Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Wawekezaji wenzangu mko poa?
Ilikuwa usiku wa fainali ya UEFA mwaka 2026, nilipoweka dau la mshahara wangu wote wa mwezi nikiwa na uhakika wa kushinda mamilioni. Baada ya filimbi ya mwisho na timu yangu kufungwa, nilibaki nimepoza macho nikiiangalia simu, huku nikijua sina hata senti ya chakula, kodi, au nauli ya kwenda kazini kesho yake.
Aibu na msongo wa mawazo nilizopitia wiki ile kutokana na kukopa kila kona ili kufunika lile gape lilinitoa jasho la damu, na hapo ndipo nilipozinduka na kugundua kuwa sikuwa nabeti kwa ajili ya burudani tena, bali nilikuwa mtumwa wa tamaa zangu.
Tukio lile lilikuwa funzo kubwa lililonirudisha kwenye mstari. Tangu siku hiyo, nilijiwekea sheria ngumu: nabeti tu kwa kiasi ambacho nikikipoteza hakitaumiza mfuko wangu wala kuiba tabasamu la familia yangu, na nikitandika mkeka wangu wa siku, iwe jua au mvua, sitandiki mwingine.
Ni nini kilitokea ukaamua kupunguza kubeti?