zumbemkuu
JF-Expert Member
- Sep 11, 2010
- 11,075
- 9,263
Mimi ni mmoja wa watu niliyekuwa nikipinga Lowassa asichaguliwe CCM sababu ni moja tu alikuwa threat kubwa kwa UKAWA. Angepitishwa Lowassa UKAWA ingebaki historia siasa haina rafiki wa kudumu wala adui hata Slaa alivyokatwa CCM alihamia CHADEMA.
Nawaomba CHADEMA na UKAWA msipoteze hii turufu huyu mtu bado yupo vinywani mwa watu wengi.Bado ana influency kubwa kwenye media ambacho ni kitu muhimu wanaomkataa asipokelewe hawaijui siasa.
Kama Lowassa akipokelewa akapeperusha bendera ya UKAWA mtauona mtikisiko wa hii nchi.UKAWA watabeba kila kitu kuanzia Ubunge hadi urais. Lowassa anatakiwa atoke hadharani aeleze uhusika wake wa Richmond naamini akiwa CHADEMA atakua huru kusema.
Ni bora ushirikiane hata na shetani ili mradi uitoe CCM madarakani nyuma ya Lowassa kuna watu wengi sana.Narudia tena kwa wanachadema wenzangu siasa haina rafiki wala adui wa kudumu.
Kama lengo kushika dola shirikiana hata na shetani umalize mchezo, kama lengo ni kupinga ufisadi tutabaki hivi hivi tunapinga ufisadi huku tukiwa wapinzani, vita ni vita tu.
Kwanini nyinyi wa ACT msimchukue?