UKAWA wanavyobabaika: Historia ya 'juisi ya maembe' kujirudia?

UKAWA wanavyobabaika: Historia ya 'juisi ya maembe' kujirudia?

Kadiri 2015 inavyokaribia, na jinsi mchakato wa kumpata mrithi wa kiti cha magogoni unavyozidi na utatanishi, ndivyo suala la katiba linazidi kuwa kizunguzungu kwa CCM.

I wonder what was JK thinking when he came up with idea of Katiba mpya.
 
Kadiri 2015 inavyokaribia, na jinsi mchakato wa kumpata mrithi wa kiti cha magogoni unavyozidi na utatanishi, ndivyo suala la katiba linazidi kuwa kizunguzungu kwa CCM.

I wonder what was JK thinking when he came up with idea of Katiba mpya.
Alidhani angweza kuwafurahisha wahafidhina na wananchi, I mean ni mtu wa kutaka kupendeza kila mmoja. Akakacha kulifikisha suala hilo CCM, mambo yalipokuwa mazuri akalipeleka huko. Wahafidhina wakakataa, wananchi wakata tofauti.
Ndipo tuliona akisema watu wajiandae kwa ujio wa S3, ghafla akaenda kuvuruga bunge la katiba.

Suala la katiba lilihitaji busara I doubt kama anazo za kutosha. Kwa mwendo wa bunge lilivyo, hakuna shaka busara hazipo ni ulaghai unaotawala.
 
JK AEDELEZA MBINU ZA KUWADAGANYA UKAWA
AWATAKA WAENDE KUJADILIANA NAYE WAKIWA NA GLASI ZA JUISI
BUNGE ALILOOMBWA LIAHIRISHWE LINAENDELEA

JK ANA LIPI IKIWA ALISHASEMA S3 ZISUBIRI AONDOKE?


Rais JK juzi amekaririwa akiwa Morogoro akiwataka Ukawa waende kujadiliana naye.

Huko nyuma, UKAWA walimuomba aende kujadiliana nao bila majibu.

Hatua hiyo ya UKAWA tuliipinga hapa duru katika msingi kuwa aliyevuruga ni JK, vipi waende kumuomba asuluhishe alichokivuruga tena akijua ni makusudi?

Hatua ya JK kuwataka UKAWA waonane naye imekuja huku bunge lilikosa mvuto na kuonekana kama mazingaombwe.

Imefika mahali mwenyekiti Sitta ameunda tume yake kuchukua maoni bila kupewa haki na sheria yoyote.
Ameshakutana na wafugaji na makundi wa wakulima wa Pamba

Vikao vya Sitta ni vya kitoto maana havina minutes na wala havitambuliki kisheria.
Ni mikutano ya chai isiyo na maana kwa kuanzia na 'tume ya sitta' pamoja na wanaoalikwa.

Anachokifanya Sitta si kuandika katiba ya wananchi, ni kutaka kuungwa mkono ili tu aonekane ameweza hata kama anajua kuweza huko ni kwa gharama kubwa ya taifa siku za mbeleni.

Samwel Sitta hajali tena usalama wa nchi hii, anachokiangalia ni masilahi yake manono yatakoanyo na vikao vinavyoendelea.

Sitta anajua wazi ndoto zake za Urais zimefikia kikomo, haaminiki na wala haitatokea, si kwa chama chake.
Anachokifanya ni kukusanya milioni takribani 150 mwisho wa kikao, huko mbele Watanzania watajua wenyewe.

Ndani ya bunge la CCM Dodoma, hali si shwari. Taarifa zisizosemwa ni kuhusu kukinzana kwa hoja hasa za muungano.

Ndani ya kamati kumekuwepo na mpasuko mkubwa, huku baadhi ya wabunge 'wakijitoa mhanga' kama Mh Ali Kesi ambaye amewaunga mkono UKAWA na tume ya Warioba kuhusu muundo.

Wimbi hilo litajitokeza wazi katika mijadala na sasa ni wazi kuwa hata ndani ya CCM-Bunge maalumu kuna mpasuko.

Kila muundo unaopendekezwa unaelekea kule kwa tume ya Warioba. Kukwepa hilo imekuwa kazi kubwa.

Ndani ya CC ya CCM wajumbe wa znz ndio wamekuwa kikwazo cha S3. Wao hawataki kusikia S3 kutokana na matatizo yao wenyewe ambapo muundo wa S2 wanauona una masilahi kwao kiuchumi, kijamii na hasa suala la mapinduzi.

Katika hali hiyo JK anajikuta akikumbana na nguvu ya umma, ndani ya CC, BMK la CCM na nguvu kubwa sana kutoka kwa makundi ya kijamii hasa wasomi wanaouona mchakato kama kituko kingine cha awamu hii.

JK anajaribu kwalaghai UKAWA ili aongee nao. Lengo ni kuwafiriji kuwa malalamiko yao yatasikilizwa.

Hiyo ndio mbinu yake, kwamba baada ya CC ya CCM kutaka mchakato uendelee, JK anataka kuwafurahisha UKAWA kwa kilemba cha UKOKA.

KWANINI UKAWA WAJIANGALIE

Juzi CC ya CCM chini ya kikwete imeamua mchakato uendelee

Ndani ya Bunge la Sitta, kanuni zimebasilishwa na sasa wanaongeza sura zile za rasimu ya mafichoni ya CCM
https://www.jamiiforums.com/great-t...-za-ccm-kuingiza-katiba-yao-ya-mafichoni.html

Katika hali hiyo UKAWA wajiulize

1. Iweje JK juzi aongoze CC kutoa msimamo wa kuendelea na siku 3 baadaye awatake UKAWA warudi katika majadiliano?
Ni majadiliano gani wakati CCM inaendelea na mipango yake tena ikiwa na tume ya Sitta ya kukutana na wafugaji/wakulima n.k.?

2. Je, UKAWA wakirudi, kanuni alizobadili Sitta zitakuwa zile zile za awali au itabidi wafuate zilizopo?
Na kama watafuata za sasa ni vipi watakwepa mkumbo wa kuchomeka vifungu vya maoni yasiyotokana na wananchi?

3. Na je, UKAWA wakirudi na Sitta kugoma kuwasikiliza, watarudi vipi kwa wananchi na kuwaeleza walisusia nini na walikubali nini na sasa wanasusia nini? Je hapo hawtaakuwa wamejichanganya na kuonekana hovyo?

Ni kwa muktadha huo, vikao vya Jaji Mutungi au JK na UKAWA ni dharau.
Haiwezekani bunge likawa linaendelea wakati kuna majadiliano.

JK alikataa kuahirishaau kuvunja bunge. Sitta kabadili kanuni na taratibu.

UKAWA lazima wawe makini, vinginevyo wanaweza kuambulia juisi za maembe kama kawaida

Tusemezane



cc MJINI CHAI
 
Last edited by a moderator:
Mkuu @Nguruvi3, kama nilisikia vizuri taarifa ya Mh. Cheyo, hakumaanisha Raisi anakutana na 'UKAWA' bali atakutana na viongozi wa vyama vya siasa. Kama ulivyosema hapo awali kwenye uzi huu, tusitegemee jipya, ile hadithi ya juisi ya maembe itajirudia.
 
Mkuu @Nguruvi3, kama nilisikia vizuri taarifa ya Mh. Cheyo, hakumaanisha Raisi anakutana na 'UKAWA' bali atakutana na viongozi wa vyama vya siasa. Kama ulivyosema hapo awali kwenye uzi huu, tusitegemee jipya, ile hadithi ya juisi ya maembe itajirudia.
Mkuu Kakalende, ni kweli, alichofanya ni kuepuka neno UKAWA ili kutolipa uzito unaostahili, na pili kulifanya kama tatizo la vyama vya siasa.

Hivi atakutana na Mrema na Hamad Rashid wa ADC ili iweje ikiwa tayari wapo Dodoma?

Ndio maana tunasema hakuna ukweli wa kumuamini. UKAWA wakikaa tenge, wanaletewa majagi ya juisi ya maembe ya kiwangwa na mchezo unaishia hapo.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu nguruvi

Ni kweli kabisa kwa mazingira yalivyo sasa ni very tricky. UKAWA hawawezi kukataa wito huu wa Rais kwa hio mwisho wa siku wataenda kukutana nae...muhimu hapa ni kwamba wakienda huko lazima wawe na ajenda na msimamo wao juu ya nini kinapaswa kufanya. Wamshauri Rais asitishe mchakato huu kwa sasa ili tuanze upya...
 
Last edited by a moderator:
Mkuu nguruvi

Ni kweli kabisa kwa mazingira yalivyo sasa ni very tricky. UKAWA hawawezi kukataa wito huu wa Rais kwa hio mwisho wa siku wataenda kukutana nae...muhimu hapa ni kwamba wakienda huko lazima wawe na ajenda na msimamo wao juu ya nini kinapaswa kufanya. Wamshauri Rais asitishe mchakato huu kwa sasa ili tuanze upya...
Mwalimu, UKAWA wana kila sababu.

1. Wakienda wamuulize Rais kuwa ile kauli yake ya kuwa ''S3 zisubiri aondoke'' ipo pale pale au ameifuta?
2. Rais anataka UKAWA wafanye nini ikiwa bunge linaendelea na kanuni zimebadilishwa na kila kitu
3. Hawa mawaziri wa JK wanoongea kila siku, wanafanya hivyo kama watu binafsi au viongozi wa serikali.
4. UKAWA wamuulize, je warudi bungeni kujadili kitu gani, rasimu ya tume ya Warioba au rasimu ya tume ya Samwel Sitta(wafugaji)
5. Wamuulize kama JK anaongea nao kama mwenyekiti au Rais. Kama ni Rais CCM wapo wapi? maana usuluhishi ni pande mbili.
6.
 
TULIYOSEMWA DURU ZA SIASA YAANZA KUTIMIA

BMK-CCM KAZI KUBWA NI KUWAFURAHISHA WAZANZIBAR

HUWEZI KUFURAHISHA WZNZ UKAUDHI WENYE MUUNGANO

SASA MUUNGANO UNAKARIBIA KUVUNJIKA KAMA GLASS


Mabandiko ya duru yanayoendelea, tulisema lengo la CCM si kuandika katiba ya nchi, ni kuwafurahisha wazanzibar wakubaliane na mfumo wa S2

Rais JK ndiye aliyefungua pazia, kwa kuwapa wazanzibar kila walichodai.
Sasa wanaondoa vifungu vya katiba watakavyo, wanapewa zawadi zisizo na audit, fursa n.k

Wazanzibar wakakuvunja katiba ya nchi, hakuna wa kuwafanya lolote.
JK akawapa haki znz 1.2 Milioni,wachache kuliko wananchi wa Ubungo sauti na nguvu katika muungano.

Kwasasa wznz wana malalamiko mengine ambayo ni Rais wa znz kuwa makamu wa rais wa JMT.

Hii maana yake Rais wa JMT atakapokuwa hayupo, atakayekaimu nafasi yake ni Rais wa SMZ.

Rais wa SMZ hachaguliwi na rais yoyote wa Tanganyika.

Ni sawa na kumchukua Rais Uhuru wa Kenya kukaimu nafasi ya Urais nchi ya Tanganyika.

Hili ni kuwafariji wznz ili wakubali mfumo wa S2 ambao kimasilahi hauna tija wala faida kwa Watanganyika.

Hali hii inaleta hasira za kuwadhalililisha na kuwadharau Watanganyika katika hali isiyoweza kuvumilika.

Hakuna Mtanganyika anayeingia SMZ kwa bahati mbaya, kuchaguliwa au kuteuliwa. Leo tumefika mahali tunakabidhi nchi yetu kwa mamluki wa znz.

Zanzibar hawajitambui kama Watanzania, wapi wanaweza kuja kutawala Tanganyika?

Kinachofuata ni kukaribisha hasira zaidi, kuamsha damu zinazochemka dhidi ya uonevu huu unaofanywa na watu 1.2 ambao nusu yao wanaishi Tanganyika.

Kimsingi, watu wapato laki 4 wanaamua mustakabali wa Tanganyika ambao ni milioni 43.

Ni kwa mtazamo huu, CCM wanacheza karata ya hasara, hatari nay a kusikitisha.

Pamoja na BMK-CCM kukosa uhalali, nia ya CCM kuwadhalilisha, kuwatusi na kuwakashifu Watanganyika inaeleza sababu za msingi za Watanganyika kutetea nchi na utaifa wao.

majadiliano yanaonekana kuendeshwa kwa hila, ubabe na maguvu, CCM watambue muungano unaelekea kuvunjika muda mfupi sana ujao.

Hakuna mahali duniani dola ilishinda nguvu ya umma.

Nguvu ya Umma ya Watanganyika ni kubwa mara 30 ya wazanzibar.

Watanganyika wataingia mitaani kudai haki zao kwa nguvu.
Wazanzibar watabeba gharama nzito sana wakati unaoelekea kutimia

Watanganyika hawatavuka bahari, watawalazimisha wznz wavuke bahari kwa miguu na baiskeli.

Hali inapoelekea ni mbaya sana kwa wznz.

Zawadi wanazoahidiwa wazaznibar ni tamu kama big G, maana ipo siku zitakuwa shubiri midomoni mwao. Siku si nyingi, watazitema wakitoka mate, jasho napengine zaidi ya hayo

Hatari hii haionekani, inakuja kimya kama dhoruba. Inatisha na inasikitisha.

Tusemezane

 
UKAWA KUKUTANA NA JK KWA JINA LA TCD

UKAWA WAGEUZIWA KIBAO NA KUSINGIZIWA

TCD ITAKUJA NA SULUHU GANI YA KISHERIA?


Habari zilizopamba magazeti ni kuhusu ''uungwana' wa Rais Kikwetekukutana na vyama vya siasa.
Habari zimegeuza ukweli ya kuwa aliyetaka kukutana na UKAWA kwa jina la TCD ni JK na si vinginevyo

Katika kuhakikisha janja inatumika, imesemwa rais anakutana na vyama vya kisiasa kupitia TCD kituo cha demokrasia.

TCD imetumika kukwepa fedheha ya JK aliyewaponda wapinzani na sasa 'anawapigia' magoti kiaina.

Kusema JK anakutana na UKAWA kungeleta dhalili na hivyo likatumika jina TCD

TCD ni jina kwasababu CCM ni mwanachama na yupo bungeni, mapalala na Chausta wapo bungeni, Mrema na TLP wapo bungeni, Hamadi Rashid na ADC wapo bungeni, Kuga Mziray na PPT wapo bungeni.

Ukweli ni kuwa JK anakutana na UKAWA kwa jina bandia, lakini huo ndio ukweli.

Kinachomsukuma JK ni baada ya kubaini nguvu ya umma inavyozidi kumbana na ukweli kuwa kuna uwezekano wa asilimia 80 kukosa muafaka katika bunge la CCM, kura za maoni au kuvurugika kabisa hata bila kuwa na pa kuanzia.

Ili kupeusha balaa hilo, propaganda zimeanza kutumika kwa kutumia viongozi wa dini.

Tayari viongozi wa kikristo kupitia taasisi zao na wale wa kiislama wametoa matamko ya kusifu uungwana wa kikwete.

Wasichojiuliza viongozi hao ni mambo haya
1. Nani alivuruga mchakato, na kwanini hawakumkemea JK alipokwenda kutibua Dodoma
2. JK alipoambiwa akutane na wapinzaini alikataa,uungwana unatoka wapi ambao ulikosekana mwezi mmoja uliopita
3. JK aliposhauriwa aahirishe bunge amekataa, leo uungwana upo wapi wakati bunge linaendelea?
5. Kwani tatizo ni kukutana au ni sababu za kisheria na kanuni?
6. Kwanini wapinzani hawakupongezwa walipotaka JK aingilie kati miezi 5 iliyopita baada ya sntofahamu

Viongozi wa dini wanatumika na nyakati hizi dini zinageuzwa kuwa miradi.

Hilo UKAWA walitambuePindi maridhiano yatakaposhindikana, na hakika yatashindikana hoja iwe juu ya UKAWA kutokuwa waungwana kama JK

Lakini pia UKAWA wajiulize. Hivi JK wanaenda kukutana naye ili iweje?

1. CCM wamepindisha sheria kwa maelekezo ya JK, sasa UKAWA wanategemea nini kuanzia hapo
2. Kifungu chenye utata ni cha kisheria na utata huo umetengenezwa na CCM, JK akiona. UKAWA wategemee nini?
3. JK keshawaambia S3 hadi aondoke, tume imepedekeza S3, CCM wanaendelea na S2 sasa UKAWA wategemee nini
4. Hivi kwanini UKAWA wadhani kuwa JK anadhamira njema katika hali ya kuachia akina Sitta wajiundie tume zao?
5. UKAWA watarudi bungeni kuanzia wapi, pale walipoondoka au hapo walipo sasa?

Ukiangalia hali ilivyo, hakuna shaka ni ulaghai tu unaoendelea.

UKAWA watapewa juisi, watarudi bungeni wakitegemea JK aliyemwaga Warioba na Salim utupu, anaweza kuwa muungwana kwao.

Laiti nginekuwa mmoja wa UKAWA nisingehudhuria mjadiliano hayo, na kama ingebidi ningeuliza maswali matatu tu na yakikosa majibu naondoka katika chumba cha mkutano na kuwaacha CCM na vibaraka wao waendelee kama wanavyotenda Dodoma.

Ningeuliza maswali haya
1. JK, je bado unaamini S3 ni hadi uondoke madarakani au umefuta kauli na kuomba wananchi radhi
2. JK, hivi uliunda tume ya kukusanya maoni kisheria, nini hatima ya maoni ya wananchi Vs maoni ya bunge
3. UKAWA warudi kujadili nini bungeni, Rasimu ya Warioba kama ilivyo au Rasimu ya Sitta kama anavyokusanya maoni

Maswali hayo yangekosa majibu, dakika 30 nigeondoka katika mkutano ili nisijeambiwa nimeshirika majadiliano na kukataa.

UKAWA wasipokuwa waangalifu,wapinzani walioletwa na CCM wanaweza kuja na mkakati mpya, kwamba sasa ni suala la vyama kupiga kura kuamua hatima. Ndipo UKAWA watajikuta katika wakati mgumu.

Duru tunasema majadiliano na JK hayana tija, ni afadhali utafutwe muafaka wa kisheria bunge likiwa limesitishwa kwa muda.

Tusemezane
 
TULIYASEMA KATIKA DURU (Bandiko 227,229)

WAZANZIBAR WATAPEWA PIPI, WATANGANYIKA WATACHUKIZWA

GOGORO ZITO LAZIZIMA CCM, ADUI HAYUPO SASA NI WAO KWA WAO


Wanajamvi, imekuwa ni ada kuangalia mambo kwa jicho la tahadhari na fikra.
Huko nyuma tuliandika CCM ni wamoja, adui yao UKAWA akiwepo.

Baada ya kuondoka, CCM watavurugana.Tulieleza sababu za kuvurugana na makundi yatakayovurugana.

Kamati za BMK-CCM zimemaliza kazi. Mambo mengi yameachwa kutokana na mgogoro au kutofautiana.
Hoja zimewagawa CCM-Bara na CCM-Zanzibar na kundi teule la CCM-Whafidhina(Rejea mabadiko 227,229).

Masuala yanayowatenga ni mfumo wa muungano, na mambo ya muungano.
CCMwahafidhina kazi yao ni kutoa pipi kwa Wazanzibar. Mfano, wameamua suala la ardhi liwe la muungano.
CCM-Bara wanasema hilo hapana, ikiwa ni hivyo basi na ile ya znz iwe pamoja.

Kuhusu kugawana mapato, gharama na matumizi hilo nalo limeleta mzozo.

CCM-Zanzibar wanataka kupata mgao mkubwa, huku wakikataa kuchangia.
CCM-Bara wanasema, hapana, hilo ni kero kwa Waanganyika na hawataeleweka mbele ya safari
Wahafidhina wanasema wapeni wazanzibar wanachotaka.

Suala la mfumo wa bunge nalo linaleta matatizo
CCM-Bara wanasema wazanzibar hawana sababu za kujadili mambo ya Tanganyika, la sivyo nao wawe na wajumbeB LW

CCM-Zanzibar wanasema wana haki kwa sababu ni bunge la JMT. Hawataki mjumbe yoyote kuingia BLW znz

Wahafidhina wanasema, wabunge wa znz waje tu hata kama hawana kazi. Kwao ni kutoa pipi ili kuwaridhisha.

Kutokana na mvutano huo, kumetokea kundi la Watanganyika wenye uchungu na hila zinazofanywa.
Kundi hili linatofautiana na CCM-Zanzibar na Wahafidhina.

Wakati CCM-Zanzibar wakidai zaidi ili wapewe uhalali kule visiwani na kuua hoja ya S3, wahafidhina wanawaunga mkono ili kufanikisha azma zao za kisiasa.

CCM-Bara wanapandwa na hasira kwa hatari inayowakabili mbele ya safari kama wataruhusu mambo yaende na kufarijiana.

Kamati zinaanza kujadili rasimu ya CCM.Kama CCM walidhani litawajenga, sasa ndio wanaelekea kubaya zaidi.

CCM wamedanganyana kuwa umma upo nyuma yao. Kuna kila ushahidi kuwa umma una hasira dhidi yao.

CCM-Bara wanaonekana kuchoka na kudekezwa kwa wazanzibar.
Wanahisi wazanzibar wamepewa kila wanachotaka na sasa wanadai hata kisicho chao.

Kundi hili la CCM-bara halipo wazi lakini katika mjadala litajitokeza.
Zile hasira za pande mbili zilizojificha kwa kofia ya chama zitafumuka na hapo patachimbika.

Ni kwasababu hizo, jana mwenyekiti wa Bunge la katiba ya CCM mh Sitta alitoa onyo kali kuwa lugha chafu hazitavumilika.

Sitta anajua undani na uhasimu uliopo, anachokifanya ni kujaribu kuzuia hayo yasitoke nje.

Asichokitambua Sitta ni kuwa ndani ya CCM wapo wazalendo wanaopenda Tanganyika yao au Zanzibar yao.
Kunawezekana kuwanyamazisha kwa masaa machache, itahitaji kauli ya mtu mmoja tu, tutaona vumbi litakavyotimuka.

Kauli hiyo itakayowasha moto haitatoka Zanzibar, itatoka kwa CCM-Bara kwasababu moja kubwa; wana reservation yaani kinyongo na uchungu wa jinsi mambo yanavyoendeshwa na hatima yao mbele ya mahakama ya wananchi.

Sitta na mbinu za kizamani......................Inaendelea
 
SITTA NA MBINU ZA KIZAMANI

AJARIBU KUFICHA KICHWA MCHANGANI MGONGO NJE

NI KIWEWE CHA BUNGE KUVUNJIKA MIKONONI MWAKE, CCM KUPARAGANYIKA

Kauli ya Sitta kuwaonya wajumbe kuhusu lugha inatokana na majadiliano ndani ya kamati za bunge la katiba ya CCM.
Sitta ametumia mbinu za kizamani kutaka kupoza hasira ambazo taratibu zinaanza kujitokeza.

Kitendo cha mbunge wa CCM kuwakana mawaziri mbele ya waandishi wa habari ni dalili njema kuwa sasa uvumilivu umewatoka.

Kilichowaweka pamoja katika kura ya wazi ni kukabaliana na UKAWA
UKAWA hawapo na hakuna tena kura ya pamoja, ni kura ya CCM dhidi ya CCM

SItta amepanga kamati za CCM kwa kuangalia zile zenye wajumbe dhaifu zianze kwanza ili kutoa taswira mambo ni mazuri. Asichokielewa mzee huyu ambaye busara ni bidhaa adimu kwake ni mambo yafuatayo.

Hoja za muundo wa bunge, mgawanyo wa mapato, matumizi, uchangiaji na rasilimali ndizo zilizopo mbele.

Wananchi wataliangalia bunge si kwasababu lina maana bali kwa hoja moja kubwa;

Ni vipi CCM itaweza kugeuza rasimu ya Warioba kukidhi matakwa, haja na matamanio yao.

Ieleweke wananchi wana hasira, hivyo udadisi wa (curiosity) yao itakuwa katika mtizamo wa rasimu ya Warioba.

Mfano, kutakuwa na mabunge mangapi na vipi mabunge hayo yatatofautiana na rasimu ya Warioaba.

Kutakuwa na kuchangia vipi gharama na wala si kugawana madaraka na vyeo

Kutakuwa na mambo gani muhimu zaidi au pungufu ya yale ya rasimu iliyotupwa ya Jaji Warioba

Udadisi huo utawasukuma wabunge wa pande zote mbili bila kujali kamati gani inaanza kujadili kwa kina.

Wabunge wa kuchaguliwa wa CCM wapo katika hali ngumu na mbaya ikizingatiwa mahakama ya wananchi inawangalia

Wabunge wa kuteuliwa hawana cha kupoteza na hivyo liwalo na liwe na pengine huo ndio utakuwa muda wa baadhi yao kuanza kujijenga kisiasa.

Kwa mweleko ulivyo, utetezi wa wananchi na masilahi ya kila upande yatakuwa mbele ya agenda.

Ndio maana tunasema hata aanze na kamati laini kiasi gani, wananchi wa zama hizi si wa kudanganyika.

Tatizo litakuwa ni ubabe wa Sitta. Of course hana cha kupoteza tena kwasababu keshapoteza kila kitu.

Itakapofika anawaletea ubabe wabunge wa CCM hasa bara hapo kutakuwa na hatari kubwa.
Sitta ni mpenzi wa wahafidhina na hivyo atataka kuwapendeza wznz. Hilo litakuwa tatizo.

Sitta haelewi kuwa muungano haungaliwi tena kwa jicho la kero za muungano.

Unaangaliwa kwa jicho la kero za Wazanzibar. Hili litaibua mengi ambayo wazanzibar hawatakuwa na utetezi nayo.

Na hapo watahamaki na ndio utakuwa mwanzo mzuri sana wa safari mpya ya ujenzi wa taifa, mwanzo wa mwisho

Hata kama CCM wataridhishana mambo yaende sawa, mbele ya mahakama ya wananchi hakuna mbunge atakayesimama kutetea chama akabaki salama. Wengi watakwenda na maji na wanajua hivyo.

Itakuwa ni kutetea nafsi zao. Kura za maoni sijui zitazaa nini kama hakuna msaada wa tume ya uchaguzi

Kwa upande wa znz, jitihada zao ni kutaka kuonyesha wamepata zaidi ya kile CUF wanachokisema.

Watajikuta wanapabana na hoja za gharama za muungano bila majibu.

Hoja zao za kutaka vyeo, nafasi za ubalozi, mikopo na misaada zitaonekana nyanya na dhalili.

Hadi sasa wznz hawana hoja ya msingi ya kudai zaidi katika S2 kwani kila walichodai, JK amewapa.

Watabaki kujenga hoja za maudhi na hilo litasaidia sana safari ya nchi yetu.

Haya yanayotokea katika bunge la waovu la CCM ni uovu. Kwa mtazamo mpana huenda ukwa mpango wa mungu.

Kuanzia leo hadi Ijumaa tutawaletea mabandiko yakionyesha timbwili in the making, the beginning of the end.

Tutawalete nyeti kutoka vyanzo vyetu vya uhakika ndani ya kamati.

Tusemezane
 
ZENGWE LAANZA KUWADHIBITI CCM'WAKOROFI''

NAPE ATUMA SALAMU KWA BMK-CCM. TUTAWATIMUA
!

Hapo juu tumeeleza jinsi Samwel Sitta alivyotoa vitisho kuhusu lugha kali.

Habari za uhakika kutoka ndani ya kamati zinasema suala la muungano na muundo wake lilileta tatizo kiasi cha Watananganyika kuhasiamiana na Wazanzibar kwa lugha nzito zinazoashiria shari mbele ya safari.

Kauli ya Sitta ilikuwa ni funika kombe mwanaharamu apite. Bahati mbaya mwanaharamu UKAWA hayupo,

Mwanaharamu aliyebaki ni Wananchi. Sitta haamini katika usemi wa wahenga 'you can foll some people for sometime, you can't fool all people at all the time''

Jana, Nape Nanuye naye kaja na zengwe lwa kuwaadabisha wabunge wa CCM walioshindwa kuhudhuria vikao.

Hili linashangaza kwasababu,Nape alipaswa kuchukua hatua kunusuru kamati za BMK-CCM zifanye kazi vema kama ndio nia yake. Hakuchukua hatua hizo.

Leo anaposema anawawajibisha, si kweli.

Ukweli ni kuwa anapeleka ujumbe kwa wajumbe wa CCM''Wakaidi' kuwa CCM itawachulia hatua wale watakaokiuka msimamo wa chama. Kwamba, wanatakiwa waseme 'ndio mzee' na matumizi ya vichwa vyao ni uharamu ndani ya chama.

Ujumbe wa Nape umelenga kuweka msisitizo kwa ujumbe wa Sitta, kwamba sasa wanaungana ili kuleta zengwe, kuwatisha CCM mambo 'yanyooke''.

Hilo wanaweza kufanikiwa kwa kuzingatia kuwa huwezi kuwa mbunge wa CCM bila kukabidhi akili zao mtaa wa Lumumba.
Na kama unatumia akili basi utakumbana na zengwe la Sitta na Nape la vistisho.

Swali wasiloweza kujiuliza, je watafanikiwa kwa akili za wananchi milioni 43 wanaotumia fikra zao mbali na mtaa wa Lumumba.
Hata kama katiba yao ya CCM itapitishwa kwa wizi na hujuma, bado kuna hoja moja,tatizo litakuwa kubwa kuliko wanavyodhani.

Ukubwa wa tatizo ni pale wabunge wao watakapokutana na nguvu ya umma.

Ni pale ambapo CCM itakuwa imewapa wapinzani silaha nzuri sana.

Huenda bunge lijalo CCM ikawa haina 2/3 na hoja ya katiba ikarudi tena CCM ikiwa haina udhibiti.

Hata kama wataiba uchaguzi kwa utaratibu waliojipangia miaka mingi, Rais ajaye atafanya kazi katika mazingira magumu sana.
Nguvu ya umma itatamalaki tu na CCM inaweza kupeleka salamu zetu kwa KANU na UNIP

Mchezo wanaocheza ni mbovu sana kwa mustakabali wa chama chao na na nchi.
Mbinu wanazofanya zitawaumbua mchana kweupe. Ni suala la muda tu.

Gogoro lililotokea ndani ya kamati tatu kuhusu matumizi, mgawanyo wa mapato na uchangiaji ni zimwi linalosubiri kutoka kwenye chupa. Siku likitoka mganga si CCM maana watakuwa nalo washabiki mtaani wakiliekeza wanakotaka.
Muungano taabani, CCM mahaututi.

Hapo S2 zitakuwa zimefikia mwisho, muungano utasomewa matanga huku watu wakijiandaa kusoma 40 ya CCM.

Katika uovu unaoendelea Dodoma, kuna faraja itapatikana.

Mungu ni mwema kwa waja wake. Huenda huu ni mpango wa mwenyezi mungu.

Tusemezane
 
CCM NA SAMWEL SITTA HOFU YAWATAWALA

SASA WATUMBUKIZA KARATA YA DINI

MWISHO WA KARATA HIYO YAWEZA KUTOKEA MAAFA

Hofu inazidi kwa CCM na Mwenyekiti Sitta wa BMK-CCM. Jitihada kutoa zawadi kwa wazanzibar zinakwama. Jana kamati zimeshauri kuwe na makamu wawili, Rais wa znz akiwa ni makamu pia wa JMT.

Hoja ilikumbana na hoja ya wazanzibar waliosema yaraka inayoandaliwa haitakanyaga ardhi ya Zanzibar.
Tayari makundi tuliyoeleza yanaanza kutoa makucha. Hadi Ijumaa ya wiki ijayo,uwezekano bunge la CCM likavunjika kwa wenyewe kupigana madongo.Tunasisitiza kwa vile UKAWA hawapo, vita ni ya familia.

Kutokana na hofu hiyo inayoonyesha na wajumbe wa CCM 'wakorofi''Sitta amekuja na mbinu ya kuwatumia viongozi wa dini. Viongozi wametoa tamko kama wajumbe wanaowakilisha taasisi za dini kundi 201

Kwanza, kuna tatizo la viongozi. Wamejichagua kama wakristo na Waislam, wakiacha makundi mengine yenye uwakilishi wa imani

Pili,hawawezi kutoa misimamo tofauti na ule wa taasisi zilizowatuma zenye mitazamo tofauti na yao

Viongoziwa dini wamekuja na hoja zisizoeleweka, kwa umakini unaweza kuona wameagizwa kwa 'motisha'

Tamko lao linafuatia tamko la Sitta na Nape ikiwa ni kuashiria hali ni tete na hivyo msaada wa viongozi wa kiroho unatakiwa.

Moja ya utetezi wao ni madai kuwa wao ni viongozi wa kiroho na wameapa kwa mwenyezi mungu na kwa katiba.
Wanachotaka tuamini ni kuwa, wakiwa viongozi wa dini ni watu wema na kauli zao ni njema

Duru tunajiuliza kama viongozi wa dini ni watu wema sana mbele ya mungu, iweje tunasikia makanisani wakichapana makonde kwa kutaka madaraka au kula sadaka?

Iweje tunasikia masheikh wakishikana wizi wa sadaka na misaada?

Iweje tunasikia makasisi na maustadhi wakikamatwa ugoni?

Iweje hawa viongozi hawaogopi makanisa na misikiti yao, leo watuambie mungu amehamia Dodoma mjengoni kwa Sitta na hivyo wao ni watu wema sana na tuwasikilize?

Iweje hawakutoa tamko kuhusu kuvurugwa kwa mchakato kuanzia mwanzo na kwamba haki ilikiukwa hata kwenye kanuni?

Iweje hawakukemea kitendo cha prof Ghai kupewa siku nzima ya kuzungumza na Warioba na tume yake waliozungumza na mamilioni ya Watanzania wapewe saa moja? Mbona hatukuwasikia wakikemea uhalifu huo leo wanataka tuwasikilize!!

Hawa viongozi ni sehemu ya mpango wa kisiasa. Madai yao dhidi ya UKAWA ni ya kupangwa na kutumwa.

Tatizo linalojitokeza ni kuhusu kuchanganya dini na siasa. CCM inawapa nguvu kwa mambo ya kisiasa.

Kesho zitazuka hoja zinazogusa imani,watatofautiana na haieleweki CCM watamtafuta nani asaidie kuwasuluhisha.

Hili jambo ni la hatari kwasababu nchi inapogawanyika kwa imani na kutoka katika secular state inatisha na kusikitisha.

Karata hii ya Samwel Sitta ni hatari sana kwa taifa.

CCM lazima wajiulize je, wana magari ya zimamoto ya kutosha siku moto utakapowaka?

CCM hawaoni ya jirani zetu au barani Afrika, na wanafikiria nini kuhusu mustakabali wa taifa hili.

Tusemezane
 
Alidhani angweza kuwafurahisha wahafidhina na wananchi, I mean ni mtu wa kutaka kupendeza kila mmoja. Akakacha kulifikisha suala hilo CCM, mambo yalipokuwa mazuri akalipeleka huko. Wahafidhina wakakataa, wananchi wakata tofauti.
Ndipo tuliona akisema watu wajiandae kwa ujio wa S3, ghafla akaenda kuvuruga bunge la katiba.

Suala la katiba lilihitaji busara I doubt kama anazo za kutosha. Kwa mwendo wa bunge lilivyo, hakuna shaka busara hazipo ni ulaghai unaotawala.

Mkuu i really wonder what kind of decision making mechanisms we have here in Tanzania. Unajua toka tuanze kufuatilia suala la katiba mpaka sasa naona kuna udhaifu mkubwa kwenye kufanya maamuzi makubwa na ya maana yanayohusu nchi yetu.

Kwanza kwenye katiba naona mambo ya ajabu sana. Toka ulipoanza kutu-update maendeleo ya suala hili bado sijaona lolote la maana kutoka kwenye bunge letu, zaidi ya sarakasi za kijinga na wana CCM kuiweka CCM mbele kuliko Tanzania.

Kuna issues nyingine nyeti zinazohusu uchumi na usalama wa Tanzania katika miaka 50 ijayo, naona zote wako mute, as if things are very good.

Nimeshangaa sana kusikia upuuzi wa suala la uraia pacha, hata sikuamini.

In the end naona JK aliamua kuchagua vilaza kwa makusudi ili wasukumwe tu kufanya maamuzi yanayoinufaisha CCM.
 
Mkuu i really wonder what kind of decision making mechanisms we have here in Tanzania. Unajua toka tuanze kufuatilia suala la katiba mpaka sasa naona kuna udhaifu mkubwa kwenye kufanya maamuzi makubwa na ya maana yanayohusu nchi yetu.

Kwanza kwenye katiba naona mambo ya ajabu sana. Toka ulipoanza kutu-update maendeleo ya suala hili bado sijaona lolote la maana kutoka kwenye bunge letu, zaidi ya sarakasi za kijinga na wana CCM kuiweka CCM mbele kuliko Tanzania.

Kuna issues nyingine nyeti zinazohusu uchumi na usalama wa Tanzania katika miaka 50 ijayo, naona zote wako mute, as if things are very good.

Nimeshangaa sana kusikia upuuzi wa suala la uraia pacha, hata sikuamini.

In the end naona JK aliamua kuchagua vilaza kwa makusudi ili wasukumwe tu kufanya maamuzi yanayoinufaisha CCM.
Mkuu tatizo la JK ni popularity. Yaani hawezi kuchukua maamuzi bila kuangalia ataudhi au atafurahisha watu wangapi. Ni kutokana na hilo taifa linakuwa na ombwe la uongozi.

JK alipochagua hao wabunge, kwanza aliongozwa na idadi ya watu watakaofurahia uteuzi wake na si weledi wa wateuliwa
Pili, akaongozwa na namna ya kufahisha makundi ya watu ndani ya CCM na si taifa kwa ujumla wake.

Suala zima la katiba ni la kitaifa. JK alipaswa kuongoza kwa kuonyesha njia, ya kuwa hili ni suala nyeti linalogusa sana taifa letu leo na miaka 50 ijayo katika maeneo uliyosema ya uchumi na usalama.
Yeye akaongaza kutoa ruhusa za CCM kutenda watakayo tena akisema wengi wapewe wachache wasikilizwe.

Huwezi kusikilizwa tu, ni lazima usikilizwe na upimwe bila kujali wingi.

JK akaongoza kamati kuu ya chama chake na kuwafunga wabunge wa CCM matarambara midomoni.
Ilipaswa awape uhuru wa kusema kwasababu wana andaa nyaraka ya nchi na si chama.

Sasa hivi anacheza na muda ili nafasi ikitokea katiba ya CCM ipitishwe. JK hajali hata kama katiba hiyo itapingwa, itakosa maridhiano na uhalali wa kisiasa. Yeye keshasema S3 zisubiri aondoke. Maana yake ni kuwa kuna mambo yanapaswa kusubiri aondoke. Kwamba leadership yake iache viporo. Huku ni kukosa '' boldness' yaani uthubutu wa kukabiliana na mambo ya kitaifa.

Hao wabunge wanaongozwa na pesa tu bila kujua athari za maaumuzi wanyoyafanya kwa vizazi vyao.

Nchi ina deni, hakuna anayejadili namna gani tutazuia matatizo hayo siku za usoni
Nchi haina maadili, watu wanakuja kutoka wanakojua wanapewa miradi na kuiba halafu tunaambiwa wamekamatwa airpot wakitroka. Hivi waliwezaje kuja na kupewa miradi bila ushirika na wazawa. Hakuna maadili na CCM wamekataa kabisa kipengele hicho kwa jinsi wanavyojadili katiba yao Dodoma.

Usalama haujadiliwi n.k
Yote hayo yanaangukia mikononi mwa JK. Vituko tunavyoviona ni legacy ya jk
 
BUNGE LAZIDI KUPOTEZA UHALALI WA KISIASA

MWANASHERIA MKUU WA ZNZ AJITOA, WAZIRI WA SHERIA ALISHAJITOA

MBINU ZINAKARIBIA KWISHA, SASA POSHO ZINATUMIKA KAMA CHAMBO


Wanaduru, awali ya yote ningeomba mpitie nyuzi hizi kama marejeo ya bandiko hili

https://www.jamiiforums.com/great-t...-za-ccm-kuingiza-katiba-yao-ya-mafichoni.html
https://www.jamiiforums.com/katiba-...wa-na-hatima-ya-muungano-15.html#post10523793

Tulieleza uwepo wa rasimu ya mafichoni ya CCM uliokuwa utumike kwa njia za ''wengi na wingi wa CCM''
Waraka huo tulieleza wazi ulikuwa umeandaliwa na nani na kwasababu zipi.
Wapo waliobeza na kuita maoni au uchambuzi kama mtambo wa majungu.

Kadri tunavyosonga mbele kila tulilowahi kulieleza ima limetokea, linatokea au litatokea.

Kwanza, wiki hii imetolewa ratiba ya bunge ikionyesha urefu wake. Habari hiyo ilipigiwa debe kwasababu moja;
Kuwarubuni UKAWA, kuonyesha kiasi cha pesa watakazopoteza wakiwa nje ya bunge ili kutokee mtafaruku na pengine baadhi yao kukacha UKAWA.

Habari kubwa ni ya Mwanasheria mkuu wa Zanzibar kujiuzulu nafasi katika kamati inayoandika rasimu ya CCM.
Kujiuzulu kwake kunafuatia kutowepo kwa waziri wa sheria wa Zanzibar.

Kwa hali hiyo, uwakilishi wa kisheria kutoka Zanzibar umeondoka na kuleta kutoaminiana au maridhiano miogoni mwa pande mbili

Sababu zilizonukuliwa zinasema mwanasheria amejiondoa kwa kuona hatari ya kujadili rasimu nje ya ile ya tume.

Hakuna ajuaye maudhui ya barua yake, kinachofahamika ni mwenyekiti wa bunge alikimbilia Dar es Salaam.
Upo uwezekano alikwenda kuonana na uongozi wa juu kuhusiana na tukio hilo linaloondoa kabisa uhalali wa kisiasa

Mwanasheria mkuu amehisi hatari ya kuandika katiba nje ya maoni ya wananchi.
Ameangalia hali ya kisiasa na kubaini tatizo. Muhimu zaidi ni kuona kamati tayari ikiwa na rasimu mbadala mkononi.

Kamati ipo chini ya mwanasheria mkuu wa zamani Chenge. Mwanasheria huyo anafahamika katika mambo yaliyolitia taifa aibu.
Duru iliwahi kumtaja kuwa mwandishi wa rasimu ya mafichoni akiwemo mwanamama aliyewahi kushika nyadhifa,taasisi za kimataifa.

Mwanasheria mkuu atatoa sababu za kisiasa zaidi ya ukweli unaojulikana.

Tatizo alililoliona ni kamati ya uandishi kuwa na rasimu mkononi huku ikinukuu hoja za wajumbe waliofundishwa na kuziandika kifundi zaidi.Kwa maana nyingine, tayari rasimu ipo kinachofanyika ni wajumbe 'walioielewa' kutoa maoni yao.

Ikumbukwe, waziri wa sheria licha ya kuwa mwana UKAWA, pia aliwahi kuwa katika mzozo na Spika wa BLW pandu kuhusu msimamo walioweka pamoja kabla ya kuondoka Zanzibar.

Hali ilivyo sasa ni kiashirio kizuri kuhusu mtazamo wa wazanzibar kuhusu katiba ya CCM inayoandaliwa.

Wapo wenye nia zao ambao kwa maslahi wanalazimika kufuata misimamo ya chama.Hao wanawakilisha kundi kubwa kule visiwani.

Wapo wanaoogopa hukumu ya wananchi watakaporejea visiwani. Nao wanasubiri muda, wataibuka na kuonyesha hisia zao.

Historia inatueleza wazi,wazanzibar wanaweza kuwa kimya wakishavuka bahari, wakirejea kwao ni watu tofauti na wale waliokuwepo Dar. Ndio maana mwakilishi wa CUF, Jusa aliwahi kusema inakuwaje wanapovuka bahari 'wana ufayata''

Swali muhimu sana kwa Sitta. Je, anategemea nini mbele ya safari ikiwa hali imeanza kuwa tete asubhi na mapema hii.

Je, hiyo rasimu ya CCM itapita? Na kama kuna shaka kwanini Sitta aendelee kupoteza fedha za umma kwa jambo lililowazi kabisa?

UKAWA waliliona tatizo kabla. Walifahamu kuhusu mbinu za rasimu ya mafichoni ya CCM iliyokuwa iingizwe kwa kutumia 'wengi na kura za wengi''

Mwenyekiti wa CCM aliwahi kusema wengi wapewe, ingawa pia wachache wasikilizwe tu.

Tusemezane
 
Ndugu yangu Nguruvi uliyoyasema ndiyo haya yanatimia; umekuwa ni nabii wa ukweli, mwonaji wa maono halisi. Kinachoendelea ni kile ambacho mtu yeyote mwenyewe kufuatilia siasa za nchi yetu alipaswa kukiona na zaidi sana wale viongozi wa vyama vya kisiasa. Safari hii wamepewa maji na juisi; kana kwamba ugomvi wetu ulikuwa ni wao kunywa juisi! Wamekubali kunywa maji!

Binafsi naona hili ni kama suala la Sungura na ile sanamu yenye ulimbo. Walinasa kwenye juisi za kwanza wanajikuta wananasa tena kwenye maji; na huko mbeleni wataitwa tena na safari hii wanaweza kupewa na wine kidogo... Hata wakijiamua kujitoa sasa sijui kama watakuwa na hoja zaidi kama wangejitoa mapema zaidi...
 
Ndugu yangu Nguruvi uliyoyasema ndiyo haya yanatimia; umekuwa ni nabii wa ukweli, mwonaji wa maono halisi. Kinachoendelea ni kile ambacho mtu yeyote mwenyewe kufuatilia siasa za nchi yetu alipaswa kukiona na zaidi sana wale viongozi wa vyama vya kisiasa. Safari hii wamepewa maji na juisi; kana kwamba ugomvi wetu ulikuwa ni wao kunywa juisi! Wamekubali kunywa maji!

Binafsi naona hili ni kama suala la Sungura na ile sanamu yenye ulimbo. Walinasa kwenye juisi za kwanza wanajikuta wananasa tena kwenye maji; na huko mbeleni wataitwa tena na safari hii wanaweza kupewa na wine kidogo... Hata wakijiamua kujitoa sasa sijui kama watakuwa na hoja zaidi kama wangejitoa mapema zaidi...
Mkuu,viongozi wa vyama vya siasa naweza kuwafananisha kwa mfano wa mbwa wakali ndani ya mageti. Pindi wanapokutana na chatu, hukunja mikia na kuitumbukiza miguuni wakisubiri huruma na hukumu ya chatu''

Katika uzi huu,tumeonyesha jinsi walivyokwenda kunywa juisi wakiambulia machozi.
Mfano mzuri ni ule wa kuahirisha maandamano, wakati wakiwa wanapata maji ya matunda, JK anasiani mswada siku hiyo hiyo walioahirisha maandamano. Wakaishia kupata kinywaji baridi.

Tumewaeleza, haiwezekani JK aliyekwenda kuvuruga mchakato akawa na suluhu au sehemu ya suluhu ya tatizo.

Mfano, JK kaunda tume na kashiriki kila hatua. Mwisho kawaanika wazee katika TV kama ze comedy.
Leo viongozi hao wanategemea nini ikiwa tume aliyoiunda mwenyewe haikuweza kuipa heshima?

Tumewaeleza pia, haiwezekani JK aacheie tatizo liendelee kwa muda mrefu na ghafla ageuke kutafuta suluhu.

Tukasema, JK na CCM hali ni tata, wanachotaka ni mahali pa kutokea ili kukinusuru chama kwa kutumia vyama vya siasa

Mazungumzo ya Dodoma yameitishwa na JK baada ya hali kuzorota na kuashiria mwisho mbaya.

Haiwezekani JK akane tume yake, halafu apate suluhu na wapinzani.Kikao cha Dodoma kililenga kukwamua mchakato.

Ghafla, kikao hicho kimebadilika na lengo ni kutafuta mbadala wa kurekebisha katiba kwa ajili ya uchaguzi.

Tuliwaonya wapinzani kuwa haiwezekani kwenda kwenye meza ya majadiliano wakati bunge la CCM linaendelea.

Tukasema hivi: Ni mwafaka gani utakaofikiwa ikiwa JK alishasema S3 hadi aondoke.

Huyu kesha apa kuwa S3 haziwezekani. UKAWA wanataka rasimu yenye msingi wa S3.
Je, walikubali kwenda kujadiliana au kwenda kupindua kiapo cha JK kwanza?

Pili, Je, kama muafaka ungefikiwa, UKAWA wangerudi bungeni kuanza na mwanzo au kuendelea na bunge lilipofikia.

Tukauliza, kwanini JK kama ana nia ya muafaka, asisitishe bunge hilo hadi kupatikane suluhu?

Hoja kwamba hakuna sheria inayomruhusu ni mfu. Ilikuwaje BMK likaahirishwa kupisha kikao cha bajeti na kwanini vifungu husika visitumike katika mazingira tuliyokuwa nayo.

NINI KINAENDELEA DODOMA

Wapinzani wameundiwa kamati ikiongozwa na wao wenyewe, CCM wakiwa sindikizaji.
Vyombo vya CCM vinaendelea na propaganda,majadiliano si kukwamua mchakato ni kutenegeneza mazingira ya uchaguzi mwakani.

Tayari wapinzani wamepewa 'wine' wakati wanasherehekea mvinyo na kilevi kidogo mada imebadilika.

CCM wamebadili mada baada ya hali kuwa mbaya. Hivi sasa bunge la Sitta halifanyi kazi kukiwa na udanganyifu wa majadiliano ya kamati n.k. Ukweli ni kuwa hali ya kisiasa ndani ya bunge ina mvutano, uwezekano wa kupata 2/3 ndani na nje ya bunge haupo. Mbinu zinaendelea kurubuni wapatikane wajumbe 17 kwa pesa na kila hali.

Hivyo Sitta ana ''buy the time'' wakati idara husika zikiwa kazini.

Kwa upande mwingine, Dodoma, JK naye anawatumia wapinzani ku'buy time'' wakati mambo yanaendelea kuwekwa sawa.

JK ana option mbili, ya kwanza ni kusikiliza kama Sitta atafanikiwa kupata 17 ili uhalali uwepo na awamwage wapinzani.

Ya pili, ni hii ya kusema mjadala wa katiba haupo na sasa ni kuhusu uchaguzi.

Utajiuliza, kama JK anajua katiba is impossible kwanini atoe pesa za umma kwa kitu anachojua matokeo yake?

Karata anayocheza hapa ni kuangalia hoja hizo mbili. Hoja ya uchaguzi ndiyo atakayoitumia kuwafunga kitanzi wapinzani na kuifungua CCM katika kitanzi.

Wiki hii lazima litatoka tamko kutoka kwenye kamati ndogo huko Dodoma ikieleze kushindikana kwa mchakato na sasa ni suala la uchaguzi wa mwakani.

Atakayetoa kauli hiyo ni kiongozi anayeongoza kamati ambaye ni wapinzani.

Hilo litawaosha CCM na wapinzani kuonekana kama wameridhia mchakato kushindwa na wameafiki habari ya uchaguzi mwakani.
JK na CCM watakuwa off the hook.

Ni suala rahisi tu la kujiuliza. Hivi JK anawezaje kuwa mwema sana kwa uchaguzi na kinyume chake katika katiba?

Hivi anawezaje kuvuruga bunge, halafu akatengeneza mazingira mengine mazuri zaidi kwa wapinzani ya uchgauzi?

Hivi kulikuwa na ulazima gani wa kukutana na JK bila pre-condition ikiwa ni pamoja na kujua agenda, kusitisha bunge kwanza n.k.?
 
Uzuri wa siasa za Tanzania, kila mtu ni political analyst!

Karibuni kwenye political ground zero ili mzionje siasa zilizo halisi na siyo hizi za kudonoa kupitia keyboard/keypad kwenye mitandao.

Hata Katibu wenu Mkuu, Dkt. Slaa alishawakaribisha katika andiko lake hili,
Mtazamo,
Kwanza ni shukuru sana kwa onto kali la Mzee wangu Mwanakijiji. Mtazamo, kwa mtazamaji wa Real Madrid na Barcelona, anayekaa nje ya uwanja ni rahisi sana kuona na kuchambua makos a ya Timu iliyoko uwanjani. Ebu mruhusu mchambuzi mkubwa wa mchezo aingie uwanjani, mwachie mwenye nusu uwanja, kipa aondoke alafu uone " yuko peke yake".alafu uone Kama hatashindwa kufunga boa. Nimwombe ndugu yangu Mwanakijiji achukue likizo, hata ya nusu mwezi tu, tumpitishe kwenye Maputo tunayopitia, Kama baada ya mud huo atatumia lugha anayotumia.
Kujenga hoja katika mlengo wa siasa za probability zenye matokeo ya aina mbili hakuhitaji kisima kirefu cha fikra!
 
Back
Top Bottom