Ndugu yangu Nguruvi uliyoyasema ndiyo haya yanatimia; umekuwa ni nabii wa ukweli, mwonaji wa maono halisi. Kinachoendelea ni kile ambacho mtu yeyote mwenyewe kufuatilia siasa za nchi yetu alipaswa kukiona na zaidi sana wale viongozi wa vyama vya kisiasa. Safari hii wamepewa maji na juisi; kana kwamba ugomvi wetu ulikuwa ni wao kunywa juisi! Wamekubali kunywa maji!
Binafsi naona hili ni kama suala la Sungura na ile sanamu yenye ulimbo. Walinasa kwenye juisi za kwanza wanajikuta wananasa tena kwenye maji; na huko mbeleni wataitwa tena na safari hii wanaweza kupewa na wine kidogo... Hata wakijiamua kujitoa sasa sijui kama watakuwa na hoja zaidi kama wangejitoa mapema zaidi...
Mkuu,viongozi wa vyama vya siasa naweza kuwafananisha kwa mfano wa mbwa wakali ndani ya mageti. Pindi wanapokutana na chatu, hukunja mikia na kuitumbukiza miguuni wakisubiri huruma na hukumu ya chatu''
Katika uzi huu,tumeonyesha jinsi walivyokwenda kunywa juisi wakiambulia machozi.
Mfano mzuri ni ule wa kuahirisha maandamano, wakati wakiwa wanapata maji ya matunda, JK anasiani mswada siku hiyo hiyo walioahirisha maandamano. Wakaishia kupata kinywaji baridi.
Tumewaeleza, haiwezekani JK aliyekwenda kuvuruga mchakato akawa na suluhu au sehemu ya suluhu ya tatizo.
Mfano, JK kaunda tume na kashiriki kila hatua. Mwisho kawaanika wazee katika TV kama ze comedy.
Leo viongozi hao wanategemea nini ikiwa tume aliyoiunda mwenyewe haikuweza kuipa heshima?
Tumewaeleza pia, haiwezekani JK aacheie tatizo liendelee kwa muda mrefu na ghafla ageuke kutafuta suluhu.
Tukasema, JK na CCM hali ni tata, wanachotaka ni mahali pa kutokea ili kukinusuru chama kwa kutumia vyama vya siasa
Mazungumzo ya Dodoma yameitishwa na JK baada ya hali kuzorota na kuashiria mwisho mbaya.
Haiwezekani JK akane tume yake, halafu apate suluhu na wapinzani.Kikao cha Dodoma kililenga kukwamua mchakato.
Ghafla, kikao hicho kimebadilika na lengo ni kutafuta mbadala wa kurekebisha katiba kwa ajili ya uchaguzi.
Tuliwaonya wapinzani kuwa haiwezekani kwenda kwenye meza ya majadiliano wakati bunge la CCM linaendelea.
Tukasema hivi: Ni mwafaka gani utakaofikiwa ikiwa JK alishasema S3 hadi aondoke.
Huyu kesha apa kuwa S3 haziwezekani. UKAWA wanataka rasimu yenye msingi wa S3.
Je, walikubali kwenda kujadiliana au kwenda kupindua kiapo cha JK kwanza?
Pili, Je, kama muafaka ungefikiwa, UKAWA wangerudi bungeni kuanza na mwanzo au kuendelea na bunge lilipofikia.
Tukauliza, kwanini JK kama ana nia ya muafaka, asisitishe bunge hilo hadi kupatikane suluhu?
Hoja kwamba hakuna sheria inayomruhusu ni mfu. Ilikuwaje BMK likaahirishwa kupisha kikao cha bajeti na kwanini vifungu husika visitumike katika mazingira tuliyokuwa nayo.
NINI KINAENDELEA DODOMA
Wapinzani wameundiwa kamati ikiongozwa na wao wenyewe, CCM wakiwa sindikizaji.
Vyombo vya CCM vinaendelea na propaganda,majadiliano si kukwamua mchakato ni kutenegeneza mazingira ya uchaguzi mwakani.
Tayari wapinzani wamepewa 'wine' wakati wanasherehekea mvinyo na kilevi kidogo mada imebadilika.
CCM wamebadili mada baada ya hali kuwa mbaya. Hivi sasa bunge la Sitta halifanyi kazi kukiwa na udanganyifu wa majadiliano ya kamati n.k. Ukweli ni kuwa hali ya kisiasa ndani ya bunge ina mvutano, uwezekano wa kupata 2/3 ndani na nje ya bunge haupo. Mbinu zinaendelea kurubuni wapatikane wajumbe 17 kwa pesa na kila hali.
Hivyo Sitta ana ''buy the time'' wakati idara husika zikiwa kazini.
Kwa upande mwingine, Dodoma, JK naye anawatumia wapinzani ku'buy time'' wakati mambo yanaendelea kuwekwa sawa.
JK ana option mbili, ya kwanza ni kusikiliza kama Sitta atafanikiwa kupata 17 ili uhalali uwepo na awamwage wapinzani.
Ya pili, ni hii ya kusema mjadala wa katiba haupo na sasa ni kuhusu uchaguzi.
Utajiuliza, kama JK anajua katiba is impossible kwanini atoe pesa za umma kwa kitu anachojua matokeo yake?
Karata anayocheza hapa ni kuangalia hoja hizo mbili. Hoja ya uchaguzi ndiyo atakayoitumia kuwafunga kitanzi wapinzani na kuifungua CCM katika kitanzi.
Wiki hii lazima litatoka tamko kutoka kwenye kamati ndogo huko Dodoma ikieleze kushindikana kwa mchakato na sasa ni suala la uchaguzi wa mwakani.
Atakayetoa kauli hiyo ni kiongozi anayeongoza kamati ambaye ni wapinzani.
Hilo litawaosha CCM na wapinzani kuonekana kama wameridhia mchakato kushindwa na wameafiki habari ya uchaguzi mwakani.
JK na CCM watakuwa off the hook.
Ni suala rahisi tu la kujiuliza. Hivi JK anawezaje kuwa mwema sana kwa uchaguzi na kinyume chake katika katiba?
Hivi anawezaje kuvuruga bunge, halafu akatengeneza mazingira mengine mazuri zaidi kwa wapinzani ya uchgauzi?
Hivi kulikuwa na ulazima gani wa kukutana na JK bila pre-condition ikiwa ni pamoja na kujua agenda, kusitisha bunge kwanza n.k.?