Mkuu Mkandara , ulisepa nilipokuuliza Tanganyika inanufaika na nini katika muungano. Nikauliza zaidi, nje ya muungano Tanganyika itakosa kitu gani. Kwanini unadhani Tanganyika inaihitaji znz. Wiki imeisha umejichimbia, hali imetulia naona unadandia treni kituo cha mbele kabisa. Hebu rudi nyuma ubebe mizigo uliyoacha tunakusubiri mkuu, tujibu maswali yetu ya Tanganyika na muungano, halau tutaendelea.Nguruvi3, Dah, nilikuwa naandika mara ghafla PC yangu ikazima na nikapoteza hata mada nilokuwa najadiliana na wewe . Nimeitafuta wala siipati hivyo nakuomba niwekee 'like' tu ili niweze kuipata tena mada hiyo ktk orodha ya msg maana nimegundua sasa ni wapi wewe huelewi ama hukosea.
Mkuu wangu wakati mwingine unauliza maswali ya ajabu kabisa. Unaposema Tanganyika inanufaika nini na huu Muungano una maana gani? Hivi nikuulize wewe hilo deni la taifa ni kiasi gani? au wewe utajibu vipi mtu akikuuliza unafaidika vipi na ndoa yako? Ni kipi kilichopo ktk ndoa yako ambacho huwezi kukipata pasipo ndoa hiyo? pengine wewe mwenzangu una akili sana tujuze nadhani ndio swali lako kwenye Utanganyika au sivyo?.Mkuu Mkandara , ulisepa nilipokuuliza Tanganyika inanufaika na nini katika muungano. Nikauliza zaidi, nje ya muungano Tanganyika itakosa kitu gani. Kwanini unadhani Tanganyika inaihitaji znz. Wiki imeisha umejichimbia, hali imetulia naona unadandia treni kituo cha mbele kabisa. Hebu rudi nyuma ubebe mizigo uliyoacha tunakusubiri mkuu, tujibu maswali yetu ya Tanganyika na muungano, halau tutaendelea.
Swali hilo ni la 'ajabu' kwasababu linakukera kwa kutambua jibu lake si zuri kwa wazanzibar unaowatetea. Chanzo cha swali hilo kinatokana na wazanzibar wanaosema 'Muungano huu hauwasadii, wananyonywa na kuonewa''Swali Tananyika inafaidika na nini.Mkandara;10113797]Mkuu wangu wakati mwingine unauliza maswali ya ajabu kabisa. Unaposema Tanganyika inanufaika nini na huu Muungano una maana gani? Hivi nikuulize wewe hilo deni la taifa ni kiasi gani?
Kuna faida za kujenga familia na kizazi. Faida za kiuchumi na kijamii.au wewe utajibu vipi mtu akikuuliza unafaidika vipi na ndoa yako? Ni kipi kilichopo ktk ndoa yako ambacho huwezi kukipata pasipo ndoa hiyo? pengine wewe mwenzangu una akili sana tujuze nadhani ndio swali lako kwenye Utanganyika au sivyo?.
Swadakta, ndiyo maana tunasema iwepo Tanganyika,Magufuli ajenge barabara za Tanganyika na Mansour ajenge za znz.Swala sio Tanganyika inanufaika vipi bali ni ukweli kwamba mikopo tunachukua, hivyo kama tunaenda kulewea, tunaibiana kujenga miradi binafsi au kuhamishia ktk mabenki ya nje haya sii maswala ya kujadili hapa. Kinachojadiliwa hapa ni mikopo inachukuliwa na bara kwa jina la Muungano na kwa minajiri ya miradi isokuwa na Muungano - Kaput!.
Ndio maana tunataka tuwaondoe katika mtego wa ufisadi, waende kukopa na kupata misaada yao. Tunataka Tanganyika ili tuhangaike na matatizo yetu bila kuwapa wazanzibar.Mimi na wewe tunajua fika kwamba ni asimia 10 hadi 20 tu ndio hutumika kama gharama halali ya ujenzi wa miradi hiyo ya kitapeli, wakati asilimia 80 inawekwa kibondoni mwa viongozi wetu wakishirikiana na Makabaila. Hili sio swali la kuniuliza mimi mkuu wangu hata kidogo. Ni hawa wameifanya mikataba hii kuwa ya siri ili wapate kuendelea kutuibiwa wananchi bora wenzetu Wazanzibar wameshtuka kuliko sisi tusioona mbali zaidi ya marefu ya kero zetu..
Sawa , tunachosema mafisadi ni sawa na vibaka. Wanaiba tu.Sasa haya sii ya kuniuliza mimi ati Tanganyika inafaidika nini na Muungano wakati tunaibiwa na viongozi ambao hawana msalie, aidha uwape serikali 2 au 3 pasipo kubadilisha mfumo huu mbaya wa Kiutawala ambao mikataba ya uwekezaji nchini ni siri ya serikali tawala. Siri ya nani ktk uwekezaji nchini uliona wapi kama sio jeuri ya kuwaibia wananchi na hasa kuficha machafu yao.
Hapa swali linabaki tunafaidika nini kwa kuwa na znz katika uchumi wetu.Na naweza kukujibu kihuni vile vile kwa kusema wewe huoni maendeleo ya Tanganyika? Tanganyika ile ya Nyerere sawa na hii ya leo?. Fedha zinazokopwa nje leo zinajenga mabarabara, madaraja ambayo JK kapewa sifa kubwa lakini deni lote ni la Taifa. Mkapa alijenga daraja kubwa na uwanja wa mpira wa Kimataifa. Au unataka nikwambie ya kwamba Tanganyika ilifaidika na Muungano kutokana na Hayati Karume ndiye alojenga jengo la Yanga pale jangwani na pia kuchangia kwa asilimia kubwa Klabu ya Simba?.
Kwamba tusijenge bandari zetu tusubiri wazanzibar. Ney.Mkuu acha hizo leo tuna mipango ya Ujenzi wa bandari na airport mpya Bagamoyo, daraja la Kigamboni, madaraja ktk kila kivuko cha mito, Meli za Kigoma, Lake Nyasa na Victoria kote huko ni miradi ya serikali kuu sio ya watu binafsi kama ilivyo Zanzibar na hii yote ni mikopo ya Kimataifa ambayo Pasipo Muungano pengine tusingeifanya maana kama Zanzibar watakuwa na International Airport na bandari ya Free Port hakuna haja wala sababu ya Ujenzi wa miradi hiyo mipya
Mkuu swali hilo halinikeri isipokuwa nimekujibu sii mara moja wala sii chini ya mara 10 tena kwa maelezo marefu sana bado huelewi.Swali hilo ni la 'ajabu' kwasababu linakukera kwa kutambua jibu lake si zuri kwa wazanzibar unaowatetea. Chanzo cha swali hilo kinatokana na wazanzibar wanaosema 'Muungano huu hauwasadii, wananyonywa na kuonewa''Swali Tananyika inafaidika na nini.
Je unadhani bila znz Tanzania haiwezi kupata mikopo au misaada mnayopigia debe.Nguruvi3,
Mkuu swali hilo halinikeri isipokuwa nimekujibu sii mara moja wala sii chini ya mara 10 tena kwa maelezo marefu sana bado huelewi.
Labda nikwambie kwa kifupi ni kwamba Tanganyika inafaidika na Muungano huu kwa kutumia fursa zilizopo za kuchukua mikopo nchi za nje kwa jina la tanzania na ikatumia ktk maswala yasiyokuwa ya Muungano. Zanzibar hawana mamlaka hayo isipokuwa kwa idhini ya Tanganyika!
Nini tena unataka kujua?
Swala sio Tanganyika wanaweza kupata Mkopo au hawawezi bila Zanzibar, kesi iliyopo mezani ni kwamba tanganyika inapata yote hivi sasa kwa kutumia Jina la Tanzania (a verdict) na ndio sababu Zanzibar wanataka bora kuvunja Muungano tuunde Shirikisho ili wao pia wapate kuwa nchi kamili yenye uwezo wa kupata mikopo na misada hiyo kama sisi. Wao kupewa mikopo na Misaada kama sisi bila idhini ya Tanganyika imeshindikana na tulishindwa kupata suluhu ktk hilo toka tume zote zilizoundwa.Je unadhani bila znz Tanzania haiwezi kupata mikopo au misaada mnayopigia debe.
Sidhani hata huko nje wanatambua znz ni kitu gani. Huwezi kumfanya panya awe tembo hata siku moja. Panya ni panya na tembo ni tembo.
Ili kuhakikisha Tanganyika haifaidiki na fursa za kutumia jina la zanzibar tunasema, tugawane majukumu.
Tanganyika izinduke na ichacharike kivyake na znz nao wapewe fursa za kwenda Paris club, washington na kwingineko kukopa na kuapta misaada. Hatuna tatizo na hilo.
Njia nyepesi kabisa, ni S3. Hilo hutaki bado unasema Tanganyika inatumia jina la Tanzania. Sasa inawezaje kwenda kupata misaada na mikopo ikiwa haipo. Mimi husema kila siku sijui hata unakumbuka ulichoandika siku iliyopita. Wewe unasema mambo yote ya muungano, halafu unasema Tanganyika ambayo imeporwa utaifa wake na Tanzania eti ikaombe misaada na mikopo(kwangu mimi naona aibu sana kuongelea hoja za misaada, ni dhalili sana) kwa jina la Tanganyika.
Wewe unayesema tuna JMT na ZNZ ndio huyo huyo unalalamika Tanganyika kuinyonya znz. Tanganyika haionekani sasa inaonyonya vipi? Ni ghost, sasa sisi tunaotaka kutenga shughuli tunaonekana hatufai. Mantiki zinatutetea sana tena kwa mantiki.
Hatuna flip flops kwasababu hoja zimesima zenyewe.
Huwezi kuwa na JMT ukiyoiita Tanganyika, halafu ukalamu Tanganyika isiyopkuwepo kunyonya kusicho. White elephant.
Pili, hao znz wanatumia jina la Tanzania kuinyonya Tanganyika. Leo hawana mchango wowote isipokuwa wamekuwa chanzo cha kuvuja na kuchukua hata kisicho chao. Deni la ndani na gharama za muungano hawazijui wanachojua ni mikopo na misaasda. Hilo hatutaki tena.
Ikishindikana , hatuna sababu za kushikiliana kwa kamba. Sisi Tanganyika hatuhitaji uwepo wa znz kwa namna yoyote.
Wana hiari ya kuja Dodoma au wabaki makwao. Tunaweza kuvunja jahazi na kugawama mbao, tutrapoteza nini?
Well said, tunataka shirikisho.Swala sio Tanganyika wanaweza kupata Mkopo au hawawezi bila Zanzibar, kesi iliyopo mezani ni kwamba tanganyika inapata yote hivi sasa kwa kutumia Jina la Tanzania (a verdict) na ndio sababu Zanzibar wanataka bora kuvunja Muungano tuunde Shirikisho ili wao pia wapate kuwa nchi kamili yenye uwezo wa kupata mikopo na misada hiyo kama sisi. Wao kupewa mikopo na Misaada kama sisi bila idhini ya Tanganyika imeshindikana na tulishindwa kupata suluhu ktk hilo toka tume zote zilizoundwa.
Tanganyika inachukua mikopo hiyo jambo ambalo kiutawala ni kosa na ndio maana wanasema Tanganyika imevaa koti la muungano, kwanza tukubali makosa hayo ya Kimfumo ili turekebishe na sio kuvunja ndoa kwa sababu Zanzibar wanaomba haki yao na wameeleza ubaya wetu. Huwezi kujibu kesi ya mashtaka kwa kusema ubaya wa mwingine yaani kama vile tunafanya hivi makusudi ili kuwadhalilisha, utetezi wako wote hauna maana, ni kujihami bila kuelewa kesi inahusu nini.
Huu ujinga wa nani anaghramia Ulinzi na Usalama wakati vifaa vya kijeshi vinatengenezwa nje kwa gharama ya wananchi wa JMT, leo wewe unakuja kubeza Zanzibar wakati hujui tunazungumzia nini inanipa wasiwasi sana na kuelewa kwako! yaani kila siku tunarudia yale yale ilihali mtu mwingine angeisha elewa na kukaa kimya maana kweli tunatumia jina la Tanzania kwa mambo yasokuwa ya Muungano, sasa sijui toka lini Ulinzi na Usalama pia yakawa sii mambo ya Muungano!
Yaani hueleweki kabisa....
Mnaotaka shirikisho ni wewe na kina nani? kama upo na hao UKAWA basi hilo mtabakia nalo wenyewe na sintowaunga mkono kabisa kwa sababu njama zenu ni dhidi ya wananchi kuitaka katiba Mpya wala sii CCM. Haya ndio mambo yalowanyima wananchi katiba mpya kwa kutanguliza kuwa Muungano wetu ni wa watu wawili na hati ya muungano ni feki wala sii CCM wala JK bali UKAWA ndio wamekuja vunja Muunganio kwani huwezi kuwa na Muungano (Union) na Shrikisho (Federation) wa pamoja!Well said, tunataka shirikisho.
Nasisi ndipo hoja yetu ilipo kuwa hutataki kuendelea kutumia jina kunyonya znz kama wanavyosema.
Lakini nao pia wasitumie jina la Tanzania kujificha na kudai wasichostahili.
Suluhu ni moja tu, tuwe na shirikisho, wao waende wanakojua nasi twende tunakojua.
Hatuna sababu za kuwazuia kupata mikopo. In fact huo ni ukatili.
Zanzibar hawatakiwi kibali cha kwenda kukopa, ili mradi watakopa kwa jina la znz na si kama ilivyo sasa.
Leo wamekopa na asilimi 88 ya mkopo ni dhamana ya Tanzania. Hilo hutataki maana tunawajua, ni wavivu sana wa kulipa na hawakawii kupitisha deni hilo kwa JMT kama walivyozoea kwa umeme kwa miaka mingi hadi tulipopiga kelele wanalipa vijisenti tunasikia.
Ni makosa JMT kuwazuia wznz kwenda kukopa. Wapewe fursa waende Paris na Washington. Ni makosa kuwazuia wasipate misaada, waende Oman alikosema Ali Salehe watapewa misaada. Hata wakitaka kuuza pande la kisiwa chao hakuna sababu za kuwazuia.
Lakini zipo sababu kama mambo yao yanaingilia maisha ya Watanganyika.
Hawawezi kuja Dar es salaam kujipangia asilimia za ajira ambazo huko kwao hazipo kwa ubaguzi wa kizanzibar. Hilo linafika mwisho kwa hiari kwa lazima.
Hawawezi kuvunja katiba ya JMT halafu wakaitumia kuja kujipatia fursa za muungano, hilo linafika mwisho kwa hiari kwa lazima.
Hawawezi kuleta ubaguzi kwa Mtanganyika nasi tukawaangalia, hilo linafikia mwisho kwa hiari kwa lazima.
Wanachaguo moja, tuvunje jahazi tugawane mbao, au tukae pamoja wakiwa na adabu na nidhamu.
Sisi hatuhitaji znz kwa lolote kwa chochote na kwa ubinafsi na roho zao za chuki dhidi ya Watanganyika, hata neema ikiwateremkia hao hawatatujali.
Kama wanatuchoma moto kukiwa na katiba ya pamoja, nje ya hapo ni nini undadhani.
In short S2 za kuwabeba wznz haziawezekani.
Zinawezekana kwa muda lakini gharama zake zitakuwa kubwa.
Serikali 3 zinaweza kuwapa unafuu, kinyume chake tuvunje jahazi tu.
We have nothing to lose, let them go!
Tunaotaka shirikisho ni Watanganyika wengi sana wale Ali Salehe aliowaita wajinga wa muungano.Mnaotaka shirikisho ni wewe na kina nani? kama upo na hao UKAWA basi hilo mtabakia nalo wenyewe na sintowaunga mkono kabisa kwa sababu njama zenu ni dhidi ya wananchi kuitaka katiba Mpya wala sii CCM. Haya ndio mambo yalowanyima wananchi katiba mpya kwa kutanguliza kuwa Muungano wetu ni wa watu wawili na hati ya muungano ni feki wala sii CCM wala JK bali UKAWA ndio wamekuja vunja Muunganio kwani huwezi kuwa na Muungano (Union) na Shrikisho (Federation) wa pamoja!
Maadam sasa tumeelewana kila mmoja ana msimamo wake nadhani hakuna haja ya kuendeleza malumbano.
Utakuwaje wewe mjinga wa Muungano ikiwa unataka Shirikisho? wewe na yeye Ali Salehe hamna tofauti lugha zenu, wajinga ni sisi tunaotaka Muungano uloasisiwa na viongozi wetu. UKAWA = HIZBU.Tunaotaka shirikisho ni Watanganyika wengi sana wale Ali Salehe aliowaita wajinga wa muungano.
Umesahau Nyerere ambaye ni muasisi alisema znz kama hawataki muungano hatawapiga mabomu. Akaongeza kusema likiundwa shirikisho la EA ni bora Tanganyika na Zanzibar zikaingia independently. Naye alikuwa UKAWA au Hizbu?Utakuwaje wewe mjinga wa Muungano ikiwa unataka Shirikisho? wewe na yeye Ali Salehe hamna tofauti lugha zenu, wajinga ni sisi tunaotaka Muungano uloasisiwa na viongozi wetu. UKAWA = HIZBU.
gfsonwin , dhamira ya kweli haipo kwa CCM.nguruvi 3 asante kwa mabandiko mazuri sana yanayoainisha mambo muhimu kuhusu swala zima la mchakato wa katiba.
nimefuatilia kwa umakini leo mjadala kati ya Nape na Mnyika kuhusu UKAWA kurudi kwenye bunge la katiba. Kimsingi kuna jambo ambalo halijakaa swala nalo ni hakuna mwenye dhamira ya kweli ya upatikanaji wa katiba mpya. nasema hayo kwasababu sion kwann pande hizi mbili zigombane kisa katiba kama wana dhamira ya haki kwa taifa hili.
to me ni afadhali katiba iliyopo ikarekebishwa uchaguzi ufanyike kama kwao uchaguzi ni priority. sidhan kama kuna ulazima wa kuwah kutemngeneza katiba ili kufit kwenye coming election manake nia yetu sio ya kupata bora katiba bali tunataka katiba bora.
so far naona kama intetion za UKAWA zimebadilika and now wana concetrate kwenye jins ya wao kuingia kwenye uchaguzi wakasahau kwamba hiyo haikuwa primary mission yao
..............................
Mchakato wa Katiba Mpya
Ndugu Wananchi;
Kama tujuavyo, Bunge Maalum la Katiba lililoahirishwa tarehe 25 Aprili, 2014 kupisha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi kushughulikia bajeti za Serikali husika, litakutana tena tarehe 5 Agosti, 2014 kuendelea na kazi yake ya kutunga Katiba Mpya.
Kwa vile Bunge Maalumu la Katiba halikuweza kumaliza kazi yake ndani ya siku 70 zilizotengwa kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, nimeliongezea Bunge hilo siku 60 kwa ajili ya kukamilisha kazi yake. Nimefanya hivyo kwa mujibu wa mamlaka niliyopewa na Sheria hiyo hiyo.
Hatua Iliyofikiwa Kabla ya Kuahirishwa kwa Bunge
Ndugu Wananchi;
Itakumbukwa pia kuwa, tarehe 16 Aprili, 2014, baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba hasa kutoka vyama vya CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi walisusia mjadala uliokuwa unaendelea Bungeni na kutoka nje.
Wakati wanatoka Bungeni, kazi kubwa ilikuwa imefanyika.
Tayari Kamati zote 12 za Bunge hilo zilikuwa zimekamilisha kujadili Sura ya Kwanza na ya Sita za Rasimu ya Tume. Sura hizo zinazungumzia utambulisho wa nchi na muundo wa muungano.
Kamati zote zilipiga kura ya kupitisha uamuzi wao kuhusu sura hizo mbili.
(A)Kamati kadhaa ziliweza kupata theluthi mbili ya kura kwa Wajumbe wa pande zote mbili za Muungano, jambo lililoonyesha dalili njema kwamba Katiba mpya inaweza kupatikana.
Baada ya hapo, taarifa ya kila Kamati iliwasilishwa kwenye Bunge zima.
Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge Maalumu la Katiba, maoni ya wachache nayo yaliwasilishwa.
Kazi iliyokuwa inafuatia, kwa mujibu wa Kanuni za Bunge ni kwa Kamati ya Uandishi kukamilisha taarifa yake na kuiwasilisha kwenye Bunge zima kwa ajili ya kujadiliwa.
(B)Baada ya Wajumbe kujadili taarifa hiyo itafuatia kupiga kura ili kuamua kuhusu Sura hizo mbili.
Kama yalivyo masharti ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, uamuzi utafanywa kwa theluthi mbili ya kura za kila upande wa Muungano wetu.
Sababu za Baadhi ya Wajumbe Kususia Bunge Maalumu la Katiba
Ndugu Wananchi;
Sote tumewasikia Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba waliosusia vikao vya Bunge hilo wakielezea sababu zilizowafanya watoke Bungeni. Walitoa matamko kwenye vyombo vya habari na pia katika mikutano ya hadhara waliyoiitisha na kuhutubia sehemu mbalimbali nchini.
(C)Sababu walizotoa zimekuwa zikiongezeka na kubadilika kadri siku zinavyosonga mbele na upepo wa kisiasa unavyokwenda.
Hivi sasa wanazungumzia mambo mawili.
(D)Kwanza, kwamba Bunge Maalumu halina mamlaka ya kuifanyia mabadiliko yo yote Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Kwa maoni yao, kazi ya Bunge Maalumu la Katiba ni kujadili na kupitisha tu Rasimu ya Katiba ya Tume na siyo kubadili cho chote.
Pili, wametoa sharti la wao kurudi Bungeni ni kuhakikishiwa kwamba, kitakachojadiliwa Bungeni ni Rasimu ya Tume. Bila ya sharti hilo kukubaliwa, wamesisitiza kutorudi Bungeni.
Mamlaka ya Bunge Maalum la Katiba
Ndugu Wananchi;
Mimi nimehusika katika kubuni wazo la kuwa na mchakato wa kuandika Katiba Mpya, na katika maandalizi ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, ya kuongoza na kuendesha mchakato huo.
(E)Kwa kweli sikumbuki wakati wo wote katika vikao vya Baraza la Mawaziri kujadili Rasimu ya Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba tulipozungumzia Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuwa haiwezi kufanyiwa marekebisho na Bunge Maalumu la Katiba.
Mimi siyo Mwanasheria na hivyo nakiri kwamba naweza kuwa na upungufu katika kuelewa maana ya baadhi ya maneno ya kisheria. Hata hivyo, sikumbuki kuwepo kwa kifungu cho chote katika Sheria kinachosema kuwa Bunge Maalumu la Katiba halina mamlaka hayo.
Tangu tulipoyasikia maneno hayo yakisemwa nimeuliza nithibitishiwe ukweli wa madai hayo bado sijaambiwa vinginevyo. Kama ukweli huo upo naomba anisaidie.
Badala yake naambiwa kuwa maneno yaliyotumika katika Sheria haiakisi dhana inayotolewa kuwa kazi ya Bunge Maalum la Katiba ni kubariki Rasimu na siyo kufanya vinginevyo.
(F)Nimeambiwa kuwa sheria inasemaTume itaanda Rasimu ya Katiba na Bunge Maalum la Katiba litatunga Katiba iliyopendekezwa.
Ndugu Wananchi;
Tarehe 30 Desemba, 2010, nilipozungumzia dhamira yangu ya kuanzisha mchakato wa kuandika Katiba Mpya nilieleza wazi nia ya kuwepo kwa uwakilishi mpana wa Watanzania katika mchakato huo.
Ndiyo maana katika Sheria tukaweka ngazi nnekatika mchakato wa kutunga Katiba.
(G)Ngazi ya kwanza ikiwa ya wananchi kutoa maoni yao juu ya kila wanachotaka kijumuishwe katika Katiba ya nchi yao.
(H)Ngazi ya pili, ni ya wananchi kupitia wawakilishi wao katika Mabaraza ya Katiba ya Wilaya na Mabaraza ya Kitaasisi kutoa maoni yao kuhusu Rasimu ya kwanza ya Katiba iliyotayarishwa na Tume.
(I)Ngazi ya tatu inajumuisha wawakilishi wa wananchi waliopo kwenye Mabaraza ya Kutunga Sheria ya Sehemu zetu mbili za Muungano, yaani Bunge la Jamhuri ya Muungano na Baraza la Wawakilishi, wakichanganyika na Wawakilishi wa makundi mbalimbali ya jamii ya Watanzania kutoka pande zote mbili za Muungano.
Hawa ndio wanaounda Bunge Maalumu la Katiba, lenye jukumu la kutunga Katiba inayopendekezwa.
(J)Mamlaka ya kutunga Katiba kwa mila na desturi za Mabaraza ya Kutunga Sheria ni uwezo wa kurekebisha, kubadili, kufuta na hata kuongeza kilichopendekezwa.
(K)Ingekuwa kilichokusudiwa ni kubariki tu lisingetumiwa neno la kutunga Katiba.
Hali kadhalika, lisingewepo sharti la kupiga kura na msisitizo wa kupata theluthi mbili kwa kila upande wa Muungano.
(L)Aidha, kama ingekuwa jukumu la Bunge Maalumu ni kubariki tu Rasimu lisingepewa siku 70 za kazi na Rais kupewa mamlaka ya kuongeza siku zaidi kadri aonavyo yeye inafaa.
Ngazi ya nne na ya mwisho, tuliweka kura ya maoni ya wananchi kukubali au kukataa Katiba inayopendekezwa na Bunge Maalumu la Katiba.
(M)Kama ingekuwa Rasimu ya Tume haiwezi kubadilishwa hata nukta kwa nini basi tuweke kura ya maoni ya kuwahusisha wananchi wote?
Ndugu Wananchi;
Tulizibuni ngazi hizi nne kwa dhana kwamba kile ambacho hakikuonekana au hakikuwekwa sawa katika ngazi moja kitaonekana na kurekebishwa katika ngazi inayofuata katika ngazi zile tatu za mwanzo. Na, iwapo Katiba iliyotungwa haitawaridhisha wananchi wanayo haki ya kuikataa. Kwa kufanya hivyo, wananchi ndiyo waliopewa turufu ya mwisho.
Ndugu wananchi;
(N)Kwa kweli, napata shida kuelewa mkanganyiko unatoka wapi na hasa wale wanaoongoza kuhoji mamlaka ya Bunge Maalumu kuwa ni wale wale waliotunga Sheria ya Mabadiliko ya Katiba tena hatua kwa hatua.
Nashangazwa zaidi ninapoona wale wale waliotunga Kanuni za Bunge Maalumu ndiyo wanaoongoza kuhoji uhalali wa kile walichokitunga.
(P)Kanuni za Bunge Maalumu la Katiba, Ibara ya 33 (8) inasema: Nanukuu: "Wakati wa mjadala, Mjumbe yoyote anaweza kutoa mapendekezo ya marekebisho, maboresho au mabadiliko yaliyomo katika Sura za Rasimu ya Katiba zinazojadiliwa kwa utaratibu ufuatao: (a) Ikiwa ni marekebisho, maboresho au mabadiliko yanayobadilisha jambo la msingi, au yanayobadilisha maudhui ya Ibara, mapendekezo ya marekebisho yatapelekwa kwa maandishi kwa Katibu siku moja kabla ya mjadala wa Ibara husika. (b) Ikiwa ni marekebisho madogo, ambayo hayabadili msingi au maana, mapendekezo ya marekebisho yatawasilishwa na mjumbe wakati wa mjadala baada ya kupata ruhusa ya Mwenyekiti". Mwisho wa kunukuu.
(Q)Kanuni hii ilipotungwa, Wajumbe wote wa Bunge Maalumu pamoja na wale ambao baadae walisusia vikao vya Bunge walikuwepo Bungeni na walishiriki kuipitisha.
Tena basi, baadhi yao walikuwa Wajumbe wa Kamati ya Kanuni iliyopendekeza Kanuni hizo. Unapowaona watu wale wale sasa wanakuwa vinara wa kuhoji mamlaka ya Bunge Maalumu la Katiba, unajiuliza maswali mengi kuhusu watu hao bila ya kupata majibu yaliyo sahihi na kutosheleza akili na ufahamu wetu.
Ndugu Wananchi,
Unaposoma Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na Kanuni za Bunge Maalumu, hii ni dhahiri kwamba wote walikuwa na uelewa wa pamoja kuhusu mamlaka ya Bunge Maalumu ya kujadili Rasimu iliyoandaliwa na Tume na kutunga Katiba inayopendekezwa kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura.
Kinachojadiliwa Bungeni ni Rasimu ya Tume
Ndugu Wananchi;
Yapo madai yanayotolewa na kuenezwa na Wajumbe waliosusia Bunge Maalumu la Katiba kwamba kinachojadiliwa Bungeni siyo Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ndiyo maana basi wanaweka sharti la kujadiliwa Rasimu ya Tume ya Jaji Warioba ndipo warudi Bungeni.
Madai haya nayo yananipa taabu kuyaelewa. Ndugu zetu hawa walishiriki siku zote 19 za Kamati 12 zilipokutana kujadili Sura yaKwanza na ya Sita za Rasimu ya Tume. Halikadhalika. walikuwepo na kushiriki kwa ukamilifu wakati taarifa za Kamati, tangu ya Kwanza mpaka ya 12,zilipowasilishwa kwenye Bunge zima. Aidha, na wao walishiriki kutoa maoni ya wachache kwa dakika 20 na kutoa ufafanuzi kwa muda wa dakika 30 kwa kila Kamati.
(R)Haya maneno ya sasa kwamba kinachojadiliwa Bungeni siyo Rasimu ya Tume ya Jaji Warioba bali nyingine kabisa ambayo wanadai eti ni ya CCM yanatoka wapi.
Mimi nadhani kuwa huenda katika Kamati kumefanyika marekebisho kwenye Rasimu ambayo hayakuwapendeza. Kama hivyo ndivyo, wawe wakweli kuhusu jambo hilo kuliko kusema mambo yasiyowakilisha ukweli halisi wa Rasimu inayojadiliwa.
(S)Matokeo yake ni kuwafanya wafuasi wao na wapenzi wao na hata watu wengine waamini kuwa kinachojadiliwa siyo Rasimu ya Tume ya Jaji Warioba bali nyingine tena ni ya CCM.
Jambo hilo si kweli na wenyewe wanajua kwamba si kweli ila sijui kwa nini wameamua kupotosha ukweli.
Ndugu Wananchi;
(T)Kinachonishangaza, zaidi ni kwamba, kama hawakuridhishwa na yaliyofanyika, kwa nini wasingetumia mifumo waliyojitengenezea wenyewe kwenye Kanuni kumaliza tofauti zao?
(U)Kanuni zinaelekeza kuwa mambo wasiyoridhika nayo yajadiliwe kwenye Kamati ya Mashauriano na Maridhiano. Ukiacha mifumo ya maridhiano ndani ya Bunge ukaenda nje kwa wananchi au vyombo vya habari na mitandao si jawabu la tatizo.
Ndugu Wananchi;
(V)Ndiyo maana nashawishika kuunga mkono wale wote wanaowasihi Wajumbe wa CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi na wengine warejee Bungeni. Watumie mifumo maalum ya Bunge iliyowekwa na Kanuni kutafuta maridhiano.
(W)Hali kadhalika, wasichoke kuwa na mawasiliano na vyama vingine vya siasa na hasa CCM kutafuta maelewano.
Mimi niko tayari kusaidia pale watakapoona inafaa kufanya hivyo kama ambavyo nimekuwa nikifanya ziku za nyuma.
(X)Nililolisema mwanzoni kabisa mwa mchakato na nalirudia tena leo kwamba, ili tuweze kufanikiwa kupata Katiba Mpya ambayo sote tunaitaka, maelewano baina ya wadau wakuu wa kisiasa ni jambo lisilokuwa na badala yake. Vinginevyo kupata theluthi mbili kwa pande zote mbili za Muungano haitawezekana.
Ndiyo maana nampongeza sana Msajili wa Vyama vya Siasa, Mheshimiwa Jaji Francis Mutungi, kwa uamuzi wa kuvikutanisha vyama vinne vikuu vya siasa kujadili namna ya kuondoa mtihani uliopo sasa katika mchakato wa Katiba.
(Y)Ombi langu kwa viongozi wa vyama hivyo ni kuitumia vyema fursa ya majadiliano kuukwamua mchakato kwa maslahi ya nchi yetu na watu wake.
(Z)Hali kadhalika nampongeza sana Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Mheshimiwa Samwel Sitta, kwa kuitisha kikao cha Kamati ya Mashauriano na Maridhiano. Bahati mbaya ni kwamba Wajumbe wa vyama vilivyosusia Bunge Maalumu hawakushiriki. Ni matumaini yangu kuwa Mheshimiwa Sitta hatokata tamaa kuendeleza juhudi za mashauriano na kwamba katika vikao vijavyo na wenzetu hawa watashiriki.
Ndugu Wananchi;
Hivi karibuni kumekuwepo pia madai yanayoelekeza lawama kwangu. Kwanza nalaumiwa eti kuwa mambo yalikuwa yanaenda vizuri mpaka pale nilipotoa hotuba ya ufunguzi wa Bunge Maalumu ndipo yalipoharibika.
Pili nalaumiwa kwamba nawezaje kuikana Rasimu ya Katiba ambayo na mimi ni mmoja wa watu waliotia sahihi katika Rasimu hiyo.
(AA)Niruhusuni nianze na hili la pili. Nadhani ndugu zetu wanaotoa madai haya yameitafsiri isivyo sahihi yangu katika Gazeti la Serikali lililotangaza rasmi Rasimu ya Katiba na Taarifa ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba baada ya Tume kumaliza kazi yake ya kuandika Rasimu ya Katiba, Rais wa Jamhuri ya Muungano amepewa kazi tatu kufanya. Kwanza, kupokea Rasimu hiyo na Taarifa ya Tume kutoka kwa Mwenyekiti jambo ambalo lilifanywa tarehe 30 Desemba, 2013. Pili, amepewa kazi ya kuitangaza rasmi Rasimu ya Katiba na Taarifa ya Tume kwa watu wote kuiona na kuisoma ndani ya siku 30. Alipewa sharti la kuitangaza katika Gazeti la Serikali na vyombo vingine vya habari. Hili nalo lilifanywa hivyo tarehe 22 Januari, 2014.
Ndugu Wananchi;
Katika kutangaza katika Gazeti la Serikali sharti linamtaka anayetangaza ajitambulishe kuwa yeye ni nani na atie sahihi yake. Kwa kufanya hivyo, hakumfanyi yeye kuwa naye ni mhusika na maudhui ya kila kinachopendekezwa na Tume. Sahihi zilizomo ndani ya Rasimu na Taarifa ya Tume ni za Wajumbe wa Tume, kamwe sahihi ya Rais haimo hivyo hawezi kulaumiwa kuwa anaikana sahihi yake. Yeye ametimiza wajibu wake wa kutangaza, akaiweka hadharini kwa umma wa Watanzania kuiona na kusoma Rasimu ya Katiba na Taarifa ya Tume vilivyotayarishwa na kutiwa sahihi na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Kazi ya tatu ni kuitisha Bunge Maalumu ambayo nayo imekamilika tangu tarehe 18 Februari, 2014.
Ndugu Wananchi,
Jambo lingine linalofanana na hilo ni yale madai kwamba nilikuwa napata taarifa ya maendeleo ya mchakato ndani ya Tume mara kwa mara, iweje leo nitoe maoni tofauti kama niliyoyatoa katika hotuba yangu kwenye Bunge Maalumu.
Ni kweli kabisa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Mheshimiwa Jaji Joseph Warioba, Makamu wake, Mheshimiwa Jaji Agustino Ramadhani na Mheshimiwa Dkt. Salim Ahmed Salim wamekutana na mimi kwa nyakati mbalimbali kuzungumzia mwenendo wa mchakato.
(AB)Lakini, hayakuwa mazungumzo ya kina kuhusu nini kiwe vipi katika maudhui na mapendekezo ya Tume.
Ukweli ni kwamba Rasimu zote mbili nilizipata mara ya kwanza nilipokabidhiwa rasmi, tena kwa uwazi.
Napenda watu wasijenge dhana kuwa nilipewa Rasimu na kuisoma kabla ya kukamilika na hivyo nilitoa maoni yangu. Tume hii ilikuwa huru na niliiacha iwe hivyo.
(AC)Sikuiingilia kwa namna yo yote ile kupenyeza mambo ninayotaka yawemo.
(AD)Kuthibitisha dhamira yangu ya kutaka Tume iwe huru katika kufanya kazi zao hata pale waliponitaka nitoe maoni niliwaomba tusifanye hivyo ili nisiwakwaze katika kufanya kazi zao, wakapata taabu ya kuwianisha wanayofikiria na mawazo yangu.
Ndugu Wananchi;
(AE)Kuhusu madai kwamba mambo yalikuwa yanakwenda vizuri na kwamba hotuba yangu iliyavuruga, napenda kusema wazi kuwa lawama hizo hazina ukweli wo wote. Ni madai yasiyokuwa na msingi. Kwani mimi hasa siku ile nilifanya lipi la ajabu.
(AF)Ukweli ni kwamba nilisema yale yale ambayo Tume yenyewe imeyasema katika Rasimu ya Katiba na Taarifa za Tume.
Niliyoyasema kuhusu malalamiko ya watu wa pande zetu za Muungano na uzuri na changamoto za miundo ya Serikali mbili na Serikali tatu ni yale yale yaliyomo kwenye taarifa za Tume.
(AG)Nimetumia takwimu zile zile za Tume. Pengine kilichoonekana kuwa kibaya ni jinsi nilivyozifasiri taarifa hizo na mapendekezo ya Tume.
Jambo lingine ambalo nimelifanya ni kutoa maoni yangu kuhusu baadhi ya vipengele vya Rasimu hususan uandishi na dhana mbalimbali zilizokuwamo. Silioni kosa langu kwa kufanya hivyo, kwani Rasimu imetolewa hadharani kwa watu kuijadili.
(AH)Na mimi kama raia ninayo haki ya kufanya hivyo kama wafanyavyo wengine. Kwa nini nilaumiwe kwa kutumia haki yangu hiyo.
(AI) Lakini, pia mimi ndiye Rais wa nchi yetu, ninayo dhamana ya uongozi na ulezi wa taifa letu.
Itakuwaje kwa jambo kubwa la hatma ya nchi yetu nilinyamazie kimya.
Watanzania wangeshangaa na wangekuwa na haki ya kuhoji Rais wao ana maoni gani.
(AJ)Bahati nzuri nilitoa maoni yangu mahali penyewe hasa, na kwa uwazi, kwenye Bunge Maalumu la Katiba.
(AK)Hata hivyo, ni muhimu kusisitiza kuwa namna nilvyotoa maoni yangu sikuwa natoa maagizo wala kushurutisha, ndiyo maana kila wakati niliwakumbusha Wajumbe kuwa mamlaka ya uamuzi ni yao.
Yangu yalikuwa maoni tu wanahiyari ya kuyakubali au kuyakataa.
Niliwataka Wajumbe wasome na kuielewa vyema Rasimu. Nilisema wasome sura kwa sura, mstari kwa mstari na neno kwa neno. Niliwaomba wajiridhishe kuhusu uandishi na dhana mbalimbali. Nilitoa mifano ya mambo yahusuyo uandishi ambayo ni vyema wayatazame. Pia nilitoa mifano ya dhana ambazo niliwasihi wajiridhishe juu ya kufaa kwake kuwepo.
(AL)Kuhusu muundo wa Serikali tatu, nilieleza wazi kuwa sina tatizo nao kama ndiyo matakwa ya Watanzania.
Lakini, nilieleza hofu yangu kuhusu mapendekezo ya Tume na kuwataka Wajumbe wafanye kazi ya ziada kuondosha udhaifu iwapo wataukubali muundo unaopendekezwa.
Nilieleza nia yangu ya kutaka tuwe na Serikali ya Muungano yenye ukuu unaoonekana, yenye nguvu ya kuweza kusimama yenyewe, inayoweza kuwa tegemeo kwa nchi Washirika, Serikali isiyokuwa tegemezi wala egemezi kwa nchi washirika na ambayo inavyo vyanzo vya uhakika vya mapato. Hivi kwa kutoa ushauri huo kwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba inageuka kuwa nongwa. Kwa kweli sielewi lawama ni ya nini?.
Naamini sistahili lawama bali pongezi kwa kuwa muwazi na kutoa ushauri wa msingi ambao utasaidia nchi kupata Katiba nzuri inayojali maslahi ya watu wa nchi yetu na ya nchi zetu mbili zilizoungana miaka 50 iliyopita.
Hitimisho
Ndugu Wananchi;
Mwisho, ni maoni yangu ya dhati kuwa mgogoro uliopo sasa katika mchakato wa Katiba hauna sababu ya kuendelea kuwepo.
(AM)Naamini hayo yote ambayo Wajumbe wa CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi wanayalalamikia yanaweza kushughulikiwa kwa ukamilifu katika mifumo ya Bunge Maalumu la Katiba iliyotengenezwa na Wajumbe wote na wao wakiwemo. Nawasihi waitumie.
Hali kadhalika, kwa kupitia mazungumzo wanayofanya na wenzao wa Chama cha Mapinduzi wanaweza kutengeneza nguvu ya pamoja kutatua changamoto za sasa na zitakazojitokeza baadaye.
(AN)Kilicho muhimu ni kwa pande zote kuwa na dhamira ya dhati ya kutoka hapa tulipo sasa.
Kama utashi wa kisiasa upo kwa kila mmoja wetu, hilo ni jambo linalowezekana kabisa.
(AP)Narudia kuahidi utayari wangu wa kusaidia kadri inavyowezekana tusonge mbele.
Mungu Ibariki Afrika!
Mungu Ibariki Tanzania!
Asanteni sana kwa kunisikiliza
Nguruvi3 je unafkiri kwamba UKAWA inaweza kuwa imara kiasi cha kuweza kupenya kupitia uchaguzi??gfsonwin , dhamira ya kweli haipo kwa CCM.
Ujio wa S3 unawatisha hasa kundi la wahafidhina. Rais Kikwete amesema, S3 ni hadi aondoke madarakani. Hapo kuna dhamira ya kweli?
Leo umemsikia, sehemu kubwa ilikuwa kukandia UKAWA. Tunauliza, hivi hakuona tatizo kwa CCM hata moja.
Bila hata ya kufikiri, ni rais huyu huyu aliruhusu Lukuvi kwenda kuhubiri kwa njia za hatari sana Kanisani.
Ni JK huyu huyu, ameshindwa kuwakemea CCM kwa kupotosha umma. Leo anapata wapi nia ya katiba?
Nadhani UKAWA wameamua kwenda katika uchaguzi mkuu. Nikisoma lengo lao ni kuhakikisha wanapunguza idadi ya wabunge wa CCM kwanza, halafu wanaingiza agenda ya katiba. Kwasasa hilo linaweza kufanikiwa kwasababu hoja ya katiba ni ya wananchi na wanakereka sana. Hivyo, down the road itakuja kuwaumiza tu CCM.
Hata hivyo, lazima UKAWA wawe makini. Wasirudie makosa ya nyuma. Wakati bunge linaendelea wao waendelee kufanya ufafanuzi kwa wananchi kila siku. Itafika mahali wananchi watadharau kama walivyodharau siku 10 za mwisho na huo ndio utakuwa mwisho wa katiba ya CCM.
Nitafafanua zaidi katika mabandiko yajayo.