Ukiachwa achika

BabaMorgan

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2017
Posts
4,869
Reaction score
13,137
Mwaka jana kuna binti aliniacha ghafla kupitia sms nanukuu "D nimefikiria nimeona hatuwezi fika mbali naomba tuachane" hapo ni baada ya dk kadhaa za kuambiana tunapendana akanipiga block kuanzia kwenye simu mpaka kwenye mitandao yake ya kijamii nikawa sina direct access ya kuwasiliana naye siku zikaenda likapita.

Na mimi mwezi uliopita nimepata katoto ka mwaka 2000 sasa alikuwa akipiga simu au kutuma sms nisipo respond kwa wakati ananijia juu hizo pigo mimi sijazoea maana kuna mood nikiwa nayo sipokei simu ya mtu yoyote labda iwe ya pesa tu sasa juzi kati tumekutana ananiletea pigo za kudeka anataka kudekezwa nilivyorudi geto nikafanya tathmini ya kina nikaona haya mahusiano hayanifikishi popote zaidi ya stress tu.

Ikabidi nimpe tofali asiwe na access ya kunipata sasa naona namba ngeni zinanipigia nikipokea mtu anajiliza namwambia nina kazi nitakupigia.

Sasa namba ngeni zinaenda kuwa na wakati mgumu kupokelewa kwenye simu yangu maana kuna loan officer wa bank fulani naye nilimblock ana mtindo wa kunipigia kwa namba ngeni.
 
Uwezi ukakuta mtu unamkataa serious alafu bado anakusumbua...

Huruma ya nini kama una acha,. acha kweli sio unasema unaacha unaishia kumpa block na kumwambia ujamwambia πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Demu alikukataa na akakupiga block kila sehemu kisha akajirudisha kwako tena na wewe ukampokea1

Wewe ni wakupigwa makofi mpaka akili zikukae sawa,nyie ndio mnasababisha wanaume wote tunaonekana laini laini,
Huyo demu alipata dume akaenda kuchezea mkia kisha akaachwa huko ndio akajirudisha kwako,

Hebu kaza kidogo uwe na roho ya kiume na maamuzi ya kiume.
 
Kusoma ni jambo moja kuelewa ni jambo lingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…