UKAWA wanavyobabaika: Historia ya 'juisi ya maembe' kujirudia?

UKAWA wanavyobabaika: Historia ya 'juisi ya maembe' kujirudia?

Nguruvi3, Dah, nilikuwa naandika mara ghafla PC yangu ikazima na nikapoteza hata mada nilokuwa najadiliana na wewe . Nimeitafuta wala siipati hivyo nakuomba niwekee 'like' tu ili niweze kuipata tena mada hiyo ktk orodha ya msg maana nimegundua sasa ni wapi wewe huelewi ama hukosea.
Mkuu Mkandara , ulisepa nilipokuuliza Tanganyika inanufaika na nini katika muungano. Nikauliza zaidi, nje ya muungano Tanganyika itakosa kitu gani. Kwanini unadhani Tanganyika inaihitaji znz. Wiki imeisha umejichimbia, hali imetulia naona unadandia treni kituo cha mbele kabisa. Hebu rudi nyuma ubebe mizigo uliyoacha tunakusubiri mkuu, tujibu maswali yetu ya Tanganyika na muungano, halau tutaendelea.
 
Mkuu Mkandara , ulisepa nilipokuuliza Tanganyika inanufaika na nini katika muungano. Nikauliza zaidi, nje ya muungano Tanganyika itakosa kitu gani. Kwanini unadhani Tanganyika inaihitaji znz. Wiki imeisha umejichimbia, hali imetulia naona unadandia treni kituo cha mbele kabisa. Hebu rudi nyuma ubebe mizigo uliyoacha tunakusubiri mkuu, tujibu maswali yetu ya Tanganyika na muungano, halau tutaendelea.
Mkuu wangu wakati mwingine unauliza maswali ya ajabu kabisa. Unaposema Tanganyika inanufaika nini na huu Muungano una maana gani? Hivi nikuulize wewe hilo deni la taifa ni kiasi gani? au wewe utajibu vipi mtu akikuuliza unafaidika vipi na ndoa yako? Ni kipi kilichopo ktk ndoa yako ambacho huwezi kukipata pasipo ndoa hiyo? pengine wewe mwenzangu una akili sana tujuze nadhani ndio swali lako kwenye Utanganyika au sivyo?.

Swala sio Tanganyika inanufaika vipi bali ni ukweli kwamba mikopo tunachukua, hivyo kama tunaenda kulewea, tunaibiana kujenga miradi binafsi au kuhamishia ktk mabenki ya nje haya sii maswala ya kujadili hapa. Kinachojadiliwa hapa ni mikopo inachukuliwa na bara kwa jina la Muungano na kwa minajiri ya miradi isokuwa na Muungano - Kaput!. Mimi na wewe tunajua fika kwamba ni asimia 10 hadi 20 tu ndio hutumika kama gharama halali ya ujenzi wa miradi hiyo ya kitapeli, wakati asilimia 80 inawekwa kibondoni mwa viongozi wetu wakishirikiana na Makabaila. Hili sio swali la kuniuliza mimi mkuu wangu hata kidogo. Ni hawa wameifanya mikataba hii kuwa ya siri ili wapate kuendelea kutuibiwa wananchi bora wenzetu Wazanzibar wameshtuka kuliko sisi tusioona mbali zaidi ya marefu ya kero zetu..

Kwa hiyo mimi na wewe hatutakiwi kutazama ati Tanganyika inafaidika vipi, wakati tunajua wazi viongozi wanavyotajirika na mikopo hiyo hiyo, fedha za EPA, Radar, IPTL, ATC, Railway, migodi na miradi kibao ambayo sisi tunakula ruzuku tu, na sasa Imeingia Tazara watu wameshaanza kucheza bingo Mcjhina kaahidi mabillioni, Zambia wametushtukia. Sasa haya sii ya kuniuliza mimi ati Tanganyika inafaidika nini na Muungano wakati tunaibiwa na viongozi ambao hawana msalie, aidha uwape serikali 2 au 3 pasipo kubadilisha mfumo huu mbaya wa Kiutawala ambao mikataba ya uwekezaji nchini ni siri ya serikali tawala. Siri ya nani ktk uwekezaji nchini uliona wapi kama sio jeuri ya kuwaibia wananchi na hasa kuficha machafu yao.

Na naweza kukujibu kihuni vile vile kwa kusema wewe huoni maendeleo ya Tanganyika? Tanganyika ile ya Nyerere sawa na hii ya leo?. Fedha zinazokopwa nje leo zinajenga mabarabara, madaraja ambayo JK kapewa sifa kubwa lakini deni lote ni la Taifa. Mkapa alijenga daraja kubwa na uwanja wa mpira wa Kimataifa. Au unataka nikwambie ya kwamba Tanganyika ilifaidika na Muungano kutokana na Hayati Karume ndiye alojenga jengo la Yanga pale jangwani na pia kuchangia kwa asilimia kubwa Klabu ya Simba?.

Mkuu acha hizo leo tuna mipango ya Ujenzi wa bandari na airport mpya Bagamoyo, daraja la Kigamboni, madaraja ktk kila kivuko cha mito, Meli za Kigoma, Lake Nyasa na Victoria kote huko ni miradi ya serikali kuu sio ya watu binafsi kama ilivyo Zanzibar na hii yote ni mikopo ya Kimataifa ambayo Pasipo Muungano pengine tusingeifanya maana kama Zanzibar watakuwa na International Airport na bandari ya Free Port hakuna haja wala sababu ya Ujenzi wa miradi hiyo mipya.
 
Mkandara;10113797]Mkuu wangu wakati mwingine unauliza maswali ya ajabu kabisa. Unaposema Tanganyika inanufaika nini na huu Muungano una maana gani? Hivi nikuulize wewe hilo deni la taifa ni kiasi gani?
Swali hilo ni la 'ajabu' kwasababu linakukera kwa kutambua jibu lake si zuri kwa wazanzibar unaowatetea. Chanzo cha swali hilo kinatokana na wazanzibar wanaosema 'Muungano huu hauwasadii, wananyonywa na kuonewa''Swali Tananyika inafaidika na nini.

Hapa unafahamu wazi kuwa Tanganyika hainufuaiki na lololte katika muungano. Zama za muungano wa kisiasa zimekwisha, sasa ni zama za muugano wa kiuchumi.

Katika uchumi znz haina fao la aina yoyote kwa Tanganyika.Hivyo muungano huu ni kuwasaidia wazanzibar kwasababu Watanganyika hawanufaiki. Hakuna la maana zaidi ya kupoteza, kubeba zigo lisilo na square likisumbua mgongoni.
au wewe utajibu vipi mtu akikuuliza unafaidika vipi na ndoa yako? Ni kipi kilichopo ktk ndoa yako ambacho huwezi kukipata pasipo ndoa hiyo? pengine wewe mwenzangu una akili sana tujuze nadhani ndio swali lako kwenye Utanganyika au sivyo?.
Kuna faida za kujenga familia na kizazi. Faida za kiuchumi na kijamii.

Lakini katika ndoa hiyo kama mke atasema hana faida nayo, nitampa talaka. Nami nikigundua hakuna faida ya ndoa zaidi ya migogoro jibu ni talaka.Matatizo ndani ya ndoa yanazungumzika, mke anapokuwa barabarani akidai mume mwizi,huyo si mke ni mjinga au mwendawazimu, mwache, Mpe talaka haraka akafungue genge lake la nyanya.
Swala sio Tanganyika inanufaika vipi bali ni ukweli kwamba mikopo tunachukua, hivyo kama tunaenda kulewea, tunaibiana kujenga miradi binafsi au kuhamishia ktk mabenki ya nje haya sii maswala ya kujadili hapa. Kinachojadiliwa hapa ni mikopo inachukuliwa na bara kwa jina la Muungano na kwa minajiri ya miradi isokuwa na Muungano - Kaput!.
Swadakta, ndiyo maana tunasema iwepo Tanganyika,Magufuli ajenge barabara za Tanganyika na Mansour ajenge za znz.

Huwezi kusema Tanganyika inanufaika na misaada na mikopo wakati wazanzibar wanalala hawajui gharama za ulinzi na usalama ambazo hawawezi kulipia hata 2%. Hilo jina Tanzania unalosema linaiba linalipiwa na wenyewe.
Zanzibar kwa maneno ya Salimin Awad wa CCM amesema hawalipi.

Ni hivi, Magufuli hana uwezo wa kufanya kazi znz kwasababu kuna magufuli wa znz.

Hebu nieleze kama ni misaada na mikopo (hoja ya kipuuzi sana) kwa wasomi, maana msomi anapofikiria misaada na mikopo inasikitisha, unaingalia vipi.Kiasi gani znz inapata kupitia jina la Tanzania.

Nikupe namba kidogo, znz inapata 4.5 ya pato la Tanzania. Ukichukua pato hilo kama Trilioni 12 ambapo znz haina mchango, kwa mwaka mmoja inapata 540 bilioni.

Kwa minajili tu ya mjadala tuseme ni bilioni 400. Mapato ya znz 2014 ni bilioni 400 na bajeti ni bilioni 710.
Tofauti ya bajeti na mapato inapatikana kwa hizo 4.5. Kamuulize Salimini Awad wa Baraza la wawakilishi.
Kamuulize Omar mzee, na Shein.

In other words, kile cha Mtanganyika bila mikopo na misaada kinagawanywa kwa wazanzibar.
Arguably wanasema ni pesa za benki kuu. Leo wakilipwa kiasi chote hawawezi ku generate kiasi kikubwa zaidi ya hicho. Yaani mapato yanayotoka Tanganyika ni makubwa kuliko wanayofanyia kazi.
Kumbuka naongelea 12 Trilioni bila misaada au mikopo.

Watanganyika tunasema, no ! tunataka kila mtu aende Washington kwa Bretton Institutions akakope kwa jina lake alipe kwa jina lake, atumie kwa jina lake na mafisadi waibe katika nchi yake.

Wazanzibar wanaoona fahari kukopa (aibu kubwa sana kwa wasomi kuzungumzia) waende Paris Club na Bretton na Oman na kwingine wakakope na kupewa misaada yao bila kuingiliwa.
Inawezekana kama tutatenga shughuli kwa serikali ya Tanganyika na Zanzibar.

Hakuna tatizo na mafisadi kwasababu ni watu na mfumo unaweza kuwakomesha siku moja akipatikana kiongozi mweledi.

Ni tatizo na mfumo wa wizi unaofanywa kwa jina la muungano. Kasehemu kadogo kasiko na mchango kanachukua pande kubwa bila sababu, hilo Watanganyika hatukubali sasa.

Halmashauri 54 za Tanganyika kwa mwaka 2014 zimetengewa bilioni 540.
Hizi zinawakilisha sehemu kubwa ya uchumi, population na size mara zaidi ya 400 ya znz.

Kituko ni kuwa Zanz yenye watu wachache kuliko halmashuri yoyote kati ya hizo 54 inapewa zaidi ya bilioni 500 kwa pesa za moja kwa moja na gharama zinzaotokana.

Mfano, wabunge 81 wa znz wanaokuja Dodoma wanalipiwa bilioni 9.6 sawa na halamashrui moja ya Tanganyika kwa mwaka.

Leo mnasema misaada, huo si msaada ni kitu gani. Leo tunajeshi linagharimu trilioni 1.2, mambo ya ndani bilioni 900 na mambo ya nje bilioni zaidi ya 400 kwa ujumla wa trilioni 3. Kati ya hizo znz inachangia sifuri, I mean zero.
Leo mnasema hawapati msaada! msaada gani zaidi ya huo.

Watanganyika tunataka tuone znz ikikopa huko nje na kupewa misaada yake bila kuwaingilia.

Lakini pia yunataka tuone wanachangia nini katika huu uungano. Hata kama ni milioni moja lazima wachangie ili waone uchungu na umuhimu wake.Hatuwezi kuendelea kulea kelele tu, tunasema ruksa nendeni Paris na Washington
Serikali 3 ndilo jibu tu
Mimi na wewe tunajua fika kwamba ni asimia 10 hadi 20 tu ndio hutumika kama gharama halali ya ujenzi wa miradi hiyo ya kitapeli, wakati asilimia 80 inawekwa kibondoni mwa viongozi wetu wakishirikiana na Makabaila. Hili sio swali la kuniuliza mimi mkuu wangu hata kidogo. Ni hawa wameifanya mikataba hii kuwa ya siri ili wapate kuendelea kutuibiwa wananchi bora wenzetu Wazanzibar wameshtuka kuliko sisi tusioona mbali zaidi ya marefu ya kero zetu..
Ndio maana tunataka tuwaondoe katika mtego wa ufisadi, waende kukopa na kupata misaada yao. Tunataka Tanganyika ili tuhangaike na matatizo yetu bila kuwapa wazanzibar.
Afadhali wameshtuka, watuunge mkono kila mtu na serikali yake.Kwanini tuwape taabu. Serikali 3 zinawasaidia wao si sisi.
Sasa haya sii ya kuniuliza mimi ati Tanganyika inafaidika nini na Muungano wakati tunaibiwa na viongozi ambao hawana msalie, aidha uwape serikali 2 au 3 pasipo kubadilisha mfumo huu mbaya wa Kiutawala ambao mikataba ya uwekezaji nchini ni siri ya serikali tawala. Siri ya nani ktk uwekezaji nchini uliona wapi kama sio jeuri ya kuwaibia wananchi na hasa kuficha machafu yao.
Sawa , tunachosema mafisadi ni sawa na vibaka. Wanaiba tu.

Tunataka znz wasiibiwe na njia rahisi ni wao kuwa na mamlaka kamili ya kuendesha mambo yao. W
aende Oman na Washington kukopa, wakusanye kodi zao na kwavile hawana mafisadi watumie katika miradi yao.

Walipie ulinzi na usalama, mambo ya ndani na kila gharama zao. Hawana sababu ya kujifunga na Tanganyika yenye maifsadi. Maifsadi watuachie tuhangaike nao.

Njia nyepesi ni serikali 3. Wakikataa serikali 3 nao ni wezi wakubwa tu kama maifasadi.
Na naweza kukujibu kihuni vile vile kwa kusema wewe huoni maendeleo ya Tanganyika? Tanganyika ile ya Nyerere sawa na hii ya leo?. Fedha zinazokopwa nje leo zinajenga mabarabara, madaraja ambayo JK kapewa sifa kubwa lakini deni lote ni la Taifa. Mkapa alijenga daraja kubwa na uwanja wa mpira wa Kimataifa. Au unataka nikwambie ya kwamba Tanganyika ilifaidika na Muungano kutokana na Hayati Karume ndiye alojenga jengo la Yanga pale jangwani na pia kuchangia kwa asilimia kubwa Klabu ya Simba?.
Hapa swali linabaki tunafaidika nini kwa kuwa na znz katika uchumi wetu.

Kama Watanganyika, hatuna faida ya aina yoyote, narudia hata leo muungano ukivunjika hakuna Mtanganyika atakayejiuliza kwanini. Huko Manyoni kuna watu hawajui znz ni nini.

Ali Swalehe anasema hivi, amezunguka mikoani na kugundua kuwa Tanganyika ina WAPUMBAVU waisojua muungano.

Ni kweli anachosema ingawa lugha yake ni mbovu, nani anashughulishwa na znz kule Manyara.
Inamhusu nini maana Manyara haitegemei znz kwa jambo lolote. Inamhusu nini mtu wa Dar es Salaam au Tanga.

Elimu ya kwa Watanganyika imefanikiwa sasa wanadai nchi yao na hakuna wa kuwazuia.

Zanzibar kila la heri kama mnataka muungano ni kwa kuwajibika, adabu na heshima!ala.
Mlipiwe bill halafu mlete mdomo.

Kinyume chake njia nyeupee, vunja jahazi tugawane mbao maana sisi hatuwahitaji.
Mkuu acha hizo leo tuna mipango ya Ujenzi wa bandari na airport mpya Bagamoyo, daraja la Kigamboni, madaraja ktk kila kivuko cha mito, Meli za Kigoma, Lake Nyasa na Victoria kote huko ni miradi ya serikali kuu sio ya watu binafsi kama ilivyo Zanzibar na hii yote ni mikopo ya Kimataifa ambayo Pasipo Muungano pengine tusingeifanya maana kama Zanzibar watakuwa na International Airport na bandari ya Free Port hakuna haja wala sababu ya Ujenzi wa miradi hiyo mipya
Kwamba tusijenge bandari zetu tusubiri wazanzibar. Ney.

Tunajenga ya mwambani, tunajenga ya Bagamoyo tunapanua ya Dar. Airport ya Kilimanjaro ni kwa Watanganyika na tutajenga nyingine nyingi tu. Watalii watakuja Kilimanjaro, wakibaikisha pesa wataenda znz.
Soko la Afrika mashariki tuna access nalo, tunajenga bandari. Hiyo bandari huru ya znz ni kwa ajili yao.
Sisi ndio soko la znz na tunaelekea kuchukua umiliki wa soko letu kwajili ya watu wetu siyo wa nchi jirani ya zanzibar.

Huu upuuzi wa kusubiri znz wajenge kwasababu ni wazuri sana hatuukubali.
Wao hawana mchango wanataka miradi ya nini. Waende Oma na Washington wakakope, wajenge International airport yao, wajenge bandari huru yao na kila kitu chao , hatuna taabu.

Hiyo isiwe sababu ya kwanyima wakaazi wa Tanga fursa za uwepo wa bandari yao, wakaazi wa Kilimanjaro au Mpanda kufanya maendeleo yao.

Wao hawataki utanzania na wameukana, sasa huruma ya nini.

Wao ni wznz bwana tunawaacha kama walivyo.
Sisi Watanganyika tutaendelea kama Watanganyika. Hawataki Utanzania kwanini unawalaizimisha mkuu. Let them go!

Zamani walikuwa anatisha tisha kuvunja muungano. Ule upambavu wa Watanganyika aliosema Ali Salehe umeondoka, Watanganyika wameshaelewa hawahitaji znz kwa lolote lile. Leo niambie, umesikia mznz gani akinyanyua pua na kusema tunavunja muungano. Tanganayika tunasema kama wazn wanataka kuvunja muungano wasije Dodoma, sisi tutaendelea na bunge la katiba kuandika katiba ya Tanganyika. Hatuwahitaji, hawana msaada wala hatuna sababu za maana za kuwa nao zaidi ya kwausaidia. Hatuwahaitaji the least to say
 
Nguruvi3,
Swali hilo ni la 'ajabu' kwasababu linakukera kwa kutambua jibu lake si zuri kwa wazanzibar unaowatetea. Chanzo cha swali hilo kinatokana na wazanzibar wanaosema 'Muungano huu hauwasadii, wananyonywa na kuonewa''Swali Tananyika inafaidika na nini.
Mkuu swali hilo halinikeri isipokuwa nimekujibu sii mara moja wala sii chini ya mara 10 tena kwa maelezo marefu sana bado huelewi.
Labda nikwambie kwa kifupi ni kwamba Tanganyika inafaidika na Muungano huu kwa kutumia fursa zilizopo za kuchukua mikopo na misaada nchi za nje kwa jina la Tanzania (muungano) na kuitumia ktk maswala yasiyokuwa ya Muungano. Zanzibar hawana mamlaka hayo isipokuwa kwa idhini ya Tanganyika!

Nini tena unataka kujua?
 
Nguruvi3,
Mkuu swali hilo halinikeri isipokuwa nimekujibu sii mara moja wala sii chini ya mara 10 tena kwa maelezo marefu sana bado huelewi.
Labda nikwambie kwa kifupi ni kwamba Tanganyika inafaidika na Muungano huu kwa kutumia fursa zilizopo za kuchukua mikopo nchi za nje kwa jina la tanzania na ikatumia ktk maswala yasiyokuwa ya Muungano. Zanzibar hawana mamlaka hayo isipokuwa kwa idhini ya Tanganyika!

Nini tena unataka kujua?
Je unadhani bila znz Tanzania haiwezi kupata mikopo au misaada mnayopigia debe.
Sidhani hata huko nje wanatambua znz ni kitu gani. Huwezi kumfanya panya awe tembo hata siku moja. Panya ni panya na tembo ni tembo.

Ili kuhakikisha Tanganyika haifaidiki na fursa za kutumia jina la zanzibar tunasema, tugawane majukumu.
Tanganyika izinduke na ichacharike kivyake na znz nao wapewe fursa za kwenda Paris club, washington na kwingineko kukopa na kuapta misaada. Hatuna tatizo na hilo.

Njia nyepesi kabisa, ni S3. Hilo hutaki bado unasema Tanganyika inatumia jina la Tanzania. Sasa inawezaje kwenda kupata misaada na mikopo ikiwa haipo. Mimi husema kila siku sijui hata unakumbuka ulichoandika siku iliyopita. Wewe unasema mambo yote ya muungano, halafu unasema Tanganyika ambayo imeporwa utaifa wake na Tanzania eti ikaombe misaada na mikopo(kwangu mimi naona aibu sana kuongelea hoja za misaada, ni dhalili sana) kwa jina la Tanganyika.

Wewe unayesema tuna JMT na ZNZ ndio huyo huyo unalalamika Tanganyika kuinyonya znz. Tanganyika haionekani sasa inaonyonya vipi? Ni ghost, sasa sisi tunaotaka kutenga shughuli tunaonekana hatufai. Mantiki zinatutetea sana tena kwa mantiki.
Hatuna flip flops kwasababu hoja zimesima zenyewe.

Huwezi kuwa na JMT ukiyoiita Tanganyika, halafu ukalamu Tanganyika isiyopkuwepo kunyonya kusicho. White elephant.


Pili, hao znz wanatumia jina la Tanzania kuinyonya Tanganyika. Leo hawana mchango wowote isipokuwa wamekuwa chanzo cha kuvuja na kuchukua hata kisicho chao. Deni la ndani na gharama za muungano hawazijui wanachojua ni mikopo na misaasda. Hilo hatutaki tena.

Ikishindikana , hatuna sababu za kushikiliana kwa kamba. Sisi Tanganyika hatuhitaji uwepo wa znz kwa namna yoyote.
Wana hiari ya kuja Dodoma au wabaki makwao. Tunaweza kuvunja jahazi na kugawama mbao, tutrapoteza nini?
 
Je unadhani bila znz Tanzania haiwezi kupata mikopo au misaada mnayopigia debe.
Sidhani hata huko nje wanatambua znz ni kitu gani. Huwezi kumfanya panya awe tembo hata siku moja. Panya ni panya na tembo ni tembo.

Ili kuhakikisha Tanganyika haifaidiki na fursa za kutumia jina la zanzibar tunasema, tugawane majukumu.
Tanganyika izinduke na ichacharike kivyake na znz nao wapewe fursa za kwenda Paris club, washington na kwingineko kukopa na kuapta misaada. Hatuna tatizo na hilo.

Njia nyepesi kabisa, ni S3. Hilo hutaki bado unasema Tanganyika inatumia jina la Tanzania. Sasa inawezaje kwenda kupata misaada na mikopo ikiwa haipo. Mimi husema kila siku sijui hata unakumbuka ulichoandika siku iliyopita. Wewe unasema mambo yote ya muungano, halafu unasema Tanganyika ambayo imeporwa utaifa wake na Tanzania eti ikaombe misaada na mikopo(kwangu mimi naona aibu sana kuongelea hoja za misaada, ni dhalili sana) kwa jina la Tanganyika.

Wewe unayesema tuna JMT na ZNZ ndio huyo huyo unalalamika Tanganyika kuinyonya znz. Tanganyika haionekani sasa inaonyonya vipi? Ni ghost, sasa sisi tunaotaka kutenga shughuli tunaonekana hatufai. Mantiki zinatutetea sana tena kwa mantiki.
Hatuna flip flops kwasababu hoja zimesima zenyewe.

Huwezi kuwa na JMT ukiyoiita Tanganyika, halafu ukalamu Tanganyika isiyopkuwepo kunyonya kusicho. White elephant.


Pili, hao znz wanatumia jina la Tanzania kuinyonya Tanganyika. Leo hawana mchango wowote isipokuwa wamekuwa chanzo cha kuvuja na kuchukua hata kisicho chao. Deni la ndani na gharama za muungano hawazijui wanachojua ni mikopo na misaasda. Hilo hatutaki tena.

Ikishindikana , hatuna sababu za kushikiliana kwa kamba. Sisi Tanganyika hatuhitaji uwepo wa znz kwa namna yoyote.
Wana hiari ya kuja Dodoma au wabaki makwao. Tunaweza kuvunja jahazi na kugawama mbao, tutrapoteza nini?
Swala sio Tanganyika wanaweza kupata Mkopo au hawawezi bila Zanzibar, kesi iliyopo mezani ni kwamba tanganyika inapata yote hivi sasa kwa kutumia Jina la Tanzania (a verdict) na ndio sababu Zanzibar wanataka bora kuvunja Muungano tuunde Shirikisho ili wao pia wapate kuwa nchi kamili yenye uwezo wa kupata mikopo na misada hiyo kama sisi. Wao kupewa mikopo na Misaada kama sisi bila idhini ya Tanganyika imeshindikana na tulishindwa kupata suluhu ktk hilo toka tume zote zilizoundwa.

Tanganyika inachukua mikopo hiyo jambo ambalo kiutawala ni kosa na ndio maana wanasema Tanganyika imevaa koti la muungano, kwanza tukubali makosa hayo ya Kimfumo ili turekebishe na sio kuvunja ndoa kwa sababu Zanzibar wanaomba haki yao na wameeleza ubaya wetu. Huwezi kujibu kesi ya mashtaka kwa kusema ubaya wa mwingine yaani kama vile tunafanya hivi makusudi ili kuwadhalilisha, utetezi wako wote hauna maana, ni kujihami bila kuelewa kesi inahusu nini.

Huu ujinga wa nani anaghramia Ulinzi na Usalama wakati vifaa vya kijeshi vinatengenezwa nje kwa gharama ya wananchi wa JMT, leo wewe unakuja kubeza Zanzibar wakati hujui tunazungumzia nini inanipa wasiwasi sana na kuelewa kwako! yaani kila siku tunarudia yale yale ilihali mtu mwingine angeisha elewa na kukaa kimya maana kweli tunatumia jina la Tanzania kwa mambo yasokuwa ya Muungano, sasa sijui toka lini Ulinzi na Usalama pia yakawa sii mambo ya Muungano!
Yaani hueleweki kabisa....
 
Swala sio Tanganyika wanaweza kupata Mkopo au hawawezi bila Zanzibar, kesi iliyopo mezani ni kwamba tanganyika inapata yote hivi sasa kwa kutumia Jina la Tanzania (a verdict) na ndio sababu Zanzibar wanataka bora kuvunja Muungano tuunde Shirikisho ili wao pia wapate kuwa nchi kamili yenye uwezo wa kupata mikopo na misada hiyo kama sisi. Wao kupewa mikopo na Misaada kama sisi bila idhini ya Tanganyika imeshindikana na tulishindwa kupata suluhu ktk hilo toka tume zote zilizoundwa.

Tanganyika inachukua mikopo hiyo jambo ambalo kiutawala ni kosa na ndio maana wanasema Tanganyika imevaa koti la muungano, kwanza tukubali makosa hayo ya Kimfumo ili turekebishe na sio kuvunja ndoa kwa sababu Zanzibar wanaomba haki yao na wameeleza ubaya wetu. Huwezi kujibu kesi ya mashtaka kwa kusema ubaya wa mwingine yaani kama vile tunafanya hivi makusudi ili kuwadhalilisha, utetezi wako wote hauna maana, ni kujihami bila kuelewa kesi inahusu nini.

Huu ujinga wa nani anaghramia Ulinzi na Usalama wakati vifaa vya kijeshi vinatengenezwa nje kwa gharama ya wananchi wa JMT, leo wewe unakuja kubeza Zanzibar wakati hujui tunazungumzia nini inanipa wasiwasi sana na kuelewa kwako! yaani kila siku tunarudia yale yale ilihali mtu mwingine angeisha elewa na kukaa kimya maana kweli tunatumia jina la Tanzania kwa mambo yasokuwa ya Muungano, sasa sijui toka lini Ulinzi na Usalama pia yakawa sii mambo ya Muungano!
Yaani hueleweki kabisa....
Well said, tunataka shirikisho.
Nasisi ndipo hoja yetu ilipo kuwa hutataki kuendelea kutumia jina kunyonya znz kama wanavyosema.

Lakini nao pia wasitumie jina la Tanzania kujificha na kudai wasichostahili.
Suluhu ni moja tu, tuwe na shirikisho, wao waende wanakojua nasi twende tunakojua.

Hatuna sababu za kuwazuia kupata mikopo. In fact huo ni ukatili.
Zanzibar hawatakiwi kibali cha kwenda kukopa, ili mradi watakopa kwa jina la znz na si kama ilivyo sasa.

Leo wamekopa na asilimi 88 ya mkopo ni dhamana ya Tanzania. Hilo hutataki maana tunawajua, ni wavivu sana wa kulipa na hawakawii kupitisha deni hilo kwa JMT kama walivyozoea kwa umeme kwa miaka mingi hadi tulipopiga kelele wanalipa vijisenti tunasikia.

Ni makosa JMT kuwazuia wznz kwenda kukopa. Wapewe fursa waende Paris na Washington. Ni makosa kuwazuia wasipate misaada, waende Oman alikosema Ali Salehe watapewa misaada. Hata wakitaka kuuza pande la kisiwa chao hakuna sababu za kuwazuia.

Lakini zipo sababu kama mambo yao yanaingilia maisha ya Watanganyika.
Hawawezi kuja Dar es salaam kujipangia asilimia za ajira ambazo huko kwao hazipo kwa ubaguzi wa kizanzibar. Hilo linafika mwisho kwa hiari kwa lazima.

Hawawezi kuvunja katiba ya JMT halafu wakaitumia kuja kujipatia fursa za muungano, hilo linafika mwisho kwa hiari kwa lazima.

Hawawezi kuleta ubaguzi kwa Mtanganyika nasi tukawaangalia, hilo linafikia mwisho kwa hiari kwa lazima.

Wanachaguo moja, tuvunje jahazi tugawane mbao, au tukae pamoja wakiwa na adabu na nidhamu.

Sisi hatuhitaji znz kwa lolote kwa chochote na kwa ubinafsi na roho zao za chuki dhidi ya Watanganyika, hata neema ikiwateremkia hao hawatatujali.

Kama wanatuchoma moto kukiwa na katiba ya pamoja, nje ya hapo ni nini undadhani.

In short S2 za kuwabeba wznz haziawezekani.
Zinawezekana kwa muda lakini gharama zake zitakuwa kubwa.

Serikali 3 zinaweza kuwapa unafuu, kinyume chake tuvunje jahazi tu.
We have nothing to lose, let them go!
 
Well said, tunataka shirikisho.
Nasisi ndipo hoja yetu ilipo kuwa hutataki kuendelea kutumia jina kunyonya znz kama wanavyosema.

Lakini nao pia wasitumie jina la Tanzania kujificha na kudai wasichostahili.
Suluhu ni moja tu, tuwe na shirikisho, wao waende wanakojua nasi twende tunakojua.

Hatuna sababu za kuwazuia kupata mikopo. In fact huo ni ukatili.
Zanzibar hawatakiwi kibali cha kwenda kukopa, ili mradi watakopa kwa jina la znz na si kama ilivyo sasa.

Leo wamekopa na asilimi 88 ya mkopo ni dhamana ya Tanzania. Hilo hutataki maana tunawajua, ni wavivu sana wa kulipa na hawakawii kupitisha deni hilo kwa JMT kama walivyozoea kwa umeme kwa miaka mingi hadi tulipopiga kelele wanalipa vijisenti tunasikia.

Ni makosa JMT kuwazuia wznz kwenda kukopa. Wapewe fursa waende Paris na Washington. Ni makosa kuwazuia wasipate misaada, waende Oman alikosema Ali Salehe watapewa misaada. Hata wakitaka kuuza pande la kisiwa chao hakuna sababu za kuwazuia.

Lakini zipo sababu kama mambo yao yanaingilia maisha ya Watanganyika.
Hawawezi kuja Dar es salaam kujipangia asilimia za ajira ambazo huko kwao hazipo kwa ubaguzi wa kizanzibar. Hilo linafika mwisho kwa hiari kwa lazima.

Hawawezi kuvunja katiba ya JMT halafu wakaitumia kuja kujipatia fursa za muungano, hilo linafika mwisho kwa hiari kwa lazima.

Hawawezi kuleta ubaguzi kwa Mtanganyika nasi tukawaangalia, hilo linafikia mwisho kwa hiari kwa lazima.

Wanachaguo moja, tuvunje jahazi tugawane mbao, au tukae pamoja wakiwa na adabu na nidhamu.

Sisi hatuhitaji znz kwa lolote kwa chochote na kwa ubinafsi na roho zao za chuki dhidi ya Watanganyika, hata neema ikiwateremkia hao hawatatujali.

Kama wanatuchoma moto kukiwa na katiba ya pamoja, nje ya hapo ni nini undadhani.

In short S2 za kuwabeba wznz haziawezekani.
Zinawezekana kwa muda lakini gharama zake zitakuwa kubwa.

Serikali 3 zinaweza kuwapa unafuu, kinyume chake tuvunje jahazi tu.
We have nothing to lose, let them go!
Mnaotaka shirikisho ni wewe na kina nani? kama upo na hao UKAWA basi hilo mtabakia nalo wenyewe na sintowaunga mkono kabisa kwa sababu njama zenu ni dhidi ya wananchi kuitaka katiba Mpya wala sii CCM. Haya ndio mambo yalowanyima wananchi katiba mpya kwa kutanguliza kuwa Muungano wetu ni wa watu wawili na hati ya muungano ni feki wala sii CCM wala JK bali UKAWA ndio wamekuja vunja Muunganio kwani huwezi kuwa na Muungano (Union) na Shrikisho (Federation) wa pamoja!

Maadam sasa tumeelewana kila mmoja ana msimamo wake nadhani hakuna haja ya kuendeleza malumbano.
 
Mnaotaka shirikisho ni wewe na kina nani? kama upo na hao UKAWA basi hilo mtabakia nalo wenyewe na sintowaunga mkono kabisa kwa sababu njama zenu ni dhidi ya wananchi kuitaka katiba Mpya wala sii CCM. Haya ndio mambo yalowanyima wananchi katiba mpya kwa kutanguliza kuwa Muungano wetu ni wa watu wawili na hati ya muungano ni feki wala sii CCM wala JK bali UKAWA ndio wamekuja vunja Muunganio kwani huwezi kuwa na Muungano (Union) na Shrikisho (Federation) wa pamoja!

Maadam sasa tumeelewana kila mmoja ana msimamo wake nadhani hakuna haja ya kuendeleza malumbano.
Tunaotaka shirikisho ni Watanganyika wengi sana wale Ali Salehe aliowaita wajinga wa muungano.

Mtanganyika atambue hana sababu za kuinyonya znz.
Waachwe waende Bretton institutions wakakope. Ni makosa kuwazuai znz kwenda kukopa.
Waacheni waende kwa nembo yao wakope na wapate misaada.

Sisi Tanganyika tumeelemewa na zigo la muungano peke yetu.
Miaka 50 hakuna unafuu inatia maumivu zaidi.

Kibaya zaidi miaka 50 tunabaguliwa zaidi kuliko kuungana.
Mtanganyika haruhusiwi kupata fursa ya aina yoyote znz isipokuwa ulinzi wa usiku.
Wakati hayo yakitokea wao wanakuja na jina la Tanzania kupata fursa za Tanganyika.

Na zaidi wamefikia mahali wanakusanyana huko znz wanakuja kukaa vikao Dar es Salaam vya kuamua watoto wao wangapi walipie HESLB bila mkopo, wakimaliza wangapi wapewe ajira (asilimia 2). Hayo wanayafanya ndani ya Tanganyika, wametuona Wajinga asemavyo Ali Salehe Alberto.

Hatuhitaji kuinyonya znz kwasababu hakuna mahali pa kunyonya.
Uchumi wa bilioni 400 unakwenda kunyonya nini.
Kibaya zaidi wamefikia hatua wanavunja katiba halafu wanatuita wajinga. Hilo sasa mwisho.

Hatuna ugomvi na znz , tunataka tu Tanganyika yetu.
Kitendo cha wao kutaka S2 ni kutaka kujibanza mgongoni mwetu wakiporomosha mitusi na kashfa.
Ni kutumia herufi NIA kupata wasichostahili. Sasa baasi, tuachwe tupumue na Tanganyika yetu.

Tunataka Tanganyika tu, tuamue mambo yetu.
Hatuhitaji kuwazuia wznz kukopa. Hatuhitaji kuwazuia misaada.

Lakini, wasituzuie na Tanganyika yetu. Wao ni nchi jirani, wameshaondoka katika Utanzania na kutuacha tumeduwaa kama alivyosema Nyerere.

Waacheni waende zao, tumechoka na uongo wa kuwaibia wakati hawana cha kuibwa.

Shirikisho tu, ili tuendelee kuwalea penye ugumu, kinyume chake njia nyeupee, hatuwazuii wala hatuwahitaji, simple as that.
 
Tunaotaka shirikisho ni Watanganyika wengi sana wale Ali Salehe aliowaita wajinga wa muungano.
Utakuwaje wewe mjinga wa Muungano ikiwa unataka Shirikisho? wewe na yeye Ali Salehe hamna tofauti lugha zenu, wajinga ni sisi tunaotaka Muungano uloasisiwa na viongozi wetu. UKAWA = HIZBU.
 
Utakuwaje wewe mjinga wa Muungano ikiwa unataka Shirikisho? wewe na yeye Ali Salehe hamna tofauti lugha zenu, wajinga ni sisi tunaotaka Muungano uloasisiwa na viongozi wetu. UKAWA = HIZBU.
Umesahau Nyerere ambaye ni muasisi alisema znz kama hawataki muungano hatawapiga mabomu. Akaongeza kusema likiundwa shirikisho la EA ni bora Tanganyika na Zanzibar zikaingia independently. Naye alikuwa UKAWA au Hizbu?
 
MBOWE NA CHADEMA, JUISI YA MAEMBE HADI LINI?

MTAJIFUNZA LINI KUTOKANA NA MAKOSA?


Kamati kuu ya CDM imemaliza kikao na kutoa matamko kuhusu kurejea bungeni.
Moja ya hoja ni ile inayosema, kamati kuu imeridhia kuendeleza mazungumzo na rais Kikwete.
Hadi hapo tunaweza kusema UKAWA wana mazungumzo na rais JK na kinachofanyika ni kuendeleza.

UKAWA wakiongozwa na CDM wamekataa kushiriki kikao cha mwenyekiti Sitta kwa kuamini kuwa ni wajumbe hao hao walioshindwa kuokoa mchakato.Hakuna uwezekano wa wao kutenda na kinyume walichoshindwa hapo awali.

Msimamo huu unaonekana kuwa mzuri kimantiki na hoja kubwa ilikuwa ni kupatikana kwa watu nje ya 'inner circle' ya CCM kukwamua mchakato.

UKAWA wametoa masharti ya kurudi ikiwa ni pamoja na kuzingatiwa kwa rasimu kama ilivyowakilishwa na kufanyiwa marekebisho vifungu na kanuni wakimaanisha kuwa rasimu iliyowakilishwa ndiyo maoni ya wananchi.

Tunaposikia neno kuendeleza mazungumzo na Rais Kikwete tunashangazwa sana.
CHADEMA chini ya Mbowe wameshiriki sana katika mijadala na JK. Kila mara wameingizwa mjini.

Mifano ipo mingi, huu hapa ni mmoja unaoelekeana sana na kile wanachokitaka sasa.
CDM waligomea idadi ya wabunge wa kuteuliwa na Rais, aina ya wawakilishi na uwepo wa tume ndani ya bunge la katiba.

JK akawaita katika kile kinachojulikana kama juisi ya maembe. Akakubali mambo yote isipokuwa moja, la kuzuia tume kuingia katika bunge. Huu ulikuwa mkenge wa kufunga mambo mengi pamoja na kisha kuwapa robo tatu na JK kubaki na lile analotaka ambalo ni tume kutoingia.

JK akaenda bungeni akiwa na rasimu zaidi ya miezi miwili mkononi huku akiwasifu wajumbe kwa kazi kubwa na nzuri waliofanya. Kilichotokea ilikuwa kuwanyanyasa wazee wa tume mbele ya umma, na hata kufikia kuwanyang'anya vitendea kazi baada ya hotuba ikiwa ni ushahidi kuwa kazi ya kuimaliza tume ilishaanza na kukamilika katika masaa machache.

JK ni 'mutuhumiwa' wa kwanza wa kuvuruga mchakato.
Leo mnakwenda kuongea naye ili aseme nini zaidi ya kile cha kuwanyanyasa wazee wetu mbele ya TV zote.

Suala lilikuwa kutafuta chombo huru kitakachomshauri rais aondoe kauli zake zilizovuruga mchakato na si yeye kuzungumza nanyi ili aondoe kauli hizo. Hilo halipo.

CDM na Mbowe wanakwenda Ikulu (kuendeleza) mazungumzo yao.
Wanasahau mtego wailiotegewa na Samwel Sitta kuhusu kurudi bungeni.

CCM wanachokitaka ni kitu kimoja tu, UKAWA warudi bungeni hata kwa masaa mawili.
Wakishaingia mbinu za kuvuruga mchakato za CCM zitawekwa hadharani.

UKAWA watakapotoka, CCM watabadili kanuni na kufanya simple majority ambayo wanayo tayari kwa kuwapiga kufuli wabunge wao.

Hapo UKAWA wataonekana katika sura hizi
1. Kwamba wamepania tu kukwamisha mchakato
2. Wanataka matakwa yao na wala si hoja ya tume
3. Hawakubaliani na taratibu

Hoja ya UKAWA kuwa wataenda kuzunguka mikoani kupinga katiba kwa kura ya maoni ni dhaifu sana.
Hawakuweza kuzuia kuibwa kwa kura katika uchaguzi, sijui wanawezaje kuzuia kura za maoni zisiibwe.

Hoja hiyo walipaswa kuifanya wakati huu, tuliona wajumbe wao wakijikita kuzungumzia znz inavyonyonywa na wala si kukiukwa kwa rasimu, na hapa Tundu Lissu anahusika sana.

UKAWA nje na Dr Slaa hawakuwa na nguvu ya kuzuia CCM kupotosha.
Leo wanasema wanaweza kuzuia kwa kutumia kura ya maoni.

Zote hizi ni dalili za kubabaika na huenda wakaishia katika juisi ya maembe kama walivyozoea.

UKAWA hawana sababu za kuhangaika kuokoa mchakato, wana sababu za kuhangaika ili kuona rasimu iliyopo inajadiliwa kwa mujibu wa sheria iliyopo , kanuni, taratibu na kwa kuheshimu maoni ya wananchi.

Hata kama uchgauzi wa mwakani utafanyika kwa katiba iliyopo, hilo ni bora kuliko 'bora katiba' itakayotuacha na matatizo makubwa kwa miaka mingine

UKAWA wana wajibu wa kusimimamia wanachokiamini ni sahihi kwa masilahi ya taifa na si kuogopa kuombwa na viongozi wa dini. Viongozi ambao hawaelezi haki inakiukwa wapi bali wanataka tu UKAWA warejee ili kumfurahisha mh Rais.

UKAWA watakwenda Ikulu kwa JK kuongea naye. Wakiwa huko wasaidizi wa JK wanaendelea na upotoshaji kama alivyosikika Bulembo akisema UKAWA warudi zishindanishwe hoja.

Utashindanishaje hoja huku CCM wakiwa tayari wameshawapiga kufuli wbunge wao?
Kama walitaka kushindanisha hoja kwanini waligomea kura ya siri.
Kwanini waligomea JK kufungua bunge baada ya Warioba.

Huko Ikulu JK kama anavyojulikana atawaambia maneno matamu sana.
UKAWA watarudi bungeni ambako kanuni zitabadilishwa haraka ili hata wakiondoka shughuli iendelee kama CCM wanavyotaka.

UKAWA wanawezaje kumwamini mwenyekiti wa CCM ambaye ni mpinzani wao, ili hali mwenyekiti huyo hakuwaamini makada wake akina Salim, Butiku, Warioba na marofesa lukuki?

Kwamba, JK anaweza kuafikiana nao zaidi ya Warioba aliyekuwa anaongea naye kila siku na mwisho wa siku 'akamwaga' mzima mzima taifa likushuhudia.

Mbowe, safari yenu imejaa kubabaika. Karata mnayocheza na JK ni mbovu. Si muda mrefu mtarudi kutueleza

Tusemezane
 
SITTA AENDELEZA UPOTOSHAJI
MBINU ZAMWISHIA, SASA ANATAMANI UBABE

HAKUNA KATIBA ISIYO NA MARIDHIANO


Kikao cha kamati aiyoiteua Sitta kimemalizika .
Wajumbe wa UKAWA hawakuhudhuria licha ya vitisho vya Sitta kuhusu kile alichokisema kama vichwa ngumu.

Hakika wamekuwa vichwa ngumu na kichwa kinamuuma Sitta wala si wao.
Anguko lake na uwezo wake kwa mambo ya kitaifa sasa hakuna shaka vimefika mwisho.

Katika taarifa yake, Sitta ametoa mapendekezo kadhaa ili kukidhi haja zake na CCM katika kuandika katiba yao

1.Kikao cha bunge maalumu kiendelee kama kilivyopangwa.
Hoja yake ni kuwa kuna mambo kama uvuvi, kilimo ambayo ni muhimu kuliko muundo wa serikali.
Sitta haelewi kuwa hakuna nyumba inayokamilika ikiwa na furniture tu bila jengo.

2.Kwamba, kikao hicho kimefanyika kwasababu akidi ya theluthi mbili ilitimia.
Sitta anafahamu yeye ndiye alichagua kamati hiyo na kujiwekea wajumbe anaojua watakidhi akidi
Kusema akidi imetimia ni kujidanganya mwenyewe, hakuna akidi inayotengenezwa na mtu na kutimia.

3.Kwamba, kuwe na mabadiliko ya kanuni ili kudhibiti utoro na ukosefu wa nidhamu
Sitta alikuwepo wakati bunge la JMT linapitisha sheria ya kuundwa bunge la katiba kwa akidi ya watu 100.
Kwa unafiki hakukemea, leo anapata wapi nguvu za kukemea uzembe alioshiriki kuutengeneza kutoka bunge la JMT

Lakini pia, kudhibiti nidhamu anakokutaka ni ili wajumbe wakubaliane naye.
Wale watakaokataa maoni yake wafukuzwe ili abaki na kundi la ‘ndiyo' mzee.

Sitta hatambui kuwa katiba inayoandikwa si yake wala watoto wake ni ya taifa na kwamba, lazima kuwe na mawazo mbadala hata kama hayapendi.

Udikteta kama wa kufukiwa Richmond, Meremeta haukubaliki zama hizi na hilo Sitta aelewe bila kumuonea aibu.
Sitta alifunika uzembe uliolitia taifa aibu na sasa anataka kurudia tena.

4. Kwamba, UKAWA wameombwa warudi na makundi ya jamii nay ale ya dini.
Sitta anapotosha kwasababu makundi ya dini yalitaka matakwa ya wananchi yasikilizwe.

Huko nyuma tuliwaonya UKAWA kuwa lazima wajibu tuhuma za viongozi wa dini wanaotumiwa.
Leo kina Sitta wanatumia viongozi wa dini katika mambo ya kisiasa.

Halafu kwa unafiki wanarudi kusema watu wasichanganye dini na siasa.
BMK ni la kisiasa na hivyo maoni ya viongozi wa dini ni sawa na yale ya wakulima na wavuvi na BMK halichagui Askofu au Sheikh kama Sitta anavyopotosha.

5.Sitta anasema makundi yanayoleta tatizo ni UKAWA na Tanzania kwanza.
Hili la Tanzania kwanza ni la chama chake cha CCM.

Wakati linaundwa Sitta alikuwa kimya leo anawezaje kusema ni tatizo wakati yeye alikuwa mshiriki wa kundi hilo.
Ushiriki wa Sitta ni pale alipotumwa na Tanzania kwanza kuhakikisha JK anahutubia na kumvuruga Warioba.

Samwel alishiriki vema na ni mwanachama wa Tanzania kwanza.
Hana moral authority ya kunyooshea kidole kundi hilo

7. Sitta anasema, makundi halali ni yale ya wajumbe wa Tanzania bara na wajumbe wa Zanzibar
Tazama mzee Sitta anavyojidhalilisha.

Kwanza, hakuna kundi la Tanzania bara. Sheria ya kuunda bunge hilo la katiba haitaji wajumbe wa Tanzania bara.

Hivyo mzee Sitta atambue kuwa sheria haimruhusu kusema achilia mbali kufikiri.
Tuna kundi la Zanzibar dhidi ya JMT. Wabunge wa bunge la JMT ni kutoka Dodoma wakiwemo wa CUF.

Vipi aseme wabunge wa bunge la JMT ni kutoka Tanzania bara.
Huu ni uongo usiopaswa kufanya na mzee wa umri wake tena akiwa mwanasheria.
Hilo lazima aambiwe ili asiendelee kutengeneza mazingira ya machafuko nchini .

Sitta amepewa nafasi ya kuendelea na bunge lake mwenyewe.
Kitu anachopaswa kukumbuka ni kuwa katiba haipatikani bila muafaka.

UKAWA wanawakilisha sehemu ya jamii.
Ni vipi Sitta anaweza kuipuuza sehemu hiyo akijivunia kuwa katiba inayoandaliwa ina mema kwa wananchi.

Samwel Sitta, CCM na wewe mtaandika katiba yenu. Muda si mrefu wananchi wa Tanzania wataandika katiba yao.
Wakati huo utakuwa nje ya system na tutakuwa na uwezo wa kukuita popote ueleze upotevu wa pesa unaoendelea kuufanya na wenzako.

Kenya walijaribu lakini nguvu ya umma ikatamalaki.
Watanzania wa leo si wa mwaka 1973 .

Sitta atafakari kama analitakia mema taifa hili siku zijazo.
Tunajua hawezi kuwa rais wan nchi hii tena, je, kinga aliyonayo JK yeye anayo?

Tusemezane
 
UKAWA NA TUME YA WARIOBA

TULIWAAMBIA MTU WA KUKWAMUA MCHAKATO SI JK

LEO AWAJIBU WAZEE WA TUME, AWANANGA UKAWA KAMA KAWAIDA

UKAWA, MTAJIFUNZA KWA NYENZO GANI MUELEWE?

Katika siku za karibuni kumekuwa na maoni kutoka kwa wajumbe wa iliyokuwa tume ya Warioba pamoja na wale wa UKAWA wakitaka Rais Kikwete aingilie kati na kukwamua mchakato.

Mabdandiko yaliyopita tumeonyesha wazi jinsi Rais alivyowachezea huko nyuma, na jinsi anavyoendelea kuwachezea hasa wapinzani.

Tumesema wazi, mchakato hautakwamuliwa na Kikwete kwasababu dhamira yake juu ya katiba imetekwa nyara na kwa udhaifu alio nao, hakuna namna ya kukabiliana na wahafidhina CCM isipokuwa kuwapigia magoti akiwa Rais wa nchi.

Wahafidhina ndio waliomuweka hapo alipo, wana mengi juu yake na hilo tu linatosha kumfanya awe dhaifu katika uongozi.

Hotuba yake ya kufungua bunge la katiba, JK alisema wazi '' S3 subirini hadi niondoke mwakani''.

Huyu si mtu mwenye dhamira njema. Alitishia na kugusia ushiriki wa majeshi yetu kitu ambacho hakikuwahi kutokea katika marais waliotangulia.

Leo ametoa hotuba ya mwezi, na hakika hakuna kipya zaidi ya kuimarisha dhamira yake na wahafidhina katika kuandika katiba yenye S2.

Kikwete ametumia muda wake na wa taifa kwa sehemu kubwa kuongelea UKAWA na wala si tatizo linalowagawa UKAWA na CCM.

Katika hotuba yake, JK hakugusia kabisa CCM ikiwa ni dalili ya kukubalina nao kama mwenyekiti.
Hotuba yake haikujibu maswali muhimu huku ikijichanganya maneno kila baada ya aya.

Haikuwa hotuba ya Rais katika kuleta ulinganifu kwa taifa, ilikuwa kuwasema na kuwajibu akina Jaji Warioba na wenzake, kuwasema UKAWA n.k.

Katika hadhi ya Rais, alichokifanya kinasikitisha.

Hapa duru tutaichambua hotuba yake katika suala la katiba mstari mmoja hadi mwingine ili tuweze kumwelewa au kutomwelewa rais.

Tutaonyesha mapungufu luluki ya hoja zake na jinsi anavyolipeleka taifa katika njia inayotisha sana

Tutelezea mkakati wa kuandika katiba ya CCM kwa kutumia wajumbe, madhara yake na kwanini JK na CCM watashindwa.

Wana jamvi tutarudi kuendelea kwa undani.

stay tuned
 
nguruvi 3 asante kwa mabandiko mazuri sana yanayoainisha mambo muhimu kuhusu swala zima la mchakato wa katiba.

nimefuatilia kwa umakini leo mjadala kati ya Nape na Mnyika kuhusu UKAWA kurudi kwenye bunge la katiba. Kimsingi kuna jambo ambalo halijakaa swala nalo ni hakuna mwenye dhamira ya kweli ya upatikanaji wa katiba mpya. nasema hayo kwasababu sion kwann pande hizi mbili zigombane kisa katiba kama wana dhamira ya haki kwa taifa hili.

to me ni afadhali katiba iliyopo ikarekebishwa uchaguzi ufanyike kama kwao uchaguzi ni priority. sidhan kama kuna ulazima wa kuwah kutemngeneza katiba ili kufit kwenye coming election manake nia yetu sio ya kupata bora katiba bali tunataka katiba bora.

so far naona kama intetion za UKAWA zimebadilika and now wana concetrate kwenye jins ya wao kuingia kwenye uchaguzi wakasahau kwamba hiyo haikuwa primary mission yao
 
Last edited by a moderator:
nguruvi 3 asante kwa mabandiko mazuri sana yanayoainisha mambo muhimu kuhusu swala zima la mchakato wa katiba.

nimefuatilia kwa umakini leo mjadala kati ya Nape na Mnyika kuhusu UKAWA kurudi kwenye bunge la katiba. Kimsingi kuna jambo ambalo halijakaa swala nalo ni hakuna mwenye dhamira ya kweli ya upatikanaji wa katiba mpya. nasema hayo kwasababu sion kwann pande hizi mbili zigombane kisa katiba kama wana dhamira ya haki kwa taifa hili.

to me ni afadhali katiba iliyopo ikarekebishwa uchaguzi ufanyike kama kwao uchaguzi ni priority. sidhan kama kuna ulazima wa kuwah kutemngeneza katiba ili kufit kwenye coming election manake nia yetu sio ya kupata bora katiba bali tunataka katiba bora.

so far naona kama intetion za UKAWA zimebadilika and now wana concetrate kwenye jins ya wao kuingia kwenye uchaguzi wakasahau kwamba hiyo haikuwa primary mission yao
gfsonwin , dhamira ya kweli haipo kwa CCM.
Ujio wa S3 unawatisha hasa kundi la wahafidhina. Rais Kikwete amesema, S3 ni hadi aondoke madarakani. Hapo kuna dhamira ya kweli?

Leo umemsikia, sehemu kubwa ilikuwa kukandia UKAWA. Tunauliza, hivi hakuona tatizo kwa CCM hata moja.
Bila hata ya kufikiri, ni rais huyu huyu aliruhusu Lukuvi kwenda kuhubiri kwa njia za hatari sana Kanisani.

Ni JK huyu huyu, ameshindwa kuwakemea CCM kwa kupotosha umma. Leo anapata wapi nia ya katiba?

Nadhani UKAWA wameamua kwenda katika uchaguzi mkuu. Nikisoma lengo lao ni kuhakikisha wanapunguza idadi ya wabunge wa CCM kwanza, halafu wanaingiza agenda ya katiba. Kwasasa hilo linaweza kufanikiwa kwasababu hoja ya katiba ni ya wananchi na wanakereka sana. Hivyo, down the road itakuja kuwaumiza tu CCM.

Hata hivyo, lazima UKAWA wawe makini. Wasirudie makosa ya nyuma. Wakati bunge linaendelea wao waendelee kufanya ufafanuzi kwa wananchi kila siku. Itafika mahali wananchi watadharau kama walivyodharau siku 10 za mwisho na huo ndio utakuwa mwisho wa katiba ya CCM.

Nitafafanua zaidi katika mabandiko yajayo.
 
Last edited by a moderator:
Wana duru,
Ifuatayo ni hotuba ya Rais ya mwisho wa mwezi. Tumechukua sehemu ya mchakato wa katiba na kupitia kifungu kimoja hadi kingine ili kuiangalia vema. Tumeiwekea herufi nyekundu ili wakati wa mjadiliano tuweze kufanya reference bila kunukuu sehemu husika. Hii itafanya mabandiko yawe mafupi, yanayoeleweka na yasiyo changanya.

Tutakuwa na mtiririko wa kuchambua vifungu hivyo vyenye alama nyekundu yapato 4. Na mtiririko utakuja kwa bandiko moja moja.

Hii ndiyo hotuba ya Rais


Mchakato wa Katiba Mpya

Ndugu Wananchi;
Kama tujuavyo, Bunge Maalum la Katiba lililoahirishwa tarehe 25 Aprili, 2014 kupisha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi kushughulikia bajeti za Serikali husika, litakutana tena tarehe 5 Agosti, 2014 kuendelea na kazi yake ya kutunga Katiba Mpya.

Kwa vile Bunge Maalumu la Katiba halikuweza kumaliza kazi yake ndani ya siku 70 zilizotengwa kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, nimeliongezea Bunge hilo siku 60 kwa ajili ya kukamilisha kazi yake. Nimefanya hivyo kwa mujibu wa mamlaka niliyopewa na Sheria hiyo hiyo.

Hatua Iliyofikiwa Kabla ya Kuahirishwa kwa Bunge

Ndugu Wananchi;
Itakumbukwa pia kuwa, tarehe 16 Aprili, 2014, baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba hasa kutoka vyama vya CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi walisusia mjadala uliokuwa unaendelea Bungeni na kutoka nje.

Wakati wanatoka Bungeni, kazi kubwa ilikuwa imefanyika.
Tayari Kamati zote 12 za Bunge hilo zilikuwa zimekamilisha kujadili Sura ya Kwanza na ya Sita za Rasimu ya Tume. Sura hizo zinazungumzia utambulisho wa nchi na muundo wa muungano.
Kamati zote zilipiga kura ya kupitisha uamuzi wao kuhusu sura hizo mbili.

(A)Kamati kadhaa ziliweza kupata theluthi mbili ya kura kwa Wajumbe wa pande zote mbili za Muungano, jambo lililoonyesha dalili njema kwamba Katiba mpya inaweza kupatikana.

Baada ya hapo, taarifa ya kila Kamati iliwasilishwa kwenye Bunge zima.
Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge Maalumu la Katiba, maoni ya wachache nayo yaliwasilishwa.
Kazi iliyokuwa inafuatia, kwa mujibu wa Kanuni za Bunge ni kwa Kamati ya Uandishi kukamilisha taarifa yake na kuiwasilisha kwenye Bunge zima kwa ajili ya kujadiliwa.

(B)Baada ya Wajumbe kujadili taarifa hiyo itafuatia kupiga kura ili kuamua kuhusu Sura hizo mbili.
Kama yalivyo masharti ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, uamuzi utafanywa kwa theluthi mbili ya kura za kila upande wa Muungano wetu.

Sababu za Baadhi ya Wajumbe Kususia Bunge Maalumu la Katiba

Ndugu Wananchi;
Sote tumewasikia Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba waliosusia vikao vya Bunge hilo wakielezea sababu zilizowafanya watoke Bungeni. Walitoa matamko kwenye vyombo vya habari na pia katika mikutano ya hadhara waliyoiitisha na kuhutubia sehemu mbalimbali nchini.

(C)Sababu walizotoa zimekuwa zikiongezeka na kubadilika kadri siku zinavyosonga mbele na upepo wa kisiasa unavyokwenda.

Hivi sasa wanazungumzia mambo mawili.
(D)Kwanza, kwamba Bunge Maalumu halina mamlaka ya kuifanyia mabadiliko yo yote Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Kwa maoni yao, kazi ya Bunge Maalumu la Katiba ni kujadili na kupitisha tu Rasimu ya Katiba ya Tume na siyo kubadili cho chote.

Pili, wametoa sharti la wao kurudi Bungeni ni kuhakikishiwa kwamba, kitakachojadiliwa Bungeni ni Rasimu ya Tume. Bila ya sharti hilo kukubaliwa, wamesisitiza kutorudi Bungeni.

Mamlaka ya Bunge Maalum la Katiba

Ndugu Wananchi;
Mimi nimehusika katika kubuni wazo la kuwa na mchakato wa kuandika Katiba Mpya, na katika maandalizi ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, ya kuongoza na kuendesha mchakato huo.

(E)Kwa kweli sikumbuki wakati wo wote katika vikao vya Baraza la Mawaziri kujadili Rasimu ya Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba tulipozungumzia Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuwa haiwezi kufanyiwa marekebisho na Bunge Maalumu la Katiba.

Mimi siyo Mwanasheria na hivyo nakiri kwamba naweza kuwa na upungufu katika kuelewa maana ya baadhi ya maneno ya kisheria. Hata hivyo, sikumbuki kuwepo kwa kifungu cho chote katika Sheria kinachosema kuwa Bunge Maalumu la Katiba halina mamlaka hayo.

Tangu tulipoyasikia maneno hayo yakisemwa nimeuliza nithibitishiwe ukweli wa madai hayo bado sijaambiwa vinginevyo. Kama ukweli huo upo naomba anisaidie.

Badala yake naambiwa kuwa maneno yaliyotumika katika Sheria haiakisi dhana inayotolewa kuwa kazi ya Bunge Maalum la Katiba ni kubariki Rasimu na siyo kufanya vinginevyo.

(F)Nimeambiwa kuwa sheria inasemaTume itaanda Rasimu ya Katiba na Bunge Maalum la Katiba litatunga Katiba iliyopendekezwa.

Ndugu Wananchi;
Tarehe 30 Desemba, 2010, nilipozungumzia dhamira yangu ya kuanzisha mchakato wa kuandika Katiba Mpya nilieleza wazi nia ya kuwepo kwa uwakilishi mpana wa Watanzania katika mchakato huo.
Ndiyo maana katika Sheria tukaweka ngazi nnekatika mchakato wa kutunga Katiba.

(G)Ngazi ya kwanza ikiwa ya wananchi kutoa maoni yao juu ya kila wanachotaka kijumuishwe katika Katiba ya nchi yao.

(H)Ngazi ya pili, ni ya wananchi kupitia wawakilishi wao katika Mabaraza ya Katiba ya Wilaya na Mabaraza ya Kitaasisi kutoa maoni yao kuhusu Rasimu ya kwanza ya Katiba iliyotayarishwa na Tume.

(I)Ngazi ya tatu inajumuisha wawakilishi wa wananchi waliopo kwenye Mabaraza ya Kutunga Sheria ya Sehemu zetu mbili za Muungano, yaani Bunge la Jamhuri ya Muungano na Baraza la Wawakilishi, wakichanganyika na Wawakilishi wa makundi mbalimbali ya jamii ya Watanzania kutoka pande zote mbili za Muungano.
Hawa ndio wanaounda Bunge Maalumu la Katiba, lenye jukumu la kutunga Katiba inayopendekezwa.


(J)Mamlaka ya kutunga Katiba kwa mila na desturi za Mabaraza ya Kutunga Sheria ni uwezo wa kurekebisha, kubadili, kufuta na hata kuongeza kilichopendekezwa.

(K)Ingekuwa kilichokusudiwa ni kubariki tu lisingetumiwa neno la kutunga Katiba.
Hali kadhalika, lisingewepo sharti la kupiga kura na msisitizo wa kupata theluthi mbili kwa kila upande wa Muungano.

(L)Aidha, kama ingekuwa jukumu la Bunge Maalumu ni kubariki tu Rasimu lisingepewa siku 70 za kazi na Rais kupewa mamlaka ya kuongeza siku zaidi kadri aonavyo yeye inafaa.

Ngazi ya nne na ya mwisho, tuliweka kura ya maoni ya wananchi kukubali au kukataa Katiba inayopendekezwa na Bunge Maalumu la Katiba.

(M)Kama ingekuwa Rasimu ya Tume haiwezi kubadilishwa hata nukta kwa nini basi tuweke kura ya maoni ya kuwahusisha wananchi wote?

Ndugu Wananchi;
Tulizibuni ngazi hizi nne kwa dhana kwamba kile ambacho hakikuonekana au hakikuwekwa sawa katika ngazi moja kitaonekana na kurekebishwa katika ngazi inayofuata katika ngazi zile tatu za mwanzo. Na, iwapo Katiba iliyotungwa haitawaridhisha wananchi wanayo haki ya kuikataa. Kwa kufanya hivyo, wananchi ndiyo waliopewa turufu ya mwisho.

Ndugu wananchi;
(N)Kwa kweli, napata shida kuelewa mkanganyiko unatoka wapi na hasa wale wanaoongoza kuhoji mamlaka ya Bunge Maalumu kuwa ni wale wale waliotunga Sheria ya Mabadiliko ya Katiba tena hatua kwa hatua.

Nashangazwa zaidi ninapoona wale wale waliotunga Kanuni za Bunge Maalumu ndiyo wanaoongoza kuhoji uhalali wa kile walichokitunga.

(P)Kanuni za Bunge Maalumu la Katiba, Ibara ya 33 (8) inasema: Nanukuu: "Wakati wa mjadala, Mjumbe yoyote anaweza kutoa mapendekezo ya marekebisho, maboresho au mabadiliko yaliyomo katika Sura za Rasimu ya Katiba zinazojadiliwa kwa utaratibu ufuatao: (a) Ikiwa ni marekebisho, maboresho au mabadiliko yanayobadilisha jambo la msingi, au yanayobadilisha maudhui ya Ibara, mapendekezo ya marekebisho yatapelekwa kwa maandishi kwa Katibu siku moja kabla ya mjadala wa Ibara husika. (b) Ikiwa ni marekebisho madogo, ambayo hayabadili msingi au maana, mapendekezo ya marekebisho yatawasilishwa na mjumbe wakati wa mjadala baada ya kupata ruhusa ya Mwenyekiti". Mwisho wa kunukuu.

(Q)Kanuni hii ilipotungwa, Wajumbe wote wa Bunge Maalumu pamoja na wale ambao baadae walisusia vikao vya Bunge walikuwepo Bungeni na walishiriki kuipitisha.

Tena basi, baadhi yao walikuwa Wajumbe wa Kamati ya Kanuni iliyopendekeza Kanuni hizo. Unapowaona watu wale wale sasa wanakuwa vinara wa kuhoji mamlaka ya Bunge Maalumu la Katiba, unajiuliza maswali mengi kuhusu watu hao bila ya kupata majibu yaliyo sahihi na kutosheleza akili na ufahamu wetu.

Ndugu Wananchi,
Unaposoma Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na Kanuni za Bunge Maalumu, hii ni dhahiri kwamba wote walikuwa na uelewa wa pamoja kuhusu mamlaka ya Bunge Maalumu ya kujadili Rasimu iliyoandaliwa na Tume na kutunga Katiba inayopendekezwa kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura.

Kinachojadiliwa Bungeni ni Rasimu ya Tume

Ndugu Wananchi;
Yapo madai yanayotolewa na kuenezwa na Wajumbe waliosusia Bunge Maalumu la Katiba kwamba kinachojadiliwa Bungeni siyo Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ndiyo maana basi wanaweka sharti la kujadiliwa Rasimu ya Tume ya Jaji Warioba ndipo warudi Bungeni.

Madai haya nayo yananipa taabu kuyaelewa. Ndugu zetu hawa walishiriki siku zote 19 za Kamati 12 zilipokutana kujadili Sura yaKwanza na ya Sita za Rasimu ya Tume. Halikadhalika. walikuwepo na kushiriki kwa ukamilifu wakati taarifa za Kamati, tangu ya Kwanza mpaka ya 12,zilipowasilishwa kwenye Bunge zima. Aidha, na wao walishiriki kutoa maoni ya wachache kwa dakika 20 na kutoa ufafanuzi kwa muda wa dakika 30 kwa kila Kamati.

(R)Haya maneno ya sasa kwamba kinachojadiliwa Bungeni siyo Rasimu ya Tume ya Jaji Warioba bali nyingine kabisa ambayo wanadai eti ni ya CCM yanatoka wapi.

Mimi nadhani kuwa huenda katika Kamati kumefanyika marekebisho kwenye Rasimu ambayo hayakuwapendeza. Kama hivyo ndivyo, wawe wakweli kuhusu jambo hilo kuliko kusema mambo yasiyowakilisha ukweli halisi wa Rasimu inayojadiliwa.

(S)Matokeo yake ni kuwafanya wafuasi wao na wapenzi wao na hata watu wengine waamini kuwa kinachojadiliwa siyo Rasimu ya Tume ya Jaji Warioba bali nyingine tena ni ya CCM.
Jambo hilo si kweli na wenyewe wanajua kwamba si kweli ila sijui kwa nini wameamua kupotosha ukweli.

Ndugu Wananchi;
(T)Kinachonishangaza, zaidi ni kwamba, kama hawakuridhishwa na yaliyofanyika, kwa nini wasingetumia mifumo waliyojitengenezea wenyewe kwenye Kanuni kumaliza tofauti zao?

(U)Kanuni zinaelekeza kuwa mambo wasiyoridhika nayo yajadiliwe kwenye Kamati ya Mashauriano na Maridhiano. Ukiacha mifumo ya maridhiano ndani ya Bunge ukaenda nje kwa wananchi au vyombo vya habari na mitandao si jawabu la tatizo.

Ndugu Wananchi;
(V)Ndiyo maana nashawishika kuunga mkono wale wote wanaowasihi Wajumbe wa CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi na wengine warejee Bungeni. Watumie mifumo maalum ya Bunge iliyowekwa na Kanuni kutafuta maridhiano.

(W)Hali kadhalika, wasichoke kuwa na mawasiliano na vyama vingine vya siasa na hasa CCM kutafuta maelewano.
Mimi niko tayari kusaidia pale watakapoona inafaa kufanya hivyo kama ambavyo nimekuwa nikifanya ziku za nyuma.

(X)Nililolisema mwanzoni kabisa mwa mchakato na nalirudia tena leo kwamba, ili tuweze kufanikiwa kupata Katiba Mpya ambayo sote tunaitaka, maelewano baina ya wadau wakuu wa kisiasa ni jambo lisilokuwa na badala yake. Vinginevyo kupata theluthi mbili kwa pande zote mbili za Muungano haitawezekana.

Ndiyo maana nampongeza sana Msajili wa Vyama vya Siasa, Mheshimiwa Jaji Francis Mutungi, kwa uamuzi wa kuvikutanisha vyama vinne vikuu vya siasa kujadili namna ya kuondoa mtihani uliopo sasa katika mchakato wa Katiba.

(Y)Ombi langu kwa viongozi wa vyama hivyo ni kuitumia vyema fursa ya majadiliano kuukwamua mchakato kwa maslahi ya nchi yetu na watu wake.

(Z)Hali kadhalika nampongeza sana Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Mheshimiwa Samwel Sitta, kwa kuitisha kikao cha Kamati ya Mashauriano na Maridhiano. Bahati mbaya ni kwamba Wajumbe wa vyama vilivyosusia Bunge Maalumu hawakushiriki. Ni matumaini yangu kuwa Mheshimiwa Sitta hatokata tamaa kuendeleza juhudi za mashauriano na kwamba katika vikao vijavyo na wenzetu hawa watashiriki.


Ndugu Wananchi;
Hivi karibuni kumekuwepo pia madai yanayoelekeza lawama kwangu. Kwanza nalaumiwa eti kuwa mambo yalikuwa yanaenda vizuri mpaka pale nilipotoa hotuba ya ufunguzi wa Bunge Maalumu ndipo yalipoharibika.

Pili nalaumiwa kwamba nawezaje kuikana Rasimu ya Katiba ambayo na mimi ni mmoja wa watu waliotia sahihi katika Rasimu hiyo.

(AA)Niruhusuni nianze na hili la pili. Nadhani ndugu zetu wanaotoa madai haya yameitafsiri isivyo sahihi yangu katika Gazeti la Serikali lililotangaza rasmi Rasimu ya Katiba na Taarifa ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba baada ya Tume kumaliza kazi yake ya kuandika Rasimu ya Katiba, Rais wa Jamhuri ya Muungano amepewa kazi tatu kufanya. Kwanza, kupokea Rasimu hiyo na Taarifa ya Tume kutoka kwa Mwenyekiti jambo ambalo lilifanywa tarehe 30 Desemba, 2013. Pili, amepewa kazi ya kuitangaza rasmi Rasimu ya Katiba na Taarifa ya Tume kwa watu wote kuiona na kuisoma ndani ya siku 30. Alipewa sharti la kuitangaza katika Gazeti la Serikali na vyombo vingine vya habari. Hili nalo lilifanywa hivyo tarehe 22 Januari, 2014.

Ndugu Wananchi;
Katika kutangaza katika Gazeti la Serikali sharti linamtaka anayetangaza ajitambulishe kuwa yeye ni nani na atie sahihi yake. Kwa kufanya hivyo, hakumfanyi yeye kuwa naye ni mhusika na maudhui ya kila kinachopendekezwa na Tume. Sahihi zilizomo ndani ya Rasimu na Taarifa ya Tume ni za Wajumbe wa Tume, kamwe sahihi ya Rais haimo hivyo hawezi kulaumiwa kuwa anaikana sahihi yake. Yeye ametimiza wajibu wake wa kutangaza, akaiweka hadharini kwa umma wa Watanzania kuiona na kusoma Rasimu ya Katiba na Taarifa ya Tume vilivyotayarishwa na kutiwa sahihi na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Kazi ya tatu ni kuitisha Bunge Maalumu ambayo nayo imekamilika tangu tarehe 18 Februari, 2014.

Ndugu Wananchi,
Jambo lingine linalofanana na hilo ni yale madai kwamba nilikuwa napata taarifa ya maendeleo ya mchakato ndani ya Tume mara kwa mara, iweje leo nitoe maoni tofauti kama niliyoyatoa katika hotuba yangu kwenye Bunge Maalumu.

Ni kweli kabisa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Mheshimiwa Jaji Joseph Warioba, Makamu wake, Mheshimiwa Jaji Agustino Ramadhani na Mheshimiwa Dkt. Salim Ahmed Salim wamekutana na mimi kwa nyakati mbalimbali kuzungumzia mwenendo wa mchakato.

(AB)Lakini, hayakuwa mazungumzo ya kina kuhusu nini kiwe vipi katika maudhui na mapendekezo ya Tume.

Ukweli ni kwamba Rasimu zote mbili nilizipata mara ya kwanza nilipokabidhiwa rasmi, tena kwa uwazi.
Napenda watu wasijenge dhana kuwa nilipewa Rasimu na kuisoma kabla ya kukamilika na hivyo nilitoa maoni yangu. Tume hii ilikuwa huru na niliiacha iwe hivyo.

(AC)Sikuiingilia kwa namna yo yote ile kupenyeza mambo ninayotaka yawemo.

(AD)Kuthibitisha dhamira yangu ya kutaka Tume iwe huru katika kufanya kazi zao hata pale waliponitaka nitoe maoni niliwaomba tusifanye hivyo ili nisiwakwaze katika kufanya kazi zao, wakapata taabu ya kuwianisha wanayofikiria na mawazo yangu.

Ndugu Wananchi;
(AE)Kuhusu madai kwamba mambo yalikuwa yanakwenda vizuri na kwamba hotuba yangu iliyavuruga, napenda kusema wazi kuwa lawama hizo hazina ukweli wo wote. Ni madai yasiyokuwa na msingi. Kwani mimi hasa siku ile nilifanya lipi la ajabu.

(AF)Ukweli ni kwamba nilisema yale yale ambayo Tume yenyewe imeyasema katika Rasimu ya Katiba na Taarifa za Tume.

Niliyoyasema kuhusu malalamiko ya watu wa pande zetu za Muungano na uzuri na changamoto za miundo ya Serikali mbili na Serikali tatu ni yale yale yaliyomo kwenye taarifa za Tume.

(AG)Nimetumia takwimu zile zile za Tume. Pengine kilichoonekana kuwa kibaya ni jinsi nilivyozifasiri taarifa hizo na mapendekezo ya Tume.

Jambo lingine ambalo nimelifanya ni kutoa maoni yangu kuhusu baadhi ya vipengele vya Rasimu hususan uandishi na dhana mbalimbali zilizokuwamo. Silioni kosa langu kwa kufanya hivyo, kwani Rasimu imetolewa hadharani kwa watu kuijadili.

(AH)Na mimi kama raia ninayo haki ya kufanya hivyo kama wafanyavyo wengine. Kwa nini nilaumiwe kwa kutumia haki yangu hiyo.

(AI) Lakini, pia mimi ndiye Rais wa nchi yetu, ninayo dhamana ya uongozi na ulezi wa taifa letu.
Itakuwaje kwa jambo kubwa la hatma ya nchi yetu nilinyamazie kimya.
Watanzania wangeshangaa na wangekuwa na haki ya kuhoji Rais wao ana maoni gani.

(AJ)Bahati nzuri nilitoa maoni yangu mahali penyewe hasa, na kwa uwazi, kwenye Bunge Maalumu la Katiba.

(AK)Hata hivyo, ni muhimu kusisitiza kuwa namna nilvyotoa maoni yangu sikuwa natoa maagizo wala kushurutisha, ndiyo maana kila wakati niliwakumbusha Wajumbe kuwa mamlaka ya uamuzi ni yao.

Yangu yalikuwa maoni tu wanahiyari ya kuyakubali au kuyakataa.
Niliwataka Wajumbe wasome na kuielewa vyema Rasimu. Nilisema wasome sura kwa sura, mstari kwa mstari na neno kwa neno. Niliwaomba wajiridhishe kuhusu uandishi na dhana mbalimbali. Nilitoa mifano ya mambo yahusuyo uandishi ambayo ni vyema wayatazame. Pia nilitoa mifano ya dhana ambazo niliwasihi wajiridhishe juu ya kufaa kwake kuwepo.

(AL)Kuhusu muundo wa Serikali tatu, nilieleza wazi kuwa sina tatizo nao kama ndiyo matakwa ya Watanzania.

Lakini, nilieleza hofu yangu kuhusu mapendekezo ya Tume na kuwataka Wajumbe wafanye kazi ya ziada kuondosha udhaifu iwapo wataukubali muundo unaopendekezwa.

Nilieleza nia yangu ya kutaka tuwe na Serikali ya Muungano yenye ukuu unaoonekana, yenye nguvu ya kuweza kusimama yenyewe, inayoweza kuwa tegemeo kwa nchi Washirika, Serikali isiyokuwa tegemezi wala egemezi kwa nchi washirika na ambayo inavyo vyanzo vya uhakika vya mapato. Hivi kwa kutoa ushauri huo kwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba inageuka kuwa nongwa. Kwa kweli sielewi lawama ni ya nini?.

Naamini sistahili lawama bali pongezi kwa kuwa muwazi na kutoa ushauri wa msingi ambao utasaidia nchi kupata Katiba nzuri inayojali maslahi ya watu wa nchi yetu na ya nchi zetu mbili zilizoungana miaka 50 iliyopita.

Hitimisho

Ndugu Wananchi;
Mwisho, ni maoni yangu ya dhati kuwa mgogoro uliopo sasa katika mchakato wa Katiba hauna sababu ya kuendelea kuwepo.

(AM)Naamini hayo yote ambayo Wajumbe wa CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi wanayalalamikia yanaweza kushughulikiwa kwa ukamilifu katika mifumo ya Bunge Maalumu la Katiba iliyotengenezwa na Wajumbe wote na wao wakiwemo. Nawasihi waitumie.

Hali kadhalika, kwa kupitia mazungumzo wanayofanya na wenzao wa Chama cha Mapinduzi wanaweza kutengeneza nguvu ya pamoja kutatua changamoto za sasa na zitakazojitokeza baadaye.

(AN)Kilicho muhimu ni kwa pande zote kuwa na dhamira ya dhati ya kutoka hapa tulipo sasa.
Kama utashi wa kisiasa upo kwa kila mmoja wetu, hilo ni jambo linalowezekana kabisa.

(AP)Narudia kuahidi utayari wangu wa kusaidia kadri inavyowezekana tusonge mbele.

Mungu Ibariki Afrika!
Mungu Ibariki Tanzania!

Asanteni sana kwa kunisikiliza
..............................
 
[SUP]MTAZAMO KUHUSU HOTUBA YA RAIS KAMA ILIVYO KATIKA BANDIKO HAPO JUU[/SUP]

[SUP]Bandiko la 1
[/SUP]

[SUP]Tutaangalia vifungu bila kufuata utaratibu wa herufi ili kuleta mtiririko unaoeleweka vema[/SUP]
[SUP]
(Kifungu AP) [/SUP]
[SUP]Rais: anasema anarudia msimamo wake kusaidia kadri inavyowezeka.[/SUP]
[SUP]Hoja zetu ; Mwezi wa 5 Rais akihutubia wafanyakazi alisema, UKAWA wapo likizo watarudi.
Huo ndio ulikuwa muda wa kuanza kutafuta suluhu.
Leo ni miezi 3 imepita, bunge linaanza tarehe 5. Rais anatarajia nini[/SUP]
[SUP]Nini kipya alichoshindwa kuiona miezi 3 iliyopita anaweza kukiona sasa.

Na wala si suala la kuombwa,wananchi walitegemea aje na majibu ya tatizo katika hotuba na si kuendelea kuwananga akina Warioba na UKAWA.[/SUP][SUP]Je, kuna chochote kinachoweza kuwaleta UKAWA na CCM pamoja katika hotuba yake zaidi ya kujiosha na lawama?[/SUP]

[SUP](Kifungu AN)[/SUP]
[SUP]Rais: kama ipo dhamira ya kisiasa tunaweza kutoka hapa tulipo, ni jambo linalowezekana kabisa[/SUP]
[SUP]Hoja: Dhamira ilipaswa kuonyeshwa na mh Rais, kwanza, kwa kuwazuia CCM wasiendelee na upotoshaji.
Pili, yeye mwenyewe kufuta kauli yake ndani ya BMK 'S3 zisubiri mwakani nikiondoka''[/SUP]
[SUP]
Rais hakuwa na dhamira, wapi anaweza kushawishi wengine kwa dhamira asiyokuwa nayo kwa kuanzia?[/SUP]

[SUP](Kifungu AL)[/SUP]
[SUP]Rais; Kuhusu mfumo wa S3 sina tatizo nao kama ndio wananchi wameutaka[/SUP]
[SUP]Hoja: Rais ana tatizo na muundo wa S3. Kwanza, mbele ya BMK alisema, S3 zisubiri aondoke.

Pili, muundo wa S3 ndio umpendekezwa na wananchi tena akithibithibitisha kwa maneno yake mwenyewe. Soma vifungu viufatavyo (G, H, I) alipoeleza matabaka ''layers' ya wananchi walivyoshiriki katika mchakato.

Matakwa hayo ndiyo yaliyopo katika rasimu ya katiba ya Warioba.
Rais anaposema kama wananchi wanataka anakosea, kwasababu tayari wananchi wametaka kupitia tume yake. Wananchi wanotaka ni wapi tena?[/SUP]

[SUP](Kifungu AE)[/SUP]
[SUP]Rais: Tuhuma kuwa mambo yalikuwa mazuri hadi hotuba yangu si kweli. Nilifanya lipi la ajabu[/SUP]
[SUP]Hoja: Katika historia ya nchi yetu hatujawahi kusikia Rais akilishirikisha jeshi katika siasa na masilahi.
Hili ni la ajabu kabisa.[/SUP]
[SUP]
(Kifungu AF)[/SUP]
[SUP]Rais: Nilisema yale yote yalitokuwemo katika rasimu na tume iliyosema[/SUP]
[SUP]Hoja: Hakuna mahali tume ilizungumzia mishahara ya wanajeshi wala changamoto zinatozotokana na jeshi/muungano
[/SUP]
[SUP](Kifungu AG)[/SUP]
[SUP]Rais: nimetumia takwimu zilizotumiwa na tume,pengine tafsiri ni tofauti[/SUP]
[SUP]Hoja: Ulipata wapi mamlaka ya kutafsiri takwimu kwa kuonyesha mshangao'' wengine wanahoji uhalali wa takwimu''
[/SUP]
[SUP](Kifungu AF)[/SUP]
[SUP]Rais: Na mimi kama raia nina haki ya kutoa maoni yangu kama wengine, kwanini nilaumiwe kutumia haki yangu?[/SUP]
[SUP]Hoja: Haki hiyo ulipewa kama ulivyosema katika kifungu(Kifungu AD) kwamba, hata tume ilipokuomba utoe maoni hukukubali kufanya hivyo.
[/SUP]
[SUP]Pamoja na nafasi hiyo,Rais amesema 'sikuingilia kwa namna yoyote kupenya mambo ninayotaka'[/SUP]
[SUP]Mh Rais, uliposhindwa kutoa maoni yako kwa tume kama Raia wengine, ulijinyima haki hiyo mwenyewe.

Hukuwa na haki ya kutoa maoni katika bunge la katiba kwasababu tayari ulishasaini maoni ya raia ambayo ulipaswa ujumuishe na yako.

Kutumia bunge la katiba ilikuwa kuingilia mchakato na si kutoa maoni yako sehemu husika kama ulivyosema (Kifungu AF).[/SUP][SUP]Wakati Rais aliogopa kuingilia maoni ya tume, aliona ni vema aingilie baada ya kupata mwelekeo wa rasimu.[/SUP]

[SUP]Inaendelea bandiko la pili.[/SUP]
 
gfsonwin , dhamira ya kweli haipo kwa CCM.
Ujio wa S3 unawatisha hasa kundi la wahafidhina. Rais Kikwete amesema, S3 ni hadi aondoke madarakani. Hapo kuna dhamira ya kweli?

Leo umemsikia, sehemu kubwa ilikuwa kukandia UKAWA. Tunauliza, hivi hakuona tatizo kwa CCM hata moja.
Bila hata ya kufikiri, ni rais huyu huyu aliruhusu Lukuvi kwenda kuhubiri kwa njia za hatari sana Kanisani.

Ni JK huyu huyu, ameshindwa kuwakemea CCM kwa kupotosha umma. Leo anapata wapi nia ya katiba?

Nadhani UKAWA wameamua kwenda katika uchaguzi mkuu. Nikisoma lengo lao ni kuhakikisha wanapunguza idadi ya wabunge wa CCM kwanza, halafu wanaingiza agenda ya katiba. Kwasasa hilo linaweza kufanikiwa kwasababu hoja ya katiba ni ya wananchi na wanakereka sana. Hivyo, down the road itakuja kuwaumiza tu CCM.

Hata hivyo, lazima UKAWA wawe makini. Wasirudie makosa ya nyuma. Wakati bunge linaendelea wao waendelee kufanya ufafanuzi kwa wananchi kila siku. Itafika mahali wananchi watadharau kama walivyodharau siku 10 za mwisho na huo ndio utakuwa mwisho wa katiba ya CCM.

Nitafafanua zaidi katika mabandiko yajayo.
Nguruvi3 je unafkiri kwamba UKAWA inaweza kuwa imara kiasi cha kuweza kupenya kupitia uchaguzi??
mimi naona ukweli bado hata UKAWA WENYEWE hawajajijua and thus CCM wanawachezea shere tu manake wanajua pa kuwashika.

nikisoma bandiko lako hapo juu #217 mie nifuraah sana manake sasa UKAWA wameshajua rais kama rais anataka nini na hivyo wao wanapaswa kujipanga kutokana na maneno haya.

ngoja nikwambaie mie naona mapungufu from siku rais alipokuwa anahutubia bunge hili manake pale alionyesha msimamo wake juu ya S3 kimsingi lile lilikuwa ni kosa manake hata kama alikuwa na nia yake ya kuwa na S2 alitakiwa aiconfine af kisa atafute watu wake ndani ya bunge awatumie kuhakikisha lile linapita. Kwa mtu kama rais kuonyesha wazi kwamba anataka nini kwangu mimi yale yalikuwa mapungufu and on top of that UKAWA haiwez kuvuka hapo manake utavukaje wakati rais kesha sema??

nafkiri kwanza hakuna hata haja ya kuendelea na hili bunge, bali watumie sheria kurudisha vifungu korofi kwa wananchi ili wananchi waamue. UKAWA wakumbuke kwamba ni umoja ambao hauna mamlaka makubwa kiasi hiko kisheria na hivyo any movement lazima isukumwe na wananch.
 
Last edited by a moderator:
[SUP]MTAZAMO KUHUSU HOTUBA YA RAIS KAMA ILIVYO KATIKA BANDIKO HAPO JUU[/SUP]

[SUP]Bandiko la 2
[/SUP]

[SUP](Kifungu A)[/SUP]
[SUP]Rais: Kamati kadhaa zimeweza kupata theluthi mbili ya kura[/SUP]
[SUP]Hoja: Kama Rais hajui kamati ngapi, wapi anaweza kuhoji takwimu za tume ya Rasimu ya Warioba?[/SUP]
[SUP]Anachokifanya ni kuogopa ukweli kuwa hiyo 2/3 haikuweza kufikia 2/3 ya kamati zote.
Ndicho chanzo cha kutumia neno ‘kadhaa''[/SUP]
[SUP]Rais hapaswi kutumia hisia ikiwa ana vyombo vinavyoweza kumpa takwimu ndani ya BMLK.[/SUP]

[SUP](Kifungu C)[/SUP]
[SUP]Rais: Sababu walizotoa zimekuwa zikibadilika kulingana na upepo wa kisiasa[/SUP]
[SUP]Hoja: Mh Rais, sababu za kwanza za CCM zilikuwa kudhoofika kwa muungano. Hawakuweza kutetea[/SUP]
[SUP]Sababu ya pili, ikawa gharama kubwa za S3. Tukauliza tuonyeshwe unafuu wa S2. Hoja hiyo ikafa
[/SUP]
[SUP]Sababu ya tatu ya CCM ni kuhusu serikali ya shirikisho kukosa mapato ya uhakika. Tukauliza mampato ya uhakika ya sasa yanatoka wapi. Hakuna jibu.
[/SUP]
[SUP]Sababu ya nne ya CCM ilikuwa kuwaenzi waanzilishi wa muungano. Tukauliza, kuua azimio la Arusha nako ni kuwaenzi. Ikafa[/SUP]
[SUP]Sababu ya tano, CCM wanasema tatizo si katiba ni umasikini. Tukauliza miaka 50 na S2 umasikini umeoungua kiasi gani. Hoja ikafa
[/SUP]
[SUP]Sababu ya sita, CCM wakasema changamoto zinashughulikiwa. Tukauliza, kwanini miaka 50 hazijafik kikomo. Hoja ikafa[/SUP]
[SUP]Sababu ya saba, S3 ina lenga kutoa nafasi za uongozi tu kwa waliaoandika katiba. Tukauliza nani aliwateua. Hoja ikafa
[/SUP]
[SUP]Sababu ya nane, S2 tumedumu nazo kwa amani na utulivu kwa miaka 50. Tukauliza, zilianza kama mvua au zialiundwa. Na lini S3 iliwahi leta vurugu. Hoja ikafa
[/SUP]
[SUP]Sababu ya tisa, Wananchi wa pande mbili wameoleana. Tukauliza, mbona kuna kuoleana kati ya Tanzania na nchi nyingine tusizo na muungano nazo. Hoja ikafa
[/SUP]
[SUP]Sababu ya kumi, Majirani zetu wanatuonea kijicho na kuna nchi za nje zinataka tusambaratike. Tukauliza, kama ni hivyo kwanini kuna hoja ya kero za muungano? Nani ameleta[/SUP]

[SUP]Kubwa zaidi ni pale Rais alipowaambia CCM, wajiandae kwa ujio wa S3. Alipkwenda bungeni akasema S3 zisubiri kwanza aondoke madarakani.
[/SUP]
[SUP]Ukiangalia mtirirko huo, ni wazi Rais anatukumbusha jinsi yeye na chama chake wanavyobadilika kutokana na upepo wa kisiasa na wala si UKAWA.[/SUP]

[SUP](Kifungu F)[/SUP]
[SUP]Rais: Nimeambiwa tume itaandaa rasimu na bunge la katiba litatunga katiba[/SUP]
[SUP]Hoja: Mh Rais, maatumizi ya maneno ni muhimu sana katika mawasiliano. Rasimu (draft) ni tofauti na kutunga.[/SUP]
[SUP]Kutunga ni kutengeneza au kuunda jambo kutoka wazo lislokuwepo. BMK haliwezi kutunga katiba kwasababu tayari lina rasimu ikiwa na mawazo ya watu.
[/SUP]
[SUP]Bunge la katiba linaandika katiba kutokana na rasimu katika muundo wa katiba inayotegemewa.
Hivyo kutumia neno kutunga kunaonyesha upungufu wa ima aliyeandika hotuba [/SUP][SUP]au mh Rais aliyeeleza kuhusu hilo.
[/SUP]
[SUP](Kifungu G,H,I) vinaonyesha ushiriki wa wananchi katika kutoa maoni. Haiwezekani bunge la katiba litunge katiba wakati wazo lipo tayari na wananchi wamelitolea maoni.[/SUP]
[SUP]Hadi hapo utaona jinsi Rais anavyojikanganya.[/SUP]
[SUP]Muhimu sana ni rais kuwa na habari za uhakika anapoongea na taifa na si kutegemea habari za ‘kuambiwa''[/SUP]

[SUP](Kifungu E,K,L,M) [/SUP]
[SUP]Rais; Ametumia vifungu hivyo kuonyesha kuwa madai ya ukawa ni BMK kuidhinisha rasimu tu kama ilivyo[/SUP]
[SUP]Hoja: Hapa Rais anapotosha sana umma. Na hakika ni jambo linalomdhalilisha. Watanzania wa leo si wa mwaka 1950.
[/SUP]
[SUP]Sote tunajua madai ya UKAWA si kutaka ‘ratification'' rasimisha rasimu bila mjadala. Kuanzia mwanzo, UKAWA na Watanzania
[/SUP]
[SUP]wamesisitiza kuwa katiba ijadiliwe. Kila litakalojadiliwa liwe katika muundo uliowekwa na rasimu.
Hakuna mahali ambapo UKAWA wametaka rasimu iidhinishwe.
[/SUP]
[SUP]Alichokifanya Rais ni kutaka kuwafanya UKAWA waonekana mazuzu mbele ya jamii.
Je, kwa Tanzania ya leo, siasa hafifu na dhilili kama hizi zinamsaidia mheshimiwa.[/SUP]

[SUP]Rais anapowadhalilisha UKAWA kwa kuwazulia maneno yasiyokuwepo si kuwa anajenga ufa, bali anakula maneno yake katika (Kifungu AP)
[/SUP]
[SUP]Kama Rais wan chi, anapokosa credibility hawezi kutegemewa kuleta pande mbili pamoja. Hoja hii haina mantiki ni dhaifu na dhalili sana.[/SUP]
[SUP]Watanzania wanajua, mheshimiwa kachapia.[/SUP]

[SUP](Kifungu P)[/SUP]
[SUP]Rais: ananukuu kanuni za bunge[/SUP]
[SUP]Hoja: Mh Rais ameshindwa kuliona au kulielewa neno ‘msingi''.
Hapa limetumika kuonyesha kuwa kama hoja itakuwa na athari kubwa katika vifungu vingine[/SUP]
[SUP]basi iwakilishwe kwa katibu wa bunge kwa maandishi.

Msingi halikutumika kama muundo. Muundo unabaki kuwa hivyo, nayale yaliyomo ndiyo msingi.[/SUP]
[SUP]Hapa ndipo CCM wanapotumia ili kuleta utata.
Hakuna mahali pameelezwa kubadili muundo wa rasimu. Ni upotoshaji wa hali ya juu.[/SUP]

[SUP]Waliotunga kanuni walikuwepo UKAWA. Hilo halimaanishi kuwa uwepo wao ndio chanzo cha utata, au uwepo wao ni tiketi ya vifungu kutumiwa vibaya.[/SUP][SUP]Na kwa kuliona hilo, ndio maana UKAWA wakasema hoja ya CCM ni kuleta yaliyo nje ya rasimu.

[/SUP]Tutaendelea bandiko la 3-5






 
Back
Top Bottom