UKAWA wanavyobabaika: Historia ya 'juisi ya maembe' kujirudia?

UKAWA wanavyobabaika: Historia ya 'juisi ya maembe' kujirudia?

Kobello
Kuhus nguvu ya serikali ya muungano, tunadhani hilo linajibika. Kazi ya BMK ndiyo hiyo ya kutafuta namna ya kuimarisha
serikali ya shirikisho. Walichokiweka ni sehemu tu ya mapendekezo kufuatana na utafiti wao ambao siyo final say.

Kuna swali ambalo UKAWA hawalijibu kwa sasa. Linaonekana kujirudia sana.
Kwamba, serikali ya muungano itakosa vyanzo vya mapato. Na hapa Kobello unaingia pia.
Swali lisiloulizwa ni hili hapa, kwani kwa sasa hivi chanzo cha uhakika cha mapato ni kipi?

Kumbukeni mzigo wote wa muungano ameubeba Mtanganyika. Sasa tuelezwe chanzo cha uhakika ni kipi.

Kuhusu vyama na asilimia 67, kumbuka kuwa znz chadema haina uzito wowote.
Bado mtinange unabaki kuwa kati ya CUF na CCM. Na hili nakuhakikishia hakuna ukaribu wa ina yoyote kati ya vyama hivyo. In fact hilo ni sehemu inayoongeza nguvu ya UKAWA kwasababu CUF commitment yake ni kubwa kuliko GNU.

Huwezi kusema CUF na CCM wanafanyakazi pamoja ikiwa sasa hivi GNU inapendekezwa ifutwe.
Hivyo, znz wapo likely kuungana na CDM kuliko CCM.

Kuhusu sera za majimbo za CDM, nadhani una jambo nao na hilo nitakuachia uendelee nao.
Hata hivyo naweka rekodi vema. Sera za majimbo hazikukataliwa na wananchi au kukubaliwa.
Nchi yetu wapiga kura hawajafikia kiwango hicho. Wetu bado wanasikiliza 'nichagueni niwaletee maendeleo''

Kutumia matokeo ya chaguzi kama uzuri wa sera ni kitu kisichofaa kabisa. Kobello, hii ni TZN siyo Marekani.

Hakuna uhusiano wa aina yoyote kati ya chaguzi na rasimu. Hata kwenye hizo chaguzi hakukuwa na suala la muundo wa muungano. Kusema chama fulani kilikataliwa kwasababu ya rasimu ni kwenda nje kabisa ya mstari, ni point isiyo na mashiko kabisa. sad!

Ndiyo maana nimesisitiza kuwa kama kuna tatizo la sera kati yako na chama kingine, hilo halihusiani na rasimu.
Na kuutendea uzi haki nadhani lisingejadilika hapa.

Hili la kusema kuna umbea wa makundi, tumelieleza kama mtazamo wetu.
Kila mmoja ana mtazamo wake na wala hajatusema mtu akubaliane nasi.

Kwa rekodi zako tulisema bunge litavunjika katika wiki 2 tangu kuzinduliwa.
Tunaomba radhi kwasababu lilivunjika wiki 3 baada ya hapo. Ukweli utabaki kuwa lilivunjika kama tulivyosema 'umbea'

Tulisema, Sitta hafai kuliongoza bunge, na sasa 'umbea' unaonekana bila kuhitaji diploma.
Tulisema, mchakato huu kikwete amekosea, ilitakiwa mkutano wa kitaifa. Nadhani wengi wanaona tatizo lililopo.

Tukasema BMK si la wanasiasa, wataharibu mchakato. Sijui kama unahitaji darubini kubaini hili
Tukasema, CCM watatumia wingi wao kuburuza bunge. Umbea huo unaonekana bila ceritificate.
n.k

Hili la ugomvi ndani ya CCM litatokea katika siku chache zijazo. Kama halitatokea tunaomba radhi, likitokea tutaukuita hapa.

Karume na Mansour wana ushaiwishi. Laiti ungelijua nini kinaendelea sasa hivi. Hilo naliacha kama lilivyo.
Siyo suala la kupiga kura kuna ushawishi wa kisiasa. Kwani hujui ushawishi ni kitu gani?

Na mwisho, maoni ya watu hutofautina, na wala hatuwezi kuwa na maono sawa.
Hivyo pasipokupenedeza njia bora ni kuvumilia.
Hatudhani name calling inaweza kututofautisha na wahuni wengine.

Ipo siku tutakualika hapa uthibitishe data zaidi.

Nilichokiona katika hoja zako ni kuwa unakubaliana na Tanganyika kubebe mzigo wa muungano. T
Tatizo una ugomvi na watu wenye agenda uipendayo.
 
KANUNI ZABADILISHWA KUFICHA DHAMBI ILIYOKUSUDIWA

UKWELI UNAONEKANA, UKAWA WALITEGEWA
.


Wanaduru tunafuatilia kwa ukaribu vituko vinavyoendelea Dodoma. Jioni hii tutakuwa na sehemu ya kueleza kwanini kanuni zimebadilishwa. Nini lengo la Sa,wel Sitta


Stay tuned
 
Nguruvi3
Katika mdahalo wa jana Jaji Warioba amesema hivi "Hakuna mawaziri wa muungano wanaotembelea Zanzibar kwa ajili ya mambo ya Muungano. Mambo yote ya muungano ni ya bara." unaweza kutufafanulia hili...
 
Nguruvi3
Katika mdahalo wa jana Jaji Warioba amesema hivi "Hakuna mawaziri wa muungano wanaotembelea Zanzibar kwa ajili ya mambo ya Muungano. Mambo yote ya muungano ni ya bara." unaweza kutufafanulia hili...
Mkandara , ufafanuzi upo. Ninakuomba kwanza urudi ukamsikilize Warioba na umnukuu kikamilifu na si mstari mmoja.
Kuna mambo ya msingi umeyaacha ili kujenga hoja unayotaka na si hoja aliyokusudia Warioba.

Ukimnukuu vizuri bila kukata maneno, mbona nitakuwa nawe tu jamvini.

NB: Enzi za Rais Mwinyi RTD iliwahi kumkariri Shehe mmoja wakati wa sakata la mabucha akisema '' Ninawahakikishieni tutamwaga damu''. Baada ya hapo habari ikawa Shehe kasema waislam watamwaga damu.

Wenye akili zetu tukatafuta mkanda mzima ili tujue Shehe alidhamiria nini na lini.

Kumbe alichokisema ni hiki '' Hali hii ya kutotusikiliza na madai yetu inaweza kupelekea taifa pabaya, tukamwaga damu. Ninawahakikishieni mambo kama haya yametokea sehemu nyingine na damu ikamwagika''
 
HOTUBA YA KIKWETE YAWASHA MOTO(JULY 31)

SITTA AZABWA KIBAO HADHARANI

JK APIGWA MWELEKA KITU UZIMA

HASIRA ZAO WAHAMISHIA KATIKA TV.


Nukuu kutoka bandiko 225, majumuisho ya mtazamo wa hotuba ya Rais
SEHEMU YA 5 (A)

MAJUMUISHO YA DHAMIRA YA HOTUBA YA JANA

Hotuba haikuwa na ufumbuzi wa tatizo bali kujivua lawama anazoelekezewa Raia. Hakufanikiwa kwani njia alizotumia hazikuwa sahihi.

Hotuba ilijaa upotoshaji dhidi ya UKAWA haina lengo la kuleta taifa pamoja.

Rais ameshindwa.


Pili, Rai alilenga kuwasema wazee wa tume. Ingekuwa busara angekaa kimya.

Wazee wa tume wamesema waliongea na rais kila hatua.
Wana duru, siku ile ile Rais alipotoa hotuba, duru ilifanya uchambuzi kuangalia mantiki, athari na faida za hotuba ya Rais ya mwisho wa mwezi.

Katika nukuu hapo, hiyo ilikuwa ni majumuisho baada ya kuweka mtazamo na uchambuzi wa hotuba.
Tulionya kuwa hotuba ya Rais ilichochoea moto ni busara angekaa kimya.

Hilo ndilo limetokea. Ndugu yangu Kobello aliyeita duru umbea, tunadhani anaendelea kupata somo kila uchao.

WAZEE WA TUME WACHOSHWA NA KUDHALILISHWA.
WASEMA LIWALO NA LIWE, HESHIMA KUHESHIMIANA

Katika mdahalo wa juzi ambao ulimshirikisha profesa Palamagamba Kabudi kuna mengi yalitokea.
Kwa muda mrefu prof amekua kimya akiacha vijana akina Pole pole, Humphrey na wengine wafafanue hoja za tume.

Hotuba ya Rais imewaudhi wazee wa tume hasa pale aliposema wamejadiliana juu juu tu.
Kutokana na kuchoshwa na dhalili wanayofanyiwa, wazee wa tume wameamua kumwaga mboga. JK alimwaga Ugali.

Mzee Warioba alianza kwa kunasa kibao hadharani mh mwenyekiti wa BMK la CCM, Samwel Sitta.
Akitumia lugha laini, Warioba alifafanua kwa undani kabisa kuhusu kazi za tume na jinsi walivyofikia muafaka.

Katika hotuba yake, Warioba alisema 'nasikia wanataka kurudi kujadili 50-50'' akawasihi wajadili katiba yote akieleza ni kwanini. Hiyo 50-50 ni maneno ya Samwel Sitta katika gazeti la Raia mwema. Sitta alisema Wazanzibar warudi kwasababu kuna mambo ya 50-50 na mengine mazuri. Warioba kamnasa kibao cha hadharani kwa kumwambia katiba ni mambo yote na hakuna maana ya kujadili nusu nusu. Kidiplomasia kabisa akimnasa vibao kikamilifu.

Mzee Warioba hakumwancha JK. Alisema wazi kabisa kuna wakati walijadiliana kwa undani kabisa na uongozi wa juu wa nchi. Kwa staha akamzabua mzee kiutu uzima.

Prof Palgamagamba alionekana kama faru aliyejeruhiwa. Yeye alianza kumtupia kombora JK kuhusu suala la miapaka ya nchi. Kaeleza kiasi mzee akaonekana hakusoma au alisoma na hakuelewa alichokisoma. Hakumuweka pembeni alimnasa hadharani mbele ya taifa baada ya kuchoshwa na ubabaishaji upotoshaji na kudhalilishwa.

Prof akamgeukia Sitta na kumzabua vibao. Alitaja sifa za wanasheria akionyesha wazi kuwa Sitta hana fani hiyo.
Ndipo aliposema hao wengine ni wababishaji.
Prof akaendelea kumgeuza shavu na kumtandika kibao kingine. Alisema kuwa kitendo cha kuwazuia wake nje ni kimyume na taratibu na wao wangesaidia sana katika ufafanuzi.

Kwa maelezo hayo Prof alinyosha mkono na kuwazabua vibao Wassira na Lukuvi walioshadidia mswada wa kuondoa tume katika bunge la katiba.

Hasira za Mzee Sitta za kuzabuliwa hadharani ndizo zilipelekea akasema TV zichukuliwe hatua.
Alijificha nyuma ya neno uzalendo, ukweli ukiwa ni kuwa alikuwa anaugulia maumivu makali yeye na mzee.

Sitta hana sababu za kulaumu TV. Duru za siasa zilishaotoa hadhari kuwa hotuba za Rais zinaligawa taifa kuliko wakati mwingine. Tulisema, wazee wa tume walikuwa na staha si kuwa hawakujua la kusema.
Leo wametoa kucha tunaona wakubwa wanavyo adhirika.

Na huu ni mwanzo wa matatizo makubwa yanayomkabli Sitta. Ile ndoto yake imeisha kabla ya majogoo.

Wa kualumiwa si TV, si mitandao si magazeti. Ni yule anayechochea kuni akijua hana la kupoteza.
Keshasema tusubiri aondoke. Walio na matatizo ni hawa tunaowaona Dodoma.

Nguvu ya umma inawasubiri 2015 nanyi mtazabuliwa makofi mkiwa hamna pa kukimbilia. Lumumba watakuwa wamefunga milango wakisubiri mpangaji mwengine, nanyi mkisaga meno maana tunawaona. Tunawasubiri.

Tusemezane.
 
Last edited by a moderator:
HOTUBA YA KIKWETE YAWASHA MOTO(JULY 31)

SITTA ''AZABWA'' KIBAO HADHARANI

JK APIGWA ''MWELEKA KITU UZIMA''

HASIRA ZAO WAHAMISHIA KATIKA TV.


Nukuu kutoka bandiko 225, majumuisho ya mtazamo wa hotuba ya Rais
SEHEMU YA 5 (A)

MAJUMUISHO YA DHAMIRA YA HOTUBA YA JANA
Hotuba haikuwa na ufumbuzi wa tatizo bali kujivua lawama anazoelekezewa Raia. Hakufanikiwa kwani njia alizotumia hazikuwa sahihi.
Hotuba ilijaa upotoshaji dhidi ya UKAWA haina lengo la kuleta taifa pamoja.
Rais ameshindwa.

Pili, Rai alilenga kuwasema wazee wa tume.
Ingekuwa busara angekaa kimya.
Wazee wa tume wamesema waliongea na rais kila hatua.
Wana duru, siku ile ile Rais alipotoa hotuba, duru ilifanya uchambuzi kuangalia mantiki, athari na faida za hotuba ya Rais

Nukuu hapo ju, hiyo ilikuwa ni majumuisho baada ya mtazamo na uchambuzi wa hotuba.
Tulionya kuwa hotuba ya Rais ilichochoea moto ni busara angekaa kimya.

Hilo ndilo limetokea.
Ndugu yangu Kobello aliyeita duru umbea, tunadhani anaendelea kupata somo kila uchao.

WAZEE WA TUME WACHOSHWA NA KUDHALILISHWA.
WASEMA LIWALO NA LIWE, HESHIMA KUHESHIMIANA

Katika mdahalo wa juzi uliomshirikisha profesa Palamagamba Kabudi kuna mengi yalitokea.
Kwa muda mrefu prof amekua kimya akiacha vijana akina wafafanue hoja za tume.

Hotuba ya Rais imewaudhi wazee wa tume hasa pale aliposema wamejadiliana juu juu tu.

Kutokana na kuchoshwa na dhalili wanayofanyiwa, wameamua kumwaga mboga.

Mzee Warioba alianza kwa kumnasa kibao hadharani mwenyekiti wa BMK, Samwel Sitta.

Akitumia lugha laini, Warioba alifafanua kwa undani kabisa kuhusu kazi za tume na jinsi walivyofikia muafaka.

Katika hotuba yake, Warioba alisema 'nasikia wanataka kurudi kujadili 50-50'' akawasihi wajadili katiba yote akieleza ni kwanini.

Hiyo 50-50 ni maneno ya Samwel Sitta katika gazeti la Raia mwema.
Sitta alisema Wazanzibar warudi kwasababu kuna mambo ya 50-50 na mengine mazuri.

Warioba ''kamnasa'' kibao cha hadharani kwa kumwambia katiba ni mambo yote na hakuna maana ya kujadili nusu nusu. Kidiplomasia kabisa akimnasa vibao kikamilifu.

Mzee Warioba hakumwancha JK. Alisema wazi kuna wakati walijadiliana kwa undani kabisa na uongozi wa juu wa nchi. Kwa staha akamzabua mzee kiutu uzima.

Prof Palgamagamba alionekana kama faru aliyejeruhiwa.
Yeye alianza kumtupia kombora JK kuhusu suala la miapaka ya nchi.

Kaeleza kiasi mzee akaonekana hakusoma au alisoma na hakuelewa alichokisoma.

Hakumuweka pembeni alimnasa hadharani mbele ya taifa baada ya kuchoshwa na ubabaishaji upotoshaji na kudhalilishwa.

Prof akamgeukia Sitta na kumzabua vibao.
Alitaja sifa za wanasheria akionyesha wazi kuwa Sitta hana fani hiyo.

Ndipo aliposema hao wengine ni wababishaji.
Prof akaendelea kumgeuza shavu na ''kumtandika'' kibao kingine.

Alisema kuwa kitendo cha kuwazuia wake nje ni kimyume na taratibu na wao wangesaidia sana katika ufafanuzi.

Kwa maelezo hayo Prof alinyosha mkono na ''kuwazabua vibao'' Wassira na Lukuvi walioshadidia mswada wa kuondoa tume katika bunge la katiba.

Hasira za Mzee Sitta za ''kuzabuliwa'' hadharani zilipelekea akasema TV zichukuliwe hatua.

Alijificha nyuma ya neno uzalendo, ukweli alikuwa anaugulia maumivu makali yeye na mzee.

Sitta hana sababu za kulaumu TV.
Duru za siasa zilishaotoa hadhari kuwa hotuba za Rais zinaligawa taifa kuliko wakati mwingine.

Tulisema, wazee wa tume walikuwa na staha si kuwa hawakujua la kusema.
Leo wametoa kucha tunaona wakubwa wanavyo adhirika.

Na huu ni mwanzo wa matatizo makubwa yanayomkabli Sitta.
Ile ndoto yake imeisha kabla ya majogoo.

Wa kualumiwa si TV, si mitandao si magazeti.
Ni yule anayechochea kuni akijua hana la kupoteza.
Keshasema tusubiri aondoke.

Walio na matatizo ni hawa tunaowaona Dodoma.

Nguvu ya umma inawasubiri 2015 nanyi mtazabuliwa makofi mkiwa hamna pa kukimbilia.

Lumumba watakuwa wamefunga milango wakisubiri mpangaji mwengine, nanyi mkisaga meno maana tunawaona. Tunawasubiri.

Tusemezane.
 

TANGANYIKA INATIA KIWEWE.

CCM KIWEWE TUPU
WANAKULA, WANATAPIKA HALAFU WANAMEZA

HOFU TU , HAWAJUI WASIMAMIE WAPI. HAWAKUMBUKI WALIKATAA NINI

Baada ya kuona ufafanuzi wa Prof Kabudi na Warioba, hatimaye Wajumbe wa BMK-CCM wameamua kujadili ibara 1-15 kwa pamoja. Kuna hoja zinazojitokeza hapa za kushangaza.

Kwanza, viongozi waandamizi wa CCM wamekaririwa mara nyingi wakimtuhumu Jaji Warioba kwa kuleta 'dude' ambalo hakutumwa kulifanyia kazi.

Mwenyekiti wa CCM ambaye ni Rais si kuwa alikaa kimya wakati Warioba anaanikwa hadharani, bali nae katika hotuba ya ufunguzi alitilia shaka takwimu za Warioba.

Midahalo iliyopita, Waziri Wassira, Waziri Lukuvi nao wamesema bila kificho, takwimu zina matatizo.Hoja yao kubwa ikiwa ni idadi ya watu waliohojiwa.

Wanaposimamia ni kuwa ili takwimu zilete maana lazima idadi ifikiie angalau 30%.
Wasira na Lukuvi wamesema katika midahalo mchana kweupe.

Leo Wajumbe wa BMK-CCM wamegawnyika katika kamati ili kujadili vifungu 1-15 vya rasimu ile ile wanayoisema ni 'utunzi' wa mzee Warioba.

Rasimu ile ile wanayotilia shaka takwimu zake na mwenyekiti wao Rais wa JMT.
Na rasimu ile ile waliyoita 'dude' na mawazo ya Warioba.

Inashangaza sana, wanawezaje kufanyia kazi takwimu wasizokubalina nazo?

Je hiyo rasimu yao itakuwa na uhalali gani, ikiwa rasimu ya Warioba ilikosa uhalali wa hadidu za rejea na takwimu?

Je, idadi ya wajumbe wa BMK-CCM inaweza kutoa takwimu halisi (400) kuliko watu waliohojiwa na Warioba(20,000)?

Hii ina maana moja, CCM hawana hoja ya msingi ya kupinga Rasimu ya Warioba.

Wanachotaka ni kukataa tu ili waandike rasimu yao pembeni.

Wakishamaliza kuandika tutawauliza, takwimu wamepata wapi na analysis ya takwimu hizo imefanyaika vipi, tukizingatia walishasema Warioba kaleta kitu asichotumwa, kisicho katika hadidu za rejea.

Huku kubabaika kunazidi kuwaanika CCM na kuwafanya waonekana kama mazuzu.

Hakuna mtu mwenye akili timamu anayezitumia vema anaweza kukaa chini na kueleza kubabaika huku kunatokana na nini na si kujitia wendawazimu bila sababu.

Hoja ilikuwa wakatae kabisa rasimu ya Warioba waliyoita 'dude' ili watengeneze yao.

Kurudi kuifanyia kazi rasimu ile ile waliyokataa kuwa si halali ni sawa na kula, kutapika na halafu kufakamia matapishi yale yale.

Aibu na dhalili sana

Tusemezane
 
Tulisema, mchakato huu kikwete amekosea, ilitakiwa mkutano wa kitaifa. Nadhani wengi wanaona tatizo lililopo.

Mkuu Nguruvi3, kuna hii dhana yako ya Mkutano wa Kitaifa umekuwa ukiirudia rudia, hivi uliwahi kufikiria hao wawakilishi katika mkutano huo watapatikanaje? Haiwezekani tukapata wawakilishi kama hawa hwa walioko kwenye BMK? Au vipi kama hiyo formula; ambayo kwa mawazo yako unaona inafaa, ya kupata wajumbe wa MKUTANO WA KITAIFA vipi ingetumika kupata wawakilishi kwenye BMK tukapata katiba bora kwa utaratibu huu wa sasa?

Kwa mtazamo wangu, kile unachokiona kwenye BMK ndio taswira halisi ya jamii yetu, utashi binafsi mtu ungependa mambo yaende vizuri kidogo lakini hao watu si wametokea miongoni mwetu? Hao ccm hawashuka kuto sayari nyingine, ni miongoni mwa ndugu zetu, shemeji, wajomba, majirani na hata wazazi wetu. Watazamo na jinsi wanavyoendesha mambo yao ujue unaitazama jamii yako kwenye kioo ukiwemo wewe mwenyewe!

Hata ikatokea muujiza tukapata katiba wanayoishadidia wale wazee wa iliyokuwa tume ya Katiba, ufikapo uchaguzi watakuja MAFISADI na kushinda kwa mtindo ule ule waliouzoea na serikali mbovu ndio matunda yake. kama umeishi Tz siku za karibuni utakubaliana na maoni yangu haya.

Labda kwa nusura ya Mungu, apatikane dikteta mzalendo kama PK atutawale kiubabe ubabe ndio nidhamu itarudi, na hii haiwezekani kwa usanii huu tunaoita demokrasia.
 
Mkuu Nguruvi3, kuna hii dhana yako ya Mkutano wa Kitaifa umekuwa ukiirudia rudia, hivi uliwahi kufikiria hao wawakilishi katika mkutano huo watapatikanaje? Haiwezekani tukapata wawakilishi kama hawa hwa walioko kwenye BMK? Au vipi kama hiyo formula; ambayo kwa mawazo yako unaona inafaa, ya kupata wajumbe wa MKUTANO WA KITAIFA vipi ingetumika kupata wawakilishi kwenye BMK tukapata katiba bora kwa utaratibu huu wa sasa?

Kwa mtazamo wangu, kile unachokiona kwenye BMK ndio taswira halisi ya jamii yetu, utashi binafsi mtu ungependa mambo yaende vizuri kidogo lakini hao watu si wametokea miongoni mwetu? Hao ccm hawashuka kuto sayari nyingine, ni miongoni mwa ndugu zetu, shemeji, wajomba, majirani na hata wazazi wetu. Watazamo na jinsi wanavyoendesha mambo yao ujue unaitazama jamii yako kwenye kioo ukiwemo wewe mwenyewe!

Hata ikatokea muujiza tukapata katiba wanayoishadidia wale wazee wa iliyokuwa tume ya Katiba, ufikapo uchaguzi watakuja MAFISADI na kushinda kwa mtindo ule ule waliouzoea na serikali mbovu ndio matunda yake. kama umeishi Tz siku za karibuni utakubaliana na maoni yangu haya.

Labda kwa nusura ya Mungu, apatikane dikteta mzalendo kama PK atutawale kiubabe ubabe ndio nidhamu itarudi, na hii haiwezekani kwa usanii huu tunaoita demokrasia.
Kakalende dhana ya mkutano wa kitaifa nairudia rudia kwasababu muhimu kabisa.

Mkutano wa kitaifa ungekuwa na mkusanyiko wa makundi ya jamii zaidi kuliko kuchukua CCM asilimia 76 bunge la JMT, 50% BLW na kisha kumpa Rais nafasi 201 ambazo 2/3 amejaza watu wake waaminifu.

Mkutano wa kitaifa ungetokea dira na muundo wa nchi tunayotaka kujenga. Kupitia mkutano huo akina Pinda wangeona kile walichoshiindwa kukisoma mitandaoni. Ni lazima suala la muungano lingeibuka na huo ndio ungekuwa wakati mzuri wa kuamua kuwe na kura ya maoni. Kingekuwa kiashirio kizuri sana kwa waliojitia upofu kama waziri mkubwa wetu.

Mkutano huo ungeweka uelekeo na vigezo katika safari ya kuandika katiba, tofauti na sasa ambapo mtu mmoja ameandika hadidu za rejea na kuipa tume ifanyie kazi.

Ni kweli Watanzania ni watu wa ajabu, lakini huenda tungalikuwa na matokeo tofauti na haya tunayoyaona.
Hata hivyo kidogo kidogo wanaamka maana inapofikia mahali madikteta wancahukia TV kuna kamwanga fulani.

Nikukumbushe kuwa serikali ilikimbia mkutano wa kitafa kwa hofu kuwa wajumbe wake wanatoka katika makundi ya jamii. Of course CCM ingekuwa na watu wake, lakini si kiwango hiki cha kufikia mahali kutumia wingi na si maarifa na weledi kwenye jambo zito kama hili. Wapo Dodoma kwasababu ya wingi tu
 
Last edited by a moderator:
Kobello
Katika mdahalo wa Serena, ukiatazama kwa umakini Vuai hakuwa anajibu maswali.
Nitakupa mfano, aliulizwa, wazanzibar kuanzia enzi za jumbe walitaka serikali 3,leo kimebadilika nini wanataka 2?
Vuai hakujibu kabisa. Alichosema ni kuwa rasimu ina tatizo la msingi kabisa bla bla bla.

Naomba utuwekee sawa hili suala la Aboud Jumbe. Uanzie na ajira ya mwanasheria mkuu mghana (how did it happen?) na utuelezee maoni yako kuhusu ugomvi wake na Seif Shariff Hamad na kujiuzulu kwake.
Naomba pia uelezee kwa vielelezo ainishi au oanishi ni kwanini unadhani in 1984 majority ya wazanzibar walitaka serikali tatu.
 
Naomba utuwekee sawa hili suala la Aboud Jumbe. Uanzie na ajira ya mwanasheria mkuu mghana (how did it happen?) na utuelezee maoni yako kuhusu ugomvi wake na Seif Shariff Hamad na kujiuzulu kwake.
Naomba pia uelezee kwa vielelezo ainishi au oanishi ni kwanini unadhani in 1984 majority ya wazanzibar walitaka serikali tatu.
Hakuna Mahali nimeongelea About Jumbe, Mghana au Seif.
Nilichofanya ni kukuonyesha kuwa Vuai hakuwa na jibu la swali aliloulizwa. Wewe ulisema amejibu vizuri.

Nimekuwekea maneno yake aliyosema na video ipo.
Alipoulizwa wazanzibar walitaka S3 siku nyingi, nini kimebadilika leo hii?
Jibu la Vua ni kuwa kuna tatizo la msingi la rasimu na bla bla bla.

Sasa unaniuliza maswali wakati swali hilo aliulizwa Vuai?
Ndugu yangu hebu jaribu kuwa calm and composed.
 
Kwa Mujibu wa taarifa zilizopo, baadhi ya wana ukawa wamerejea bungeni. Hali hii ilitarajiwa kwa sababu kuu kadhaa:

• Kwanza - ukawa ni umoja, na sio ushirikiano au mkataba. Umoja huu hauna Nguvu za kisheria, kwa mfano kuwa na memorandum of understanding.

•Pili, ukawa ni umoja wa viongozi kuliko umoja wa wanachama na mashabiki wa vyama Vikuu vitatu vya upinzani - Chadema, CUF na NCCR Mageuzi. Kwa ufafanuzi Rahisi - kwa mfano Wakati ni Rahisi kwa viongozi wa CUF kuwa na umoja na viongozi wa chadema na NCCR Mageuzi, ni Vigumu kwa wanachama na wajenzi wengi wa vyama hivi kufanya hivyo. Tuchukulie wafuasi wa vyama vifuatavyo - kwa kawaida, wafuasi qa vyama (undecided voters) huwa ni wengi kuliko wanachama. Kiuhalisia, ni Kheri kwa mfuasi wa CUF kuunga Mkono CCM kuliko chadema; ni kheri kwa mwanachadema kuunga Mkono CCM kuliko CUF, na kadhalika na kadhalika. Hoja ya msingi Hapa ni Kwamba ukawa hawajafanya kazi ya maana Katika kushusha umoja wa viongozi uende chini kwa wananchi.

• Tatu, ukawa hauna mwono zaidi ya katiba mpya. Katiba mpya haileti maendeleo ya kiuchumi na kijamii, badala yake inaweka tu misingi ya kisheria kufanikisha Hilo. Kinachobadilisha maisha ya wananchi ni Dira na Sera Zenye sura Mbili- kwanza Dira na sera ambazo wananchi wanashirikishwa Katika utungaji wake, na Pili, sera ambazo wananchi wanashirikishwa Katika utekelezaji na usimamizi - decentralization by devolution kwa mfano, n.k. Suala la kusogeza zaidi serikali ya Tanganyika kwa wananchi kuliko kwa Hali ya sasa ambapo serikali Yao Ndio hiyo hiyo ya muungano ni mfano mmoja wapo.

Ni Katika muktadha wa hoja ya Tatu hapo juu - yani ukawa kukosa mwono zaidi ya katiba mpya, Ndio viongozi Kama Zitto, pamoja na mapungufu Yao, wana hoja pale wanaposema Kwamba ukawa haitadumu. Huu ni Ukweli mchungu, na badala ya ukawa Kujibu hoja Kama hii kwa majibu rojorojo Kwamba zitto Hana mamlaka ya kuisemea ukawa, ilitakiwa ukawa wajipange na kuja na Dira na sera mbadala kwa CCM ambazo watazinadi Kama sehemu ya mikakati Yao ya kuliongoza taifa baada ya katiba mpya kupatikana. Nje ya hapo, hata katiba mpya ikipatikana, wananchi wengi wataona Kwamba hata CCM ikijirekebisha Hapa na pale itaweza tu kutumia katiba mpya kuleta maendeleo n.k. Kwa maana nyingine, Dira ya nchi kwa sasa ni vision 2025 ambayo kimsingi ili replace azimio la Arusha Rasmi mwaka 1995. Vision 2025 ni Dira iliyotungwa na wahisani - Washington consensus, sio wananchi Wala wawakilishi wao. Ndio maana serikali imekuwa inawajibika zaidi kwa wahisani kuliko wananchi. Pamoja na promises za vyama Kama chadema Kwamba vitakuja na Dira mpya, bado hakuna dalili Kwamba Dira hiyo itakuwa grass root founded and driven, kuna kila dalili Kwamba ikulu ya ukawa itakuwa business as usual kwa maana ya Kwamba sana sana kitakachobadilika itakuwa tu ni usimamizi zaidi wa Mapato, matumizi, na uadilifu. Pamoja na muhimu wa masuala Kama haya, yote itakuwa ni kazi bure iwapo usimamizi wa rasilimali za nchi utakuwa Katika muktadha wa Dira na sera ambazo ni more donor driven kuliko grassroots driven. Ukawa wana fursa nzuri iwapo wataangalia masuala Kama haya. Kwa Hali ya sasa, ukawa ni ushirikiano wa vyama vitatu Katika muda Mfupi na wa Kati:
1. Kupatikana kwa katiba ya wananchi.
2. Kushirikiana uchaguzi mkuu ujao kuibwaga CCM.

Ushirikiano wa muda mrefu haupo - kwa mfano, Mbali na hoja yangu ya awali hapo juu Kwamba ukawa ni kwa viongozi zaidi kuliko wanachama na wapenzi wa vyama husika, vyama hivi havina itikadi Zenye kuelekea kutafuta kitu kinachofanana. Mbaya zaidi, kuna mapengo makubwa sana baina ya itikadi za vyama, ndoto, matarajio na matamanio ya wananchi walio wengi kijamii na kiuchumi na Dira na sera ambazo Zipo more donor driven and determined kuliko grassroots driven and determined.

Ukawa needs to come up with a comprehensive plan now or never. Bila ya hivyo, kutopatikana kwa katiba mpya kutakuwa ni Ushindi kwa CCM, na upatikanaji wa katiba mpya itakuwa ni Ushindi kwa wananchi kuliko ukawa kwani bila ya kujipanga, wananchi wengi watasahau ukawa baada ya katiba mpya kupatikana kutokana na hoja za awali hapo juu.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Hakuna Mahali nimeongelea About Jumbe, Mghana au Seif.
Nilichofanya ni kukuonyesha kuwa Vuai hakuwa na jibu la swali aliloulizwa. Wewe ulisema amejibu vizuri.

Nimekuwekea maneno yake aliyosema na video ipo.
Alipoulizwa wazanzibar walitaka S3 siku nyingi, nini kimebadilika leo hii?
Jibu la Vua ni kuwa kuna tatizo la msingi la rasimu na bla bla bla.

Sasa unaniuliza maswali wakati swali hilo aliulizwa Vuai?
Ndugu yangu hebu jaribu kuwa calm and composed.
Im cool, calm and collected.
Wazanzibar hawakutaka serikali 3 1984. Hatuna uhakika huo. hata data za tume ya Nyalali iliyokuja miaka sita baadae, haikuonyesha kuwa wazanzibari walitaka serikali 3.
Swali hilo halikuwana msingi kwa maoni yangu.
 
Im cool, calm and collected.
Wazanzibar hawakutaka serikali 3 1984. Hatuna uhakika huo. hata data za tume ya Nyalali iliyokuja miaka sita baadae, haikuonyesha kuwa wazanzibari walitaka serikali 3.
Swali hilo halikuwana msingi kwa maoni yangu.
Swali lilikuwa la msingi sana. Na hapa nafafanua.

1. Jumbe aliondolewa kwa hoja ya S3. Kilichomuondoa si hoja bali utaratibu aliotaka kutumia.
Akiwa Rais wa nchi, kitendo cha kutaka S3 kilimaanisha kuwa kiongozi wa nchi hakuridhika na mfumo uliopo.

2. Tume ya Nyalali ilikuja na maoni ya S3. Tume hiyo iliundwa wakati wa chama kimoja. Ni dhahiri ule upendeleo na aibu kwa Rais ilifika mahali hauvumiliki. Tume ikaja na S3 kama suluhu.

3. Tume ya Kisanga iliyoundwa na Rais nayo ilikuja na S3. Mkapa akamtukana mzee wa watu kwa kufanya kazi aliyomtuma. Kumbuka, wakati huo Mkapa alikuwa mwenyekiti wa CCM

4. Tume ya Warioba iliyoundwa kuchunguza mgogoro kule visiwani, pamoja na mambo mengine ilikuja na S3.
Warioba alikuwa makamu wa Rais na Waziri mkuu. Tume yake iliundwa mara tu baada ya kuacha nyadhiifa ikimaanisha alikuwa na kumbu kumbu za matatizo ya muungano kuliko kiongozi mwingine.

5. Zikaundwa tume za akina Amina Salum Ally, Shamhuna n.k. ambazo zote zimekuja na madai ya kutenga shughuli za Tanganyika na muungano. Hazikusema S3, kimantiki zilimaanisha hivyo. Huwezi kutenga Tanganyika, ukawa na JMT na Znz halafu ukajidanganya kuna S2

6. Upinzani ZNZ umekuja na suala la S3 tangu umeanzishwa. Umeungwa mkono na wananchi wa Zanzibar kwa wingi kiasi cha kushawishi hata muungano wa mkataba.

7. Waziri kiongozi wa znz juzi amekaririwa akisema Tanganyika imevaa koti la muungano. Ndivyo akina Pandu walivyosimamia mambo ya muungano yakiondolewa katika muungano bila taratibu na hawakusema neno.

8. Wajumbe wa BLW kwa pamoja walipitisha katiba ya 2010 ambayo kimsingi ilikuka katiba ya JMT na kwenda kinyume na makubaliano ya muungano. BLW lakamnyang'anya Rais wa JMT mamlaka, likaja mamlaka ya kutenda mambo juu ya katiba ya JMT. Hayo yote ni kiashiria kuwa znz ilishaondoka katika muungano wa S2 na Tanzania kwa ujumla.

9. Tume ya Warioba nayo imekuja na maoni ya S3. Sijui una maoni gani kuhusu takwimu na uchambuzi wa tume, ninachoweza kusema ni kuwa unakubaliana na Warioba unless uthibitishe hapa vinginevyo. Mimi ninaweza kukuthibitishia kuwa unakubaliana na Warioba.

10. Watanganyika wanataka waepuke lawama, wawe na uwezo wa kusimamia mambo yao kama wenzao wa znz.
Hilo ndilo limeongeza hamasa kwasababu, tayari wazanzibar wameshawatenga isipokuwa pale tu ambapo znz wana masilahi na Tanganyika. Kimsingi muungano haupo kiuhalisia isipokuwa kwa majina tu.

Ni kwa mantiki hizo, watu waliokuwa wanalalamika na wanaoendelea kulalamika kuhusu mfumo wa sasa ni wengi.
Kwa bahati nzuri upande wa Tanganyika umeliona hilo, kwamba katika S2, ni muungano wa znz kuvizia jina na masilahi.

Huyo Vuai mwenyewe ameshakaririwa akisema CCM inashughulikia kero. Kero ni muungano kwasababu huwezi kukereka bila sababu za msingi.

Leo tunashangaa akina Shamsa Nahodha Vuai wakidai Tanganyika imevaa koti wakati huo huo wapo Dodoma kulinda mfumo uliovaa koti. Leo tunashangaa akina Mohamed Kahatibu, Borafia, Raza na wengine, wanapowenda BLW wanalaani muungano. Wapo Dodoma kujadili mfumo unaowaumiza.

Ni kwa msingi huo, wengine tunajumuika na muulizaji wa swali kwa Vua Ali, je ni kitu gani kimebadilika kutoka S3 hadi S2 wanazoziita Laanatullah ya Nyerere?
 
wana duru leo asbh nimeskiliza kwa makini sana Prof Lipumba akiomba serikali/rais aairishe bunge kisha BJMT lipitishe sheria ili BLK livunjike.

ninashangaa sana anaposema anahitaj mariddhiano ya kisiasa, tena kwa kulalamika na kuomba as if anaomba huruma ya raisi. Kwangu mimi nimefikiri UKAWA inaweza kutumia alternative way ambayo ni wao kutokusubiri huruma za rais bali watoke waende mtaani wawape elimu wananchi kusudi wananchi waelewe kwamba mwisho wa yote wao ndio waamuzi so wanaweza kuipiga hii katiba chini na rais asiipitishe.

UKAWA waache kuwa slay wawe serious manake ukitaka kumshinda adui yako uwe na mbinu zaid ya moja na usiogope vita................wakisema wasubiri huruma za rais hazitakuwepo na leo Sitta kesha sema quorum itatimia.

Nikionacho mimi ni kwamba tayari approach waliyotumia imefeli, ni bora wangebaki bungeni wawe wanawachanganya humo humo mwisho wa siku ingeonekana kuna ulazima wa kulivunja hili bunge. kwasasa UKAWA wamekalia kuti kavu na mbaya zaid wao wakumbuke ni kifungu kimoja tu kinachowapa shida lkn kuna vifungu vingi sana ambavyo walitakiwa navyo wavirekebishe.
 
wana duru leo asbh nimeskiliza kwa makini sana Prof Lipumba akiomba serikali/rais aairishe bunge kisha BJMT lipitishe sheria ili BLK livunjike.

ninashangaa sana anaposema anahitaj mariddhiano ya kisiasa, tena kwa kulalamika na kuomba as if anaomba huruma ya raisi. Kwangu mimi nimefikiri UKAWA inaweza kutumia alternative way ambayo ni wao kutokusubiri huruma za rais bali watoke waende mtaani wawape elimu wananchi kusudi wananchi waelewe kwamba mwisho wa yote wao ndio waamuzi so wanaweza kuipiga hii katiba chini na rais asiipitishe.

UKAWA waache kuwa slay wawe serious manake ukitaka kumshinda adui yako uwe na mbinu zaid ya moja na usiogope vita................wakisema wasubiri huruma za rais hazitakuwepo na leo Sitta kesha sema quorum itatimia.

Nikionacho mimi ni kwamba tayari approach waliyotumia imefeli, ni bora wangebaki bungeni wawe wanawachanganya humo humo mwisho wa siku ingeonekana kuna ulazima wa kulivunja hili bunge. kwasasa UKAWA wamekalia kuti kavu na mbaya zaid wao wakumbuke ni kifungu kimoja tu kinachowapa shida lkn kuna vifungu vingi sana ambavyo walitakiwa navyo wavirekebishe.
Nilishawahi kuandika kuhusu hili. UKAWA hawawezi kumtegema JK katika mchakato huu.
JK hana nia ya katiba mpya, na kama anayo basi amefungwa na wahafidhina.

Unakumbuka alisema wanaCCM wawe tayari kwa S3. Akaenda bunge la katiba na kuvuruga kila kitu.

UKAWA wana nguvu ya umma lakini hawajaweza kuitumia kikamilifu the least to say
 
UKAWA MPANGO ULIOKUSUDIWA UNATEKELEZWA

MTAVURUGWA KWA KUTAWANYWA KWA KUTUMIA MBINU ZA DOLA

YALE YA ZNZ MSIDHANI NI SINEMA.

Bandiko moja huko nyuma tuligusia matukio ya Zanzibar yakihusisha siasa na vyombo vya dola.
Tulisema UKAWA ina nguvu za ushawishi visiwani na kundi jingine linalounga mkono UKAWA

Kundi la maridhiano limejtokeza kuwa na ushawishi sana wa siasa za Zanzibar.
Maridhiano lina watu maarufu kama mzee Hassan Moyo ambaye ni kada wa CCM, Jusa Ismail-kada wa CUF, akina Mansour Himid aliyefukuzwa CCM na karibuni kujiunga na CUF.

Katika kundi la maridhiano, Mansour Himid anaonekana kuwa na ushawishi mzito sana kuhusu hoja ya mamlaka kamili ya Zanzibar.

Kwa bahati nzuri au mbaya Mansour si mjumbe wa BMLK-Zanzibar. Hata hivyo, ushawishi wake unabaki kuwa na nguvu sana mitaani.

Mansour yupo mahabusu kwa kutuhumiwa kumiliki silaha. Hakuna ajuaye dhamana yake na ahtaima ya kesi .

Mansour Himid ni mtoto wa brigedia Yusuf Himid ambaye alikuwa mkuu wa kwanza wa majeshi ya Zanzibar baada ya mapinduzi.
Ni shemeji yake Rais Aman Karume na ni mume wa Fatma Karume.

TUHUMA ZA MADIWANI

Hivi karibuni kumekuwa na tuhuma za madiwani wa CDM dhidi ya njama za uhalifu walizopanga kwa kushirikiana na CCM.

Makada wamewataja viongozi wa juu katika serikali kama mawaziri na wanachama wa CCM wakiwemo viongozi ngazi ya kitaifa n.k.

Ushahidi wa madiwani kwa maneno ni mkali kiasi cha umma kudhani kungekuwa na uchunguzi wa kubaini ukweli au uongo.

Kinyume chake Jeshi la Polisi likasema limesikia habari hizo malalamiko kupitia vyombo vya habari na hakuna hatua zozote inazotegemea kuchukua.

Jana, kada mmoja wa ACT-Tanzania ambaye na mwanachama wa CDM wa zamani naye kajitokeza katika TV kutoa madai dhidi ya njama na mauaji yaliyopangwa na viongozi wa CDM.

Kada huyo naye ni sehemu ya waliotajwa katika suala la madiwani kama kiongozi aliyetumiwa na CCM katika kuratibu njama za mauaji na uhalifu kwa mujibu wa vyombo vya habari

Kuna habari kada huyo amechukuliwa kwa mahojiano zaidi Polisi.

Ikumbukwe kwamba Mchange hatuhumiwi kwa lolote bali ameitwa kutoa maelezo kuhusu anachokifanya.

Jeshi la Polisi halikusubiri malalamiko kama ilivyo kuwa kwa habari za mauaji ya viongozi wa CDM .

KUANA ''scenario'' TATU ZINAZOWEZA KUTOKEA

1. Polisi wametaka habari zaidi ukizingatia kuna kesi nyingi zisizo na majibu''
2. Mchange anaweza kutuhumiwa kwa madai ya uchochezi n.k.
3. Mchange anaweza kuwa shahidi upande wa Serikali kuhusiana na madai yake.

MCHANGE KUWA SHAHIDI

Serikali ya CCM ambayo ndio ina vyombo vya dola inaweza kuanza uchunguzi wa madai yalitolewa na mchange.

Uchunguzi huo utamhusisha mchange kama shahidi, lakini utakwenda mbali zaidi ya hapo.

Wale wote waliotajwa na Mchange itabidi waitwe kuhojiwa au wakamatwe wakati uchunguzi unaendelea.

VIONGOZI WANAWEZA KUKAMWATWA

Kuna uwezekanao mkubwa sana viongozi wa CDM wakakamatwa ili kuwa sehemu ya uchunguzi.

Ingawa wengi wanadhani Mchange amekamatwa ili kuwajibika, hiyo inaweza kuwa ni kweli.

Lakini watu wasisahu kuwa inaweza kuwa ni mapngo mahususi wa CCM kutokana na haya yafutatayo;

1. Kashfa ya madiwani ilikuwa nzito sana kwa upande wa CCM na wangependa habari igeuge na kukifanya CDM chama cha kigaidi ili kulinda na kufunika kashfa iliyowahusu viongozi waandamizi wa CCM.

2. CCM wangependa viongozi wa CDM wawe katika misuko suko tu ya hapa na pale.

Wanajua CDM ni sehemu muhimu ya UKAWA. Kwavile wamefanikiwa kunyamazisha baadhi ya sauti visiwani, watakapomudu kunyamazisha za CDM watakuwa wamekamilisha azama yao ya kuvunja UKAWA kwa maana mbili;

i) CCM kuendeleza uhalifu wa rasimu ya katiba baada ya nguvu ya UKAWA kupungua
ii) CCM kuondoa tishio la UKAWA kwa mustakabali wake siku za usoni.

Hivyo, zoezi linaloendelea sasa hivi likImhusisha Mchange lina madhara mbele ya safari.

Litatumiwa kuwakamata UKAWA kwa upande wa CDM na kuwaweka busy na kesi ili mambo yaendelee kama ilivyopangwa na CCM.

Kwa matazamo wa duru, tunawaaasa viongozi wa UKAWA na hasa CDM wawe tayari kwa matatizo ya kisaikolojia yajayo

UKAWA, nao wajiandae kusimama imara kutakapotokea mtikisiko uliokusudiwa. Imeanza znz na sasa ni bara

Tusemezane
 
MPANGO ULIOKUSUDIWA UMEKWAMA KIUFUNDI

KAULI ZA KUBEZA MADAI YA MADIWANI ZINALETA MKWAMO

UKAWA WAENDELEE KUWA MACHO. NGOMA BADO MBICHI SANA

Tutaenedeeleza shemu ya bandiko hapo juu.

stay tuned
 
MPANGO ULIOKUSUDIWA UMEKWAMA KIUFUNDI

KAULI ZA KUBEZA MADAI YA MADIWANI ZINALETA MKWAMO

UKAWA WAENDELEE KUWA MACHO. NGOMA BADO MBICHI SANA

Bandiko la awali tumeeleza jinsi ambavyo mambo 'yanaendeshwa' kiufundi hasa kipindi hiki cha BMK
Tulieleza yaliyojiri Zanzibar na tukio la kijana mmoja kwenda kwenye TV kutoa tuhuma za ugaidi.

Tulisema kijana huyo hakwenda kwa bahati mbaya na wala alichosema kilikuwa kwa bahati mbaya.
Tukatoa nadharia 3 zinazoweza kutumika kutokana na kauli za kijana na mwanachama wa zamani wa Chadema.

Nadharia ya tatu ilieleza jinsi gani kijana huyo anaweza kutumika kama shahidi kwa upande wa serikali.
Hiyo maana yake ni kuwa kinachofuata ni viongozi husika waliotajwa kukamatwa.

Kukamatwa kwa viongozi hao kuna lengo la kuwanyamazisha kama ambavyo yule mwingine wa visiwani alivyofanyiwa.
Siku si nyingi serikali ikatoa kauli ya kufuatilia madai hayo kwa undani hasa kumulika Chadema.

Duru hatuelewi kama ni mipango au ni bahati mbaya, iwavyo na iwe, tujue kuwa Chadema kuna jambo limewasaidia sana.
Kitendo cha kutoa mkanda wa video ya madiwani yenye tuhuma nyingi dhidi ya viongozi wa chama na serikali ya CCM ilikuwa karata kubwa sana.

Baada ya mkanda huo, jeshi la Polisi lilisema haliwezi kufanyia kazi habari za vyombo vya habari na kwamba hakuna aliyelalamika. Hilo limewafunga mikono baadhi ya wana mkakati wa kijana aliyetumwa Star TV.

Maana yake ni kuwa kwasasa kuna tatizo la kufanyia kazi habari za kijana aliyetoa madai.
Haiwezekani jeshi la Polisi likafanya uchunguzi kwa habari kama zile zile zilizotolewa na madiwani.
Hapo kutakuwa na double standard kwasababu hakuna mtu aliyelalamika nkuhusu tuhuma za ugaidi kama zilivyotolewa na kijana.

CDM WASIBWETEKE NGOMA BADO MBICHI

Itakuwa ni kosa kubwa kwa Chadema kama wataridhika na hali ilivyo wakitumaini kuwa ushahidi wa madiwani unaweza kuwa kinga dhidi ya madai ya kijana. Kwasasa inaonekana hiyo, lakini CCM watakuja na mbinu mpya.

Kuna uwezekano akatokea mtu mmoja na kulalamika akitumia maneno ya kijana Mchange. Mtu huyo anaweza kulalamika jeshi la polisi lifanye uchunguzi wa madai yaliyotolewa na kijana.

Hapo ndipo uchunguzi unaweza kufanyika na kuanza kamata kamata. Hoja kubwa itakuwa ni kushughulikia malalamiko yaliyotolewa na kijana Mchange kutoka kwa mhusika 'XX'.
Chadema watakapolalamika kwanini madai yao hayakufanyiwa uchunguzi, jibu litakuwa 'hakuna aliyelalamika''

Ni kwa muktadha huo, bado kuna tatizo na lisipoangaliwa litageuzwa na kuwaumiza CDM.

Yote haya yanatokea ili kupoteza mwelekeo wa watu kuhusu BMK.
Kwamba watu watajikita katika kujadili zaidi matatizo ya viongozi kuliko yanayoendelea Dodoma.

Huo unaweza kuwa ni mwanzo wa mwisho wa UKAWA. Kitakachotokea ni kuanza kuwagawa, kesi nyingi kuwaweka bize na kuingiza 'rupia' ili kurubuni baadhi yao.

Hivyo UKAWA waliangalie hili kama tatizo linalowahusu pia maana mkono haukamiliki kidole kimoja kikiwa hakipo au kinaumwa.

Tusemezane
 
Back
Top Bottom