Ukiona watu/mtu anaacha mada iliyomezani na kushambulia personality, kabila, rangi, nchi etc ujue huyo au hao watu hawana majibu ya hoja, au ni mazuzu. Hoja ya jamaa ni hoja nyeti sana na ameweza kutoa mifano michache tu. Bottom line elimu yetu dhaifu na social life yetu ya kiswahili na uswahili vimetuathili sana, hatuko serious kwenye almost mambo yote ya msingi, Wewe fikilia nchi imefikia mahali ili upande cheo lazima uwe chawa na kila mtu anajitahidi kuwa chawa, ujinga mtupu. Vijana wameacha kufanya mambo ya maendeleo,tumeishia kuwa mashabiki wa mipira, watu wa kubeti, watu wa kupenda starehe kuliko kazi. Yaani ni aibu sana kama nchi.
Nakubali kujua kiingereza sio kipimo cha akili, ila tutabishana mpaka kesho lazima tuandae kizazi chetu kiweze kukabiliana na utandawazi wa kidunia. Sisi ni wabishi ila ukweli unabakia palepale. Mawasiliano na report nyingi za kiserikali zinaandikwa kizungu, mahakama, report za kibenki, masomo yote sekondari mpaka university. Just imagine unajifunza masomo magumu kwa kutumia lugha husiyoielewa unategemea nini,halafu mjinga mmoja anapinga. Kama tuko smart basi tubadilishe hata lugha ya kufundishia.Hatuwezi kwa sababu ni wavivu na upeo wetu ni mdogo kweli.
Wewe ukitaka kujua utoporo wa wabongo, anzisha mada ngumu zinazohitaji critical thinking na wide analysis, hapo ndipo utawajua wabongo tulivyo mbumbumbu. Angalia jinsi walivyomshambulia mtoa mada aliyejitolea kuusema ukweli. Ifike mahali tubadilike. Hatuwezi kujilinganisha na wakenya kabisa, sisi ni mbumbumbu