Elections 2015 UKAWA na Lowassa unganeni mchukue nchi, wakati ndio huu, mkipuuzia huu ushauri basi tena!

Lowasa ameshaitumikia tanzania kwa zaidi miaka 38 akiwa kiongozi ndani serikali ya ccm imewafanyia nini watanzania zaidi kutuingiza hasara kubwa na mkataba wa kampuni ya Richmond .
Ningekuwa mshauri wa Lowasa ningeshauri baada ya kutumia pesa nyingi kusaka madaraka na kuishia jina lake KUKATWA kwenye tume ya maadili angetulia na kuangalia zaidi afya yake ndo ya umuhimu kuliko huo uraisi anaoutaka kwa nguvu kiasi hicho .
Macho na masikio ya watanzania wanasubiri kwa hamu kubwa kutangazwa rasmi mgombea uraisi kupitia #UKAWA rasmi kesho .
UKAWA NDO TUMAINI JIPYA KWA WATANZANIA WOTE.mkuu Pasco umeshapitia humu safari ya matumaini bado inaendelea?
 
Last edited by a moderator:
Naomba nitoe hoja kwa wale wote wanaotudanganya kwa mgongo wa uchafu ohoo mara ufisadi wa Lowassa waje hapa na waseme huo ufisadi ni upi na uchafu ni upi? na ni nani aliye msafi ndani ya CCM ukianzia na uongozi wa juu? Nitajie hata kiongozi 1 wa CCM ambaye ni msafi hapa?

Tuache hizi hoja nyepesi za ufisadi na uchafu ambao hauwezi kuuthibitishia umma ili kuwafitini watu hasa UKAWA ili waache kutumia nafasi hii ili kuiondoa CCM madarakani. Na kama hamjui, basi naomba niwape siri sasa, mpaka sasa CCM wana hofu sana na move yoyote atakayochukua Lowassa. Kila siku na mbinu zao zote wanataka Lowassa asijiunge CHADEMA wala UKAWA. CCM wanataka kuona kama Lowassa akiondoka CCM, then ajiunge ACT, kwani kwao itkuwa imewasaidia sana na watashinda ki urahisi sana. CCM wana hofu sana iwapo Lowassa atajiunga CHADEMA na UKAWA ikaendelea kuwa pamoja.
 
Mkuu umeongea jambo la maana sana.Na hili ndilo tulilokua tunalijadili hapa kwetu muda mfupi uliopita nashangaa baada ya kuingia humu nakuta huu uzi.
Lowassa ni kete pekee iliyobakia ya UKAWA kuingia Magogoni.Ni ukweli usiopingika kwamba kwa hali ya sasa hakuna mwanaUKAWA yeyote mwenye nguvu/mvuto wa kupambana na Magufuli kwa sasa.

Kumchukua Lowassa na kumtangaza kama mgombea wao wa urais kutarahisisha sana safari ya miaka nenda rudi ya Upinzani kuingia Ikulu.
Lowassa anakubalika na watu wengi sana, mimi binafsi ni mwanaUKAWA ila nilikua nimeapa kumpigia Lowassa kura yangu kama angepitishwa kama mgombea wa CCM.
Lowassa ni mwanaCCM tena mkongwe.Hakuna mbinu chafu za CCM ambazo yeye hazijui.
Kubwa ni ile ya wizi wa kura.

Ni ndoto kwa upinzani kuamini kwamba wataenda Ikulu wenyewe tena walewale maana mgombea kutoka upinzani ni Slaa ambaye kiukweli amepoteza mvuto wa kisiasa tofauti na mwaka 2010.
 
Uzi wako una mantiki nzuri sana, sema UKAWA wanaanzaje kumsafisha kwa wananchi ili aeleweke vizuri?

Wananchi gani? na kumsafisha kwa lipi? Je kuhusu Richmond unakumbuka Mwakyembe alisemaje bungeni? ni kwanini hakusema yote? Muulizeni awaambie, je zaidi ya Lowassa ni nani alitia mkono kwenye Richmond?

Lowassa haitaji kusafishwa na hakika hii nafasi UKAWA wasiache hata kidogo.
 
Sijawahi kuona ushauri wa hovyo kama huu wa kwako hapa.

Hakuna haja ya kuiondoa ccm madarakani ikiwa tutaweka wagombea wale wale mafisadi walioua nchi yetu. Ukiitoa ccm kwa kuwa imekuwa fisadi na mafisadi ndio hao hao kina Lowasa, halafu unampa uongozi wa nchi fisadi gumegume yule yule Lowasa, utakuwa ama una maradhi ya akili ama huna msingi wala sababu ya maana ya kutafuta mabadiliko. Utakuwa unatafuta mabadiliko kwa maslahi yako binafsi na si ya umma kitu ambacho UKawa hakikubaliki.

LAWASA AKIGOMBEA URAISI KWA CHAMA CHOCHOTE HATUMPIGII KURA SISI WATANZANIA HALISI TUNAOTAKA TANZANIA YETU ASILIA.

Hueleweki unapoongelea Lowasa awe mgombea wa UKAWA, huku references and standards zako zote ziko ccm!. Kwa kuwa ccm wote ni mafirauni na hakuna msafi, basi ukawa wasimamishe tu hilo fisadi nao? Wewe vipi lakini?

UKaWA inachukua nchi without haja ya mkono wa mafisadi!.

Hii kumtengenezea njia mwenye safari ya matamanio, imebuma, tafuta mlango mwingine. Labda jaribu kwa Zito au IPPT Maendeleo!, Ukawa kumejaa nahata hivyo access denied!.

teh teh teh teh kwani ufisadi ni mtu au ni system?? Labda nikuulize swali dogo tu, hebu tufanye EL ameweza kuwa Rais kupitia UKAWA, wewe unaamini EL atawashawishi UKAWA wote wawe wezi na kutuibia waTanzania?? Vipi ikiwekwa mifumo ambaye haimpi Rais mwanya wa kufanya hivyo?? Yaani wewe unaamini pamoja na Intergrity kubwa ya Dr. Slaa as PM, Lipumba as Minister of Finance, Lisu kama Waziri wa Sheria wataingizwa mkenge wawe wanasaini mikataba ya kukandamiza watanzania, wawe wanapitisha miswada ya kulinda viongozi e.t.c.. Unayaamini hayo?? Na kama unayaamini, una uhakika gani kwamba hata tukiwapeleka kama walivyo sasa hawatoyafanya hayo??

teh teh teh hawa ndio elites wa JF bana.. wako humu tangia 2008.. Mara nyingi nyie mkisema kitu ndio kinakuwa final say humu teh teh teh.. Mnatukuzwa sana na sie tulioingia humu 2014 teh teh teh
 
CHADEMA changamkieni hilo Dili, wananchi tumeichoka CCM, mkishindwa sasa msubiri 2025.

They'd rather die with honour standing than with pride while sitting! Hakuna haja ya ENL kwenda UKAWA, hajawahi kuhitajiwa na hatahitajiwa kamwe.
 
Wananchi gani? na kumsafisha kwa lipi? Je kuhusu Richmond unakumbuka Mwakyembe alisemaje bungeni? ni kwanini hakusema yote? Muulizeni awaambie, je zaidi ya Lowassa ni nani alitia mkono kwenye Richmond?

Lowassa haitaji kusafishwa na hakika hii nafasi UKAWA wasiache hata kidogo.

Mkuu UKAWA wasipomchukua Lowassa wasahau kabisa kuhusu Magogoni. Hakuna golden chance kama hii.
Na huu utakuwa mwisho wa CCM.
 
Sijawahi kuona ushauri wa hovyo kama huu wa kwako hapa.

Hakuna haja ya kuiondoa ccm madarakani ikiwa tutaweka wagombea wale wale mafisadi walioua nchi yetu. Ukiitoa ccm kwa kuwa imekuwa fisadi na mafisadi ndio hao hao kina Lowasa, halafu unampa uongozi wa nchi fisadi gumegume yule yule Lowasa, utakuwa ama una maradhi ya akili ama huna msingi wala sababu ya maana ya kutafuta mabadiliko. Utakuwa unatafuta mabadiliko kwa maslahi yako binafsi na si ya umma kitu ambacho UKawa hakikubaliki.

LAWASA AKIGOMBEA URAISI KWA CHAMA CHOCHOTE HATUMPIGII KURA SISI WATANZANIA HALISI TUNAOTAKA TANZANIA YETU ASILIA.

Hueleweki unapoongelea Lowasa awe mgombea wa UKAWA, huku references and standards zako zote ziko ccm!. Kwa kuwa ccm wote ni mafirauni na hakuna msafi, basi ukawa wasimamishe tu hilo fisadi nao? Wewe vipi lakini?

UKaWA inachukua nchi without haja ya mkono wa mafisadi!.

Hii kumtengenezea njia mwenye safari ya matamanio, imebuma, tafuta mlango mwingine. Labda jaribu kwa Zito au IPPT Maendeleo!, Ukawa kumejaa nahata hivyo access denied!.

Kwa hoja zako hizi basi subiri baada ya October 2015 utapata majibu murua. Kujifariji ni kuzuri sana na nakutakia kila la kheri. Angalizo, usitegemee nguvu nyingi ambayo CHADEMA imewekeza sana kwenye siasa itaendelea kuwa hivyo iwapo UKAWA haitashinda uchaguzi huu.
 
Naomba nitoe hoja kwa wale wote wanaotudanganya kwa mgongo wa uchafu ohoo mara ufisadi wa Lowassa waje hapa na waseme huo ufisadi ni upi na uchafu ni upi? na ni nani aliye msafi ndani ya CCM ukianzia na uongozi wa juu? Nitajie hata kiongozi 1 wa CCM ambaye ni msafi hapa?

Tuache hizi hoja nyepesi za ufisadi na uchafu ambao hauwezi kuuthibitishia umma ili kuwafitini watu hasa UKAWA ili waache kutumia nafasi hii ili kuiondoa CCM madarakani. Na kama hamjui, basi naomba niwape siri sasa, mpaka sasa CCM wana hofu sana na move yoyote atakayochukua Lowassa. Kila siku na mbinu zao zote wanataka Lowassa asijiunge CHADEMA wala UKAWA. CCM wanataka kuona kama Lowassa akiondoka CCM, then ajiunge ACT, kwani kwao itkuwa imewasaidia sana na watashinda ki urahisi sana. CCM wana hofu sana iwapo Lowassa atajiunga CHADEMA na UKAWA ikaendelea kuwa pamoja.

Achana nao hao mkuu, wamesahau ule usemi usemao JIWE LILILOKATALIWA NA WAASHI......
Lowassa akitangazwa kama mgombea urais kupitia UKAWA CCM na yule Mkwere mswahili watatundikiwa dripu za masaa.
UKAWA hakuna mtu yeyote anayeweza kupambana na mgombea wa CCM. Ndio maana hata sasa hakuna attention kubwa ya kusubiri atakayetangazwa maana kila mmoja ameshajua ni Slaa na hana mvuto kabisa.
 
Kwa namna vyama vinavyounda UKAWA vinavyojipambanua kwa jamii binafsi sidhani kama ni wazo zuri kumkaribisha Lowassa na kumpa mikoba ya kuwania uraisi. Hii maana yake itakuwa UKAWA wanachotaka ni kushika dola pasipo kujali mtu wanayemsimamisha ni msafi au mchafu kiasi gani.

Tuonyeshe kwa vitendo kile tunachokihubili majukwaani na si kumtumia mtu mchafu kushida kwa sababu tu anaushawishi kwa wananchi.
 
Malengo ya UKAWA ni ukombozi wa nchi hii na wala sio kwamba iwe isiwe lazima waende ikulu
Kutakuwa na maana gani sasa kuingizwa Ikulu na Lowassa tukijua wazi kwamba tutakuwa tumewaingiza Rostam, chenge na Karamagi? Kuna mapinduzi gani sasa ambayo UKAWA italeta ikiwa ni walewale waliosababisha tuiunge mkono UKAWA kwa kuwakataa ndio tunaungana nao?

Bahati mbaya Lowasa amezungukwa na walafi, ndio maana tunaona ushauri mwingi wa kumtaka lazima apiganie kuingia Ikulu ili mirija yao ijichomeke
 
teh teh teh teh kwani ufisadi ni mtu au ni system?? Labda nikuulize swali dogo tu, hebu tufanye EL ameweza kuwa Rais kupitia UKAWA, wewe unaamini EL atawashawishi UKAWA wote wawe wezi na kutuibia waTanzania?? Vipi ikiwekwa mifumo ambaye haimpi Rais mwanya wa kufanya hivyo?? Yaani wewe unaamini pamoja na Intergrity kubwa ya Dr. Slaa as PM, Lipumba as Minister of Finance, Lisu kama Waziri wa Sheria wataingizwa mkenge wawe wanasaini mikataba ya kukandamiza watanzania, wawe wanapitisha miswada ya kulinda viongozi e.t.c.. Unayaamini hayo?? Na kama unayaamini, una uhakika gani kwamba hata tukiwapeleka kama walivyo sasa hawatoyafanya hayo??

teh teh teh hawa ndio elites wa JF bana.. wako humu tangia 2008.. Mara nyingi nyie mkisema kitu ndio kinakuwa final say humu teh teh teh.. Mnatukuzwa sana na sie tulioingia humu 2014 teh teh teh

Hakuna kitu ambacho hua kinanikera kama kuwatukuza hawa waliowahi kujiunga humu.
Wengi wao ni MAPOPOMA YALIYOTUKUKA tu.
Kuna watu wamejiunga huku baada yao na ndio magreat thinkers wa ukweli.
Mtu apimwe kwa hoja na sio muda aliojiunga humu.
 
Ningeweza kuelewa kama EL angekuwa alifika 3 bora huko kwenu na kutolewa kwa mizengwe. Lakini pamoja na mapesa yake ameshindwa kupenya kwenye kamati yenu ya maadili. Mngalikuwa na kamati ya afya, kulikuwa na uwezekano mkubwa kuwa nako asingeweza kupita.

Hivi ni lazima EL awe rais? Mpelekeni kwa wataalamu "wamtibu" hilo tatizo la obsession.

Kwani UKAWA kumejaa vichwa maji kiasi washindwa kupambanua mambo mepesi kiasi hiki?
 
Malengo ya UKAWA ni ukombozi wa nchi hii na wala sio kwamba iwe isiwe lazima waende ikulu
Kutakuwa na maana gani sasa kuingizwa Ikulu na Lowassa tukijua wazi kwamba tutakuwa tumewaingiza Rostam, chenge na Karamagi? Kuna mapinduzi gani sasa ambayo UKAWA italeta ikiwa ni walewale waliosababisha tuiunge mkono UKAWA kwa kuwakataa ndio tunaungana nao?

Bahati mbaya Lowasa amezungukwa na walafi, ndio maana tunaona ushauri mwingi wa kumtaka lazima apiganie kuingia Ikulu ili mirija yao ijichomeke

Kinachoangaliwa ni sera ya chama na sio mtu.Una uhakika gani kama huyo Slaa, Mbowe n.k hawajazungukwa na walafi?
Hizi ni siasa tu, usimuamini mtu kupitiliza kwa maneno yake ya jukwaani.

Kama ndio hivyo kuna yeyote aliyeamini yale yaliyokuwa yanafanywa na Zitto kabla ya ukweli kuwa dhahiri kua naye sio msafi kama anavyohubiri?

UKAWA sio wajinga, nao wana system yao hivyo usidhani kama wakimsimamisha Lowassa kama mgombea wao watalala bila kumfuatilia nyendo zake.
Chama hakiendeshwi na mtu bali katiba ya chama.Ndio maana Zitto alitimuliwa pamoja na uZitto wake, leo hii yuko wapi?
 
aje ukawa na aseme uchafu wa ccm ndani ya ukawa. kugombea ni big no. labda kwenye kampaign atambee na mgombea wa ukawa kumnadi ili kura ambaxo angepewa ziende ukawa. apa ni mmemwaga mboga nami namwaga bugari
 
Ningeweza kuelewa kama EL angekuwa alifika 3 bora huko kwenu na kutolewa kwa mizengwe. Lakini pamoja na mapesa yake ameshindwa kupenya kwenye kamati yenu ya maadili. Mngalikuwa na kamati ya afya, kulikuwa na uwezekano mkubwa kuwa nako asingeweza kupita.

Hivi ni lazima EL awe rais? Mpelekeni kwa wataalamu "wamtibu" hilo tatizo la obsession.

Kwani UKAWA kumejaa vichwa maji kiasi washindwa kupambanua mambo mepesi kiasi hiki?

Kumbe unajua kama kuna mizengwe? Sasa unahoji nini Lowassa kutokuingia 5 bora?
Huoni kama napo ilifanyika mizengwe pia?

Kwanza ukae ukijua taratibu za kumpata mgombea wa CCM zilikiukwa.Ulitakiwa uanze mkutano mkuu wa kupendekeza majina matano ya kuingia kamati kuu ili yatoke majina matatu ya mwisho.

Lakini kilichofanyika ni vice versa na ndio mizengwe yenyewe iliyotumika kumkata Lowassa jina.
 
Back
Top Bottom