#COVID19 Ukiacha Chanjo za Corona, kuna kitu gani cha maana kilichofanywa na Serikali ya awamu ya 6?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Serikali ya awamu ya 5 ilipoingia madarakani tuliona mageuzi ya kutisha na amsha amsha ya maendeleo kila mahali, miradi iliibuliwa na kutekelezwa kwa kasi, ikawa ndio kama tumezinduka toka usingizini.

Hii serikali ya awamu ya 6 inanishangaza sana, toka imeanza hadi sasa imekuwa ni Corona na Tozo mwanzo mwisho, yaani zaidi ya hivyo viwili hakuna kingine, kama si Corona basi ni Tozo. Huku Madelu anakamua Tozo, huku Gwajima ananunua chanjo, huku wanakamua Tozo, huku wananunua chanjo, baasi, hakuna lingine.

Tunaomba serikali itupe tumaini kwamba inajali maslahi ya wananchi, hata kama ni kwa kutudanganya tu, iachane na kelele za Corona, anaetaka kuchanjwa achanjwe lakini isiwe kwa kupiga promo kubwa hasa kupitia waziri, mnapofanya shinikizo kubwa mnatupa wasiwasi wananchi na kututisha kwamba Tozo zetu zilikuwa ni kwa lengo maalum tofauti na yale mliyoainisha kwamba ni malengo ya tozo.

Mi naogopa siku kuja kusikia Chanjo zimesababisha upotevu wa trillion 5 za fedha za Tozo, ufisadi wa namna hiyo unaweza ukasababisha wengine tunaopenda nchi tukapata magonjwa ya moyo na pressure, naogopa sana. Sina ushahidi wowote, ila ni hisia mbaya niliyoanayo kiasi napata strong connection kati ya timing ya Tozo na ununuzi wa chanjo za mikopo ya bei na masharti ‘nafuu’.

=================================

Update: 08/09/2021
Naona kumbe hizi Tozo zinaweza zikatumika kuulipa huu mkopo unaoenda kuteketezwa kununua chanjo hewa kwa matrillioni, inaumiza sana. Hizo pesa tunajenga flyover ngapi? Badala yake tunaenda kununua Johnson and Johnson


===============================
Update: 27/09/2021

👆🏽 Haya sasa, hapa ndio mjue kwanini watu tulikuwa tunapigia kelele hizo juhudi za madalali wa chanjo za kutuibia pesa kwa mgongo wa Corona, matokeo yake ndio hayo sasa, sasa kaeni kimya mnyolewe, pumbavu kabisa!
 
Utakufa kwa KIHORO utafikiri umechomwa chanjo ya tako 🤣🤣🤣

Ukiachana na bidii uliyonayo ya kununua bando la kumsifia kibwengo Magu na kuponda chanjo, ni kitu gani cha maana umeshafanya mpaka sasa ???
 
Serikali ya awamu hii imeturahisha vijana kutoweka mkazo wa kukamata vijana tunao piga mimba wanafunzi.
Hapo awamu hii wameweza
 
kubambikiza kesi
kumsafirisha bibi wa zenji kwa ndege
safar za ndege za kutosha
services za ndege za kutosha
vitisho kwa walipa kodi et tuhamie burundi
vitisho kwa walipa kodi kuhusu tozo
maneno matupu
......##tutaonana 2025
 
CHANJO NA TOZO NDO MAENDELEO YA WATU KAMA CHADEMA WALIVYOSEMA.TUMEACHANA NA MASUALA YA MAMIRADI YA SERIKALI KWANI HAYO NI AMENDELEO YA VITU. KWANZA MAGUFURI ALIFANYA SIS SERIKALINI TUSHINDWA HATA KUIBA SABABU YA UFUATILIAJI WAKE LAKINI SASA SAFI,,TUNAOERDIEMS ZA KUFA MTU ZA KUHAMAISHAH CHANJO NA TOZO
 
 
Kuna maslahi gani muhimu kwako kuliko afya yako mwenyewe, uhai ndio kitu peke unachotakiwa kukijali. Vitu vingine vyote unaweza kuvitafuta hata kesho. Uhai ukipoteza ndio wako- unazikwa na kuanza kusahaulika taratibu.
 
Update: 08/09/2021
Naona kumbe hizi Tozo zinaweza zikatumika kuulipa huu mkopo unaoenda kuteketezwa kununua chanjo hewa kwa matrillioni, inaumiza sana. Hizo pesa tunajenga flyover ngapi? Badala yake tunaenda kununua Johnson and Johnson

 

Haya sasa, ndio tushapigwa hivyo...
 
SASA WEWE MTOA MAADA UNATAKA TUFE NJAA,, SASAHIVI HIZI DEAL ZA CHANJO NDO ZINATUPA ULAJI
 
KUMKAMATA , KUMSAFIRISHA NA KUMPEKUA GAIDI. NA USHAHIDI HAKUNA 😀
 
KUMKAMATA , KUMSAFIRISHA NA KUMPEKUA GAIDI. NA USHAHIDI HAKUNA 😀
Ninachojiuliza, chanjo za mwanzo hata nusu hatujazitumia, tunaenda kukopa chanjo za bilioni 300, maana yake nini? Hizi tozo hazina kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…