Ukiachana na tabia za kimtandao wewe ni mtu wa aina gani?

Ukiachana na tabia za kimtandao wewe ni mtu wa aina gani?

Kwanza mtu huwezi kufake miaka nenda rudi, unless wewe ni maarufu na una verified ID.

Hapo utajitahidi kukwepa baadhi ya maneno.

Ila with fake IDs most people are mostly real.
Kuna mwingine ni afisa wa serikali, kuna mambo ofisini au serikalini anaona hayapo sawa ila anaogopa kukemea, huyo hashindwi kuja humu kukemea mambo hayo.
Na kwenye hilo analokemea kama hakutakuwa na mabadiliko ataendelea kukemea mtandao lakini ukimkuta ofisini huwezi kumdhania kama ni yeye.

Nje ya mada, niliwahi kukaa na mke wa kigogo mmoja mkubwa sana nchini, alinishangaza alipokuwa anafurahia taarifa za kigogo wa twitter zinazomhusu Magufuli, tena akawa anazizosoma kwa sauti huku mumewe anamsikiliza tu.

Lakini hiyu mtu akiwa ofisini atajifanya hata kigogo wa twitter hajawahi kumsikia.
 
Back
Top Bottom