wa ccm kuwa Watanzania wazalendo wajenzi wa taifa, Lowasa akiwa mmoja wao. Na baada ya October, Watanzania wote watatakiwa kuwa na uwajibikaji kwa taifa katika m isingi ya UKaWA lowasa akiwe mmoja wao awe ndani ama nje ya ccm.
Suala la uongozi hattutampigia kura kwa kuwa hatutaikomboa nchi kwa kuongozwa na fisadi. Lakini uanachama sidhani kama kuna mtu anamzuia kwa kuwa Milango ya kujiunga nadhani iko wazi kwa Watanzania wote ili kukuza chama na kuondoa itikadi za kifisadi za ccm kwakuwafanya wapya.
Ahsanteni,