Ukiachana na dunia kulizunguka jua na kujizungusha kwenye muhimili wake nadhani kuna mzunguko mwingine ambao wanasayansi hawajaugundua

Je sayari zingine linazizungukia vipi ili kila moja iendane na muda ulMuda
MUda upo hata kama hakuna jua,weka vizuri swali mkuu
Yaani kama linakamilisha mzunguko wake kwa masaa 24 basi sayari zote sitakuwa na siku yenye urefu wa masaa 24 ya hapa duniani
Masaa 24 ni vipimo tu,jua haliathiriwi na masaa.

Yaani leo saa ikigoma jua litaendelea kupiga kazi halitasomama.

Hali kadhalika jua kama hatulioni dakika zitaendelea kwenda tu kuonesha kwamba hakuna mafungamano ya jua na saa.
Mpona mizunguko inatofautiana muda kwa kila sayari?
Hayo mambo ya sayari zongine KUHUSU MUDA bado ni theory tu hazijathibitishwa ukweli wake mpaka ifikie hatua ya kujengea haoja hapa
 
Sawa mkuu lakini acha tuendelee kuhoji mitazamo yetu kwa wengine.
 
Mkuu swala sio kuelezea hapa swala ni kuanza kuelezea vitu ambavyo unaweza kuvipata na vimeelezewa vizuri zaidi kwa wahusika bila kuwa vimemenywamenywa! Nachoweza kutoa ni muongozo wa upite wapi na wapi uangalie kipi na kipi.. si kwamba mtu haelewi ila akijifikiria yeye mwenyewe hadi kukielewa ilikuwa tabu kidogo! ..😅
Swala ni passion mkuu mi nachotaka uelewe Kwanza hizo concept then ndo nijue tunaanzia wapi!
Mfano hapo umeandika gravitational force!! Hivi unahabari gravity haifai kuitwa force!! ... But how..?? Ndo maana nikakuambia msome Albert Einstein utajua mengi zaidi.. mkuu mi sikupi samaki tu bali nakupa ndoano ukalowe samaki kabisa..😅
 
Sawa mkuu.

Nipe njia nipite wapi na niaze kusoma kitu gani ili iwe rahisi kwangu kuelewa haya mambo.
 
Hoja ya sayari zingine kuwepo unaikubali ila hoja ya kuwa kila sayari kuwa na muda wake katika kuzamisha jua hiyo unasema ni nadharia! Sasa ili jua lizunguke dunia basj sayali zote ziko katikati ya obit ya jua? Je unaamini katika hilo
 
Mataga utasikia ooh mabeberu ndo wameleta baridi hii. Dame shit wakwende huko na umbulula wao
 
Sawa mkuu.

Nipe njia nipite wapi na niaze kusoma kitu gani ili iwe rahisi kwangu kuelewa haya mambo.
Okay kama utakuwa na muda wakutosha fatilia kwanza general relativity kama ilivyoelezewa na Albert Einstein kiujumla fatilia theory za huyu jamaa kama unamuda wa kutosha lakini. Ila kama utataka kuwa specific fatilia space how is it!,what is time kwa mujibu wa Albert Einstein, gravity.. mengine utayakuta huko then ukielewa hayo machache utapata mwanga wa kujibu maswali yako.. mcheki YouTube Brian Greene ndo anaelezea vizuri haya manadharia au Jim Al Khalil. Mkuu jiandae muda wako mengine tutakuwa tunaelekezana tu.
 
Kujibu swali lako sithani kama kuna mzunguko ambao haujulikani.

Mbali na mizunguko uliyosema jua nalo linazunguka katika mhimil wake na pia linazunguka centre ya milkway galaxy.


Kuhusu baridi kali ni kweli inachangiwa na mzunguko wa dunia kwa jua na orbirt yetu sio duara bali ni elliptical hivyo kuna mda dunia ipo karibu sana na jua na kuna mda ipo mbali na jua (aphelion) hii ni baridi ya kawaida maana computer za nasa zimekadiria miaka elfu hamsini ijao elliptical orbit italeta ICEAGE
 
Dar saiv kuna baridi tuache masihara kwa wanaokaa kuanzia mbezi kurudi kibahaa hawatopInga hili
 
Dar saiv kuna baridi tuache masihara kwa wanaokaa kuanzia mbezi kurudi kibahaa hawatopInga hili
Hoja hapa kwa nini imedumu kwa muda mrefu hivi? Nini kimetokea?
 
Halafu kuna huu mzunguko wa kutafuta Passpoti huko Uhamiaji huo ndio mzunguko mkuu.
 
Mkuu,

Haya mazungumzo mazuri na muhimu sana. Ni muhimu kwenda na data, but you are definitely on to something here.

Definitely kuna mizunguko mingi zaidi ya uliyotaja ambayo wanasayansi wameigundua na imeandikwa, kwa hivyo tujielimishe kwanza kuhusu hiyo iliyogunduliwa na iliyoandikwa kabla ya kuongelea sana ambayo haijagunduliwa, ambayo nayo inawezekana ipo.

Kuna mizunguko kama ya solar system kuzunguka kitovu cha galaxy hujaitaja, ingawa sifikirii kwamba hii inaweza kuwa na impact kwenye hali ya hewa.

Sijaona ukitaja mambo kama ice ages. Kama hujazisoma hizi, anza kusoma zaidi hapa Ice age - Wikipedia

Kuna mambo mengine hata si mizunguko per se, ila mambo kama sunspots, yani, maeneo ya jua ambayo yanakuwa na joto la chini na kusababisha imbalance katika nishati ya jua tunayoipokea, na hivyo kuweza kusababisha baridi sehemu ambazo hatujazoea.

Kama hujasoma zaidi kuhusu sunspots ona hapa .

Kwa hivyo kuna mambo mengi ya kujifunza.

Ila, kuna mjadala mkubwa kuhusu climate change na jinsi gani inasababishwa na shughuli za watu kama vile kukata miti, kuongeza hewa za Carbon kwenye hewa yetu, na mambo mengine mengi kama hayo. Kuna watu wanasema mabadiliko haya ya hali ya hewa kwa kiasi kikubwa yanatokana na shughuli za watu, na watu wanaweza kubadili muelekeo huu kwa kubadili maisha yao, kuacha kukata miti na kupanda miti zaidi, kuacha kutumia vibaya nishati na kupunguza utoaji wa Carbon kuipeleka kwenye hewa yetu. Na kuna wanaosema kuwa mabadiliko haya yanatokana na mabadiliko ya asili zaidi kama hizo ice ages na sunspots, mambo ambayo yako nje ya uwezo wetu kuyabadilisha.

Kwa sasa, ushahidi mwingi wa kisayansi, pamoja na wanasayansi wengi wasomi, wanakubali kwamba mabadiliko ya hali ya hewa yanasababishwa na maisha ya watu, si mambo ya kiasili, na tuna muda mchache sana wa kuzuia na kusahihisha mabaya haya yanatotokana na matumizi mabaya ya nishati. Wanasayansi wasomi wa mambo haya wanaokubali hivi ni wengi kuliko wanaokubali kwamba haya ni matokeo ya mizunguko na mambo ya kiasili tu.

Labda kwa sasa niseme hivi kama sehemu ya kuanzia tu, halafu, tuweze kupata chachu zaidi ya kuendeleza mjadala kuanzia hapa.

Shukurani The Monk kwa heshima kubwa ya mualiko hapa.
 
Mkuu Kiranga sisi wengine hizo elimu za nyota na mambo hayo tunayajua kidogo sana. Tunapoona mabadiriko kama haya tunahisi kuna mambo ya kimfumo zaidi ya hii mifumo tuliyoisoma shule za misingi na secondari. Mambo ya ice
Sawa mkuu. Ngoja nipitie hiyo "ice age" nione ni kitu gani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…